Kitisho cha Dr. Slaa si zaidi ya Mrema - Kinana

Kitisho cha Dr. Slaa si zaidi ya Mrema - Kinana

Ni maneno yenye ukweli Mrema hakuwa na kashfa ndani ya jamii iliyomzunguka na kama zilikuwepo hazikujulikana; Slaa dhambi ya uwongo inamsuta; sijawahi kuona kiongozi asiye na maadili kama Slaa; hainingii akilini kuona mtu anayejinadi ni kiongozi wa jamii kutelekeza familia yake kwa ajili ya kimada na leo atumie majukwaa ya kisiasa kujinadi eti ni mtetezi wa wanyonge ikiwa alishindwa kuitetea familia yake hasa watoto dhidi ya tamaa zake za kimwili leo ataweza kuwatetea watanzania?

Chama
Gongo la mboto DSM
Mkuu mke Dr si mlimpa Udiwani mkawa mnajichukulia kwenye mikutano kama kawaida yenu (Mwigulu Mchemba) sasa wewe ulitegemea huyo mzee wetu afanyeje??? Hata Mandela aliachana na mke mzinzi!!
 
Tuache unafiki, kama mtu hakunyimi usingizi mipango ya kipuuzi kuzushia wengine inatoka wapi? Si ukae kimya tujue kweli haikunyimi usingizi. Halafu mbinu nyingine za kitoto kweli, mara kadi, mara babu mara ooh, ukiona hivi ujue hali mbaya umebanwa kweli. Vumilieni fanyeni kazi tunataka maisha bora kwa kila mtanzania, HATUJASAHAU.
 
Katibu wetu mkuu anza ziara mikoani tumekumiss mbaya hasa hapa kwetu Sumbawanga nape alizomewa wewe utashangiliwa
 
Hivi Mrema alikuwa na nguvu gani 2005? Si bora angesema Lipumba maana ndiye aliyekuwa mshindi wa 2 akifuatiwa na Mbowe.

Mrema ni 1995
bhana.

mkuu soma post ya kwanza vizuri, nadhani umeshamix mambo hapa.
 
Tuache unafiki, kama mtu hakunyimi usingizi mipango ya kipuuzi kuzushia wengine inatoka wapi? Si ukae kimya tujue kweli haikunyimi usingizi. Halafu mbinu nyingine za kitoto kweli, mara kadi, mara babu mara ooh, ukiona hivi ujue hali mbaya umebanwa kweli. Vumilieni fanyeni kazi tunataka maisha bora kwa kila mtanzania, HATUJASAHAU.

Mkuu wangu hawa watu ni vituko
 
Mrema katika uchaguzi huo alikuwa na wabunge wakuchaguliwa kama 19,chama chake hakijawahi kuwa na kambi rasimi ya upinzani bungeni.Slaa chama chake kilipata wabunge wa kuchaguliwa 23 chama chake ndiyo chenye kambi rasimi ya upinzani bungeni.Slaa kwenye uchaguzi mkuu alipata kura nyingi kuliko mrema .wakati wa mrema ushindi wa kishindo,kisigino na wakimbunga upande wa ccm uliendelea.Slaa alipoingia kwenye kinyang'anyilo cha urais alikomesha ushindi wa kishindo,kisigino na wakimbunga upande wa ccm.sasa Kinana ametumia vigezo gani? Ili amwone Dr slaa hamnyimi usingizi na alie wapa wakati mgumu ni Mrema?au anajikosha kuwa migogoro inayozuka ndani ya Chadema haifadhiliwi na chama chake? au ndiyo kuweweseka kwenyewe?.
 
Mkuu Tukundane nikurekebishe kidogo-Hakuna mgogoro wowote CHADEMA. Nape kulipa wahuni wa BAVICHA waliofukuzwa ndiyo useme kuna mgogoro?
 
Ndo yeye huyo na Serikali imekaa kimyaaa. Ingekuwa wewe chombo chako kimekamatwa na nyara kama zile hahahaha, mbona jera unaiona hivi hivi.
 
Kivuli cha Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa kinazidi kukiyumbisha chama tawala CCM.

Baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kuanzisha kampeni za kila aina ya vituko dhidi ya Dr Slaa na kuonekana kugonga mwamba sasa kampeni hizi zimechukua sura mpya baada ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kujitosa.

Akizungumza na gazeti la Dira Tanzania Kinana amezungumzia kishindo cha Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Slaa na kusema hakimnyimi usingizi.

Kinana amesema pamoja na nguvu za kisiasa alizo nazo Dr Slaa kwa sasa lakini anaamini CCM ilikuwa na wakati mgumu zaidi mwaka 1995 kwani nguvu za Augustine Mrema wa wakati huo zilikuwa kubwa kuliko za Dr Wilbroad Slaa wa sasa.

Source:
DIRA TANZANIA.

UuuuuuuuuuuuWiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.......!!!!!! WEKA MBALI KABISA NA TEMBOoooooooo.....!!!!!!!!!
 
achana kabisa na mtu anayeongozwa na nguvu za mungu.
 
Kivuli cha Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa kinazidi kukiyumbisha chama tawala CCM.

Baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kuanzisha kampeni za kila aina ya vituko dhidi ya Dr Slaa na kuonekana kugonga mwamba sasa kampeni hizi zimechukua sura mpya baada ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kujitosa.

Akizungumza na gazeti la Dira Tanzania Kinana amezungumzia kishindo cha Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Slaa na kusema hakimnyimi usingizi.

Kinana amesema pamoja na nguvu za kisiasa alizo nazo Dr Slaa kwa sasa lakini anaamini CCM ilikuwa na wakati mgumu zaidi mwaka 1995 kwani nguvu za Augustine Mrema wa wakati huo zilikuwa kubwa kuliko za Dr Wilbroad Slaa wa sasa.

Source:
DIRA TANZANIA.

kwani kipindi mrema alivuna viti vi ngapi bungeni na alipata % ngapi ya kura??mrema alikuwa ana nguvu ya soda!promotion ilikuwa kubwa kuliko show yenyewe.
 
Kitu cha muhimu hapa ni kudhihirika kwa fikra mgando za CCM. Wanaamini bado Tanzania ya leo ni sawa ni ya mwaka 1995.
 
Kivuli cha Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa kinazidi kukiyumbisha chama tawala CCM.

Baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kuanzisha kampeni za kila aina ya vituko dhidi ya Dr Slaa na kuonekana kugonga mwamba sasa kampeni hizi zimechukua sura mpya baada ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kujitosa.

Akizungumza na gazeti la Dira Tanzania Kinana amezungumzia kishindo cha Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Slaa na kusema hakimnyimi usingizi.

Kinana amesema pamoja na nguvu za kisiasa alizo nazo Dr Slaa kwa sasa lakini anaamini CCM ilikuwa na wakati mgumu zaidi mwaka 1995 kwani nguvu za Augustine Mrema wa wakati huo zilikuwa kubwa kuliko za Dr Wilbroad Slaa wa sasa.

Source:
DIRA TANZANIA.

Mpotofu huyu...analeta mind games kwenye mambo yanayogusa mioyo na hisia za watu

1995 pamoja na kuwa tayari nilikuwa na mahaba makubwa na mabadiliko, ni wazi kuwa Mrema asingeweza kuunda serikali..halafu waziri awe nani?Masumbuko Lamwai..??na nani mwingine?...ni wazi NCCR-Mageuzi haikusheheni viongozi bora wa kutosha wa kuunda serikali..kwa hivyo hata sisi tuliokuwa na hamu kubwa ya mabadiliko tayari tulishaona upungufu huu wa kimatayarisho wakati huo na kujitilia shaka..

Isitoshe elimu ya demokrasia kwa umma ilikuwa chini sana 1995 ukilingana na sasa hivi..nani mwaka 1995 angeweza kumwambia mwananchi wa huko Shinyanga vijijini kuwa umasikini wake unatokana 100% na utawala wa CCM naye aelewe na kukubali??...Kinana asubiri 2015 tutamwambia vizuri.
 
Wananchi tunamacho na masikio hivyo tulisikia na kuona ya Mrema wa mwaka 1995 na sasa tunaona ya Dr. Slaa. Penda usipende CCM haijawahi kuyumbishwa kama sasa hivi na Dr. Slaa. Mrema alileta vuguvugu tu na baada ya uchaguzi CCM waliendelea kama jana na juzi.

Lakini tokea uchaguzi umefanyika 2010 mpaka leo wanagongana tu kuhusu Dr. Slaa na CHADEMA. Mfano sasa wameamua kuzunguka nchi nzima na kuchukua television zote prime time ili watangaze wanayodai kuwa ni mafanikiao yao.

Yote haya ni kwasababu Dr. Slaa na CHADEMA wamesema kuwa CCM hawajanya hata robo ya ahadi zao na wanatumia vibaya hela za umma.

Haya yote kipindi cha Mrema hata harufu yake haikuwepo. Kitendo cha Kinana kusema kama ni kweli alisema ni ushahidi tosha kuwa Slaa ni moto mwingine.
 
Hivi huyu KINANA si ndio agent wa pembe za ndovu au nimechanga majina

Ndio yeye huyo na serikali imekaa kimyaa. Ingekuwa wewe sasa ndo chombo chako kimekamatwa na nyara za serikali kama hizo hahaha, mbona jera unaiona ile pale mbele yako
 
Inanikumbusha waziri wa habari wa IRAQ wakati wa vita vilivyomuondoa Sadam madarakani. Jina lake kama vile Comical Abdurahman, au nimekosea?
Mkuu atakuwa ni AL SAYEEF
yule jamaa sitamsahau maana alikuwa anajitahi kweli kweli kukanusha kila kitu kibaya dhidi ya Sadam Husein huku Bongo tukamfanisha na Ramadhan Ally Mapuri ambaye alikuwa Waziri wa mambo ya ndani na Katibu mwenezi wa CCM!!
 
Dr Slaa kama wanadhani sio tishio wajue nyuma yake kuna wananchi wenye hasira na maisha duni wakati wachache wanatumbua nchi vilivyo!sasa hao wananchi ndio tishio ambao wako nyuma ya Dr Slaa
 
Back
Top Bottom