BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,009
- Thread starter
- #81
Yaani Kitine aliyeiba US$64,000 mwaka 1997 akishirikiana na Mkapa leo ana nguvu za kusema nchi inaongozwa kienyeji? Huyu ndie alitakiwa apelekwe kisutu faster faster kwa kuiba na kutumia madaraka vibaya....tunapoteza muda kuwajadiri akina Masha wakati ushahidi wa wizi wa Kitine ni more convincing.
Kwanza Kitine atueleze jitihada alizofanya kuzirudisha US$64,000 alizoiba ndipo atupe msimamo wake juu ya mapungufu ya serikali ya sasa. Vinginevyo anakuwa kama padre anayehubiri kuacha usherati baada ya kushinda tuzo kadhaa za usherati.
Kama ndiyo hivyo basi hakuna kiongozi yeyote mstaafu ambaye ana sifa ya kuongea kuhusu uongozi mbovu ndani ya nchi yetu maana wote ambao wako hai wana tatizo moja au jingine. Mzee Rukhsa tunajua ufisadi wa Mama Siti na yeye mwenyewe kugawa viwanja kwa ndugu, jamaa na marafiki. Cleopa Msuya aliwahi kutwambia kwamba kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe, Malecela tunajua matatizo yake mbali mbali hata Mwalimu alishamuona hastahili kuwa Rais wa nchi yetu. Salim Ahmed ataambiwa ni Mwarabu alikaa nje ya nchi miaka mingi hajui lolote kuhusu Tanzania hivyo hana wajibu wa kutia neno lolote kuhusu uongozi mbovu ndani ya nchi yetu. Sumaye naye ni fisadi alitumia nafasi yake kama PM kujikusanyia utajiri wa hali ya juu ambao hakuwa nao kabla ya kuwa Waziri Mkuu, Kawawa naye ni mwasherati alikuwa na wake zaidi ya mmoja.
Wote wakae kimya tu na kuiacha Tanzania ikiendelea kuangamia kutokana na kuongozwa na watu wasiokuwa na hata chembe ya maadili ya uongozi, wasio na ujasiri na waliojaa woga wa hali ya juu na siku zote wataweka mbele maslahi yao, ya marafiki zao ambao ni mafisadi na chama chao cha kifisadi badala ya yale ya nchi.
Mungu inusuru Tanzania maana badala ya kupima uzito wa maneno yaliyosemwa sasa tunaangalia nani kayasema na kama aliyesema si mtu safi basi hayana sifa ya kujadiliwa na kuyatafakari maana ni upupu tu!!!!
Si ajabu viongozi wengi wastaafu wameamua kukaa kimya huku nchi ikiendelea kuangamia maana wakiamua kukemea hali ya uongozi ndani ya nchi yetu basi mafisadi, watetezi wao na hata baadhi ya Watanzania wataamua kuwachafua tena na kuwaambia kaa kimya wewe hustahili kusema lolote wewe na matokeo yake nchi inaendelea kuangamia na matokeo yake mafisadi wanaendelea kupata nguvu na kushamiri kila kukicha!!!!
Oh! Tanzania unaelekea wapi nchi yangu!!!!!
Last edited: