Kitine: Nchi sasa yaongozwa kienyeji

Kitine: Nchi sasa yaongozwa kienyeji

Simple. Kuna uwezekano mkubwa watu wako kwenye desperation ya kupata mabadiliko. Na anapoona mabadiliko hayatokei yupo tayari ku-compromise principles zake.

Mabadiliko unayataka yaje tena kwa haraka. Lakini hakuna wasemaji. Wabunge wameshindwa kusema. Wananchi wanajirusha kwenye mdundiko. Na kilichobakia ni wewe kukubaliana na mtu yoyote mwenye guts.

Hii sawa na mwanamke aliyesubiri mchumba au mume mwenye sifa fulani kwa muda mrefu. Lakini kutokana na mwenye sifa anazotaka kuwa in short supply anahamua kukubali mtu yoyote yule kwa mategemeo kuwa anaweza kumbadilisha baadaye. Anasahau kuwa watu wazima ni vigumu kubadilisha tabia zao.

You can put lipstick on a pig, but it's still a pig.

Zakumi kwa kifupi ni kwamba Ktine ni fisadi na Watanzania wengi tutaendelea kumuweka katika kundi la mafisadi walioweka mbele maslahi yao badala ya yale ya Taifa na kutumia mianya iliyopo ili kukidhi haja yao ya kujipatia utajiri wa haraka haraka. Pamoja na hili la Kitine kuwa fisadi mimi kwa maoni yangu aliyoyasema Kitine yana ukweli mtupu na umuhimu mkubwa kutokana na hali halisi ilivyo nchini mwetu na hakuna sababu zozote za msingi za kuyapuuza aliyoyasema Kitine. Kutoyapuuza yaliyosemwa na Kitine hakubadilishi wala kuondoa ukweli kwamba Kitine ni Fisadi.
 
Zakumi kwa kifupi ni kwamba Ktine ni fisadi na Watanzania wengi tutaendelea kumuweka katika kundi la mafisadi walioweka mbele maslahi yao badala ya yale ya Taifa na kutumia mianya iliyopo ili kukidhi haja yao ya kujipatia utajiri wa haraka haraka.

- Finally sasa ninakuelewa mkuu, hapa tupo pamoja sana.
 
Kifupi ni hivi....

Kitine is just another disgruntled old guard. He is speaking louder on behalf of other disgruntled elites (Viongozi wa sekta za siasa, dola, biashara, jamii na zinginezo). Hili kundi linahusisha wale walioshindwa katika mchakato wa 2005 ndani ya CCM, wale ambao bado wanatamani kuona Tanzania ya Nyerere, wale wanaona kuwa wenzao wanakula bila ya kuwakumbuka lakini zaidi kuna wale ambao wanaona wenzao wanafakamia kwa kiasi kikubwa na ulimbukeni wa hali ya juu kiasi cha kutishia uhalali waTABAKA TAWALA ambalo wao pia ni wanachama hai na wanaamini kuendelea kuwepo kwa tabaka hilo ni muhimu kwa maslahi yao na vizazi vyao..

Kwa kifupi KITINE na wenziwe wanatenda MAZURI kwa nia ISIYO NJEMA..

Mwisho wa siku kunakuwa na nafasi kwa walalahoi na walalahai wa Tanzania kufaidika kama watajipanga vyema...

omarilyas
 
- Finally sasa ninakuelewa mkuu, hapa tupo pamoja sana.

FMES ungeweka basi paragraph yote badala ya kuweka nusu...🙂 maana hayo uliyoamua kuyaacha nayo yana uzito mkubwa. Just thinking aloud
 
Zakumi kwa kifupi ni kwamba Ktine ni fisadi na Watanzania wengi tutaendelea kumuweka katika kundi la mafisadi walioweka mbele maslahi yao badala ya yale ya Taifa na kutumia mianya iliyopo ili kukidhi haja yao ya kujipatia utajiri wa haraka haraka. Pamoja na hili la Kitine kuwa fisadi mimi kwa maoni yangu aliyoyasema Kitine yana ukweli mtupu na umuhimu mkubwa kutokana na hali halisi ilivyo nchini mwetu na hakuna sababu zozote za msingi za kuyapuuza aliyoyasema Kitine. Kutoyapuuza yaliyosemwa na Kitine hakubadilishi wala kuondoa ukweli kwamba Kitine ni Fisadi.

