JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Moja kati ya changamoto kubwa ambayo Watanzania tunayo kwenye huduma zenu ni kuhusu kuwahudumia wateja au watu wenye uhitaji.
Niende moja kwa moja kwenye hoja yangu ya msingi, kwa miezi kadhaa nimekuwa nakwaruzana na watu wa TANESCO kuhusu huduma kwa wateja “Customer Service”.
Inawezekana shida ni kubwa zaidi ya tunavyoiona sisi Wananchi ambao tupo ndani ya TANESCO.
Kwanza walichoamua badala ya kupiga simu ipokelewe eneo husika ulilopo, mteja akiwa na changamoto anapiga simu kwenye namba ambazo nadhani zinapokelewa makao makuu kisha unatoa taarifa yako ili nao wafikishe kwenye mkoa au eneo ulilopo ndipo uweze kusaidiwa.
Inawezekana walikuwa na mkakati wao, lakini mara kadhaa imetokea napia simu kwanza haipokelewi, maelezo yanakuwa mengiiiiii lakini hupati huduma.
Wana namba yao ya WhatsApp ambapo unaona namba ipo online lakini ili ufanikiwe kupata huduma kazi ipo.
Ukipiga hiyo namba wanakata, ukituma sms hawajibu.
Imenitokea hiyo mara kadhaa na kuna muda nikalazimika kuanza kusambaza ujumbe kuonesha nimepiga simu na kutuma SMS kwenye namba lakini zijasikilizwa licha ya wao kudai namba hiyo ya Huduma kwa Wateja ni ya dharura.
Wakipokea ni mara nyingi wanakupa maneno mazuri kuwa changamoto yako imepokelewa na inafanyiwa kazi, baada ya hapo utaisoma namba, wanaingua sana.
Unaweza kuwa na dharura kubwa lakini ili upate huduma ya kidharura labda uwe na namba ya mtu mwenye cheo TANESCO au uwe unafahamiana na staff ndio utapata huduma fasta, tofauti na hapo ni hasira tupu.
Nadhani moja kati ya mambo yanayoweza kufanywa ili huduma ziboreshwe kwanza ni kuvunja kitengo hicho na kuunda upya, kubadilisha usimamizi wa mtu anayesimamia au Serikali iruhusu ushindani wa kuuza umeme isiwe TANESCO peke yake, inawezekana wanabweteka na wanaona hakuna sehemu nyingine ya kukimbilia.