Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

Naomba kidogo nikuelekeze namna ya uandishi mzuri kwani nathamini juhudi zako.

Unapotumia nukta kutenganisha maneno nukta zinakuwa tatu tu kama hivi...

Nadhani unajua kuwa ukitumia herufi kubwa tupu ni kuwa unapiga kelele.

Tumalize na matumizi ya lugha...usichanganye lugha Kiswahili na Kiingereza
labda kwa neno moja au mawili kwa nia kuazima na lazima uziwekee
"inverted comas."

Wajua kuwa unaweza kujulikana jinsi ulivyo yaani tabia yako kutokana na lugha
yako unavyoandika?

Ukisoma madras kuna somo linafunzwa linaitwa adabu ya elimu.

Ungependa nilisomeshe hapa ukumbini kwa faida ya wanaukumbi?

Hii ni elimu ya bure. Haitozwi.

Taratibu tutafika.
 
Unataka uone mkono wa Nyerere na Kanisa Katoliki?

Hilo nimelieleza katika kitabu.

Nakushukuru kwa mchango wako wenye mantiki.
 
Sijui kama umeandika kunijibu mimi au mwingine.

Kama ni mimi ah nakiri mapungufu ya uandishi kama yapo, na kama nimekuudhi mimi ni muungwana nasema samahani.
Nitafanya editing bila kuathiri maudhui yangu ili kuondoa kile kilichokuudhi.

Sijui kama kuna mapungufu ya adabu maana hakuna mahali nilipotukana, kama yapo samahani.

Elimu yangu ni ndogo sana inayonitosha. Hiyo ya madrasa nikiihitaji nitawaomba wahusika kwa wakati wangu binafsi.

Sitaomba radhi kwa hoja zangu kwani huwa ninasema na kuandika ninachokiamini mimi hata kama hakimpendezi mtu.
 
Unataka uone mkono wa Nyerere na Kanisa Katoliki?

Hilo nimelieleza katika kitabu.

Nakushukuru kwa mchango wako wenye mantiki.

Nimefuatilia mjadala huu na japo sijakisoma kitabu, nafikiri kitabu hicho kitafaa kusomwa. Na nitakisoma. Lakini nafikiri ulivyokiwakilisha hapa JF si kwa ajili ya kukitangaza tu ndio maana umekuwa ukitoa 'exerpts' ili kutupa kitu kama utangulizi hivi kwa sisi ambao bado hatujasoma.

Lakini pamoja na kwamba umepata support kutoka kwa baadhi ya watu ambao wamekisoma au hawajakisoma, kuna watu pia ambao kabla ya kuku-support au kuku-criticise bado wangependa kujibiwa masuali mawili au matatu kutokana na "exerpts" ulizoweka.

Sasa bahati mbaya majibu yako kuhusu hayo maswali yamekuwa yanakuja visivyo. Mimi naamini kama ulifanya utafiti na kupata data safi ungeweza kujibu tu hayo maswali. Kujibu hapa haimaanishi kuwa tutaacha kusoma kitabu chako. Sana sana ukijibu hapa utazidi kutupa morali zaidi wa kusoma hicho kitabu, of course pamoja na vingine.

Kutokana na kutojibu maswali ya ndugu Jasusi na ndugu Nguruvi3, mimi naomba nikuulize swali moja tu, no offense intended!

Kama mtafiti wa kihistoria, IS IT NOT POSSIBLE THAT YOU FIRST HAD YOUR OWN CONCLUSIONS BEFORE YOU GATHERED EVIDENCE?

Samahani kwa kuchanganya lugha.
 
Naomba kidogo nikuelekeze namna ya uandishi mzuri kwani nathamini juhudi zako.

Unapotumia nukta kutenganisha maneno nukta zinakuwa tatu tu kama hivi...

Nadhani unajua kuwa ukitumia herufi kubwa tupu ni kuwa unapiga kelele.

Tumalize na matumizi ya lugha...usichanganye lugha Kiswahili na Kiingereza
labda kwa neno moja au mawili kwa nia kuazima na lazima uziwekee
"inverted comas."

Wajua kuwa unaweza kujulikana jinsi ulivyo yaani tabia yako kutokana na lugha
yako unavyoandika?