Kuna yule kijana aliyepiga makelele Mbwa Mwitu !!!!! Mbwa Mwitu !!!!!. Watu walipojitokeza, wakasema alikuwa anatania tu. Alirudia hivyo kama mara mbili.

Mara ya nne mbwa mwitu kweli alitokea na alipopiga kelele watu wakafikiri kuwa anatania.

Kwa maoni yangu ndugu Kitine anatania tu na sio serious. Kibaya zaidi ni kuwa waandishi wa habari wa Tanzania bado wana matatizo. Kwanini hawakuandika na kuhoji matukio yake ya nyuma 😕

Haya mambo ya kusema kuwa aliwahi kuwa waziri, mkuu wa makachero amesema nchi inakwenda kienyeji ni sawa na kwamba jamaa alistaafu kazi zake kwanini nzuri na sasa amehamua kurudi ulingoni kulitetea taifa.
 
Kwa maoni yangu ndugu Kitine anatania tu na sio serious.

Fisadi Kitine anatania tu , nchi haiendeshwi kienyeji. Je na sisi wengine tunaoamini hivyo tunatania tu na nchi haiendeshwi kienyeji ?. Je tunakubaliana na Chiligati na mafisadi wenzake kuwa tunao utawala wa sheria na haki ? Je tunaoona na kudai kuwa serikali hii ni ya kisanii, hatuko serious ? Namwona Chiligati kwa mbwembwe anang'aka, "unaona ? - hata vichwa wa JF wamekataa - hii ni nchi ya sheria na haki wala haiendeshwi kienyeji.

Kwa nderemo na vifijo mafisadi wanasherehekea kupata "support" ya JF. Je inawezekana kuwa huu ni mpango maalum uliosukwa ku"divert attention" kututoa kwenye mada hii inayohusu tamko la Fisadi Kitine - uongozi wa kienyeji - na kutuelekeza kwenye historia yake ? Kwa nini thread nyingine haianzishwi kumjadili Fisadi Kitine na kutuachia hii tujadili jinsi nchi inavyoongozwa sasa ?

😉Kwa kuwa Fisadi kalikana tamko lake - naomba kuliteka😉
 
  • Thanks
Reactions: BAK
go on KITINE.....! kuna wanaojaribu kukushawishi uachane na UZALENDO! songa mbele.....! kama ulivyoweka bayana katika TBC asubuhi hii, endelea na moyo huo huo wa MASLAHI YA TAIFA MBELE!!!!!!!
BRAVO KITINE!
 
Kina Kitine na watukwazao Tanzania!

Johnson Mbwambo Februari 25, 2009
Raia Mwema~Sauti ya Watu

HEBU fikiria: Inawezekanaje nchi iliyopendelewa na mwenyenzi Mungu (kama Tanzania) kwa kupewa ardhi nzuri yenye rutuba, mito kibao, maziwa kibao, bahari, madini mbalimbali, wanyamapori na maliasili nyingine chekwaa, ishikilie nafasi za mwanzo kwa umasikini duniani?

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2007 ilionyesha kuwa Tanzania ni nchi ya 14 kwa umasikini zaidi duniani (kuna umasikini na umasikini zaidi!). Nina hakika ripoti ya miaka ya karibuni itaonyesha picha mbaya zaidi ya hiyo.

Lakini hata kama wewe si muumini wa ripoti hizo za UN, utasema nini kuhusu ripoti nyingine ya hapa hapa nyumbani iliyoandaliwa na watawala wenyewe ambayo nayo kwa kiasi kikubwa inafanana na ripoti hiyo ya UN?

Nazungumzia ile ripoti iliyotokana na utafiti wa Ofisi ya Takwimu ambayo matokeo yake yalitangazwa na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo, mwaka jana, Oktoba 3. Kwa mujibu wa Mkullo, utafiti huo – Household Budget Survey ulionyesha kuwa Watanzania masikini wameongezeka hadi kufikia milioni 12, na kwamba kipato cha Watanzania walio wengi kwa siku ni wastani wa Sh. 460 tu!

Kama hali ni hiyo, jiulize tena: Yawezekanaje nchi iliyobarikiwa na mwenyenzi Mungu kwa kupewa maliasili hizo kibao, raia wake walio wengi wawe na kipato cha siku cha wastani wa Sh. 460 tu? Sh. 460 ambazo wala hazitoshi kukupa mlo mmoja tu uliokamilika kwa siku!

