Sina ugomvi na fikra yako na unavyoamini. Mimi nimendika kama nilivyoona katika utafiti.
Nyerere amesoma kitabu na akaombwa atoe maelezo yake.
Kwa nini hakufanya hivyo mimi siwezi kujua. Padri Sivalon kaandika kitabu
"Kanisa Katoliki na Siasa Tanzania Bara..." kaeleza yale niliyoeleza na mengine
makubwa na mazito.
Waislam tumeyasoma na imetuthibitishia dhana yetu.
Si Kanisa Katoliki wala Nyerere wametoa majibu.
Ikiwa wewe unataka kumjibia Nyerere na Kanisa Katoliki uhuru
huo unao na nitakusikiliza kwa makini.
Mohammed,
Hata kijitabu cha kasisi Sivalon ninacho. Lakini hakuna mahala kaandika kuwa kanisa la Katoliki lilihimiza au kuchochea kufutwa kwa EAMWS.
Hiyo ndiyo point yangu. Kama ulifanya utafiti toa basi ushahidi wa kuhusika kwa kanisa Katoliki katika kufutwa kwa EAMWS. Kama hakuna ushahidi basi kiri tu kuwa ni dhana yako tuendelee na mjadala. Nyerere kadhalika hakujibu kitabu cha Jumbe. Lakini hii haikifanyi kuwa factual badala ya opinionated.
Lakini wewe umejiannoint kuwa mwana historia lazima ukumbuke kuwa unabeba wajibu wa kuwa factual. Mimi siwezi kumsemea Nyerere na siwezi kulisemea kanisa Katoliki, lakini wewe umetoa allegation ya kuhusika kwa kanisa hilo una wajibu wa kutoa ushahidi. Tuendelee.