Kitine: Nchi sasa yaongozwa kienyeji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitine: Nchi sasa yaongozwa kienyeji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 19, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,820
  Trophy Points: 280
  Kitine: Nchi sasa yaongozwa kienyeji

  na Edward Kinabo
  Tanzania Daima~Sauti ya watu​


  MKURUGENZI Mkuu mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Dk. Hassy Kitine, amesema taifa linakabiliwa na tatizo kubwa la uongozi, ambalo halijawahi kutokea katika historia ya nchi.

  Kitine ambaye aliiongoza idara hiyo nyeti kwa karibu miaka 30 zama za Serikali ya Awamu ya Kwanza na ya Pili, alisema ukosefu huo wa uongozi umesababisha nchi iongozwe kienyeji.

  Kachero huyo namba moja kwa miaka mingi, ambaye alilazimika kujiuzulu wadhifa wa uwaziri wa nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) wakati wa utawala wa Benjamin Mkapa, mwishoni mwa miaka ya 1990 kutokana na kuhusishwa na kashfa ya mkewe kufuja fedha za umma kiasi cha shilingi milioni 40, alirejea kutoa kilio chake cha miaka mingi cha kuporomoka kwa maadili ya uongozi nchini.

  Kitine ambaye aliwahi pia kuwa Mbunge wa Makete kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), alitoa matamshi hayo mazito katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam jana, alipozungumza na waandishi wa vyombo kadhaa vya habari.

  “Hali tuliyofikia si nzuri, tena niseme ni mbaya sana. Kuna kuporomoka kwa kiasi kikubwa kwa maadili ya uongozi. Na hii nawaambia, nchi haijawahi kuwa katika hali mbaya huko nyuma kama ilivyo sasa. Kwa hali tuliyofikia, ni vigumu kurekebisha maadili ya uongozi.

  “Tatizo kubwa ni viongozi kukosa integrity (uadilifu). Kwanza ni integrity ya viongozi wenyewe, pili ni commitment (wito), tatu ni nationalism (utaifa). Haya ndiyo yalikuwepo wakati wa Mwalimu,” alisema Dk. Kitine.


  Akizungumza kwa kujiamini kama ilivyo kawaida yake, Kitine alisema viongozi wengi wa serikali wamepoteza sifa kuu tatu za uongozi ambazo ni kuwa na uadilifu, wito na kuweka mbele utaifa, sifa ambazo alisema ndizo zilikuwa nguzo ya uongozi wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanza, chini ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

  “That was possible (hilo liliwezekana) chini ya Mwalimu. Kama alikuwa akifanya kosa, basi kosa hilo lilikuwa likitokea tu wakati akifanya jambo kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania.

  “Philosophy (falsafa) ya Mwalimu, ilikuwa kwanza Mungu, pili Tanzania, halafu yeye binafsi. Kila kiongozi anayetofautiana na Mwalimu tu hulifikisha taifa hili kubaya, if you differ with him, utaishia kubaya,” alisema Dk. Kitine akionyesha hali ya masikitiko.


  Alisema uteuzi mbaya wa viongozi, hususan ule wa mawaziri, umechangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa viongozi wasio waadilifu, wengi wao wakijihusisha na vitendo vya rushwa.

  “Haiwezekani viongozi wakateuliwa kwa misingi ya mitandao …sijui, kwa msingi wa politics of division (siasa za makundi) ndani ya chama. Haiwezekani nchi ikaendeshwa kienyeji. Integrity should be number one (uadilifu unapaswa kuwa kitu cha kwanza kuzingatiwa).

  “Mtu anajiuzulu, anafukuzwa uwaziri kwa sababu ya kashfa, kwa sababu ya kukosa maadili, halafu anabakia kuwa mbunge na mjumbe wa kamati kuu ya chama, nini hii? Hii haifai. Waziri akikosa uadilifu anatakiwa aondolewe mara moja nyadhifa nyingine zote alizobakiwa nazo. Nadhani hii itasaidia,” alisema Dk. Kitine pasipo kutaja jina la kiongozi yeyote.

  Kitine ambaye wakati wote wa mazungumzo yake alisema alikuwa anataka kujadili masuala muhimu na si watu, alieleza namna asivyo na imani na hatua zinazochukuliwa na serikali katika kukabiliana na tatizo la rushwa kubwa.