Ukitafakari kwa kina maswali hayo, majibu yako hayatakuwa tofauti na yale yaliyosemwa wiki iliyopita na mtu aliyeongoza Usalama wa Taifa kwa miaka 30, Hassy Kitine; yaani kinachotuponza sisi Watanzania ni uongozi mbovu.

Hata kama integrity ya Kitine ilipungua kutokana na kashfa ile ya matibabu ya mkewe, lakini kwa mtazamo wangu, hajakosea sana anaposema kuwa uongozi wa nchi ni mbovu. Na wala yeye si wa kwanza kusema hivyo. Wamekuwepo wazito wengi tu kabla yake waliojenga ujasiri wa kueleza kusikitishwa kwao na namna mambo yanavyokwenda nchini. Watu kama Jaji Warioba, Cleopa Msuya, Rashid Kawawa, Joseph Butiku, Chediel Mgonja (marehemu) n.k.

Hebu jiulize: Kama hatuponzwi na uongozi mbovu, inakuaje tushikilie nafasi za mwanzo katika orodha ya nchi masikini duniani; ilhali tuna utajiri mkubwa mno wa maliasili ambazo Mungu ametuzawadia?

Lakini ninapotafakari suala la mustakabali wa taifa letu, swali jingine linalosumbua kichwa changu ni hili: Inakuaje Tanzania - nchi yenye wazawa waliosoma na wenye bongo zinazochemka na wachapakazi hodari wanaosifiwa mno nje, ikubali miaka nenda rudi kuongozwa na viongozi wabovu wasiojali sana kuinua maisha ya wananchi wake?

Kwa wale waliobahatika kusafiri nje ya nchi, watakuwa wamewahi kuzisikia sifa nzuri za utendaji kazi za wataalamu wa kutoka Tanzania walio nje; hususan nchi za Kusini mwa Afrika.

Mwaka 2005 Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alipata kusema kwamba katika mkutano mmoja nje ya nchi aliwahi kuulizwa ni kwa nini Tanzania, ambayo ina maliasili nyingi mno, ipo nyuma mno kimaendeleo wakati mara nyingi ilikuwa ikiongoza katika kuchanganua mambo na katika uelewa wa fikra na mbinu za uchumi katika ulimwengu mzima hususan katika dunia ya tatu?

Bahati mbaya Mkapa hakueleza alijibu vipi swali hilo aliloulizwa ugenini; lakini ukweli ni kwamba hali iko hivyo kwa sababu hapa nyumbani, miaka nenda rudi, uongozi ni mbovu.

Tuna watawala na si viongozi, vinginevyo utaielezea vipi hali ya kung'ara na kuonyesha maajabu kwa Watanzania huko nje wakati hapa nyumbani ni kiza totoro?

Labda nitoe mifano michache. Kwa waliobahatika kutembelea mji wa Windhoek, Namibia watakuwa wanaifahamu Tanzania Club. Nilipata kuitembelea klabu hiyo ambako Watanzania hukutana jioni kujiburudisha na kubadilishana mawazo. Nikiwa hapo nilishituka kuona idadi kubwa ya Watanzania wanaofanya kazi za kitaalamu katika idara nyeti za serikali ya nchi hiyo.

Mmojawao – John Nyoka alinisisimua zaidi. Huyu alitokea makao makuu ya Idara ya Magereza Dar es Salaam akiwa ameazimwa na serikali ya Namibia kusaidia katika kuleta mageuzi kwenye idara kama hiyo ya Namibia. Kazi aliyoifanya John Nyoka ni kubwa mno na Wanamibia wanamheshimu mno kwa mageuzi aliyoyaleta katika Idara hiyo. Amekaa Namibia kwa zaidi ya miaka 13 na Serikali ya Namibia wala haipendi arejee Tanzania.

Lakini John Nyoka katokea wapi? John Nyoka katokea makao makuu ya Idara ya Magereza, Dar es Salaam ambako hakuna mageuzi yoyote makubwa yaliyofanywa na idara hiyo tangu mkoloni alipoondoka. Kama mkoloni alijenga gereza la kuchukua wafungwa 60, limebaki hivyo hivyo bila kupanuliwa na sasa wanakaa 600! Kama chumba kimoja katika rumande kilikuwa kikikaa watuhumiwa 10 wakati wa ukoloni, sasa kinakaa 100!

