Kitine: Nchi sasa yaongozwa kienyeji

Kitine: Nchi sasa yaongozwa kienyeji

Tunakubaliana kwamba Kitine ni mnafiki, hana credibility kukanya wenzake.

Ila kipande hicho hapo cha kukejeli Waamerika Weusi kwamba walimfanya Ferguson kuwa hero si kweli.

Ferguson alionekana mwehu baada ya, pamoja na mengine mengi bizarre, kudai kwamba anataka Bill Clinton aje mahakamani kuwa shahidi wa mauaji ya kwenye train ya Long Island. Uchambuzi wako wa kutukana weusi hapo umepotoka. Wasingekuwa ma hero wa Wamarekani Weusi wewe na mimi tusingekuwa na uhuru wa kwenda kuzunguka zunguka huru Marekani na kunywa kwenye water fountain za kila mtu na kubeba maboxi. Tusiwatukane.

Tubaki kwa haya kwetu: Huyu ex-embezzler Kitine hana moral authority kukemea ufisadi.

- Nimechagua kutojibu, bwa! ha! ha!? ah! ha! maana mjadala huu ni safi hahutaji kuchafuliwa, wrong number bwa! ha! ah!.
 
Kwa maana nyingine wote waliruhusiwa tena kutoa maoni yao kuhusu mwenendo wa nchi bila kujali usaliti wao walioufanya dhidi ya Serikali halali ya Mwalimu ambayo ilichaguliwa na Wananchi.

Ni wapi Kambona na Bibi Titi walitoa maoni kukemea uhaini?

Hatuongelei mhaini kukemea fisadi hapa, elewa tafadhali.

Tunaongelea fisadi kunyooshea kidole fisadi.

Mfano wako potofu, historia potofu!

Kitine wako mnafiki.
 
Kambona na Bi Titi Mohamed na wengineo walishiriki katika kutaka kuipindua serikali halali ya Mwalimu iliyokuwa madarakani. Baadhi walikimbia nchi na wengine walifunguliwa mashtaka na kuonekana na hatia ya usaliti na kufungwa akiwemi Bibi Titi Mohamed.

Mwalimu aliwasamehe wote na Kambona pamoja na usaliti wake dhidi ya serikali aliporudi nchini toka Uingereza alijiingiza tena kwenye mambo ya siasa na Bibi Titi alirudi CCM. Kwa maana nyingine wote waliruhusiwa tena kutoa maoni yao kuhusu mwenendo wa nchi bila kujali usaliti wao walioufanya dhidi ya Serikali halali ya Mwalimu ambayo ilichaguliwa na Wananchi.

Kitine pia pamoja na ufisadi wake ana haki kama Mtanzania mwingine yeyote yule kutoa maoni yake kuhusu mwenendo wa nchi yetu. Tunachotakiwa kufanya Watanzania si kujadili ufisadi uliofanywa na Kitine bali yale aliyoyazungumza kuhusu uongozi katika nchi yetu je yana ukweli wowote au ni upupu tu? je, yanastahili kuyajadili na kuyatafakari kwa manufaa ya nchi yetu? Mimi na wengine wengi tunaona Kitine ana haki ya kutoa maoni kuhusu mwenendo wa uongozi ndani ya nchi yetu. Hata Chiligati na Msekwa wametamka wazi kwamba Kitine kama Mtanazania yeyote yule ana haki kabisa ya kutoa maoni dhidi ya serikali iliyokuwa maoni yake. Hawakujaribu hata kidogo kutaka kuonyesha kwamba kwa kuwa ni fisadi basi hastahili kusema lolote lile kuhusu mwenendo wa uongozi ndani ya nchi yetu.

Hakuna nchi yoyote duniani inayozuia raia wake hata wale ambao ni wasaliti ama mafisadi kutoa maoni yao kuhusu serikali zao na Tanzania haitakuwa ya kwanza kufanya hivyo kesho, wiki ijayo wala miaka 20 ijayo. Alichokisema Kitine kina ukweli kama Watanzania tunakikimbia na kutotaka kujadili yale yaliyosemwa na Kitine basi iko siku tutakuja kuyakumbuka maana mficha ugonjwa kifo humuumbua.

- Kitine hakusema anything new ambacho mimi na wewe hatujawahi kukisema hapa forums, huo ndio ukweli wenyewe,

- Baba mlevi hawezi wakemea watoto wake wasiwe walevi.
 