  Kwa mujibu wa kachero, mwanasiasa na mwanazuoni huyo, hatua hizo ambazo zinahusisha baadhi ya watu wenye majina makubwa kufikishwa mahakamani, zimechukuliwa kwa ajili tu ya maandalizi ya uchaguzi ujao.

  “Nilikuwa kiongozi wa kwanza kuzungumzia rushwa kubwa miaka 10 iliyopita. Nilisema ndiyo inayovuruga uchumi kuliko hata rushwa ya nesi, hakimu, polisi,.… hakuna hata mkubwa mmoja aliyekamatwa. Ilinigharimu sana, na mimi nilipata adhabu ya kuzuiliwa kikao kwa miezi miwili, kama huyu nani huyu, Zitto (Kabwe). Wakati huo ilikuwa ndani ya CCM.

  “Mimi nadhani hatua hizi zinazochukuliwa hazilengi kukomesha tatizo la rushwa, ni siasa tu za uchaguzi,” alisema Dk. Kitine.

  Alipoulizwa nini kifanyike ili kukabiliana na tatizo hilo la uongozi mbaya, pamoja na mambo mengine, alielekeza changamoto zake kwa Idara ya Usalama wa Taifa.

  “Usalama wa Taifa should be completely clean (unapaswa kuwa safi kabisa). Idara hii inatakiwa kuwa, juu ya mambo ya rushwa, iwe safi kabisa. Usalama wa Taifa ndiyo unayoteua viongozi, ndiyo inayoshirikiana na rais kwa kumshauri katika kuteua mawaziri. Sasa kama Usalama wa Taifa ukiwa mchafu ndio tunapata viongozi wala rushwa. Nafikiri vigezo vinavyotumika kuteua viongozi pia vina matatizo,” alisema Dk. Kitine.

  Kada huyo wa CCM ambaye kitaaluma ni mchumi na mwanasheria, akizungumzia hali ya uchumi nchini, alisema kwa kiasi kikubwa uchumi umeshikiliwa na wageni kuliko wazawa, na kuelezea kusikitishwa kwake juu ya kuwepo kwa pengo kubwa kati ya matajiri na maskini.

  Akitoa mfano alisema, miongoni mwa mambo yanayoonyesha kuparaganyika kwa mambo ni kukithiri kwa idadi ya ombaomba mitaani.

  “Mwalimu asingeruhusu watu hawa waombeombe barabarani. Kazi za Watanzania ni udereva teksi, daladala, mabasi, kazi ya uboi ndani ya nyumba na kazi ya kufagia barabarani. Hizi ndizo kazi za Watanzania na hawa ndio wenye mali.

  “Uchumi huu wa Watanzania si wa kwao. Watanzania ambao ni matajiri hawazidi hata watano. Hakuna sera bora za kusaidia kutumia maliasili zetu ili zitupe fedha ya kujenga shule, madaraja, hospitali…..” alisema Dk. Kitine.

  Akizungumzia utendaji wa kazi wa Bunge katika kusimamia utendaji wa serikali, Kitine alisema kazi inayofanywa na taasisi hiyo hivi sasa ni kubwa kuliko ilivyopata kuwa wakati wowote huko nyuma.

  Hata hivyo katika kuusifia utendaji wa kazi wa Bunge, aliupongeza mchango mkubwa na muhimu wa wabunge wa upinzani katika kuiimarisha taasisi hiyo muhimu.

  “Ni Bunge zuri kuliko lilivyowahi kuwa huko nyuma. Linaonyesha kila dalili za uhuru. Upinzani unafanya kazi nzuri. Bunge liko wazi zaidi na wabunge wanatoa michango mingi yakinifu, yenye manufaa kwa taifa. Likiendelea hivi tutafika mahali pazuri,” alisema.
   
