Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Mohamed Said, Mar 3, 2011.

 1. Mohamed Said

  Mohamed Said Verified User

  #1
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 10,765
  Likes Received: 5,759
  Trophy Points: 280
  MAISHA NA NYAKATI ZA ABDULWAHIS SYKES (1924 -1968)

  Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika na Mohamed Said

  Pitio la Kitabu

  Kitabu hiki kilipochapwa kwa mara ya kwanza 1998 kwa Kiingereza nchini Uingereza na kilipoanza kuzagaa katika maktaba na maduka ya vitabu mjini London yanayouza vitabu kuhusu Afrika Watanzania wengi waliokuwa Uingereza walisisimuliwa na yale yaliyokuwa ndani ya kitabu hiki. Kubwa zaidi ilikuwa kule kufunuliwa kwa mara ya kwanza kuwa kumbe TANU chimbuko lake si Julius Nyerere bali ni marehemu Abdulwahid Sykes. Hii ilikuwa habari mpya kwa wengi hasa ikizingatiwa kuwa Nyerere mwenyewe hakuwahi kumtaja Abdulwahid Sykes kama mwenzake katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. Hili lilikuwa la kwanza. Kitu cha pili kilichosisimua wasomaji ni kuwa mwandishi kwa kutulia kabisa alionyesha bila woga na kutafuna maneno kuwa TANU kilikuwa chama kilichojengwa katika migongo ya Waislam. Hili alilishaijisha kwa kueleza wazalendo waliokuwa bara ambao kwa umoja wao na wengi wao wakiwa Waislam walipambana na ukoloni wa Kiingereza.

  Kubwa zaidi la kusisimua ilikuwa kitabu kilieleza bila kupepesa macho au kutafuna maneno njama alizofanya Nyerere kwanza kumfuta Abdulwahid Sykes katika historia yake binafsi, TANU na katika harakati za kudai uhuru. Lakini kilichotibua sege la nyuki ni pale katika kuhitimisha kitabu mwandishi alipoweka wazi mipango ya Nyerere akishirikiana na Kanisa Katoliki baada ya uhuru kupatikana kupanga njama za kuzuia maendeleo ya Waislam. Katika kipande hiki msomaji atakutana na Mufti Sheikh Hassan bin Amir aliyekuwa mufti wa Tanganyika na Zanzibar na mwanasiasa shupavu. Msomaji ataziona juhudi za Sheikh Hassan bin Amir katika kupambana na njama za Nyerere na Kanisa Katoliki na nini kilimfika msomi huyu maarufu wa Kiislam. Kwa wakati ule Nyerere akiwa hai ilihitaji ujasiri mkubwa kwa yeyote yule kusema au kuandika hayo.

  Nakala za kitabu zilifika Tanzania na kila aliyesoma alipatwa na mshtuko mkubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na nje yake. Kitabu kiliwaudhi wapenzi wa Nyerere na wapo waliomwendea kwa kutaka afanye jambo kukomesha "uongo" wa mwandishi. Wengine hawakuamini kuwa huyo anayejiita Mohamed Said kama kweli yupo. Wengine walitaka kujua kama kweli akina Sykes na baba yao ndio waasisi wa vyama vya Waafrika katika Tanganyika katika 1929 hadi 1954 TANU ilipoasisiwa. Hii ilikuwa bahari kubwa kwa wapenzi wa Nyerere ambao wasingeweza kuogelea bila ya msaada wake Baba wa Taifa. Mawimbi ya bahari hii yalikuwa marefu na yakija kwa kasi. Juu ya haya yote Waswahili wana msemo "penye ukweli uongo hujitenga." Nyerere asingeweza kuthubutu kukana mchango wa marehemu Abdulwahid kwake yeye binafsi na kwa TANU. Abdulwahid ndiye aliyempokoea Dar es Salaam ile ya miaka ya 1950 na akamjulisha kwa wenyeji wa mji. Wapenzi wa Nyerere hadi leo ukiwauliza Nyerere alisema nini kuhusu ukweli kuwa si yeye aliyeasisi TANU wamekuwa kimya.