Ukisoma madras kuna somo linafunzwa linaitwa adabu ya elimu.

Ungependa nilisomeshe hapa ukumbini kwa faida ya wanaukumbi?

Hii ni elimu ya bure. Haitozwi.

Taratibu tutafika.

Mimi nadhani nina haki ya kuhoji mada iliyoletwa hapa. Ufahamu wangu hauniruhusu kulishwa kwa kijiko. Nimesoma kitabu 'Untold History..' nimesoma hiki pia n.k.

Kinachoshangaza Mohamed hajibu hoja na amejikita katika kashfa. Asichokijua ni kuwa wasomaji hapa ni wa dini na makabila yote.

Mohamed, naomba kama una muda uangalie maandiko yangu humu JF utafaham tabia yangu.

Kwa vile umejitolea kunieleza tabia yangu ikoje nakuomba unieleze hapa ili nijifunze ikibidi kwani sisi ni wanadamu na hakuna aliyekamilika miongoni mwetu. Hoja yako(wino mwekundu) sio tu imenidhalilisha, pia imenisikitisha. Utanisafisha endapo utaielezea tabia yangu kama unavyoijua kutokana na maandiko yangu ili jamii isiwe na shaka zaidi. tafadhali
 
Mimi nadhani nina haki ya kuhoji mada iliyoletwa hapa. Ufahamu wangu hauniruhusu kulishwa kwa kijiko. Nimesoma kitabu 'Untold History..' nimesoma hiki pia n.k. Kinachoshangaza Mohamed hajibu hoja na amejikita katika kashfa. Asichokijua ni kuwa wasomaji hapa ni wa dini na makabila yote.
Mohamed, naomba kama una muda uangalie maandiko yangu humu JF utafaham tabia yangu.
Kwa vile umejitolea kunieleza tabia yangu ikoje nakuomba unieleze hapa ili nijifunze ikibidi kwani sisi ni wanadamu na hakuna aliyekamilika miongoni mwetu. Hoja yako(wino mwekundu) sio tu imenidhalilisha, pia imenisikitisha. Utanisafisha endapo utaielezea tabia yangu kama unavyoijua kutokana na maandiko yangu ili jamii isiwe na shaka zaidi. tafadhali

"Ukisoma madras kuna somo linafunzwa linaitwa adabu ya elimu."
 
"Ukisoma madras kuna somo linafunzwa linaitwa adabu ya elimu."

Nadhani suala hili ni la Mohamed, kufuatana na maandiko yangu amejua tabia yangu. Tafadhali nijuze ili unisaidie na pia uiondolee jamii shaka juu yangu. Kuacha kama ulivyoandika hujaisaidia jamii ulioikusudia kunielewa. Nimeridhia ueleze unachokijua toka kwangu. Tafadhali.
 
Mohammed,
Nakushauri wakati unapomjibu mchangiaji kong'oli kwanza "Reply with quote" ili yule unayemjibu ajue unajibu thread gani. Hii itasaidia mtiririko wa mada.
 
Nimefuatilia mjadala huu na japo sijakisoma kitabu, nafikiri kitabu hicho kitafaa kusomwa. Na nitakisoma. Lakini nafikiri ulivyokiwakilisha hapa JF si kwa ajili ya kukitangaza tu ndio maana umekuwa ukitoa 'exerpts' ili kutupa kitu kama utangulizi hivi kwa sisi ambao bado hatujasoma.

Lakini pamoja na kwamba umepata support kutoka kwa baadhi ya watu ambao wamekisoma au hawajakisoma, kuna watu pia ambao kabla ya kuku-support au kuku-criticise bado wangependa kujibiwa masuali mawili au matatu kutokana na "exerpts" ulizoweka.

Sasa bahati mbaya majibu yako kuhusu hayo maswali yamekuwa yanakuja visivyo. Mimi naamini kama ulifanya utafiti na kupata data safi ungeweza kujibu tu hayo maswali. Kujibu hapa haimaanishi kuwa tutaacha kusoma kitabu chako. Sana sana ukijibu hapa utazidi kutupa morali zaidi wa kusoma hicho kitabu, of course pamoja na vingine.

Kutokana na kutojibu maswali ya ndugu Jasusi na ndugu Nguruvi3, mimi naomba nikuulize swali moja tu, no offense intended!