  Last edited: Feb 19, 2009
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Feb 19, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Vipi kuhusu bosi wake Mkapa? What does he have to say about him?
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,556
  Likes Received: 18,263
  Trophy Points: 280
  Kitine ni very bold, jamaa ana msimamo usio tetereka na anajiamini ilaa hii isije ikawa ni strategy ya maandalizi ya 2010.
  Alichosema Kitine ni kweli ila hili la integrity Kitine anamsema Mkulu mwenyewe maana hana, sasa hao wenye integrity atawajuaje?. Watu wa UWT kama kweli wangefanya vetting on integrity, Mkulu angepitia wapi?. Kama ni integrity, mwenyeji wa Magogoni angekuwa 'Mpemba' aliyeenguliwa kwa zengwe.
  Hata hivyo, ule msemo wa 'Samaki mmoja akioza... Hauapply kwenye hili la integrity maana hili ni individual. Bado tuna viongozi wengi tuu wazuri, wenye integrity tatizo ni namna ya kuupata uongozi Tanzania unakuwa justified by the 'End' and not
  'The means', kitu ambacho waadilifu wa kikweli kweli, hawawezi. za kuupata uongozi,
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huyu wakati wake ndio rushwa imechipuka na kuota mizizi sasa anataka kuchonga, yeye mwenyewe inatakiwa achunguzwe, mali alizojilimbikizia zimetokana na mshahara na marupurupu yake tu? aueleze uma, mali zake kazitowa wapi?
   
 5. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #5
  Feb 19, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Natoa big 5 kwa dingi Kitine,Ujasiri alio nao tangu enzi hizo unafaa kupigiwa mfano wa kuigwa.Kama tukiwa na Kitine kumi upinzani hakika CCM na Jamaa zake woote wameondoka.Namfagilia sana huyu mzee kwa kuwapiga kikumbo vijana wake aliowaacha UWT.Hawa nao ni bora twende tu,Hawana msaada tena kwa Taifa zaidi ya kujitafutia trip na kujipatia un-accountable allowances.
  Kuna ukweli usiopingika kuwa nchi haina DIRA,Lakini nani aseme?Wakuu wengine amkeni mtoe utandu mnene mweusi machoni mwa wananchi,Ila waache kuchapa usingizi ifikapo 2010.
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Feb 19, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,598
  Trophy Points: 280
  ni mkweli kabisa achilia mbali matatizo yake yaliyowahi kumkumba..sio kigezo cha yeye kunyamaza...nchi kwelii inaendeshwa kisanii bora liende,visasi na kumkomoa fulani....kumlinda fulani.....na kulipana fadhila....wazee wote wanaona..hawana jinsi ila kusema ukweli lada dhamira zitawasuta watabadilika...hao watawala wetu...kwa kweli usanii juu ya usanii......sijui nani atakuja kutukomboa jamii yetu.....hasa hiiki kizazi cha usanii....na mtandao
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Feb 19, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Naaunga mkono maelezo yote ya kitine!
  Watanzania tuamke jamani!
   
 8. M

  Midas Touch Member

  #8
  Feb 19, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 74
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  Namkubali sana Mzee Kitine. He always practice what he preaches and walks his talks! Alitufundisha ECONOMICS pale Mlimani 1994 na mambo alikuwa anayaweka wazi sana hasa yale ambayo ni CRITICAL to the State, huwa ni Mzalendo kwelikweli.

  Ni kweli kuwa nchi inaendeshwa kienyeji tu, One-man-show! The "One-man" I mean few corrupt people in the "INNER-CIRCLE" that's why they never have been bold enough kukemea rushwa kwa uzalendo halisi. Rushwa inakemewa jukwaani tu. Hata mawaziri wa zamani waliopelekwa mahakamani ni "Screen-plays" tu, na WENGINE hawatapelekwa kamwe kwasababu ETI ni "Wanamtandao". Na kwamba ETI wamepata ajali za KISIASA ndio maana wamejiuzulu! Wewe uliona wapi "Job description" ya waziri inampa waziri kipengele cha kutumia BUSARA zake halafu akishatumia hizo BUSARA ZAKE ZA KIFISADI unamshtaki kwa kudai katumia MADARAKA vibaya! IGIZO linaendelea hivyo hivyo then, the EX-MINISTER acquited! Yaani HANA HATIA na hiyo ni 2012. Flashback to the "NALAILA KIULA Drama". BIG UP Kitine!
   