Hata Chiligati na Msekwa wametamka wazi kwamba Kitine kama Mtanazania yeyote yule ana haki kabisa ya kutoa maoni dhidi ya serikali iliyokuwa maoni yake. Hawakujaribu hata kidogo kutaka kuonyesha kwamba kwa kuwa ni fisadi basi hastahili kusema lolote lile kuhusu mwenendo wa uongozi ndani ya nchi yetu.

- Hata Msekwa na Chiligati, hawakujaribu kum-challenge Kitine kwa sababu ya kulijali taifa letu, Mkulu wangu BAK vipi leo?
 
- Kitine hakusema anything new ambacho mimi na wewe hatujawahi kukisema hapa forums, huo ndio ukweli wenyewe,

- Baba mlevi hawezi wakemea watoto wake wasiwe walevi.

Hata kama mimi na wewe tumekwishasema lakini hiyo haimkatazi Kitine wala kumnyima haki yake ya kuzungumzia kitu ambacho kimeshazungumzwa. Hakuna mahali popote palipoandikwa kwamba Mtanzania mwingine hana haki ya kuzungumza chochote kile ambacho Watanzania wenzake wameshakizungumza hata kama ni fisadi au msaliti.

Baba Mlevi anaweza kabisa kuwaambia wanae, kwamba mnaona mimi nilivyoharibikiwa kimaisha kutokana na kuendekeza kilevi, nawaomba msigise kilevi cha aina yoyote ile kwa faida yenu na vizazi vyenu vijavyo na watoto wakaamua kumsikiliza Baba yao.
 
- Wananchi mimi niliwahi kuwa waziri nikaiba sana na sasa niko na maisha mazuri kuliko yenu, lakini tafadhali msirudie kuiba kama mimi kwa sababu mtakuwa mnaongoza taifa kienyeji.

Author - Kitine
 
- Wale wale nothing new, wala msaada kwa taifa Bwa! ha! ha! ha! ah! ah!

Issue ya Colin Ferguson uliyoileta ni crap!

Colin-Ferguson-mugshot.jpg

Ni wapi Kambona na Bibi Titi walitoa maoni kukemea uhaini?

Hatuongelei mhaini kukemea fisadi hapa, elewa tafadhali.

Tunaongelea fisadi kunyooshea kidole fisadi.

Mfano wako potofu, historia potofu!

Kitine wako mnafiki.

Wewe ndiyo unaona potofu. Msaliti na fisadi wote ni wavunja nchi. Kama Mwalimu aliwaruhusu wasaliti akina Bibi Titi, Kambona na wengineo waliotaka kuipindua serikali yake na si ajabu kumuua na kuwaruhusu tena kujishughulisha na mambo ya siasa, basi hivyo hivyo bila kujali ufisadi wa Kitine tunaweza kabisa kuyachambua yaliyosemwa na Kitine kama yana ukweli na yanastahili kujadiliwa na Watanzania wengine kwa manufaa ya nchi yetu.

Hakuna nchi yeyote duniani ambapo Raia ananyimwa haki ya kutoa maoni yake eti kwa sababu ya yale mabaya aliyoyafanya miaka ya nyuma.
 
Bahati mbaya wakati Kitine akizungumza na magazeti sisi wana JF hatukuwepo. Lakini kwenye TBC tumemuona live. Sasa tufuate lipi? Unajua tena magazeti yetu yanavyojua kuongeza chumvi. Namshauri Kitine, next time akizingumza na magazeti asome a written statement na asijibu maswali ya ziada ama sivyo anaweza kujikuta kawekwa mahala pabaya na UWT.

- Tupo pamoja hapa mkuu, Kitine Kitine na Kitine panapofuka moshi lazima chini kuwepo moto, sasa ngoja tusubiri alichokuwa anakilenga tutakijua tu soon!
 
- Hata Msekwa na Chiligati, hawakujaribu kum-challenge Kitine kwa sababu ya kulijali taifa letu, Mkulu wangu BAK vipi leo?

Msekwa na Chiligati wangekuwa wanalijali Taifa basi wasingefumbia macho uozo na ufisadi uliojaa ndani ya chama na serikali. Hawa wanajali maslahi yao binafsi na ya chama chao cha kifisadi, vinginevyo kama wangekuwa na uchungu wa kweli wa nchi yetu basi wangeshayakemea mengi ambayo yanaendelea lakini kwao wao kila kitu ni shwari kabisa hakuna tatizo lolote!!! Kitu ambacho si cha kweli.
 
