Bolt kwanini hamna namba ya huduma kwa wateja? Mtu una dharura kupata msaada mpaka usubiri majibu Instagram, kweli?

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
423
1,055
Wakuu kwema? Twende moja kwa moja kwenye mada.

Huduma ya Bolt ukititokea unataka kuwasiliana nao labda umepoteza kitu au una malalamiko kwenye huduma yao, hakuna chaguo la kuwapata moja kwa moja kwa njia ya simu kwanini? Wanakimbia nini?

Yaani wameweka njia ya kuwasiliana nao kwa njia ya email pekee au uende kwenye mitandao ya kijamii.

Kweli mtu unadharura mpaka uende insta usubiri kujibiwa? Kwanini hakuna njia ya simu ambayo ukiwasiliana mtu unapata msaada wa haraka hapo hapo?

Hii ni njia ya kukimbia kuwajibika, hata suala la usalama kwenye bolt ni sifuri. Ukipata huduma mbovu ukiweka malalamiko dereva anakupigia kukukoromea kwa kumlalamikia. Hii ni hatari mtu anaweza hata kukuvizia kukudhuru.

Unasahau simu kwenye gari dereva anakuzingua kuirudisha anataka cha juu, huku huna namna ya kuwasiliana na huduma kwa wateja kwa haraka kupata msaada, eti inabidi uende insta au utumie email ndio uwasiliane nao upate msaada! Bolt mko serious kweli na biashara nyie?

Jambo hili linafanya hata madereva wawe viburi, maana huna njia ya kufikisha haraka tatizo lako mwisho wa siku unapotezea tu. Hii sio sawa. Kwani kusajili namba kwaajili ya huduma zenu inachukua muda gani mpaka mtuache wateja katika hali hii?
 
Ni taxi mtandao gani ipo na huduma kwa wateja kupitia simu.
Uzuri wa taxi mtandao ni kuwa mawasiliano ya dereva utakuwa nayo hata baada ya kupata huduma hivyo kama kuna changamoto inakuwa rahisi kufuatilia kwa kumpigia simu aliyekupa huduma.
Ukipata changamoto njia watakayotumia bolt ni hiyo hiyo ya kumpigia simu aliyekupa huduma kitu ambacho unaweza kukifanya kwa kuwa mawasiliano unayo. Zaidi sana watakachokusaidia bolt ni kushughulika na mtoa huduma kulingana na vigezo na mashariti yao.
 
Back
Top Bottom