Jiulize:John Nyoka aliwezaje kuleta mageuzi makubwa katika Idara ya Magereza ya Namibia ambayo yeye na wenzake walishindwa kuyaleta hapa Tanzania tulipokuwa naye? Nina hakika jibu ni lile lile – uongozi mbovu wa hapa nyumbani.

Lakini nina mfano wa Mtanzania mwingine – Profesa Silas Lwakabamba. Huyu wakati akiwa Kitivo cha Uhandisi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alikatishwa tamaa na watawala wetu kiasi kwamba aliitikia wito wa Rais Kagame wa kwenda kumwanzishia chuo cha aina yake Afrika cha sayansi na teknolojia.

Na ndivyo alivyofanya. Profesa Lwakabamba aliondoka na wahadhari kadhaa na kwenda Kigali ambako Novemba 1997 walisimamia uanzishaji wa chuo kikuu kinachojulikana kama Kigali Institute of Science Technology (KIST), na yeye kuwa mkuu wa kwanza wa chuo hicho.

Chuo hicho sasa kimetimiza miaka minane na sifa zake zinafahamika kote Afrika. Kinatoa wahitimu walioiva kweli kweli katika nyanja zote za sayansi na ambao wakiwa chuoni hupimwa kwa kupelekwa kusimamia au kujenga miradi mbalimbali ya jumuiya vijijini kama vile madaraja (suspended bridges), shule, masoko na hata kuwafundisha wanavijiji namna ya kutengeneza madishi ya tv au kutengeneza nishati kutokana na vinyesi vya mifugo yao.

Kwa hakika, kama vijiji vya Rwanda vimepiga sana kasi kimaendeleo katika kipindi cha miaka minane iliyopita, mchango wa chuo kikuu hicho cha KIST ni mkubwa. Na ukitaja KIST huko Rwanda unamtaja Profesa Lwakabamba.

Hata kama Profesa Lwakabamba si Rector wa chuo hicho, lakini ukweli unabaki pale pale; kwamba ndiye aliyekianzisha na kukilea na kukipa mwelekeo; kiasi kwamba sasa kinafahamika kote Afrika na Ulaya kwa jinsi kinavyooanisha aina ya mafunzo kinachotoa na mahitaji ya jamii vijijini.

Nilikitembelea chuo hicho miaka minne iliyopita na nilishangaa kukuta kwamba idara zote kubwa zilikuwa zikiongozwa na Watanzania. Na hata sasa makamu mkuu wa chuo hicho kwa upande wa taaluma ni Mtanzania – Profesa John Mshana.

Niliporejea nyumbani nilishawishika kukitembelea kitivo cha uhandisi cha UDSM alikotokea Profesa Lwakabamba. Nilichojionea huko nikilinganisha na nilichokiona KIST, nashindwa hata nianzie wapi kusimulia. Wenyewe UDSM waliniambia kwamba sasa kitivo hicho si chochote si lolote; yaani ni a shadow of its past.

Hebu jiulize tena: Kama Profesa Lwakabamba aliweza kuanzisha chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha aina yake kule Kigali, kwa nini alipokuwa UDSM alishindwa kukigeuza kitivo cha uhandisi cha chuo hicho kuwa cha aina yake Afrika kama alivyofanya kule Rwanda? Jibu ni lile lile – uongozi mbovu usio na visheni kuanzia UDSM yenyewe hadi ngazi za juu serikalini.

Ninaweza kuiendeleza orodha hii ya Watanzania wenzetu walioonyesha maajabu nje ya nchi kwa uchapaji kazi wao mzuri, lakini nafasi haitoshi. Hata hivyo, niseme pia kwamba hata hapa nyumbani wako maofisa serikalini ambao hung'ara sana huko nje na kusifiwa mno wanapokwenda kuhudhuria mikutano na kutoa mada katika makongamano na mikutano ya kimataifa, lakini ukiuangalia utendaji kazi wao hapa nyumbani, unaweza kuzimia!

Angalau namjua mmoja katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) ambaye haishi kusafiri nje kwenda kutoa mada kuhusu mabadiliko ya tabianchi (climate change) au kuenea kwa hali ya ujangwa (desertification).

Asasi za nje zinampapatikia mno kumwalika Mtanzania huyu kutoa mada kutokana na uelewa wake mkubwa katika masuala hayo; lakini ukiangalia na kupima amefanya nini hapa nyumbani kuhusu climate change au desertification, utashangaa kuona kwamba hakuna alichofanya na kwamba yawezekana ana mwaka hajatembelea eneo lolote vijijini linalotishiwa kugeuka jangwa!

Hebu tena jiulize: Inakuaje ofisa huyu wa Serikali ya Tanzania anaonekana nje kuwa ni ‘mali' wakati hapa nyumbani hakuna chochote kikubwa na cha maana alichokifanya cha kupigia makofi? Jibu linaweza kuwa lile lile – uongozi mbovu (Kitine anauita uongozi wa kienyeji!). Yawezekana kabisa hapa nyumbani anakwazwa na uongozi mbovu unaomzunguka serikalini; sawa na walivyokwazwa wale Watanzania wengine waliokimbilia nje kufanya kazi.

Ni kweli huko nje kuna mishahara mizuri, lakini si mishahara mizuri pekee inaowafanya wang'are. Pamoja na mishahara mizuri, kuna nyenzo bora za kazi na nidhamu ya hali ya juu. Lakini vitu vyote vitatu – mishahara mizuri, nyenzo bora za kazi na nidhamu ya kazi, haviwezi kupatikana kama uongozi ni mbovu.

Ndugu zangu, nihitimishe tafakuri yangu kwa kusema kwamba mpaka hapo Watanzania tutakapozinduka usingizini na kuwang'oa madarakani viongozi wabovu kwa njia ya kura zetu, tutaendelea kuishi kwenye nyumba za udongo na majani; ilhali wenzetu mafisadi serikalini na kwenye asasi za umma wanaishi katika mahekalu ya Sh. milioni 800 au Sh. bilioni 3!

Watanzania masikini tutaendelea kula mlo mmoja dhaifu kwa siku wa Sh. 460; ilhali watawala huwapeleka wake na watoto zao kula dinner kwenye hoteli za kitalii nchini!

Kina Kitine na wengine kadhaa wanaosononeshwa na umasikini wa Watanzania vijijini, wamenena na kusema kwamba tatizo letu ni uongozi mbovu. Wakati tunasubiri wengine nao walonge; hebu natujiulize: Miaka nenda rudi tunashindwaje kutumia kura zetu kuwaondoa madarakani watawala wabovu na nafasi zao tukawachagua viongozi? Maana; hakika, tunahitaji viongozi na si watawala!

Tafakari.
 
BAK BAK

Naona unabadilisha mjadala. Anyway !!!!!!!!!!!!!!!!. Je hao wote waliotajwa wangepewa pesa na nafasi walizonazo kufanya hivyo walivyofanya nje ya nchi, wangeleta matokeo hayo 😕

Kwa mazoea yangu, hata watanzania waliochukua makaratasi ya ukimbizi au ya mazabe nje ya nchi wanafanya kazi nzuri sana.

Lakini wakirudi ndani wanarudi kwenye tabia zao. Hii ni Phenomena. Labda kujuana kumezidi.
 
Zakumi,
Nadhani ni mindset. Kuna wakati rafiki yangu mmoja alirudi Bongo baada ya kufanya kazi Marekani kwa muda mrefu. Alipangiwa kazi pale Foreign Affairs.
Sasa akipewa assignment kwa kuwa amezoea kufanya kazi chap chap alikuwa hailazi. Na hii ikatambuliwa na waziri wake akawa anamchukua visafari safari vya nje. Wenzake wakaanza kulalamika kuwa anajipendekeza na anataka kuwaletea Umarekani ( yaani kufanya kazi zako chap chap)
Sasa ukijikuta katika mazingara kama hayo unakuwa frustrated. Nina hakika hii mindset imetapakaa katika wizara nyingi hapo nyumbani. Ukipendekeza kitu kipya wanaona wewe unataka kuwaharibia modus operandi yao wanaanza kukupikia majungu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
The guy is talking sense. I do not have his details, but what he is talking about is relevant, current and serious!
When one party rules a country for 50 years without a break, members of that party begin to think that they have the right to do whatever they think fit and right for their party and themselves! It is human and natural!
Tanzania, like so many african countries is losing the battle against poverty, diseases, and lack of education amongst its masses, the so called "walalahoi"
There are no rules of engagement to tackle real development goals that should be a priority. The results are dire! Sufferings common! Corruption endemic! Life unbearable!