Issue ya Colin Ferguson uliyoileta ni crap!

Colin-Ferguson-mugshot.jpg

- Unajua Invisible aliwahi kutuambia kwamba wewe ni mama mtumzima mwenye heshima sana na kwamba ukidharauliwa inakuwa sio vizuri maana itaonekana tunawatenga kina mama,

- Ukamsumbua Mkandara weee na simu kwamba aongee na mimi, wewe sio hivi wala vile, sasa here you go, karibu sana mkuu haya bring it on now I am ready kwa majibu!

Wazee wa sauti ya umeme - FMES!
 
Kambona na Bi Titi Mohamed na wengineo walishiriki katika kutaka kuipindua serikali halali ya Mwalimu iliyokuwa madarakani. Baadhi walikimbia nchi na wengine walifunguliwa mashtaka na kuonekana na hatia ya usaliti na kufungwa akiwemi Bibi Titi Mohamed.

Mwalimu aliwasamehe wote na Kambona pamoja na usaliti wake dhidi ya serikali aliporudi nchini toka Uingereza alijiingiza tena kwenye mambo ya siasa na Bibi Titi alirudi CCM. Kwa maana nyingine wote waliruhusiwa tena kutoa maoni yao kuhusu mwenendo wa nchi bila kujali usaliti wao walioufanya dhidi ya Serikali halali ya Mwalimu ambayo ilichaguliwa na Wananchi.

Kambona na Bibi Titi hawakuwa relevant tena baada ya masoo yao.

Bubu Ataka Kusema said:
Kitine pia pamoja na ufisadi wake ana haki kama Mtanzania mwingine yeyote yule kutoa maoni yake kuhusu mwenendo wa nchi yetu.[/quote]
Bubu Ataka Kusema said:
Na ndivyo alivyofanya na hakuna aliyemkataza na sisi tunatumia haki yetu ku-opine dhidi ya kile alichosema. Kuna tatizo gani hapo Bubu?

Bubu Ataka Kusema said:
Tunachotakiwa kufanya Watanzania si kujadili ufisadi uliofanywa na Kitine bali yale aliyoyazungumza kuhusu uongozi katika nchi yetu je yana ukweli wowote au ni upupu tu? je, yanastahili kuyajadili na kuyatafakari kwa manufaa ya nchi yetu?[/quote]
Bubu Ataka Kusema said:
Kwa nini tusijadili ufisadi uliofanywa na Kitine? Kwa nini? Yote yanajadilika hapa. Hakuna kilicho off limits...at least as far as I'm concerned...

Bubu Ataka Kusema said:
Mimi na wengine wengi tunaona Kitine ana haki ya kutoa maoni kuhusu mwenendo wa uongozi ndani ya nchi yetu. Hata Chiligati na Msekwa wametamka wazi kwamba Kitine kama Mtanazania yeyote yule ana haki kabisa ya kutoa maoni dhidi ya serikali iliyokuwa maoni yake. Hawakujaribu hata kidogo kutaka kuonyesha kwamba kwa kuwa ni fisadi basi hastahili kusema lolote lile kuhusu mwenendo wa uongozi ndani ya nchi yetu.

Hakuna hapa aliyesema Kitine hana haki ya kutoa maoni yake. We are just calling him out on his hypocrisy. That's all. Do you have a problem with that Bubu?

Bubu Ataka Kusema said:
Hakuna nchi yoyote duniani inayozuia raia wake hata wale ambao ni wasaliti ama mafisadi kutoa maoni yao kuhusu serikali zao na Tanzania haitakuwa ya kwanza kufanya hivyo kesho, wiki ijayo wala miaka 20 ijayo. Alichokisema Kitine kina ukweli kama Watanzania tunakikimbia na kutotaka kujadili yale yaliyosemwa na Kitine basi iko siku tutakuja kuyakumbuka maana mficha ugonjwa kifo humuumbua.

Again, sijui kwa nini hutaki ufisadi wa Kitine ujadiliwe wakati yeye mwenyewe ndio kafungua mdomo wake kukemea ufisadi wakati na yeye ni fisadi mstaafu.
 
