Kitine: Nchi sasa yaongozwa kienyeji

Kitine: Nchi sasa yaongozwa kienyeji

frederick sumaye hakukosea pale aliposemaga "tujihadhari na viongozi ambao wanatumia kalamu[wizi wa kalamu na kuchafuana].....watatumia bunduki kusalia madarakani..."...

kikwete anapoelekea ni kwenye udikteta ....siasa za makundi..etc..

JK Nchi ilimshinda siku nyingi, tangu kipindi kile alichovunja baraza la mawaziri.
 
Gee!!! Kwa maana nyingine wewe unaona sawa tu wachukuaji kutuachia 3% ya mapato ya dhahabu yetu na wao kuchukua 97%!!! Inaelekea na wewe ni mooja wa wale walioweka maslahi ya chama mbele badala ya Watanzania!!

Wabunge wengi wa bunge letu wanatoka CCM chama ambacho kiongozi wake ni Kikwete. Watanzania haturidhishwi kabisa na utendaji wa Bunge hilo. Kiongozi wa Serikali wa shughuli za Bungeni ni Waziri Mkuu. Siyo siri kwamba Watanzania haturidhiki na Bunge na Kikwete angweza kabisa kuwaita Spika na Pinda kama kiongozi wa CCM na pia Rais wa nchi ili kuhakikisha utendaji wa Bunge unakidhi matarajio ya Watanzania na siyo kuliburuza buruza Bunge na kuminya uhuru wa wawakilishi wa Wananchi kama anavyofanya Sitta. Amezuia kashfa ya Vitambulisho kujadiliwa Bungeni. Amezuia kashfa ya Kiwira kwa mara nyingine tena kujadiliwa Bungeni. Kikwete angekuwa ameweka maslahi ya nchi mbele angweza kabisa kukemea maamuzi haya ya spika, lakini yuko kimyaaaaaaa kwa maana nyingine anaridhika na utendaji mbovu wa Wabunge na pia Sitta kuminya uhuru wa Wabunge.

Sijui hapa unataka kusema nini!!!

Mwalimu mwenyewe pamoja na kuwa ndiye alimsaidia Mkapa kuwa Rais tayari alikuwa ameshaaza kuhoji maamuzi na sera za Mkapa. Mbona unakurupuka sana!? Hivi hukumbuki ni nani waliotamka kwamba Kikwete ni chaguo la Mungu!? Kwa hiyo kama watu walikuwa wanasimamisha misafara ya Kiwete na sasa kuna kila dalili uongozi wa nchi umemshinda basi watu wanyamaze tu na kuiacha nchi iangamie!!!? Hivi ni kipi hasa unataka kutetea hapa!?😕

Whaaaaaaaat!? Are you in your right mind!!!? 😕

BAK BAK:

Kwanza sipo hapa kutetea JK. Lakini vilevile ni lazima kukubali kuwa watanzania mmeoza katika ngazi zote.

Mwanakijiji amebandika mkataba wa Richmond hapa JF. Nimeusoma na nimeangalia signatories wake. Signatories zaidi ya 11 walianguka saini zao wakiwakilisha Serikali au Tanesco. Na wengi walikuwa katika nafasi zao za kazi kabla JK ajachukua urais.

Sasa mnataka rais awe effective wakati wananchi wote mmeoza.

Ngoja nikupe kipande cha 'Liyumba Revealed' ambacho kwa sababu zako binafsi umeacha ku-copy and paste.

He spent his life serving the Central Bank of Tanzania, building up strong connections within the corridors of power during the last five years of the third phase regime.

He rose and conquered Dar es Salaam, with his quickly generated wealth feeding a lavish lifestyle and an appetite for posh cars.

He broke into the high life nine years ago, after serving the bank for three decades, and he took to his new lifestyle like a fish to water.

His home in Kawe, a suburb of Dar es Salaam, is estimated to be worth about $1m while another home located in Mbezi, whose documents he presented before the court, is worth close to $800,000. This is only what he has chosen to disclose, excluding the fancy cars and other assets he has accrued.

Tales of his personal life - the women, the payoffs - were fodder for the gutter press, but no one dared touch him for fear of repercussions from his strong connections.
....
 
frederick sumaye hakukosea pale aliposemaga "tujihadhari na viongozi ambao wanatumia kalamu[wizi wa kalamu na kuchafuana].....watatumia bunduki kusalia madarakani..."...

kikwete anapoelekea ni kwenye udikteta ....siasa za makundi..etc..