Kama mtafiti wa kihistoria, IS IT NOT POSSIBLE THAT YOU FIRST HAD YOUR OWN CONCLUSIONS BEFORE YOU GATHERED EVIDENCE?

Samahani kwa kuchanganya lugha.

Wapendwa,
Mtaona kwenye michango yangu katika thread hii, nimetoa wito wale ambao hawajakisoma kitabu hiki, wajitahidi kukisoma ili kumuelewa mwandishi na pia kupata ujumbe wa mtoa mada.

Hapo kwenye bold ndicho hasa kitu cha kujiuliza na pengine mtoa mada angeweka bayana ujumbe wake.

Kwa wale waliosoma kitabu, watakubaliana nami kuwa hicho kitabu hakina tofauti sana na Biographies nyingine kwa maana kinamhusu Adulwahid Sykes.Mwandishi yeyote wa biography anachofanya ni kutafuta "angle' ya "kumtoa" mlengwa wa hiyo biography. Kwa huyu Sykes kilichofanyika nionavyo mimi bila kuingia kwa undani katika politics za hiki kitabu ni kama ifuatavyo:

1. Kuonyesha mchango wa Familia ya Sykes katika harakati za kupigania uhuru

2. Kuonyesha kwamba Sykes pamoja na wakazi wa DSM ambao wengi wao wakati ule walikuwa Waislam walivyotokea kutoa michango yao mbalimbali katika harakati za uhuru ( tukumbuke DSM ndio yalikuwa makao makuu ya shughuli nyingi za kiutawala)

3. Kwamba waliona usomi wa Nyerere kama msaada utakaosaidia kufanikisha azma yao ( japo nashangaa walikuwepo akina Mwapachu wasomi wa Makerere wa enzi hizo na wametajwa katika kitabu! kwanini hawakuwapa hawa na wakampa Nyerere bado kwangu ni kitendawili!)Na hapa wanamlaumu Nyerere kwa kuwaacha katika kutambua Waislam kama wadau wakuu wa kuleta Uhuru! Huenda wanayo haki kudai hivi.

4. Kwamba akina Sykes ( three brothers) wakitokea Afrika ya Kusini kuja kukomboa Tanzania! Ina maana watanganyika by then walikuwa mabwege wasio na werevu wowote wa kudai haki zao hadi waje ma-TX? Hapa kwangu naona ni walakini..na pengine watajitokeza watanganyika wengine waandike historia kuziba pengo hili. Si tumeambiwa hiki kitabu kinalenga kusahihisha historia iliyopotoshwa?

Nitaishia hapa kwa sasa....mengi zaidi baadae!
WoS
 
Wapendwa,
Mtaona ........

Hapo kwenye bold ndicho hasa kitu cha kujiuliza na pengine mtoa mada angeweka bayana ujumbe wake...
...kudai haki zao hadi waje ma-TX? Hapa kwangu naona ni walakini..na pengine watajitokeza watanganyika wengine waandike historia kuziba pengo hili ...Si tumeambiwa hiki kitabu kinalenga kusahihisha historia iliyopotoshwa?

Nitaishia hapa kwa sasa....mengi zaidi baadae!
WoS

Thanks, WoS!

Bring more, whenever you can.
Bahati mbaya kwa sasa nipo kwenye kona za ajabu na mbali sana duniani siwezi kukipata hicho kitabu, ningekisoma sasa hivi. Hata hivyo nategemea nikirudi tu Tz kitakuwa kitabu cha kwanza kununua. Kumbe hao akina Sykes sio wazaramo? Looks like an interesting book.

Na labda kinaweza kikaamsha na waandishi wengine pia ambao watapenda kuandika biographies za mashujaa wetu mbambali.
 
Ahsanteni wachangajiaji wote. Sipendi kufanya mada hii kuwa ya majibishano kati yangu na Mohamed. Nimejitahidi sana kuwa muungwana kama ilivyo kawaida na nitajitahidi kuwa hivyo.

Mada inapoletwa hapa ipo wazi kwa kuchangiwa, kwa kukubaliana au kutokubaliana la msingi hoja, busara na hekima zitawale. Hivi ndivyo imekuwa tangu mada ilipoanza.