Anomalies include:
In a country where a president may start a "business" using state house as his base...
In a country where a president and his cabinet minister may decide to privatize and sell to themselves a public company at a price of their own choosing...
In a country where a prime minister may send personal "memos" to other ministers and principal secretary instructing them to award govt tenders to a company of his choice....
In a country where attorney general may choose single-handedly to change a govt contract, offer advice and expertise and in return get a kick-back that is deposited in a foreign country bank account...
In a country where the personnel and admistration manager of the central bank may swindle his own bank and country, accumulate wealth and endulge in a spending spree unseen before....

And many more........

All the above may happen once again, as Tanzanians are NOT ORGANIZED.

1. There need to be measures/guidelines/legal frameworks against each of the above anomalies and many more which I have not mentioned. These should be independent of ANY INDIVIDUALS. As life has shown, a president may also be corrupt! So it is nonsense to rely on an individual to be the saviour of all these calamities.
2. There need to be a culture of RULE OF LAW. It is the parliament that sets rules/measures/guidelines/legal frameworks/constitution etc. It is up to the legal system to judge and judge INDEPENDENTLY. It is up to the government to execute peoples will set through parliament or councils. I have always been baffled when I hear that police commissioner or even prime minister has ordered this and that! How come?!
 
Zakumi,
Nadhani ni mindset. Kuna wakati rafiki yangu mmoja alirudi Bongo baada ya kufanya kazi Marekani kwa muda mrefu. Alipangiwa kazi pale Foreign Affairs.
Sasa akipewa assignment kwa kuwa amezoea kufanya kazi chap chap alikuwa hailazi. Na hii ikatambuliwa na waziri wake akawa anamchukua visafari safari vya nje. Wenzake wakaanza kulalamika kuwa anajipendekeza na anataka kuwaletea Umarekani ( yaani kufanya kazi zako chap chap)
Sasa ukijikuta katika mazingara kama hayo unakuwa frustrated. Nina hakika hii mindset imetapakaa katika wizara nyingi hapo nyumbani. Ukipendekeza kitu kipya wanaona wewe unataka kuwaharibia modus operandi yao wanaanza kukupikia majungu.

Jasusi:

Hayo ndio mambo ya bongo. Kuna utamaduni ambao umeenea katika sehemu zote za maisha yetu na haitasaidia kupigia kelele serikali wakati wenyewe maisha yetu ndio yalivyo.

Nipo hapa mtoni na vijana wengi kwenye vijiwe stori zao ni kurudi bongo kuendeleza uenyeji.
 
Zakumi,
Nadhani ni mindset. Kuna wakati rafiki yangu mmoja alirudi Bongo baada ya kufanya kazi Marekani kwa muda mrefu. Alipangiwa kazi pale Foreign Affairs.
Sasa akipewa assignment kwa kuwa amezoea kufanya kazi chap chap alikuwa hailazi. Na hii ikatambuliwa na waziri wake akawa anamchukua visafari safari vya nje. Wenzake wakaanza kulalamika kuwa anajipendekeza na anataka kuwaletea Umarekani ( yaani kufanya kazi zako chap chap)
Sasa ukijikuta katika mazingara kama hayo unakuwa frustrated. Nina hakika hii mindset imetapakaa katika wizara nyingi hapo nyumbani. Ukipendekeza kitu kipya wanaona wewe unataka kuwaharibia modus operandi yao wanaanza kukupikia majungu.

Kaka nakubaliana nawe aslimia 1000
 
Wakuu,
Hapa kidogo nadhani nitakubaliana na FMES...
Point zake za awali kidogo nilikuwa nje isipokuwa nimefikiria kitu kimoja tu ambacho kinaleta maana zaidi ni kuhusiana na mtoa hoja mwenyewe!.
Hivi huyu Kitine kama angekuwa JELA na akazungumza maneno haya tungeendelea bado KUAMINI maneno yake kwa uzito tuliouchukua sasa hivi?..
Sasa nini tofauti ya huyu mtu kuwa jela na ifisadi alioufanya kwani kosa ni kutuibia hizo millioni 40, guys tunazungumzia 4 million US dollar hapa! na mtu yuko nje ati kastaafishwa..
Ushauri wangu kwake ni kuwa:-Nchi ilianza kuongozwa kienyeji toka siku aloweza kuiba fedha hizo (iwe hata mkewe) na hakuchukuliwa hatua yoyote zaidi ya kujiuzuru.. Hata mimi ningestaafu kwa robo ya fedha hizo, nisingesubiri kikawaka moto!..
Ukweli ni kwamba, kichwa cha mada hii kinapotosha zaidi kwani Nchi kuongozwa kienyeji haikuanza jana..
 
