Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,199
- 10,932
Hivi karibuni Benjamin Netanyahu alisikika akisema anataka jeshi lake liingie Rafah na kufanikisha mpango wake wa kuwamaliza Hamas kabla mwezi mtukufu wa Ramadhani haujaingia hapo Machi 10.
Baada ya kitisho hicho Misri imekuwa ikitishia kuvunja mkataba wa camp david baina yake na Israel.Hata hivyo kitendo cha kupeleka Jeshi kujenga ukuta mwengine ndani ya upande wake pembezoni mwa jangwa la Sinai kunaweza kukazusha wasi wasi juu ya nia yake hasa.
Jee ujenzi huo ni kambi nyengine kwa ajili ya watu wa Gaza au ni kwa ajili ya kambi ya jeshi lake kulinda mpaka huo.
Na jee kitendo cha Israel kusitisha kwa muda zoezi la kuingia Gaza kwa kutumia vikosi vya ardhini wamesikia nasaha za walimwengu kwamba kutasababisha madhara makubwa bila kutoa tija au ni kusubiri ujenzi huo unaofanywa na Misri ukamilike.
Wasi wasi huo umekuja baada ya picha za satelite kuona ukuta mkubwa ukijengwa takriban maili mbili upande wa Misri kutoka ukuta mwengine iliyojenga hapo awali wenye seng'enge juu yake.
Gaza si eneo la Israel na linakaliwa na watu wenye uhusiano mkubwa na Misri.Kilichotarajiwa kufanywa na Misri ili kuwalinda na kuwasaidia watu wa Gaza na kuingiza jeshi lake upande wa pili ndani ya Gaza ili kuzuia israel isifike hapo katika kuwawinda kwao Hamas.