Kama alivyoeleza WomanofSubstance, inaweza kuwa mleta mada alikusudia kuandika wasifu (Biography) ya familia husika. Tufahamu kuwa hakuna wasifu unaojitosheleza bila ya kuwa na wahusika au vitu vinavyohusika. Ni katika maelezo hayo yakajitokeza maswali ya msingi kabisa ambayo mwandishi alikuwa na fursa ya kuyaeleza kikamilifu kuwasaidia wasomaji kama mimi.

Ni bahati mbaya kuwa hata pale wachangiaji walipojaribu kumuonyesha mapungufu (gap) yatokanayo, mwandishi alikuwa na dhana ya kushambuliwa. Hii ikamuondoa katika kusudio lake na akajikuta kwingine kabisa.(drawn in) na kupoteza lengo ima la 'biography' au 'history' kama alivyokusudia. Soma post # 123, #139, #141, #142 uone jinsi alivyotaharuki na kujichanganya ishara ya kuwa hakuwa tayari kutetea kile anachokijua.

Mwandishi alileta dibaji 'preface'' ili watu wasome, na tupo tuliosoma kitabu, sasa kuna ubaya gani kuhoji tusichokijua? Tunapohoji anakuja na majibu ya kushangaza. Mfano '' kwani nyie ndio wasemaji wa kanisa''. Mimi naweza kuwa mpagani, je sipaswi kusoma na kuhoji eti ni lazima niwe mkristo au Muislam.!!! Sihoji masuala ya kitaaluma kwa kuzingatia imani, ninatumia ufahamu. Leo wakristo wanahoji imani yao, Waislam wanahoji masuala ya imani yao, ni vipi mimi nisihoji hata la historia isiyozidi miaka 60.

Kama wasomaji mtafuatilia mtagundua kuwa hakuna mahali ilipohojiwa mada kwa njia ya kashfa ingawa yapo majibu ya kashfa. Mwandishi aelewe kuwa anapoleta mada hapa itajadiliwa na watu wenye upeo mbali mbali wa kuelewa na pengine ufahamu mzuri zaidi. Awe tayari kusimamia kile anachokiamini ni sahihi, awe tayari kukiri mapungufu, awe tayari kuleta hoja zenye uthibitisho na sio dhana. Kama mada hii aliikusudia kuifanya riwaya angetueleza mapema, midhali ameikusudia kama ''kurekebisha historia'' basi mada yake itafanyiwa kazi kikamilifu bila woga au kumuone haya. Jukumu la kulinda heshima yake ni lake mwenyewe bila kuvunja heshima za wengine.

Mwisho: Ndugu Mohamed Said, kwa kuelewa ''maandishi yangu yana ashiria tabia gani ''kama ulivyosema (post # 142) narejea kukuomba uifahamishe jamii kuhusu hilo bila kunipendelea, kunionea au kunionea haya. Kinyume cha hapo unaendelea kunidhalilisha kwa vile jamii ipo njia panda haijui tabia yangu kama walivyonizoea. Utanitendea haki kama utaifahamisha jamii mimi nina tabia gani ili jamii inihukumu. Kukaa kimya hakutanisadia mimi zaidi ya kuendelea kunivunjia heshima na dhalili, tafadhali, tafadhali sana wafahamishe.

Ahsante
Nguruvi3
 
Nguruvi

Naona kama alolengwa kwenye uandishi ni Ogah na post yake #137

Ndio yenye...........

Na CAPS
 
Kitabu kinaanza kwa kueleza baadhi ya koo maarufu za Dar es Salaam ya 1900 zilizokuwa
na ushawishi katika siasa za mji.

Akina Plantan, Sykes na Aziz Ally.

Kisha kinarudi hadi mwishoni kwa 1800 Mozambique kwenye kijiji cha Lukunyi kijiji ambacho
Von Wissman alikwenda kuchukua mamluki wa Kizulu kuja kupigana na wananchi wa Tanganyika
Bushiri bin Harith na Chifu Mkwakwa wa Kalenga.

Hapo ndipo unapokutana na askari wa Kizulu Kleist Mbuwane na shemeji yake Chifu Mohosh na kwa
pamoja wakaja na askari wengine 400 ndani ya manowari ya Kijerumani hadi Pangani na hapo ndipo
walipoanza vita dhidi ya wazalendo wa Tanganyika.

Kleist Sykes alizaliwa hapo Pangani 1894...

Katika hali ya kustaajabisha kabisa Kleist alitunza kumbukumbu za wazee wake na akaandika maisha yake.

Nyaraka hizi ndizo zilizotumiwa na John Iliffe wa Chuo Kikuu cha Cambridge kuandika historia ya African
Association katika miaka ya 1960.

Ni nyaraka hizi hizi na nyingine za ukoo wa Sykes ndiyo zilizoniwezesha na mimi kutafiti na kuandika historia
ya TANU nikipitia maisha ya mjukuu wa Sykes Mbuwane, marehemu Abdulwahid Sykes.

Baada ya kuchapa kitabu hiki kwa Kiingereza (Minerva Publishers, London 1998) wasomi wengi walivutiwa na kazi hii na nilipokea mialiko mingi kutoka sehemu tofauti kwenda kuhadhir kuhusu kitabu hiki na historia ya kupigania uhuru waTanganyika.

Yes in deed Nanren it is really a very interesting book.

Jaribu Amazon huenda wana nakala ya Kiingereza.
 
Umekwenda mbali sana.

Ikiwa umepata hisia kuwa nimetoka katika uungwana nakutaka radhi nisamehe.

Ninaposema mathalan mbona wenyewe Wakatoliki wako kimya sina maana kuwa nisiulizwe hapana.

Kinashonishangaza ni kuwa mbona hawa wanashikilia sana hilo ilhali mtuhumiwa mwenyewe yuko buheri wa hamsa ishirini hasemi kitu?

Mwisho ni kuwa unapoandika kutoka moyoni hamaki zikapanda hiyo inajulisha kuwa huyu ni mtu mwepesi wa kukasirika.

Mimi nikikaa darasani na wahadhiri wakiwadhihaki wazee wangu ati wamekutwa wakinywa kahawa na tende Nyerere akawaamsha.

Sikukasirika ila siku moja nikanyoosha kidole nikamwambia mwalimu wangu, "Je ushapata kumsikia mtu anaitwa Abdulwahid Sykes?"

Pazuri hapa kwa takriban robo saa nilimpa historia fupi ya TANU nikitoka kutoka mtu hadi mtu pamoja na mchango wa babu yangu Salum Abdallah.

Nikamaliza kwa kusema hawa wote niliokutajia hawamo katika historia ya uhuru wa Tanganyika lakini michango yao haina kifani.

Darasa zima lilikuwa kama limemwagiwa maji na hakika nilimuona mwalimu wangu kalowa. Akajizoazoa akaniuliza iwapo ninao ushahidi kwa yale niliyosema.

Nikamjibu kuwa sihitaji shahidi mimi ni kizazi cha watu hao waliopigania uhuru wa nchi hii. Baba yangu ni shahidi wangu yeye kayaona yote kwa jicho lake.

Kuanzia siku ile mwalimu yule akawa anahadhir kwa adabu. Nashukuru nilimwelewesha sisi Waswahili ni nani.

Sikuwa mtu wa kukasirika na hii kudai ushahidi kwangu utaona si kitu kigeni.

Na mimi wala sikumdai mtu ushahidi kwa historia iliyopotoshwa nikiiamini kuwa dawa ni kurekebisha kwa kuandika historia ya kweli. Hili nimelifanya na matokeo yake yako wazi kwa kila mtu kuona.

Watu hudhani hilo ni jambo kubwa sana kuwa "huna ushahidi" hivyo ulosema yote hayana maana.

Ushahidi kwa lipi mie hujisemea.
 
Samahani naomba nikuulize swali dogo tu kama muendelezo wa hii mada:

Katika kudai uhuru na kama sehemu ya historia, je, ukiacha waislamu, wengine waliobakia wakiwemo wakristo na wapagani hawakutaka kupata uhuru? Je walikuwa wanataka kubakia chini ya ukoloni?

Labda turudi nyuma kidogo kwenye hIstoria.Harakati za kudai uhuru hazikuanza na TAA wala TANU wala wakazi wa DSM.