PM:

Matatizo yako kwanza unataka rais abadilishe tabia zenu. Rais ana-reflect tabia zenu. Watanzania ni porojo, wezi na wabadhirifu.
 
PM:

Matatizo yako kwanza unataka rais abadilishe tabia zenu. Rais ana-reflect tabia zenu. Watanzania ni porojo, wezi na wabadhirifu.
Zakumi,
Wewe uko kundi gani? Unaposema abadilishe tabia zenu wewe unatoka nchi gani?
 
BAK BAK:

Sasa mnataka rais awe effective wakati wananchi wote mmeoza.

Ngoja nikupe kipande cha 'Liyumba Revealed' ambacho kwa sababu zako binafsi umeacha ku-copy and paste.....

Duh!!! Usitudhalilishe Watanzania kiasi hicho. Labda ni wewe pekee yako uliyeoza. Huna mamlaka yoyote ya kuamua nini kiwe posted hapa ukumbini. Invisible kishatoa ruhusa kwa magazeti mbali mbali ya ndani na nje ya nchi kuwekwa hapa ukumbini kwa maana nyingine kucopy and paste ni ruhusa!!! Kama inakukera basi tafuta threads nyingine. Kweli kuna watu wanajua kujidhalilisha eti Watanzania wote mmeoza lakini wewe mwenyewe hukujiweka kwenye kundi la waliooza!!! Ama kweli ukistaajabu ya Mussa....
 
I see, ukweli unauma. Huko tayari kulaumu kuwa nchi inaongozwa kienyeji lakini hutaki kukubali kuwa mnaishi kienyeji.

For every rule there is an exception. Hivyo suala langu la utanzania ni exception.
 
I see, ukweli unauma. Huko tayari kulaumu kuwa nchi inaongozwa kienyeji lakini hutaki kukubali kuwa mnaishi kienyeji.

For every rule there is an exception. Hivyo suala langu la utanzania ni exception.

Tungekuwa tunaishi kienyeji basi tusingeona kasoro yoyote kwamba nchi inaendeshwa kienyeji. Lakini leo hii kila kona ya Tanzania Watanzania, na hata walio nje ya nchi, wamechoka wanaipigia kelele Serikali kwa utendaji wa mambo mbali mbali ingekuwa wanaishi kienyeji basi wangenyamaza kimya na kuacha bora liende maana hawaoni kasoro yoyote. What is exceptional about suala lako la Utanzania?
 
PM:

Matatizo yako kwanza unataka rais abadilishe tabia zenu. Rais ana-reflect tabia zenu. Watanzania ni porojo, wezi na wabadhirifu.

Zakumi nakupa Kumi mwanangu. Well said;

Rais tulimchagua wenyewe tena tukawa tumwita "handsome boy", na kwetu kilikuwa kigezo mojawapo cha kumchagua kuiongoza nchi. Sasa jamaa unatafuna vyake na the few, the blessed, the fisadis, tunapiga mayowe. What did we expect him to be? He is a reflection of our own-selves. Drag and Grab.

Watanzania tumejaa porojo tupu hata huyo Kitine hana usafi wowote, njaa tupu inamsumbua. Ameshiriki kwenye ufisadi wa kila aina hapo nchini na issue ya mkewe is just the tip of the iceberg. Hiyo nyumba anayokaa aliyouziwa kama mtumishi wa serikali wakati alikuwa siyo mtumishi wa serekali at the time, na hao waliomuuzia (sijui hata kama ameilipia hebu NHC watupe data) ni hao hao serikali hiyo anayoiita ya kihuni. Mzee wangu watakugeukia wenzako, hayaa.

Watanzania kelele nyiingi wakikosa mgao ila wakipata, basi serikali inapigwa vita. Hebu tuwe wakweli.

ZalendoHalisi
 
Tunayajua yote hayo ya ufisadi wa Kitine na Mkewe. Je, alichokisema Kitine kwamba nchi inaendeshwa kienyeji kina ukweli wowote au hakina ukweli wowote? Kinastahili kujadiliwa na Watanzania au kidharauliwe tu kwa kuwa ni porojo?