  Msomi maarufu wa Chuo Kikuu cha Cambridge John Illife ambae ameandika sana historia ya Tanganyika alikasirishwa na msimamo wa mwandishi khasa pale aliposema kuwa inastaajabisha kuwa Illife ingawa alitegemea nyaraka za akina Sykes katika kuandika historia ya African Association inastaajabisha hakuona umuhimu wa kutaka kumhoji marehemu Abduwahid aliyekuwa katibu na rais wake kati ya 1951 hadi 1953. Akiandika pitio la kitabu hiki katika Cambridge Journal of African History Illife alimshambulia mwandishi katika njia ambayo haikuwa staili yake msomi mkubwa kama yeye. Illife alikuwa ameghadhibishwa kwa kuambiwa katika kitabu kuwa alimzuia mwanafunzi wake katika Idara ya Historia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka wa 1969, Daisy Sykes ambae alikuwa binti ya Abdulwahid asiandike maisha ya baba yake. Daisy wakati huo msichana mdogo alikuwa amekasirishwa na jinsi TANU na magazeti yake yote, "The Nationalist" chini ya uhariri wa Benjamin Mkapa na "Uhuru" yalivyoshindwa kumwandika baba yake kwa hadhi aliyostahili. Magazeti hayo yaliripoti kifo cha Abdulwahid Sykes kwa kuwa Nyerere alikwenda mazikoni. Hapakuwa na jingine. Brendon Grimshaw ambae alikuwa Mhariri Mkuu wa "The Tanganyika Standard" na akimfahamu vyema Abdulwahid ndiye aliyendika tanzia ya maana katika "Sunday News" akasema kuwa Nyerere asingelifika pale alipofika kama si kwa msaada wa Abdulwahid Sykes na ni juhudi za ukoo wa Kleist ndiyo uliowezesha watu wa Tanganuyika kuwa na chama cha siasa. "The Standard" na "Sunday News" wakati ule lilikuwa gazeti huru halikuwa na hofu ya Nyerere. Hii ilikuwa mwaka 1968.

  Kilipotoka kitabu hiki mwaka 1998 walikuwepo watu walioona ukweli wa kuwa historia ya TANU bado haijaandikwa na kuna baadhi ya shutuma zilizoelekezwa kwake Nyerere ni muhimu yeye mwenyewe akazijibu akiwa hai kwa faida ya jamii isijesemwa kuwa kasingiziwa, walimsubiri afe ndipo wamzushie la kumzushia. Mmoja wa kundi hili la pili alikuwa marehemu Prof. Haroub Othman. Yeye alimkabili Nyerere uso kwa macho na kumuomba atoe majibu kujibu shutuma za waandishi wawili. Kwanza ajibu shutuma za Sheikh Ali Muhsin Barwani aliiyekuwa kiongozi wa Zanzibar Nationalist Party (Hizbu) katika kitabu chake "Conflict and Harmony in Zanzibar" na kitabu cha Mohamed Said "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (19241968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika." Sheikh Ali Muhsin akimtuhumu Nyerere kwa kupeleka mamluki Zanzibar kuipindua serikali ya wananchi na Mohamed Said akimtuhumu kwa chuki dhidi ya Waislam na kupotosha historia ya uhuru wa Tangnayika. Prof. Haroub alimshauri Nyerere kuwa njia nzuri ya kuiweka historia yake na uhusiano wake na Waislam sawa ni kwa yeye kuandika historia ya maisha yake. Hadi Nyerere anaingia kaburini hiili halikufanyika.

  Kitabu hiki ni muhimu kwa Waislam na wananchi wote kwa ujumla kukisoma na kuwahimiza watoto wao nao wakisome wapate kujifahamu na kufahamu changamoto za udini na chanzo chake. Ndani ya kitabu hiki mwandishi amejitahidi kukusanya mashujaa waliotupwa waliopigania uhuru wa Tanganyika hata kabla hawajasikia jina la Nyerere wala kuona sura yake, wazalendo kama Hassan Suleiman na Juma Ponda wa Dodoma. Wazalendo waliohutubia mikutano ya hadhara na kuhamasisha watu kudai uhuru hata Nyerere hawamjui kama Titi Mohamed na wengine wengi kutoka katika majimbo ya Tanganyika. Ukikianza kitabu hiki huwezi kukiweka chini hadi umefika mwisho.

  Kitabu hiki kinapatikana Ibn Hazim Bookshop Mtoro na Manyema na Tanzania Publishing House, Samora Avenue.
   
 2. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2011
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  naam kumekucha
   
 3. G

  Gathii Senior Member

  #3
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 164
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nimesoma article yako...sina jibu kwa sasa la jumla ila nafahamu kitu kimoja kuwa Imeandikwa Nyerere alipokelewa hapa Dar es salaam kama wakuja kutoka bara na wenyeji wakampa support kufika alipofika,mengine yanahitaji kwenda deep...nitafanya hivyo kisha nitarudi tena jamvini siku zijazo...mimi ni mkristu tena mkatoliki.
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Nitakitafuta baada ya kukisoma ndio nitapata la kuongea...
   
 5. JAPHET MAKUNGU

  JAPHET MAKUNGU Member

  #5
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  History has nothing to do with our present, but it helps in the future! -Malcom X.
   
 6. Mohamed Said

  Mohamed Said Verified User

  #6
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 10,765
  Likes Received: 5,759
  Trophy Points: 280
  Naam kumekucha.