 9. Ndamwe

  Ndamwe Senior Member

  #9
  Feb 19, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ingekuwa kama wakati wa mwalimu wanaoitakia mema nchi yetu wangeandaa maandamano kuunga mkono matamshi ya huyu mzee. Hongera kitine
   
 10. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #10
  Feb 19, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Kazi nzuri Mzee Kitine,inahitaji ujasiri kuyasema haya hasa ikiwa ndani ya CCM.
  Chama kiyachukulie haya matamshi kama changamoto na si uongo kuwa umaarufu wa uanamapinduzi wa CCM unaanza kuingia dosari.
  Hata hivyo lazima tukubali kuwa si viongozi wote wenye mtizamo na akili kama za Nyerere.Mwalimu alikuwa akitenda yale anayoyaongea.
  JK anakazi kubwa ya kurudisha uadilifu katika chama na baadaye kuondoa wanachama wasio waadilifu.Hili ndio la msingi ,lakini kubwa zaidi ni kupanga maendeleo ya wananchi na kuonyesha dira ya ari,nguvu na kasi mpya vinaelea katika ubora upi wa maisha kwa mtanzania.
   
 11. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #11
  Feb 19, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Sasa kweli nimeamini upinzani wa kweli utatoka CCM...! THE BIG THE UP....!
  Kumbe idadi ya wazalendo wa kweli ni ndefu tu.....!
  KITINE added!
   
 12. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #12
  Feb 19, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hassy Kitine is one of very few people ambaye alikuwa karibu na Mwalimu; ni msomi mzuri na pia ni jasiri asiyeogopa kile anachoamini kukisema! Ni kweli kabisa kuwa viongozi wetu wengi hawana integrity kwasababu UWT siku hizi hawamshauri vizuri au muungwana mwenyewe hafuati ushauri wa UWT ama sivyo we could not end up with members of the CABINET wanaovuta bangi na matokeo yake ndio vioja tunavyoviona!! Haya sio majungu, tunao mawaziri wanaojulikana siku nyingi kuwa ni wavuta bangi na ndio maana hata majibu yao bungeni ni ya kisanii. Kama uwt wangekuwa wanafanya vetting ya viongozi , wale waliofukuzwa ikulu wakati wa enzi ya Mkapa kwa utou wa nidhamu wasingekuwa kwenye cabinet hata kwa kigezo cha UANAMTANDAO hiyo ndiyo inaitwa good governance. Lakini muungwana aliutaka UKULU akaupata sasa anatabasamu tu wakati cronies wake wanaikomba nchi.
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  Feb 19, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kila atakayeusema vibaya utawala huu ataonekana shujaa tu. Mambo hayakuanza kuharibika leo. Taabu ya viongozi wetu wengi wa zamani wanayaona mabovu wakishawekwa kando.
   
 14. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #14
  Feb 19, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,968
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Wildcat unabusara sana wewe ndio mfuatiliaji mzuri wa mambo ya siasa
   
 15. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #15
  Feb 19, 2009
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Heko Kitine! Tunawaomba wale wote waliowekwa kando waungane na Dr. Kitine katika kufichua huu utawala ulioenda kombo kwa kusingizia utawala bora. Mbona Enzi za Mwalimu hapakuwa na Wizara ya Utawala Bora?
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  Feb 19, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Kitine na Mkapa, Mwalimu's people tena damu damu, Mwalimu alipokuwa ana-retire akapelekwa Canada kula nchi, akilipiwa kila kitu na serikali yaani hela zetu walipa kodi anachokifanya hakieleweki, Mkapa kuwa rais tu akamuomba kurudi great friends akarudi, Mkapa akatumia ubabe na nguvu za ajabu within a month Kitine ni mbunge na waziri ofisi ya Mkapa, all this time hajaona ubovu wa uongozi wetu wala tatizo la integrity,

  - The next thing Kitine anaota urais, ghafla kaanza kuvaa kanzu na barakashia bungeni, nini kaambiwa rais anayefuata Mkapa lazima awe Muisilamu, mara oooh mawaziri ni wala rushwa, haya Kitine tuambie majina yao, akadai oooh no waandishi wamekosea sikusema vile, next mke wake amechukua maelfu ya dola za walipa kodi kwenda kutibiwa nje, kumbe ameenda kuzifanyia shopping bila kwenda Hospital wala kwa Daktari yoyote huko Canada na wala haumwi chochote, sasa all this time Kitine haoni ubovu wala tatizo la integrity na uongozI wetu,

  - The next thing Kitine amehonga honga na kujaribu kuzuia uchunguzi wa kamati ya bunge kuhusiana na wizi wa mkewe wa hela zetu walipa kodi alizotumia nje tena kwa uharibifu sana, wabunge kuja juu sana ndio Kitine baada ya kubanwa sana na wabunge kukubali kujiuzulu na kulazimishwa kulipa nusu ya zile pesa tena katika mazingara yaliyojaa uhuni uhuni, badala ya mkewe kwenda jela kwa wizi wa mchana wa hela zetu walipa kodi, all this time Kitine haoni matatizo ya uongozi wetu na integrity yake kua hovyo!