Kawawa naye sidhani kama anasumbuliwa na njaa au kanyimwa mgao na mafisadi. Alichokisema Kawawa juzi kinashabihiana sana na alichokisema Kitine kuhusu uongozi wa nchi yetu. Je, na Kawawa naye hoja zake tuzitupilie mbali na kuiacha nchi ikendelea kutikiswa na mafisadi?
 
kaka huwezi kutegemea tena reference za kawawa kwani kutokana na uzee....kumbukumbu zimepungua..kila anachosema anaandikiwa..tu!so kikwete akitaka tamko litoke mdomoni kwa kawawa anachofanya wanaandaa hotuba wanampa mkewe husna anampa anaisoma basi!!!..uzee si tatizo lingine!
 
Wana JF hapa anachosema Zakumi na Zalendohalisi ni tabia yetu watz kukumbatia uovu.Nina imani kabisa wapiga kura wamehusika kuchagua viongozi wenye mapungufu kwenye ngazi mbalimbali baada ya kupewa T-shirt,kanga,kapero na vijisent vidogo.Sasa iweje jamii kama hiyo isitambulike kuwa inakumbatia rushwa? badala yake tunalaumu tu viongozi wakati tunajua wazi ni sisi wenyewe tuliwachagua baada ya kurubuniwa na rushwa?Mimi naamini wahusika wakuu ni sisi wapiga kura,nafikiri ni kipindi muafaka kwa kila mmoja wetu kuelemisha umma kwa kila nafsi itambue rushwa ni mwanzo wa kukaribisha uongozi dhaifu na kuhatarisha utengemano kwenye jamii.
Tukielemisha ubaya wa rushwa katika mchakato wa uchaguzi ni imani yangu tutapata viongozi bora wenye kuleta maendeleo endelevu.
 
Nsaji M

Huko sahihi lakini.

Bila shaka umeishi vijijini hama umevitembelea na kuona hali ya umasikini uliokithiri.
Hali hii huzidishwa zaidi miezi michache kabla ya uchaguzi na hivyo wananchi hao kujikuta hawana uchaguzi zaidi ya kupokea TAKRIMA hizo za vikofia,fulana na shs 200au 500 kila mmoja walau akapate chumvi baada ya kuikosa mwezi mzima.

Wanautambua udhalilishwaji huo na unyonge huo lakini hawana namna ya kujinasua, ni wakati ambapo wanakuwa hawana hata senti ya kununua panado achilia mbali vifua kuwa nje!!, atakataaje fulana?. Hali hii imewekwa na mfumo wa utawala tulionao. Kwa pamoja turekebishe hali hii kwanza,tujadiri katiba leo na si kesho, wananchi wawezeshwe kwanza kujinasua na umaskini.Iwe kabla ya uchaguzi!!
 
kaka huwezi kutegemea tena reference za kawawa kwani kutokana na uzee....kumbukumbu zimepungua..kila anachosema anaandikiwa..tu!so kikwete akitaka tamko litoke mdomoni kwa kawawa anachofanya wanaandaa hotuba wanampa mkewe husna anampa anaisoma basi!!!..uzee si tatizo lingine!

Kwanza uzee unatofautiana kati ya mtu na mtu. Wengine wanaweza kuwa hata na miaka 100 au hata zaidi na bado kumbukumbu zao zinafanya kazi bila matatizo yoyote, na Kawawa anaweza kuwa ni mmoja Wazee kama hao. Kwa hiyo hiyo hotuba aliyoitoa Kawawa, Kikwete aliandaa hotuba ili itolewe na Kawawa kisha hapo hapo Kikwete ageuke na kuwapiga marafuku Wazee wastaafu waliokuwa ndani ya serikali na CCM wasimkosoe ha ha ha ha ha huo utakuwa ni usanii wa hali ya juu.
 
Zakumi nakupa Kumi mwanangu. Well said;

Rais tulimchagua wenyewe tena tukawa tumwita "handsome boy", na kwetu kilikuwa kigezo mojawapo cha kumchagua kuiongoza nchi. Sasa jamaa unatafuna vyake na the few, the blessed, the fisadis, tunapiga mayowe. What did we expect him to be? He is a reflection of our own-selves. Drag and Grab.

Watanzania tumejaa porojo tupu hata huyo Kitine hana usafi wowote, njaa tupu inamsumbua. Ameshiriki kwenye ufisadi wa kila aina hapo nchini na issue ya mkewe is just the tip of the iceberg. Hiyo nyumba anayokaa aliyouziwa kama mtumishi wa serikali wakati alikuwa siyo mtumishi wa serekali at the time, na hao waliomuuzia (sijui hata kama ameilipia hebu NHC watupe data) ni hao hao serikali hiyo anayoiita ya kihuni. Mzee wangu watakugeukia wenzako, hayaa.

