Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,192
- 10,926
Pamoja na Israel kushindwa kufikia malengo yake ya kivita iliyojiwekea na japo imeshawahamisha wapalestina wa Gaza huku na huko bila mafanikio lakini bado imeweka nia thabiti ya kushambulia eneo la Rafah.
Umoja wa mataifa na kila mmoja wameshatoa angalizo kuwa kushambulia eneo hilo kutasababisha vifo vingi sana kwa wapalestina na kwamba huenda kukaleta mfarakazo mkubwa baina ya Israel na Misri ambao tayari wana mkataba wa kiusalama baina yao unaoheshimiwa kikamilifu na Misri.
Benjamin Netanyahu katika mazungumzo na Anthony Blinken leo amekataa kata kata mapendekezo ya Hamas ya kumaliza vita na akasisitiza kuwa hatosimamisha vita mpaka Israel ipate ushindi ulio wazi dhidi ya Hamas na kwamba ushindi huo uko karibu.
Katika mazungumzo yake mengine Netanyahu amesema ameshatoa amri ya jeshi kushambulia Rafah ambako amedai kuna mahandaki chini yake yanayounganisha na Misri,madai ambayo Misri imekanusha.
Moja ya lengo la wahafidhina wa kiyahudi ni kuwasukuma nje ya Gaza wapalestina na kwa hapo walipo ni kwamba waingie jangwa la Sinai.
Baadhi ya wasemaji wa serikali ya Misri wameshasema kitendo hicho cha Israel kitapelekea kuvunjika kwa mkataba wa Camp David na kwamba hawatoruhusu Israel kudhibiti eneo hilo kama inavyotaka.
Wasemaji wa Israel wamedai tayari Israel imeshaiarifu Misri juu ya kushambulia Rafah na kwamba wasiwe na wasiwasi kwani baada ya mashambulio hayo jeshi la Israel litaondoka eneo hilo.
Madai ya kuarifiwa Misri kuhusu kushambuliwa Rafah yanatiliwa shaka kwani hapo majuzi rais Elsisi alikataa kutpokea simu ya Benjamin Netanyahu kuzungumzia suala lolote lile na tayari Misri imeshatishia kukatisha mahusiano ya kibalozi na Israel.
Pamoja na yote hayo na unyeti wa mashambulio hayo jee Misri imeshapeleka majeshi yake mpakani kujitayarisha na kuzuia athari zake kuingia nchini mwao au kuzuia Israel kudhibiti mpaka huo.
Uzito wa jambo hilo na kauli za kila upande hakuonekani harakati za dhati za Misri kuulinda mpaka huo au kutaka kuzuia janga kubwa zaidi kuwapata wapalestina pindi wakishambuliwa.
Wasemaji wa mashirika ya kibinadamu wamesema kwa huruma kwamba wapalestina hapo walipofika wamechoka kutokana na shida za vita na hata nguvu zimewaishia kukimbia na kuhama kuelekea popote pale kwengine.
Watoto wengi wa kipalestina walio Gaza wametajwa kuwa na mshtuko mkubwa kutokana na vifo vya wenzao waliowashuhudia.Wazee wa kipalestina nao pamoja na uchofu wamejaa huzuni za kupotelewa na watoto na ndugu zao.