Tunajua kabisa kulikuwa na mapambano dhidi ya Wajerumani -Mwenyewe umeandika kuwa ukoo wa Sykes ulikuja kama mamluki waliokodiwa na Wajerumani waje wapambane dhidi ya Wazawa Watanganyika waliokuwa wanadai uhuru wao dhidi ya Wakoloni ! Hii inatufundisha nini kwenye hii hii historia unayotaka kuiandika?

Je Uzalendo wa hawa akina Sykes uko vipi? Naamini kuwa mtu hawezi kuhukumiwa kwa makosa ya watu wengine na hivyo hivyo usiwahukumu baadhi ya Wakristo walioshindwa kujitokeza mstari wa mbele kudai uhuru!

Pili, je waliopambana kwenye vita vya majimaji wote walikuwa waislam? Si kweli pia walikuwepo wapagani? Kwanini mara zote tunapenda kuleta udini kwenye majadiliano yanayohusu Tanzania na historia yake?

Mimi binafsi napenda sana historia na inaelezea kwanini nilikuwa mmoja wa watu wa mwanzo kukisoma kitabu chako na kukienzi kama source ya habari za kihistoria.Inanisikitisha sana kuona kitabu sasa kinageuzwa silaha ya kupambana kidini badala ya KUBAKIA hazina ya maarifa.

Samahani kama nimesomeka ndivyo sivyo.

WoS
 
Kitabu hiki ni muhimu kwa Waislam na wananchi wote kwa ujumla kukisoma na kuwahimiza watoto wao nao wakisome wapate kujifahamu na kufahamu changamoto za udini na chanzo chake. Ndani ya kitabu hiki mwandishi amejitahidi kukusanya mashujaa waliotupwa waliopigania uhuru wa Tanganyika hata kabla hawajasikia jina la Nyerere wala kuona sura yake, wazalendo kama Hassan Suleiman na Juma Ponda wa Dodoma. Wazalendo waliohutubia mikutano ya hadhara na kuhamasisha watu kudai uhuru hata Nyerere hawamjui kama Titi Mohamed na wengine wengi kutoka katika majimbo ya Tanganyika. Ukikianza kitabu hiki huwezi kukiweka chini hadi umefika mwisho.

Kitabu hiki kinapatikana Ibn Hazim Bookshop Mtoro na Manyema na Tanzania Publishing House, Samora Avenue.

Mohamed,

Kwa kuzingatia umuhimu wa kitabu hiki, je unaweza kuweka 'soft copy' hapa JF ili hata tulio mbali na hayo maduka uliyoyataja tufaidike?

SMU
 
Hayo usemayo yote nimeyasema katika kitabu.

Uhuru wa Tanganyika umepiganiwa na mashujaa wengi lakini Waislam kote utakapokwenda ndiyo
walikuwa mstari wa mbele na sababu zake zipo nimezieleza kwa urefu katika kitabu.

Katika kitabu kuna kisa kizuri sana cha Joseph Kimalando kutoka Kilimanjaro na juhudi zake za kuipiga vita
TANU ingawa yeye alikuwa mmoja kati ya wale wazalendo 17 walioasisi TANU 7 Julai 1954. Utaona jinsi
alivyopambana na Yusuf Olotu mmoja wa waasisi wa TANU Kilimanjaro.

Mzee Olotu leo hakuwepo katika historia hadi kitabu hiki kilipomrejesha.

Mzee John Rupia nimemtaja sehemu nyingi. Kuanzia TAA 1950 hadi kufikia TANU 1954 wafadhili
wakubwa wa harakati walikuwa John Rupia, Abdulwahid Sykes, Ally Sykes na Dossa Aziz.

Baada ya 1954 ndiyo wakaingia wafadhili wengine kupitia Baraza la Wazee wa TANU chini ya uenyekiti
wa Sheikh Suleiman Takadir kama Mshume Kiyate, Mwinjuma Mwinyikambi, Mohamed Jumbe Tambaza nk.

Katika vitu vinavyonistaajabisha sana ni kuona jinsi Wakristo wanavyoiogopa historia hii. Ajabu ya Rahman.
Ukitaja tu historia hii basi hofu kubwa inakuja.

Hili nililijua mimi kwa mara ya kwanza mwaka 1987 wakati Usalama wa Taifa walipokusanya gazeti zima la
Africa Events (London) kwa kuwa ndani kulikuwa na makala yangu ikieleza mchango wa Waislam katika
uhuru wa Tanganyika.