Kitine: Nchi sasa yaongozwa kienyeji

na Edward Kinabo
Tanzania Daima~Sauti ya watu​

MKURUGENZI Mkuu mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Dk. Hassy Kitine, amesema taifa linakabiliwa na tatizo kubwa la uongozi, ambalo halijawahi kutokea katika historia ya nchi.

Kitine ambaye aliiongoza idara hiyo nyeti kwa karibu miaka 30 zama za Serikali ya Awamu ya Kwanza na ya Pili, alisema ukosefu huo wa uongozi umesababisha nchi iongozwe kienyeji.

Kachero huyo namba moja kwa miaka mingi, ambaye alilazimika kujiuzulu wadhifa wa uwaziri wa nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) wakati wa utawala wa Benjamin Mkapa, mwishoni mwa miaka ya 1990 kutokana na kuhusishwa na kashfa ya mkewe kufuja fedha za umma kiasi cha shilingi milioni 40, alirejea kutoa kilio chake cha miaka mingi cha kuporomoka kwa maadili ya uongozi nchini.
.

- Hebu tizama the backwardness ya hii habari, inaanza vizuri halafu inaharikibika yenyewe!
 
- Unajua Invisible aliwahi kutuambia kwamba wewe ni mama mtumzima mwenye heshima sana na kwamba ukidharauliwa inakuwa sio vizuri maana itaonekana tunawatenga kina mama,

- Ukamsumbua Mkandara weee na simu kwamba aongee na mimi, wewe sio hivi wala vile, sasa here you go, karibu sana mkuu haya bring it on now I am ready kwa majibu!

Wazee wa sauti ya umeme - FMES!

Haya umeshaanza kwenda personal badala ya kukata issue. Haya ndio unayoyaita maslahi yako kwa Taifa?

Sasa kwa vile ni mama wa heshima akiona uongo asiseme! Issue ya Ferguson uliyoileta ni crap. Endelea kukata issue zingine.
 
Again, sijui kwa nini hutaki ufisadi wa Kitine ujadiliwe wakati yeye mwenyewe ndio kafungua mdomo wake kukemea ufisadi wakati na yeye ni fisadi mstaafu.

Ha ha ha Nyani hebu lete ushahidi wa popote pale nilipoandika kwamba sitaki ufisadi wa Kitine ujadiliwe hapa ukumbini. Nilichosema ni kwamba Watanzania tunatakiwa kuyapima yaliyosemwa na Kitine kama yana ukweli kuhusiana na uongozi wa nchi yetu, na kama kuna umuhimu wa kuyajadili bila ya kujali kama Kitine mwenyewe ni fisadi. Mjadala wa Kitine kama fisadi na mjadala wa aliyoyasema kuhusiana na nchi kuendeshwa kienyeji ni vitu viwili tofauti.

Hata siku moja sijawahi kuzuia au kupinga mjadala wowote hapa ukumbini ukiondoa ile ya kashfa, kejeli na matusi dhidi ya dini zetu kubwa mbili. Kama wanachama wanataka kujadili ufisadi uliofanywa na Kitine basi rukhsaaaaaa kufanya hivyo, lakini mimi na wengine tunasema aliyoyasema Kitine kuhusu nchi kuongozwa kienyeji yana ukweli, na yanastahili kabisa kujadiliwa kwa mapana na marefu ili labda viongozi waliopo madarakani wabadilishe mienendo yao ya kukingia vifua mafisadi ambao ni rafiki zao, kusaini mikataba ya rasilimali zetu ambayo haina maslahi kwa Watanzania na kuweka mbele maslahi ya Watanzania badala ya kuweka mbele maslahi yao binafsi na ya chama chao cha kifisadi. Hayo ndiyo niliyoyasema.
 
FMES....please wala usijibu vitu ambavyo havihusiani na Kitine....just let it go...
 
Kitine pia pamoja na ufisadi wake ana haki kama Mtanzania mwingine yeyote yule kutoa maoni yake kuhusu mwenendo wa nchi yetu. Tunachotakiwa kufanya Watanzania si kujadili ufisadi uliofanywa na Kitine bali yale aliyoyazungumza kuhusu uongozi katika nchi yetu je yana ukweli wowote au ni upupu tu? je, yanastahili kuyajadili na kuyatafakari kwa manufaa ya nchi yetu?

Bubu, hebu nipe tafsiri/maana ya hayo yaliyoko kwenye bolded text....
 
Back
Top Bottom