Kidatu,
Mkuu haya ni maneno (fikra) ya Mwalimu Nyerere na zilikuwa SIASA tu kutaka kutisha watu na kukatisha tamaa..Katika makosa makubwa ya mwalimu ni ktk kurithisha iwe kitaifa au familia yake. Mzee huyu alikuwa hana kipaji hicho kwani kila aliyemchagua iwe ktk familia au Taifa wote ni BOMU!..
Hivyo tusitake kuamini maneno yake, wewe kama unataka kugombea uongozi ingia ktk siasa..Upizani wa kweli utaletwa na Mtanzania! hawa wote ni wababaishaji tu wanatafuta KULA!
Bravo Bravo !!!!!!!!!!!!!
Mkandara, kwenye siasa kuna watu sio president material, sio mawaziri material na wao wanajijua. Lakini kutokana na kuwa siasa inayo nafasi nyingi ya kutoa ulaji, basi watu watampamba mtu hili wapate ukuu wa mkoa wilaya au ukatibu.
Sasa hawa watu wanaweza kumpamba mkuu wa nchi, na slogans za kisiasa zikawa kweli na kufanywa imani.
Tukirudi kwenye mada. Siasa za Tanzania zina mtazamo wake. Ukiwemo kwenye kundi la BIG BOYS, yaani Rais, mawaziri, mkuu wa mkoa, wabunge, huwezi kuona matatizo ya nchi kutokana na mtazamo wa wananchi.
Na mtu yoyote aliyetolewa nje ya U-BIG BOYS atataka kurudi kule kwa mbinu zozote zile. Tulishaona wanatoa shillingi katika bajeti kwa malalamiko mbalimbali. Hili kutulizwa wanapewa vyeo na kunyamaza. Hivyo sioni maneno ya Kitine kuwa yana Good Intentions.
Kitine anaona nchi inaongozwa kienyeji. Kuongoza kienyeji, ni kuongoza nchi bila kufuata katiba au misingi ya sheria.
Mpaka sasa nchi haijaongozwa kienyeji. Pamoja na kutongozwa kienyeji ni lazima tukubali kuwa ufanisi wa serikali katika kuleta mabadiliko ya wananchi wake ni mdogo sana. Na sababu kubwa ni KATIBA na MUUNDO MZIMA WA SERIKALI.
Kwa mfano rais anachagua mawaziri kutokana na wabunge. Kama wananchi mmechagua WABUNGE WEZI na MABOMU hao mawaziri wazuri watatoka wapi
😕.
It really amuse me kuona Chenge, Lowasa wanapokewa kwa vishindo majimboni kwao wakati wameliliza taifa.
Hawa watu, hata kama rais waliwachagua kwa kuwapendelea, bado walikuwa na TALENTS na Elimu ya kulisaidia taifa lao but they choose not to do that. Na hapa huwezi kum-prove wrong anayesema NDIVYO TULIVYO.
DR. Kitine, na u-DR wakati alikuwa na TALENTS and EDUCATION kulisaidia taifa lake wakati alipokuwa one of the BIG BHOYS, lakini alichagua kufanya kinyume.
Kwa kuanzia mimi naona KATIBA ya NCHI ni Berlin wall na sio CCM na tusubiri kugawanyika kwa CCM. KATIBA isiifanye CCM au chama cha siasa kuwa kikubwa kuliko nchi.
Kuna msemo huko Algeria kuwa: In other countries, the state owns the army, but in Algeria the army owns the state.
Likewise: In Tanzania, the constitution has allowed one political party to own the country. Na kama kuna uenyeji basi hapa ndio unapoanzia. Watanzania amkeni kutafuta constitution itakayosisitiza transparency na accountability.
Hizi AD-HOC solutions za kusikiza wanasiasa, hazita tufikisha sehemu yoyote.
Watanzania tear down this wall (Katiba).