Ilyas Abdulwahid Sykes (Jaluo) ndani ya Maktaba

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,264
Picha hiyo huyo ni Ilyas Abdulwahid Sykes. Jina la utani udogoni tukimwita "Jaluo."

Kanitembelea nyumbani kwangu na hapa namwonesha Maktaba iliyohifadhi historia ya baba yake marehemu Abdulwahid Sykes.

Baada ya kifo cha baba yake Ilyas na kaka yake marehemu Kleist walikwenda kusoma Canada ambako baba yao mdogo Abbas Sykes alikuwa balozi.

Kleist alirejea nyumbani Tanzania lakini Ilyas yeye hakurudi.

Nimemwonesha katika Maktaba kitabu cha maisha ya Abdulwahid Sykes (1989) na kitabu cha maisha ya Julius Nyerere (2020) vikiwa pamoja; vitabu vya historia ya maisha ya marafiki wawili waliosimama bega kwa bega kupigania uhuru wa Tanganyika hadi ukapatikana 1961.

1696880876045.png
1696880985889.png

1696881061456.png

1696881086158.png

Asalaam, mtoa hoja hii maktaba yako unaruhusu kutembelewa?,au wapi unaweza kupata baadhi ya vitabu vyako?
 
Nkanini,
Hapa ni nyumbani kwangu ukija kama kunisalimia utaiona lakini si maktaba ya watu kusoma au kuazima vitabu.

Vitabu vyangu vinpatikana: Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa Mtoro, Manyema, Mtambani na KIchangani.
Shukraani mno mkuu,nitatembelea hizo sehemu ulizotaja, InshaAllah
 
Nkanini,
Hapa ni nyumbani kwangu ukija kama kunisalimia utaiona lakini si maktaba ya watu kusoma au kuazima vitabu.

Vitabu vyangu vinpatikana: Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa Mtoro, Manyema, Mtambani na KIchangani.
Definitely Mtambani ndio karibu mno na mimi
 
Nkanini,

Hapa ni nyumbani kwangu ukija kama kunisalimia utaiona lakini si maktaba ya watu kusoma au kuazima vitabu.

Vitabu vyangu vinpatikana: Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa Mtoro, Manyema, Mtambani na KIchangani.
Kwanini unaweka vitabu vyako maduka ya Misikitini tu? Huoni haja kaweka na kwenye maktaba za Makanisa Kama St. Joseph.
 
Why mkuu umpangie mwanadamu mwenzako maisha yake?,ni uamuzi wake na heshimu hilo, tunga vitabu vyako na kaviweke huko hakuna atakaye kuuliza why umeviweka hapo
 
The Apostle,
Haya maduka si ya misikiti lakini yalifunguliwa maduka haya jirani na misikiti kwa kuwa yalikuwa yanauza vitabu vya dini ya Kiislam na kuwa karibu na msikiti ni aula zaidi kuliko duka kuwa pengine popote.

Miaka ya nyuma wenye maduka ya vitabu walikuwa wakikiogopa kitabu cha Abdul Sykes.

Mimi siuzi kitabu mimi ni mwandishi kazi hiyo ni ya maduka ya kuuza vitabu na wao ndiyo wenye uamuzi wa kitabu kipi wanakitaka katika maduka yao.
 
Jabulani,
Kuna hotel niliiona Mbabane 1990 inaitwa Jabulani.

Ahsante.

Kwa miaka mingi sasa nafanya tafiti ya maneno ya lugha tofauti na asili yake (linguistic anthropology).

Neno Jabulani maana yake ni furahini (rejoice) kwa zawadi ya Mungu, lipo katika Kiarabu pia ""Jibran" likimaanisha hivyohivyo.

Mfano mwengine wa wazulu "Chaka" Zulu, hilo neno "Chaka" ni Sheikh.

Kuna mwandishi mzuri sana wa zamani wa Kilebanon anaitwa Khalil Jibran, ukipata kazi zake huyo utafaidi sana kwa mtu anaependa kujisomea,, halafu akiandika Kiarabu na Kingereza kiasi. Kazi zake nyingi zimetafsiriwa kwa lugha gtofauti tofauti.
 
Maalim Faiza,
Twaib.
 
Why mkuu umpangie mwanadamu mwenzako maisha yake?,ni uamuzi wake na heshimu hilo, tunga vitabu vyako na kaviweke huko hakuna atakaye kuuliza why umeviweka hapo
Povu linakutoka utafikiri umeulizwa wewe!
Angalia mleta Uzi - mkongwe, Mzee wetu Mohamed Said ailvyojibu kistaarabu.
 
Yeah huyo ndiye Nkanini, hazunguki na ku sugar coat issue, naisema as its, sorry kama unapendelea comments za kisiasa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom