Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,191
- 10,925
Kimya kingi kina mshindo. Hatimae nchi ya Misri imeamua kuongeza askari wake maeneo ya mpaka wa Rafah na lango la Karem Shalom.
Uamuzi huo umekuja baada ya maonyo ya awali na kufuatia taarifa ya jeshi la Israel kwamba liko mbioni kupeleka askari wa miguu eneo la Rafah walipojikushanya wapalestina zaidi ya milioni 1 waliokimbizwa kutoka maeneo mengine ya jimbo la Gaza.
Kazi za mwanzo za jeshi la Misri itakuwa ni kuziba matundu ya kuta na seng'enge ambayo yalisababishwa na Israel miezi miwili iliyopita iliposhambulia sehemu hiyo kutokea angani.
Shambulio hili lililobomoa sehemu za makuta hayo lililfanyika wakati Israel ilipokuwa ikishinikiza kuwasukuma wapalestina waingie nchini Misri.