Hapo ndipo nilipopata nguvu ya kujua udhaifu wa Nyerere kuwa ala! kumbe si simba kitu anaweza akatiwa hofu
na akaogopa!

Kwa kalamu tu wala si bunduki.

Nyakati hizi ni mpya usiogope haya.

Soma kitabu kisha zungumza.

Nakusihi kisome kitabu.

Ni njia nzuri uliyotumia ya ku-advertise kitabu chako.
 
Nimefuatilia mjadala huu na japo sijakisoma kitabu, nafikiri kitabu hicho kitafaa kusomwa. Na nitakisoma. Lakini nafikiri ulivyokiwakilisha hapa JF si kwa ajili ya kukitangaza tu ndio maana umekuwa ukitoa 'exerpts' ili kutupa kitu kama utangulizi hivi kwa sisi ambao bado hatujasoma.

Lakini pamoja na kwamba umepata support kutoka kwa baadhi ya watu ambao wamekisoma au hawajakisoma, kuna watu pia ambao kabla ya kuku-support au kuku-criticise bado wangependa kujibiwa masuali mawili au matatu kutokana na "exerpts" ulizoweka.

Sasa bahati mbaya majibu yako kuhusu hayo maswali yamekuwa yanakuja visivyo. Mimi naamini kama ulifanya utafiti na kupata data safi ungeweza kujibu tu hayo maswali. Kujibu hapa haimaanishi kuwa tutaacha kusoma kitabu chako. Sana sana ukijibu hapa utazidi kutupa morali zaidi wa kusoma hicho kitabu, of course pamoja na vingine.

Kutokana na kutojibu maswali ya ndugu Jasusi na ndugu Nguruvi3, mimi naomba nikuulize swali moja tu, no offense intended!

Kama mtafiti wa kihistoria, IS IT NOT POSSIBLE THAT YOU FIRST HAD YOUR OWN CONCLUSIONS BEFORE YOU GATHERED EVIDENCE?

Samahani kwa kuchanganya lugha.

Heshima kwako nanren,

Hapo kwenye nyekundu umenifilisi maneno ya kuandika

Wapendwa,
Mtaona kwenye michango yangu katika thread hii, nimetoa wito wale ambao hawajakisoma kitabu hiki, wajitahidi kukisoma ili kumuelewa mwandishi na pia kupata ujumbe wa mtoa mada.

Hapo kwenye bold ndicho hasa kitu cha kujiuliza na pengine mtoa mada angeweka bayana ujumbe wake.

Kwa wale waliosoma kitabu, watakubaliana nami kuwa hicho kitabu hakina tofauti sana na Biographies nyingine kwa maana kinamhusu Adulwahid Sykes.Mwandishi yeyote wa biography anachofanya ni kutafuta "angle' ya "kumtoa" mlengwa wa hiyo biography. Kwa huyu Sykes kilichofanyika nionavyo mimi bila kuingia kwa undani katika politics za hiki kitabu ni kama ifuatavyo:

1. Kuonyesha mchango wa Familia ya Sykes katika harakati za kupigania uhuru
2. Kuonyesha kwamba Sykes pamoja na wakazi wa DSM ambao wengi wao wakati ule walikuwa Waislam walivyotokea kutoa michango yao mbalimbali katika harakati za uhuru ( tukumbuke DSM ndio yalikuwa makao makuu ya shughuli nyingi za kiutawala)
3. Kwamba waliona usomi wa Nyerere kama msaada utakaosaidia kufanikisha azma yao ( japo nashangaa walikuwepo akina Mwapachu wasomi wa Makerere wa enzi hizo na wametajwa katika kitabu! kwanini hawakuwapa hawa na wakampa Nyerere bado kwangu ni kitendawili!)Na hapa wanamlaumu Nyerere kwa kuwaacha katika kutambua Waislam kama wadau wakuu wa kuleta Uhuru! Huenda wanayo haki kudai hivi.
4.Kwamba akina Sykes ( three brothers) wakitokea Afrika ya Kusini kuja kukomboa Tanzania! Ina maana watanganyika by then walikuwa mabwege wasio na werevu wowote wa kudai haki zao hadi waje ma-TX? Hapa kwangu naona ni walakini..na pengine watajitokeza watanganyika wengine waandike historia kuziba pengo hili ...Si tumeambiwa hiki kitabu kinalenga kusahihisha historia iliyopotoshwa?