  Sasa leo he is supposed to be a hero kwa sababu amesema maneno ya kuponda serikali ya CCM, akitukana ubovu ule ule uliomponya yeye na mkewe, sometimes huwa ninajiuliza hivi vita tunavyopigana na mafisadi, kwa mfano tukiwatoa mafisadi wote leo, eti ni kweli tutaweza kuweka viongozi wapya ambao hawatakuwa mafisadi? Ningeelewa kwamba Kitine sasa ameamua kwamba wananchi wa Tanzania wameonewa vya kutosha na kuweka mfano anataka mkewe afunguliwe mashitaka kwanza ya kuiba hela zetu walipa kodi huko nyuma maana sasa anataka to come clean, no sasa yeye na Mbilinyi ni mashujaa against uozo wa uongozi wetu uliowaponya.

  Tuangalie sana ndugu zangu tusije kua kama wenzetu weusi huko US, kabla ya Obama kukosekana kwa real heros kuliwafanya kuanza kuamini hata yule Ferguson aliyeuwa wazungu kwenye LIIR Train bila sababu kuwa shujaa, badala ya a murdereeer!

  Mungu Aibariki Tanzania!
   
 17. N

  Ndivyo Ilivyo JF-Expert Member

  #17
  Feb 19, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kitine na Mbilinyi ni watu wanaofuata mtiririko wa viongozi wale wale kama tulionao wa CUF kule Zanzibar. Wamefanya maovu ya kutupwa walipokuwa madarakani (tumewapa nyadhifa) eti sasa wanajitia kuwa watetezi wakubwa na wanataka waitwe mashujaa. Pamoja na kuwa wanayodai kutetea ni mambo ya msingi nafikiri hawatufai. Tuyachukue mawazo yao lakini sio wao wenyewe. Hizo ni chapa zile zile za akina Seif Sharif Hamad na wenzake.
   
 18. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #18
  Feb 19, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Pamoja na kuwa tunatakiwa kuijudge hoja yake, lakini personality yake nayo tunaweza kuitumia kuipima hoja yake. Ni Kitine huyuhuyu ambay alilazimika kujiuzulu kwa kashfa. Ile ilikuwa ni manuva ya kisiasa. Nakumbuka mmoja wa watu waliotoa hoja za kumkandamiza Kitine Bungebni alikuwa Membe. Kwa nini nisiamini kwua bado Kitine and grudges na membe na lengo la maoni yake haya ni kutoaka kumchafua kama mmoja wa walioko serikalini?
  Kama walivyoasema waungwana walionitangulia, uchafu nchi hii haukuanza leo, kwa nini Kitine amenyamaza kimya muda wote na anaamua kusema leo, tena kwa kuita magazeti machache tu?
  Arudi nyuma na atueleze kiini na uchafu tunaoushuhudia sasa hivi aone kama na yeye hatokuwa mmoja wa waliotufikisha hapa tulipo leo
   
 19. F

  Felister JF-Expert Member

  #19
  Feb 19, 2009
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  I conqure with your urgument; thank you
   
 20. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #20
  Feb 19, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Mkulu wangu Mpitanjia, hold on right there, Membe hakumkandamiza Kitine no yeye alisema ukweli tena against his boss kumbuka wakati huo Kitine alikuwa his boss kule uwt, lakini kwa ushujaa Membe stood up na kuweka ukweli wazi kwamba mke wa Kitine hakuwa mgonjwa wala hakwenda kwa madakitari kule Canada, alikuwa anafanya shopping na hela zetu za kodi ya wananchi na akatoa ushahidi ndio kwa mara ya kwanza Kitine aka-back off na kulazimishwa kujiuzulu.

  - Kama sio Membe, Kitine tayari alishaweza kuizima hii ishu kienyeji enyeji, akisaidiwa na rais Mkapa, sasa kama ameamua kuwa mkweli basi aruhusu sheria ichukue mkondo kwenye wizi wa mkewe, au?
   
Loading...