  Sheikh Suleiman Takadir (Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU Makao Makuu, New Street Dar es Salaam) alikuwa akipanda jukwaani pale Mnazi Mmoja siku za mwanzo za TANU alikuwa anaanza na kibwagizo hiki: "Kwaaaacha!" (yaani kumekucha) na wananchi wana TANU wakijibu kwa pamoja: "Kweupeeee." Kisha anasoma dua halafu anamkaribisha Mwalimu Nyerere kuhutubia.

  Yote haya utayapata katika kitabu hicho.

  Hakika kumekucha.
   
 7. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako Mohamed said,

  Mzee wangu hii si mara ya kwanza kusoma habari za Abdulwahid Sykes hapa jamvini,mwaka jana ulikuja na hoja kama hii ikapigwa ban na mod kwasababu mjadala ulijikita zaidi kwenye udini sijui kama na hii itachukua mkondo kama ule wa mwanzo ni mapema mno kutabiri ingawa tayari nahisi kaharufu ka udini.
   
 8. MFUKUZI

  MFUKUZI JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 932
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  MOHAMED SAID!!! Sielewi unataka kuwaambia nini watanzania maana hueleweki. Hivi Nyerere kukiongoza TANU na kuongoza kudai uhuru unataka kutuambia waislamu wa kipindi hicho pamoja na wingi wao walihongwa na nyerere ili wamchague awe kiongozi na hatimaye kuwa Rais wa kwanza wa Tanzania.

  Unasema amedidimiza elimu ya waislam, kwanza hujatuambia kipindi cha hao wakina sykes shule za waislamu zilikuwa ngapi na za wakristo zilikuwa ngapi then useme nyerere alitaifisha shule za waislam na kuwapa wakristo.

  Lazima tujiulize, TAA kilianzishwa muda mrefu miaka ya 1920s kama sikosei na wengi wa wanachama wake walikuwa waislamu, hivi kwa muda wote huo hawakujua tanganyika ilikuwa chini ya ukoloni mpaka wakashindwa kudai uhuru mpaka wakamsubiri nyerere kukibadilisha TAA na kuwa TANU? ambapo ilimchukua nyerere miaka 7 kutoka 1954 - 1961 kuiletea tanganyika uhuru.

  Acheni kupotosha watu, udini hauwasaidii watanzania. mawazo yako ni mgando.

  SASA HIVI TUNATAKIWA KUIJENGE TANZANIA MPYA KWA KUPAMBANA NA MAFISADI NA KUTETEA RASILIMALI ZA NCHI YETU ILI ZIJE ZISAIDIE VIZAZI NA VIZAZI VYA TANZANIA IJAYO.

  WATU TUNATAKA KATIBA MPYA ITAKAYOKIDHI MAHITAJI YETU YA SASA NA MIAKA 100 IJAYO CHA KUSHANGAZA WEWE UNATAKA UTUREJESHE ETI KWENYE HISTORIA ILIYOSAHAULIKA. NATAKA NIKWAMBIE HAITUSAIDII KWANI HILO SI TATIZO LINALOTUTATIZA KWA SASA

  MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE

  ASLAAM ALEYKUM!!!!
   
 9. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ishu siyo historia tu kuna kitu ambacho waliokitunga wanakitaka. Badala ya kuzunguka na kupotezeana muda wangesema wanataka nini,
   
 10. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hapa ndiyo utaona mitanzania ovyo ovyo isiyopenda kujifunza, inayojifanya kujuwa kila kitu...wakati haina lolote....ukimuuliza mtu katika kitabu hicho kimeandikwa nini, hana jibu, atakwambia kamsikia profesa nani sijuwi au dokta nani sijuwi, yeye mwenyewe hajawahi kusoma hata utangulizi. Kitabu hicho hapo, kisome na mtu atowe maini kama alivyosoma na si kama alivyosikia. Hongera shk. Mohamed kwa kazi yako hii, Mungu akulipe kheri.
   
 11. Mohamed Said

  Mohamed Said Verified User

  #11
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 10,765
  Likes Received: 5,759
  Trophy Points: 280
  Hakika ilichukua miaka saba tu uhuru kupatikana. Je unajua sababu yake urahisi ule?

  Soma kitabu utakuta mengi ya kuelimisha na utajua kwa nini ilichukua muda mfupi hivyo Tanganyika kujigomboa na bila damu kumwagika.

  Siri ya mafanikio yale ni umoja wa wananchi na TAA katika umri wake wa miaka 21 ilikuwa imefanya kazi kubwa ya kujenga mwamko wa siasa wa Watanganyika.

  Lakini kinachoshangaza uhuru ulipopatikana walioandika historia wakasema TAA hakikuwa chama cha siasa bali cha "starehe" na hao waasisi wa siasa zile wakafutwa katika historia akabakia Baba wa Taifa peke yake.