Watanzania kelele nyiingi wakikosa mgao ila wakipata, basi serikali inapigwa vita. Hebu tuwe wakweli.

ZalendoHalisi

ZH:

Hilo ndilo naloamini. Mtanzania anamaliza leo shule, hataki hata kutafuta experience, atakachotafuta ni kazi yenye ulaji. Iwapo kwenye kila sekta kumejazana watu wanaotafuta ulaji, huyo rais wa kuleta mabadiliko hatatoka wapo?

Kwenye nchi ambayo mwizi kama liyumba, mwizi BOT, anakuwa instant celebrity unategemea nini 😕
 
Nsaji M

Huko sahihi lakini.

Bila shaka umeishi vijijini hama umevitembelea na kuona hali ya umasikini uliokithiri.
Hali hii huzidishwa zaidi miezi michache kabla ya uchaguzi na hivyo wananchi hao kujikuta hawana uchaguzi zaidi ya kupokea TAKRIMA hizo za vikofia,fulana na shs 200au 500 kila mmoja walau akapate chumvi baada ya kuikosa mwezi mzima.

Wanautambua udhalilishwaji huo na unyonge huo lakini hawana namna ya kujinasua, ni wakati ambapo wanakuwa hawana hata senti ya kununua panado achilia mbali vifua kuwa nje!!, atakataaje fulana?. Hali hii imewekwa na mfumo wa utawala tulionao. Kwa pamoja turekebishe hali hii kwanza,tujadiri katiba leo na si kesho, wananchi wawezeshwe kwanza kujinasua na umaskini.Iwe kabla ya uchaguzi!!

Nsaji:

Nimemwambia BAK katika posti zangu zilizotangulia kuwa katiba ya sasa ilifanya kazi kuanzia 1967-1977, baada ya hapo imekuwa mzigo.

Lakini yeye bado ana matumaini kuwa siku moja CCM itagawanyika au watatokea watu majasiri ndani ya CCM kuleta mabadiliko.
 
Hivi kweli matatizo ya uongozi tuliyonayo yanasababishwa na katiba? katiba yetu pamoja na mapungufu yake mengi lakini si chanzo cha uongozi mbovu tuliokuwa nao sasa. Hivi kumfukuza kazi Idrissa Rashid Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO tunahitaji katiba mpya? Hivi kutangaza kwamba Kiwira iliuzwa katika mazingira ya kutatanisha hivyo serikali imeamua kuirudisha chini ya miliki ya Watanzania tunahitaji katiba mpya? 😕

Kitine aliposema wengi mkamdiscredit kwamba ni fisadi hastahili kusema lolote lile bali akae kimya. Sasa Kawawa kasema yale yale yaliyosemwa na Kitine Oooh! Kawawa mzee kaandikiwa hotuba na Kikwete. Mtasema lolote lile ili kufunga mjadala wa hali ya uongozi nchini mwetu na wakati huo huo nchi ikizidi kuelekea pabaya. Labda ashuke Mungu ndiyo mtakubali yanayosemwa kuwa yana ukweli na yanastahili kujadiliwa na Watanzania ili kutafuta njia za kuinusuru nchi yetu.
 
Zakumi,
I would like to hear your take on what we simple people of Tanzania are supposed to do to do away with this corrupt inefficient system we have. Doing nothing in no option.
 
ZH:

.... hataki hata kutafuta experience, atakachotafuta ni kazi yenye ulaji. Iwapo kwenye kila sekta kumejazana watu wanaotafuta ulaji, huyo rais wa kuleta mabadiliko hatatoka wapo:

Atafute experience ya nini, kwani "Korola" au "Nissan Shot Chasis" zitamsubiri, na Blakberi itaning'inia kiunoni lini? Inabidi auufuate mkondo wa mto amasivyo hafiki popote.

Kinachoudhi zaidi ni hao hao wanaoshiriki kwenye "uchafu" kujidai kuupinga "uchafu" wanaoukumbatia na kujidai yao ni madogo ila ya wenzao mazito. Tusi tusi tu. Unaposeama ufisadi wako ni mdogo huenda ni kwa vile hukupata nafasi ya kuzoa mabilioni, na kama "Uliyumba" ungekatiza maeneo yako/yangu ingekuwa ni wewe ama mimi na wala siyo Liyumba.

Ni afadhali kukubali tu kuwa wenzako washirika wamekuzudi kete basi nahene.
 
Back
Top Bottom