Nitaishia hapa kwa sasa....mengi zaidi baadae!
WoS

Heshima kwako WoS, Bahati mbaya sijakisoma kitabu cha MS lakini tangu mwanzo nilitoa angalizo kwamba mjadala utajikita zaidi kwenye udini kwakuwa kitabu chake kakiandika kwa waislamu,wengine wasiokuwa waislamu wakisome ili kumnufasha kiuchumi mwandishi wa kitabu.
 
Wakati bado nakitafuta kitabu hiki nikisome, sio vibaya ningeongea ya kwangu machache, ninayoelewa kuhusu Nyerere na Elimu ya Tanzania.

Ni ukweli usiopingika, wakati wa ukoloni, nchi zote zilizotaswaliwa na Waingereza walifanya mtihani mmoja tuu wa Cambridge (GCE). Wote waliofaulu, walitoka shule za misheni, ukizingatia wWaisalmu wao walifundisha Madrasa tuu. Hata waislamu wote waliosoma na kuendelea, wamesomea shule za mishen.

Baada ya Uhuru, Nyerere akaelezwa kuwa wanapasi kwenda shule za serikali, wote ni Wakristu, tena wa maeneo fulani fulani, Kilimanjaro, Bukoba, Mbeya etc, Dodoma, Singida, Mtwara, Lindi hakuna, wote wanafeli.

Ndipo mwaka 1971, Waziri wa Elimu akiwa Elinawinga, Serikali ilitaifisha shule zote za misheni, ili Wailamu nao wawe huru kupata elimu na kusitisha matumizi ya mitihani ya Cambridge ili kila mkoa uwe na pass mark yake. Ni kuanzia hapo ndipo angalau watu wa Pwani, mwambao na Waislamu na watub wa makabila madogo madogo, wakaanza kuinukia kielimu. Kama sio Mwalimu, wasomi wote Tanzania, wangekuwa makabila fulani, na dini fulani.

Kwa mfano kabila la Wagogo wa Dodoma, ukiondoa wale waliokuwa mapadiri, kina Severino Supa etc, Wasomi wao wakuu wa kwanza ni Job Lusinde na mdogo wake John Malacela, na hawa waliweza kupata elimu hiyo baada ya kelelewa mission, pale Mvumi Mission. Wagogo wengine hawakupata bahati kama hiyo, wakati shule za serikali za Mazengo na Msalato, zikifurika vichwa vya Kihaya na Kichagga.

Pass rate ya kuingia sekondari ilibadilishwa kwa kila mkoas, kwa mikoa ambayo ni vichwa sana, ilibaki juu, na mikao ambao sio vichwa kama Singida na mikoa ya pwani, pass rate ilishushwa ndipo watu kama JK wakafanikiwa kupenya kielimu, vinginevyo ingekuwa ile ile, wengine tungeishia kuwasikia tuu.

Mimi binafsi nimesoma Ilboru, pale waliletwa wanafunzi toka familia masikini za Singida na Usukumani. Mwalimu Mkuu enzi hizo akiitwa Mushi kwa jina la utani BINO, alihakikisha wanafunzi hawa wanamaliza shule. Wengine walikuja wadogo kabisa, wakawa wanapatiwa mpaka maziwa fresh kila asubuhi.

Kutokana na hali duni za baadhi yao, tangu waliporipoti shule form 1, hawakuweza tena kurejea makwao mpaka wanemaliza form four. Uzoefu ulitlithibitisha kuna wengine wakirudi shule, hawaruhusiwa tena kurudi shuleni. Ni kwa mtindo huu, ndipo wanafunzi wengi wa Kiislamu waliweza kusonga mbele kielimu, vinginevyo wangeishia Madrasa tuu!.

Sasa kama haya yote Mwalimu aliyafanya, na watu hawayaoni, unategemea nini?. Waislamu wenye shukrani, watamshukuru sana Mwalimu, na wale wasio na shukrani, watalaaniwa.

Ngoja nikipata kwanza kitabu nikisome ndipo nikichambue kwa kina!.

Pasco.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom