- Masikini ya Mungu, unahitaji msaada ambao mimi sina.
Wewe ndio unahitaji msaada wa kuondoa hiyo arrogance yako. Sina la kukusaidia.
- Masikini ya Mungu, unahitaji msaada ambao mimi sina.
Nilichosema ni kwamba Watanzania tunatakiwa kuyapima yaliyosemwa na Kitine kama yana ukweli kuhusiana na uongozi wa nchi yetu, na kama kuna umuhimu wa kuyajadili bila ya kujali kama Kitine mwenyewe ni fisadi. Mjadala wa Kitine kama fisadi na mjadala wa aliyoyasema kuhusiana na nchi kuendeshwa kienyeji ni vitu viwili tofauti.
- Mkulu BAK ni kweli kabisa tunahitjai kujadili maneno ya Kitine, lakini ni lazima tuanze na yeye kama kweli tuko serious, Taiwan wana matatizo kama yetu, guess what wameanza na rais wao wa zamani kwanza.
Rukhsaaaaa kabisa kujadili ufisadi alioufanya Kitine kwa mapana na marefu, lakini wakati huo huo aliyoyasema kuhusu nchi kuendeshwa kienyeji yana ukweli na kwa maoni yangu na wengine hapa ukumbini hakuna sababu yoyote ya kuyapuuza maneno yake inabidi nayo tuyatafakari maana ni tatizo kubwa nchini kwetu na kama hili la kuendesha nchi kienyeji likiachwa kuendelea kuota mizizi basi Watanzania tutakuja kujuta na kulia kilio cha kusaga na meno maana inaweza kabisa ikawa ni too late kufanya lolote lile la kuinusuru nchi yetu kuotokana na janga kubwa linaloinyemelea.
Bubu, hebu nipe tafsiri/maana ya hayo yaliyoko kwenye bolded text....
Oooh..sasa hivi imekuwa rukhsa kujadili ufisadi wa Kitine wakati mwanzoni ulisema "Tunachotakiwa kufanya Watanzania si kujadili ufisadi uliofanywa na Kitine".....
Why the change of heart Bubu?
Maana yangu ni kwamba aliyoyasema Kitine na ufisadi alioufanya ni mambo mawili tofauti, Hebu angalia kichwa cha habari cha hii thread. Nilichokuwa napinga mimi ni kuyapuuza aliyoyasema Kitine kwa sababu tu ni fisadi, lakini kama kuna mjadala unaotaka kuanzishwa kuhusu ufisadi alioufanya Kitine basi ni rukhsa kabisa kufanya hivyo. Narudia tena ufisadi alioufanya Kitine usiwe sababu ya kuyapuuza aliyoyasema ambayo yana ukweli. Kikwete kawafungulia mashtaka akina Mramba na Yona kwa waliyoyatenda wakati wa awamu ya Mkapa, Kitine naye anaweza kabisa kufunguliwa mashtaka kwa ufisadi aliofanya wakati wa awamu ya tatu.
Ha ha ha ha ha haya vidole viliteleza lakini kamwe siwezi kuzuia mjadala wa fisadi yoyote yule hapa ukumbini. Hawa mafisadi wanachangia sana katika kurudisha nyuma maendeleo ya nchi yetu na hata siku moja siwezi kuwatetea.
Mjadala wa Kitine kama fisadi na mjadala wa aliyoyasema kuhusiana na nchi kuendeshwa kienyeji ni vitu viwili tofauti.
Anaongelea nini hapo, matatizo ya viongozi wasiohimiza kilimo cha mbolea? Hebu jifunze kusema ukweli kama ukitaka kusema wewe Bubu.
"Mimi nadhani hatua hizi zinazochukuliwa hazilengi kukomesha tatizo la rushwa, ni siasa tu za uchaguzi,"
"Mtu anajiuzulu, anafukuzwa uwaziri kwa sababu ya kashfa, kwa sababu ya kukosa maadili, halafu anabakia kuwa mbunge na mjumbe wa kamati kuu ya chama, nini hii? Hii haifai. Waziri akikosa uadilifu anatakiwa aondolewe mara moja nyadhifa nyingine zote alizobakiwa nazo..."
"Tatizo kubwa ni viongozi kukosa integrity...Kuna kuporomoka kwa kiasi kikubwa kwa maadili ya uongozi."
"Nilikuwa kiongozi wa kwanza kuzungumzia rushwa kubwa miaka 10 iliyopita. Nilisema ndiyo inayovuruga uchumi kuliko hata rushwa ya nesi, hakimu, polisi..."
"Usalama wa Taifa should be completely clean . Idara hii inatakiwa kuwa,...Sasa kama Usalama wa Taifa ukiwa mchafu ndio tunapata viongozi wala rushwa..."
Sasa wewe apologist wa Kitine unataka kupotosha mchana mchana hapa kwamba huyu fisadi hakuongelea ufisadi.
Naona sasa umeamua kuropoka. Kuna tofauti kubwa kati ya kusema aliyoyasema Kitine kwamba nchi inaendeshwa kienyeji yana ukweli na kuapologise on Kitine's behalf. Hakuna popote pale ambako nimemtetea Kitine kwa ufisadi alioufanya alipokuwa madarakani katika awamu ya tatu, kama hukuelewa basi narudia tena. Nimesema hivi aliyoyasema Kitine kwamba nchi inaendeshwa kienyeji yana ukweli na hakuna sababu zozote za muhimu za Watanzania kuyapuuza pamoja na ufisadi alioufanya Kitine.. Usiniwekee maneno ambayo sikuyasema kabisa.
Sasa hayo niliyoyandika hapo juu yanahusiana nini na aliyoyasema Kitine? Je, unakubali kama uongizi wa nchi unaiendesha nchi kienyeji? Je, unakubali kama aliyoyasema Kitine yana ukweli na yana umuhimu wa kujadiliwa na Watanzania? Hata katiba ya Tanzania haimkatazi msaliti au fisadi kutoa maoni yake kuhusu mwenendo wa nchi yake na hakuna nchi yoyote ile dunniani inayomkata msaliti au fisadi kutoa maoni yake. Watapima uzito na ukweli wa yale aliyoyasema na kuona kama yana umuhimu wa kuyatafakari.
Wewe unataka mtu yeyote yule ambaye si safi asiwe na ruhusa ya kusema lolote lile kuhusu hali ndani ya nchi yake hata kama lina ukweli, hili sikubaliani nalo na wala halikubaliki katika nchi nchi nyingine nyingi duniani. Akizungumza upupu tutasema huyu kazungumza upupu hatuna haja ya kupoteza muda wetu kujadili upupu aliouzungumza, lakini akizungumza ukweli wa mambo basi mimi kwa maoni yangu aliyoyazungumza yanastahili kabisa kupewa uzito unaostahili.
hiki kidingi kinaboaaa......- Unajua Invisible aliwahi kutuambia kwamba wewe ni mama mtumzima mwenye heshima sana na kwamba ukidharauliwa inakuwa sio vizuri maana itaonekana tunawatenga kina mama,
- Ukamsumbua Mkandara weee na simu kwamba aongee na mimi, wewe sio hivi wala vile, sasa here you go, karibu sana mkuu haya bring it on now I am ready kwa majibu!
Wazee wa sauti ya umeme - FMES!
Tunachotakiwa kufanya Watanzania si kujadili ufisadi uliofanywa na Kitine bali yale aliyoyazungumza
hiki kidingi kinaboaaa......
"Haiwezekani viongozi wakateuliwa kwa misingi ya mitandao …sijui, kwa msingi wa politics of division (siasa za makundi) ndani ya chama. Haiwezekani nchi ikaendeshwa kienyeji. Integrity should be number one (uadilifu unapaswa kuwa kitu cha kwanza kuzingatiwa).
"Mtu anajiuzulu, anafukuzwa uwaziri kwa sababu ya kashfa, kwa sababu ya kukosa maadili, halafu anabakia kuwa mbunge na mjumbe wa kamati kuu ya chama, nini hii? Hii haifai. Waziri akikosa uadilifu anatakiwa aondolewe mara moja nyadhifa nyingine zote alizobakiwa nazo. Nadhani hii itasaidia," alisema Dk. Kitine pasipo kutaja jina la kiongozi yeyote.
Mkuu haya ni maneno (fikra) ya Mwalimu Nyerere na zilikuwa SIASA tu kutaka kutisha watu na kukatisha tamaa..Katika makosa makubwa ya mwalimu ni ktk kurithisha iwe kitaifa au familia yake. Mzee huyu alikuwa hana kipaji hicho kwani kila aliyemchagua iwe ktk familia au Taifa wote ni BOMU!..Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM na huu ndiyo mwanzo.
- Mkulu BAK ni kweli kabisa tunahitjai kujadili maneno ya Kitine, lakini ni lazima tuanze na yeye kama kweli tuko serious, Taiwan wana matatizo kama yetu, guess what wameanza na rais wao wa zamani kwanza.