Ushauri wangu kwake ni kuwa:-Nchi ilianza kuongozwa kienyeji toka siku aloweza kuiba fedha hizo (iwe hata mkewe) na hakuchukuliwa hatua yoyote zaidi ya kujiuzuru..

Sawa kabisa Bob! Nchi imeanza kuongozwa kienyeji enyeji (sijui nini hasa maana yake) tokea hata yeye hajawa waziri lakini yeye anataka kukwepa kuwajibika. Binadamu tuko rahisi sana kuona kasoro za wengine na kuliko kujikosoa wenyewe.

Sasa sijui anataka kutuambia yeye na mkewe walipofuja zile hela anazotuhumiwa kufuja nchi ilikuwa inaongozwa kitaalam....mijitu mingine bana...ni bora ikae kimya tu
 
BAK BAK

Naona unabadilisha mjadala. Anyway !!!!!!!!!!!!!!!!. Je hao wote waliotajwa wangepewa pesa na nafasi walizonazo kufanya hivyo walivyofanya nje ya nchi, wangeleta matokeo hayo 😕

Kwa mazoea yangu, hata watanzania waliochukua makaratasi ya ukimbizi au ya mazabe nje ya nchi wanafanya kazi nzuri sana.

Lakini wakirudi ndani wanarudi kwenye tabia zao. Hii ni Phenomena. Labda kujuana kumezidi.

Nadhani Jasusi amekujibu vizuri. Kwa kuongezea tu haiwezekani Mtanzania aliyeishi nje kwa muda mrefu ambaye ameshakuwa ni mchapa kazi hodari akirudi aanza tena kuzembea eti kwa kuwa yuko Bongo. Tatizo ni kama hilo alilokwambia Jasusi na wakati mwingine Bongo unatakiwa kuwa na kigod father ambacho kitajidai kinakkupigia debe kwa 'wakubwa' ili upate promotion.

Uzuri wa nje juhudi za kazi zako zinaonekana na wakubwa wala huhitaji kuwa na kigod father mambo yanajipa yenyewe na unaona unapanda tu kutokana na vyei vyako na utendaji mzuri wa kazi zako. Bongo hili hakuna bila kuwa na God Father utachapa kazi mtindo mmoja lakini juhudi zako kamwe hazitakuletea mafanikio ya kupanda cheo.
 
Wakuu,
Hapa kidogo nadhani nitakubaliana na FMES...
Point zake za awali kidogo nilikuwa nje isipokuwa nimefikiria kitu kimoja tu ambacho kinaleta maana zaidi ni kuhusiana na mtoa hoja mwenyewe!.
Hivi huyu Kitine kama angekuwa JELA na akazungumza maneno haya tungeendelea bado KUAMINI maneno yake kwa uzito tuliouchukua sasa hivi?..
Sasa nini tofauti ya huyu mtu kuwa jela na ifisadi alioufanya kwani kosa ni kutuibia hizo millioni 40, guys tunazungumzia 4 million US dollar hapa! na mtu yuko nje ati kastaafishwa..
Ushauri wangu kwake ni kuwa:-Nchi ilianza kuongozwa kienyeji toka siku aloweza kuiba fedha hizo (iwe hata mkewe) na hakuchukuliwa hatua yoyote zaidi ya kujiuzuru.. Hata mimi ningestaafu kwa robo ya fedha hizo, nisingesubiri kikawaka moto!..
Ukweli ni kwamba, kichwa cha mada hii kinapotosha zaidi kwani Nchi kuongozwa kienyeji haikuanza jana..

Mkandara sina haja ya kudownplay ufisadi uliofanywa na Kitine lakini the correct amount siyo $4 millioni ni $40,000, $4 million ni sawa na shilingi milioni 400.

Inawezekana kabisa kwamba nchi kuendeshwa Kienyeji haikuanza jana, lakini haya tunayoyaona sasa ya mafisadi wa mabilioni kukingiwa kifua na kuachiwa kuendelea kupeta ndani ya serikali na chama hayakuwa makubwa kiasi hiki na kashfa hazikuwa nyingi kama ilivyokuwa sasa. Haya yakusema maslahi ya chama ni muhimu kuliko maslahi ya Taifa na hakuna hata kiongozi mmoja wa juu kupinga kauli hiyo yasingetokea enzi za nyerere maana aliyetoa kauli hiyo Nyerere angemsemea hovyo na ndiyo maana hata yeye mwenyewe aliwahi kutamka kwamba CCM siyo Mama au Baba kwa maana nyingine haikuwa na umuhimu mkubwa kiasi hicho katika maisha ya Mwalimu.
 
Wakuu,

Sasa nini tofauti ya huyu mtu kuwa jela na ifisadi alioufanya kwani kosa ni kutuibia hizo millioni 40, guys tunazungumzia 4 million US dollar hapa! na mtu yuko nje ati kastaafishwa..

Kaka siamini kama uko "out of touch" kiasi hiki?

Ni 64,000 USD kama sikosei. Sio USD 4 million. Mzee aliingizwa mkenge na mama watoto aliyekuwa akishirikiana na wajanja wa kinigeria huko CANADA. Mtandao walijua hilo na wakang'amua kuwa Mzee hawezi kuthubutu kusimama kusema kuwa Mama watoto amemsaliti.....

omarilyas
 
Sawa kabisa Bob! Nchi imeanza kuongozwa kienyeji enyeji (sijui nini hasa maana yake) tokea hata yeye hajawa waziri lakini yeye anataka kukwepa kuwajibika. Binadamu tuko rahisi sana kuona kasoro za wengine na kuliko kujikosoa wenyewe.

Sasa sijui anataka kutuambia yeye na mkewe walipofuja zile hela anazotuhumiwa kufuja nchi ilikuwa inaongozwa kitaalam....mijitu mingine bana...ni bora ikae kimya tu

Nchi imeanza kuendeshwa kienyeji tangi TANU kuangamizwa na lidudu linaloitwa CCM kuanzishwa......hata Mwalimu alizidiwa nguvu na wajanjawajanja na ndio kisa cha UBABE wa Hayati Sokoine kujaribu kuokoa jahazi. Bahati mbaya alikuwa hajafanikiwa kupiga kichwa na manyang'au wakaibuka kama MBOGO aliyejeruhiwa baada ya yeye kutangulia kwa Mwenyezimungu na baadae wakapata Mzee Ruksa mambo yakawaendea vizuri zaidi....

Sasa kuhusu Kitine kwa kweli sina hakika alikuwa upande gani wa mchakato huu wa kubomoa Tanzania tangia enzi hizo....

Kuna mtu anaweza kuchimba na kutuhabarisha kisa cha Mwalimu kumpeleka mapumzikoni Canada akitoka Idara ya Usalama wa Taifa? Je alikuwa ni mwezeshaji ama kikwazo cha dira mpya ya manyang'au ya kubomoa Tanzania Asili....

omarilyas
 
Kusema nchi imeendeshwa kienyeji tokea enzi za Nyerere ni sawa na kufananisha KICHEFUCHEFU na KIPINDUPINDU. Tanzania ni mahututi hivi sasa.
  1. Ni lini nchi yetu ilikuwa na mawaziri n.k, mamilionea (in $$$ terms) na wanaozitawanya waziwazi bila rais kuwachunguza au kuwachukuliwa hatua?
  2. Ni lini tulikuwa na wabunge, wakurugenzi wa mashirika n.k. waliotuhumiwa wazi kuibia taifa mamilioni bila kuchukuliwa hatua?
  3. Ni lini nchi iliwahi kukumbatia matapeli kama RICHMOND & DOWANS waziwazi licha ya uhalifu walioifanyia nchi?
  4. Ni lini nchi yetu imekuwa na raisi aliye OMBA-OMBA kila kukicha badala ya kupanga mipango binafsi ya maendeleo?
Ukweli ni kuwa haijawahi tokea nchi kuendeshwa kirushwa-rushwa na kizembe bila mwelekeo kwa kiasi hiki, hata mzee Rukhsa alikuwa na nafuu. Tuombe akina Kitine's waongezeke na sasa waanze kumtaka raisi Kikwete ajiuzulu.
 
Back
Top Bottom