Kitine: Nchi sasa yaongozwa kienyeji

Kitine: Nchi sasa yaongozwa kienyeji

Mkuu YNIM huo ni mkopo.........wala hukuiba........na sijui kama ulipewa deadline ya kulipa.....however tutawabana vijukuu vyako.........

Wee Nyani......acha hizo........mi nakufahamu........wewe ni mhaya...oops msukuma and.... maaan you are not clean at all (joke)........

Hehehehehe....umeshaanza na wewe....eti unanifahamu....Lol
 
Hamtakaa kimya.
Usipokuwa na credibility, usipokuwa na imani ya watu, hatuwezi jua kama unataka kufukuza hawa drunk drivers wenzako ndani ya gari, ndani ya chama, ili wewe ushike usukani wakati na wewe pia jalada lako la idara ya usafirishaji lina historia ya kuendesha gari la wizara while intoxicated with pombe ya ufisadi. Tunakukemea!

Kwa hiyo kwa sababu anayetupa tahadhari aliwahi kuwa dereva mlevi kwa jina la Kitine, sisi abiria twendelee kutuna tu ndani ya hili gari hata kama dereva wake mlevi anatupeleka kuzimu. Hiyo tunayokazania kuwa credibility itatufaa nini wakati gari litakapoacha njia na kuanza kutumbukia bondeni....
......the choice is obvious​
 
Last edited:
Hamtakaa kimya.

Abiria aliyelewa anayo moral authority ya kukemea dereva aliyelewa kwa sababu yeye hajafanya baya kwa kupanda kiti cha nyuma kurudi nyumbani baada ya kulewa, ndio maana abiria walevi wetu hawa wakawa na huyu designated driver, ambae kumbe nae kalewa.

Kitine ni dereva mstaafu ambae siku za nyuma alikuwa (assuming ame recover) alikuwa drunk driver wa wizara, fisadi. Sasa anakemea drunk drivers wengine, baada ya yeye kufukuzishwa kwenye usukani na kuwa abiria mwenzetu; anasema tuwafukuze madereva walevi ndani ya gari, ndani ya chama, kabla ya yeye kutubu kwamba na yeye mlevi mkongwe alipokuwa dereva wa wizara aliua!

Abiria tunasema sawa, tunasikia hata ya huyu recovered vilain anaetuambia tukemee mafisadi.

Tunaanza na wewe, Kitine.

Tunasema, Kitine acha unafiki kukemea mtu. Umekamua mali ya umma, huna credibility, huna moral authority.

Usipokuwa na credibility, usipokuwa na imani ya watu, hatuwezi jua kama unataka kufukuza hawa drunk drivers wenzako ndani ya gari ili wewe ushike usukani wakati na wewe pia jalada lako la idara ya usafirishaji lina historia ya kuendesha gari la wizara while intoxicated with pombe ya ufisadi. Tunakukemea!

Well thought analysis
 
Mlevi Kuhani alimuona Mlevi Masau kuwa sio Daktari.....leo Mlevi Kuhani anatuambia Mlevi Kitine hafai kusikilizwa.....halafu walevi wa JF tunampa THANKS.......eti walevi hatuna moral authority.........eehh......what a mess!!
 
I concur - it is a real mess !!

“Mtu anajiuzulu, anafukuzwa uwaziri kwa sababu ya kashfa, kwa sababu ya kukosa maadili, halafu anabakia kuwa mbunge na mjumbe wa kamati kuu ya chama, nini hii? Hii haifai. Waziri akikosa uadilifu anatakiwa aondolewe mara moja nyadhifa nyingine zote alizobakiwa nazo. Nadhani hii itasaidia", alisema Kitine.

“Hatuwezi kuwavua watu uanachama au nyadhifa zao ndani ya chama kwa sababu hiyo tu. Yeye aliyesema hivyo atutajie ni kiongozi gani wa serikali ambaye pia ni kiongozi wa chama, ameshathibitika kuwa hana maadili halafu kama chama tumeendelea kumwacha. Atuambie…..hakuna,” alijibu Chiligati.

"Hali tuliyofikia si nzuri, tena niseme ni mbaya sana. Kuna kuporomoka kwa kiasi kikubwa kwa maadili ya uongozi. Na hii nawaambia, nchi haijawahi kuwa katika hali mbaya huko nyuma kama ilivyo sasa. Kwa hali tuliyofikia, ni vigumu kurekebisha maadili ya uongozi", akaongeza Kitine.

“Kwa mfano, hilo alilosema nchi inaongozwa kienyeji, maana yake nini? Nchi kuongozwa kienyeji maana yake hakuna mfumo wa utawala kabisa, hakuna utawala wa sheria. Mahakama hazipo wala Bunge halipo…serikali haipo. Kungekuwa na hali hiyo, ingekuwa sawa na kusema nchi inaongozwa kienyeji",akadakia Chiligati.

“Mzee Kitine ameongea jambo ambalo ninaliongea kila siku kwamba, kuna tatizo kubwa serikalini. Tuhuma za ufisadi zimeshamiri sana, watendaji hawachukui maamuzi, wanasiasa wenye nyadhifa serikalini wamejaza nafasi na hawako tayari kuwajibika. Tunahitaji muafaka wa kitaifa kwenye mambo mengi,” akaingilia Zitto.

............ the choice is simple​
 
Hihihihihihiii...Ogah..come on now, u knew I was gonna get a good laugh outta this one...
 
nimemwona kitine kwa macho yangu na kumsikia kwa masikio yangu kwenye taarifa ya habari ya TBC jana akikanusha kuhusu aliyoyasema na kusingizia vyombo vya habari kuwa eti vinamkosanisha na viongozi wenzake
 
Kwani yeye bado ni Kiongozi? Kwani ni kiongozi wa nani na wapi?
 
Mag3 asante kwa kutuonyesha hii drama inavyokwenda. Realy the choice is ours! hapana haja ya kubishana zaidi. Thread inaweza kuishia hapa.🙂
 
nimemwona kitine kwa macho yangu na kumsikia kwa masikio yangu kwenye taarifa ya habari ya TBC jana akikanusha kuhusu aliyoyasema na kusingizia vyombo vya habari kuwa eti vinamkosanisha na viongozi wenzake

Kwa kuwa Kitine ni FISADI, hili lilitegemewa na hiki kitendo chake cha kukanusha kinaashiria kitu kimoja - ujumbe umefika na MAFISADI wenzake wako restless. Ipo siku watatafunana wenyewe kama manyang'au mzoga utakapokwisha.
 
Labda pia anathibitisha kwamba yeye ni fisadi na ndio maana anachelea kutochonganishwa na mafisadi wenzie. Si unajua tena waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba.
 
Last edited:
nimemwona kitine kwa macho yangu na kumsikia kwa masikio yangu kwenye taarifa ya habari ya TBC jana akikanusha kuhusu aliyoyasema na kusingizia vyombo vya habari kuwa eti vinamkosanisha na viongozi wenzake

- There you go, unaona sasa huyu anatakiwa kuongelea Kisutu sio kwenye majukwaa ya siasa, yaani nimeyasema jana tu hata wino haujakauka tayari ameshakana maneno yake mwenyewe, yaani aibu tupu!
 
Ona nilichosema jana kuhusu Kitine na kukana maneno yake mwenyewe:-

- Kitine na Mkapa, Mwalimu's people tena damu damu, Mwalimu alipokuwa ana-retire akapelekwa Canada kula nchi, akilipiwa kila kitu na serikali yaani hela zetu walipa kodi anachokifanya hakieleweki, Mkapa kuwa rais tu akamuomba kurudi great friends akarudi, Mkapa akatumia ubabe na nguvu za ajabu within a month Kitine ni mbunge na waziri ofisi ya Mkapa, all this time hajaona ubovu wa uongozi wetu wala tatizo la integrity,

- The next thing Kitine anaota urais, ghafla kaanza kuvaa kanzu na barakashia bungeni, nini kaambiwa rais anayefuata Mkapa lazima awe Muisilamu, mara oooh mawaziri ni wala rushwa, haya Kitine tuambie majina yao, akadai oooh no waandishi wamekosea sikusema vile, next mke wake amechukua maelfu ya dola za walipa kodi kwenda kutibiwa nje, kumbe ameenda kuzifanyia shopping bila kwenda Hospital wala kwa Daktari yoyote huko Canada na wala haumwi chochote, sasa all this time Kitine haoni ubovu wala tatizo la integrity na uongozI wetu,

- The next thing Kitine amehonga honga na kujaribu kuzuia uchunguzi wa kamati ya bunge kuhusiana na wizi wa mkewe wa hela zetu walipa kodi alizotumia nje tena kwa uharibifu sana, wabunge kuja juu sana ndio Kitine baada ya kubanwa sana na wabunge kukubali kujiuzulu na kulazimishwa kulipa nusu ya zile pesa tena katika mazingara yaliyojaa uhuni uhuni, badala ya mkewe kwenda jela kwa wizi wa mchana wa hela zetu walipa kodi, all this time Kitine haoni matatizo ya uongozi wetu na integrity yake kua hovyo!

Sasa leo he is supposed to be a hero kwa sababu amesema maneno ya kuponda serikali ya CCM, akitukana ubovu ule ule uliomponya yeye na mkewe, sometimes huwa ninajiuliza hivi vita tunavyopigana na mafisadi, kwa mfano tukiwatoa mafisadi wote leo, eti ni kweli tutaweza kuweka viongozi wapya ambao hawatakuwa mafisadi? Ningeelewa kwamba Kitine sasa ameamua kwamba wananchi wa Tanzania wameonewa vya kutosha na kuweka mfano anataka mkewe afunguliwe mashitaka kwanza ya kuiba hela zetu walipa kodi huko nyuma maana sasa anataka to come clean, no sasa yeye na Mbilinyi ni mashujaa against uozo wa uongozi wetu uliowaponya.

Tuangalie sana ndugu zangu tusije kua kama wenzetu weusi huko US, kabla ya Obama kukosekana kwa real heros kuliwafanya kuanza kuamini hata yule Ferguson aliyeuwa wazungu kwenye LIIR Train bila sababu kuwa shujaa, badala ya a murdereeer!

Mungu Aibariki Tanzania!
 
....Hata kama ni usanii........ukweli unabaki pale pale......period!
 
Ubovu wenyewe, ninyi mlianza kumkumbatia na kumpachika u-hero........tuliwaambia kuwa msimsikilize, ninyi hamkusikia!! Nasikia bado kidogo tu Chadema wampe kadi ya uanachama!!! Kaaaaaaaazi kweli....😕
"................the choice is obvious"!!! wapi bana wewe!!

Ifuatayo ni mojawapo ya post yangu mapema kabisa

Asante BAK, sidhani hapa kuna anayemtetea FISADI Kitine hata moja - la hasha. Kitine hata akikamatwa leo wala sitakosa usingizi na nitakuwa miongoni mwa wale watakaopaza sauti kutaka asulubiwe. Kwa hasira ningeweza hata kumzaba kibao......

Lakini gari tulilolipanda linakaribia milima ya Kitonga na anatokea Kitine anatupa tahadhari kuwa dereva wetu anaonekana kalewa na uwezo wake wa kutufikisha salama uko mashakani. Na kweli tukiangalia anavyolikokota gari roho zetu ziko mikononi......

.....the choice is simple.

What's so hard to understand ? kaaaaaazi kweli kweli.🙄
 
nimemwona kitine kwa macho yangu na kumsikia kwa masikio yangu kwenye taarifa ya habari ya TBC jana akikanusha kuhusu aliyoyasema na kusingizia vyombo vya habari kuwa eti vinamkosanisha na viongozi wenzake

Bahati mbaya wakati Kitine akizungumza na magazeti sisi wana JF hatukuwepo. Lakini kwenye TBC tumemuona live. Sasa tufuate lipi? Unajua tena magazeti yetu yanavyojua kuongeza chumvi. Namshauri Kitine, next time akizingumza na magazeti asome a written statement na asijibu maswali ya ziada ama sivyo anaweza kujikuta kawekwa mahala pabaya na UWT.
 
Hana lolote anataka hela ya mboga tu, hizi siasa za Tanzania kweli pasua kichwa.
 
Tuangalie sana ndugu zangu tusije kua kama wenzetu weusi huko US, kabla ya Obama kukosekana kwa real heros kuliwafanya kuanza kuamini hata yule Ferguson aliyeuwa wazungu kwenye LIIR Train bila sababu kuwa shujaa, badala ya a murdereeer!

Tunakubaliana kwamba Kitine ni mnafiki, hana credibility kukanya wenzake.

Ila kipande hicho hapo cha kukejeli Waamerika Weusi kwamba walimfanya Ferguson kuwa hero si kweli.

Ferguson alionekana mwehu baada ya, pamoja na mengine mengi bizarre, kudai kwamba anataka Bill Clinton aje mahakamani kuwa shahidi wa mauaji ya kwenye train ya Long Island. Uchambuzi wako wa kutukana weusi hapo umepotoka. Wasingekuwa ma hero wa Wamarekani Weusi wewe na mimi tusingekuwa na uhuru wa kwenda kuzunguka zunguka huru Marekani na kunywa kwenye water fountain za kila mtu na kubeba maboxi. Tusiwatukane.

Tubaki kwa haya kwetu: Huyu ex-embezzler Kitine hana moral authority kukemea ufisadi.
 
Kambona na Bi Titi Mohamed na wengineo walishiriki katika kutaka kuipindua serikali halali ya Mwalimu iliyokuwa madarakani. Baadhi walikimbia nchi na wengine walifunguliwa mashtaka na kuonekana na hatia ya usaliti na kufungwa akiwemi Bibi Titi Mohamed.

Mwalimu aliwasamehe wote na Kambona pamoja na usaliti wake dhidi ya serikali aliporudi nchini toka Uingereza alijiingiza tena kwenye mambo ya siasa na Bibi Titi alirudi CCM. Kwa maana nyingine wote waliruhusiwa tena kutoa maoni yao kuhusu mwenendo wa nchi bila kujali usaliti wao walioufanya dhidi ya Serikali halali ya Mwalimu ambayo ilichaguliwa na Wananchi.

Kitine pia pamoja na ufisadi wake ana haki kama Mtanzania mwingine yeyote yule kutoa maoni yake kuhusu mwenendo wa nchi yetu. Tunachotakiwa kufanya Watanzania si kujadili ufisadi uliofanywa na Kitine bali yale aliyoyazungumza kuhusu uongozi katika nchi yetu je yana ukweli wowote au ni upupu tu? je, yanastahili kuyajadili na kuyatafakari kwa manufaa ya nchi yetu? Mimi na wengine wengi tunaona Kitine ana haki ya kutoa maoni kuhusu mwenendo wa uongozi ndani ya nchi yetu. Hata Chiligati na Msekwa wametamka wazi kwamba Kitine kama Mtanazania yeyote yule ana haki kabisa ya kutoa maoni dhidi ya serikali iliyokuwa maoni yake. Hawakujaribu hata kidogo kutaka kuonyesha kwamba kwa kuwa ni fisadi basi hastahili kusema lolote lile kuhusu mwenendo wa uongozi ndani ya nchi yetu.

Hakuna nchi yoyote duniani inayozuia raia wake hata wale ambao ni wasaliti ama mafisadi kutoa maoni yao kuhusu serikali zao na Tanzania haitakuwa ya kwanza kufanya hivyo kesho, wiki ijayo wala miaka 20 ijayo. Alichokisema Kitine kina ukweli kama Watanzania tunakikimbia na kutotaka kujadili yale yaliyosemwa na Kitine basi iko siku tutakuja kuyakumbuka maana mficha ugonjwa kifo humuumbua.
 
Back
Top Bottom