  Kwa nini walitaka kuviza juhudi za waliowatangulia? Unajua sababu zake?

  Soma kitabu utapata mengi ya kunufaisha.
   
 12. Mohamed Said

  Mohamed Said Verified User

  #12
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 10,765
  Likes Received: 5,759
  Trophy Points: 280
  Bill Shankly,

  Liverpool Manager wa 1970s.

  Hajapatapo kuona manager kama yeye.

  Usitishike na hicho unachoita "udini." Mimi naandika historia kama ninavyoijua.
  Ikiwa wahusika wa jamvi hili wataona labda sielimishi na wakanipiga marufuku
  hiyo itakuwa bahati mbaya.

  Situkani wala sikejeli mtu.

  Napenda majadiliano tuondoe nakama inayokabili nchi yetu.
   
 13. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #13
  Mar 3, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,130
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  mi muislam pure lakiniiiiiiiiiii............
   
 14. G

  Gathii Senior Member

  #14
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 164
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sheikh mimi sijakuelewa nini kilichofichwa??

  Nyerere alipokelewa hapa Dar es salaam na wenyeji (ambao obviously wengi wakiwa waislamu kwa sababu za kihistoria zaidi) na akshirikiana nao mpaka Uhuru ulipopatikana..ukisoma kuundwa kwa TAA kunaonyesha wapi Nyerere alitoka na kina nani walimsaidia,embu niambie nini lichofichwa mzee?

  Na kwa hiyo nini unashauri sasa kama madai yako ni ya kweli.
   
 15. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2011
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  Mohammed Said strikes again. MODS naomba hii thread muilinde,they previous one mliifunga,naomba mtumie njia ya PM,kuwaonya distracters. Kuna mengi tulijifunza ambayo tulikuwa hatuyajui kwenye ile previous thread-many thanks
   
 16. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Historia hailazimishwi jamani...hawa kina Mohamed Said sijui wanataka nini maana hawako clear. Je mnataka historia ipi iandikwe upya mkuu? Mnataka neno "Waislam" liongezwe kwenye list ya wapigania uhuru au mnataka nini? Hamueleweki. Labda mkijipanga vizuri mkaja na hoja wahusika watawasikia kuliko ilivyo sasa. Kitabu chenyewe unasema kinauzwa kwa mtoro. Mimi kafir na mtoro wapi na wapi Sheakh? Mimi naona strategies zenu zipo weak na hayo mnayoyataka kwa stahili hii hamtafanikiwa. Badilikeni muwe Watanzania zaidi kuliko sasa mnaonekana wadini kwanza Utanzania baadae!
   
 17. Mohamed Said

  Mohamed Said Verified User

  #17
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 10,765
  Likes Received: 5,759
  Trophy Points: 280
  Ukisoma kitabu kwenye utangulizi na shukurani utamkuta marehemu Hassan Upeka (alikuwa TANU Intelligence toka 1956) akieleza jinsi alivyokataliwa kutoa "notes" za Abdulwahid Sykes kwa jopo lililokuwa likiandika kitabu: "Historia ya TANU 1954 hadi 1977 chini ya uongozi wa kada wa TANU/CCM Dr. Mayanja Kiwanuka.

  Marehemu Hassan Upeka yeye atakueleza kwa ulimi wake mwenyewe nini kilikuwa kinafichwa.

  Mimi sizungumzi hapo.
   
 18. Mohamed Said

  Mohamed Said Verified User

  #18
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 10,765
  Likes Received: 5,759
  Trophy Points: 280
  Mimi maisha yangu nikinunua vitabu Cathedral Bookshop (duka la vitabu la Kanisa Katoliki) ingawa ni Muislam.

  Vipi wewe unashindwa kununua kitabu Ibn Hazm Bookshop?

  Epuka hamaki utakuwa msomi makini na utaheshimika hata kwa wale ambao hawakubaliani na fikra zako.

  Hata hivyo kitabu kinauzwa vilevile Tanzania Publishing House (TPH).
   
 19. N

  Ndevu mbili JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 382
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kweli kumekucha.
  Mungu ampe maisha marefu pia azidi kuweka vizuri hiyo ta'arikh.
  Hicho kitabu nimetumiwa kutoka Nairobi nimejifunza historia ya Mwl Nyerer.
  Sh Moh'med Saidi mungu akupe afya na uzima .
  Kilinunuliwa Kshs 550/-
  Sijui huko Bongo.
   
 20. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0

  Kama vinauzwa Tanzania Publishing House (TPH) naweza kununua kule kwenu tatizo wakituona tu wanatushuku sio wenzao ndio maana hata kwenda mtu unashindwa!
   
Loading...