Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

Huu ujanja wa kutaka kuwaongeza Wpagani katika Tanzania hauwezi kusaidia kitu kwa kuwa hawapo.

Kwa kweli ukitaka tuwe na mjadala mzuri ni lazima kwanza usome kitabu ujilete katika hali ya kujua.

Vinginevyo itakuwa tunazungushana humo kwa humo na hii haina tija.
 
Sheria ya kunakili hainiruhusu kufanya hivyo.

Hiki ni kitabu kilichochapwa na Phoenix Publishers Nairobi.
 
Mbogoni kitabu chake kiliruhusiwa kuingia nchini na maudhui ni hayo hayo lakini kitabu cha Hamza Njozi "Mwembechai Killings" kilipigwa marufuku ukikutwa nacho ni kosa la jinai na maudhui ni hayo hayo.

Labda nikuulize serikali inaogopa nini?

Sasa hizo nukuu za Mbogoni hazina maana yoyote ikiwa yeye ataruhusiwa kusema peke yake.

Waislam tunakijua kinachoogopewa.
 
Huu ujanja wa kutaka kuwaongeza Wpagani katika Tanzania hauwezi kusaidia kitu kwa kuwa hawapo.

Kwa kweli ukitaka tuwe na mjadala mzuri ni lazima kwanza usome kitabu ujilete katika hali ya kujua.

Vinginevyo itakuwa tunazungushana humo kwa humo na hii haina tija.

Pagan: definition-Not belonging to 0ne of the world's main religions. (collins dictionary)

Kwa taarifa ni kuwa enzi hizo za kupiginia uhuru dini za Uislam na Kikristo zilikuwa hazijaenea kama ilivyo sasa. Mathalani, nimekwenda mahali panaitwa west kilimanjaro huko hakukuwa na msikiti (1997). Nimefika sehemu za ndani pangani huko hakuna kanisa(2002)

Nenda maeneo ya Longido na serengeti utapata hali halisi iliyokuwepo 1950.

Kusema kuwa hakuna wapagani ni kupotosha umma kwa kiasi kikubwa. Mtu kuitwa Mohamed au John bado hakujamdhihirisha kuwa ana dini au ni muumini wa dini fulani. Fikiria kama unaitwa Mohamed na unapiga ramli na madogori uislam wako upo wapi. Kama unaitwa John na unaua albino kwa imani za kishirikina dini ipo wapi.

Kama tutasema ni uislam na ukristo tu ndio dini tunazozijua, vipi Buddha, Hindu tutawaweka wapi. Hata zama za kupiginia uhuru wapo wahindi na walikuwa na mchango wao hata kama ni wachache.

Nimeandika hili kupanua uwezo wetu wa kuifikiri tunapojenga hoja. Hoja iliyopo mbele ni kuwa je wapagani walikuwa na role gani katika kupigania uhuru. Kama ilikuwepo au la inapaswa kujibiwa na si kwa jibu jepesi kuwa enzi hizo hawakuwepo.

Once you engage into an intellectual discourse you must prepare for ups and downs, emotion will derail you from the gist. You must be well versed with technical terminology and be candid.
I have used the names Mohamed and John to make my point clear, it is not representing a name (s) of any one inside or outside this valuable discussion.
 
Bwana Saidi Mohamed, hebu angalia hiki kipande katika kitabu chako

Upon reaching Mwembe Togwa (now known as Fire) at the junction of (Ronald Cameroon Road (now United Nations Road) and Morogoro Road Mwalimu Nyerere met Mshume Kiyate.

Mwalimu Nyerere told Mshume Kiyate that he was going to Kariakoo Market to buy provisions but he did have a single sent in his pocket. Mshume Kiyate dipped his hand into his pocket and gave Mwalimu Nyerere two hundred shillings.

Nadhani hapo kwenye "sent" ulimaanisha "Cent", anyway swali langu ni hili, je Mwalimu alikuwa na Senti moja mfukoni au alikuwa hana Senti hata moja?.

Na kama alikuwa hana senti hata moja mfukoni , je alikuwa anakwenda kariakoo kununua provisions zipi?
Na kama alikuwa na senti moja tu, je kwa wakati huo angeweza kununua provisions zozote kiasi cha kumfanya afunge safari kwenda kariakoo?
 
Bwana Saidi Mohamed, hebu angalia hiki kipande katika kitabu chako

Nadhani hapo kwenye "sent" ulimaanisha "Cent", anyway swali langu ni hili, je Mwalimu alikuwa na Senti moja mfukoni au alikuwa hana Senti hata moja?.

Na kama alikuwa hana senti hata moja mfukoni , je alikuwa anakwenda kariakoo kununua provisions zipi?
Na kama alikuwa na senti moja tu, je kwa wakati huo angeweza kununua provisions zozote kiasi cha kumfanya afunge safari kwenda kariakoo?

Kumbuka, hizo zilikuwa enzi za neema na kuaminiana, yote yanawezekana, alikuwa na senti moja au alikuwa hana hata senti moja, its not an issue. Ulikuwa unaweza kwenda kutafuta provisions hata kama huna senti, kama mwenyeji wako ni mtu kama Abdulwahid Sykes, kwa enzi hizo, aaaahhhhh, inawqeza kuwa as simple as:

Nyerere: "Shikamoo Kaka"

Kiyate: "Marahaba Juliasi, habari za nyumbani?"

Nyerere: "habari za nyumbani, si njema bwana, nakwenda kutafuta chochote, lakini, mnhhh nna senti moja tu mfukoni.

Kiyate: "aaah, sisi kaka zako tupo wewe una wasiwasi gani, usijali kabisa bwana, mbona mambo madogo tu, shika hizi, wewe bwana kashughulikie zile barua za kupeleka kwa gavana bwana, haya mambo ya nyumbani tuachie sisi"
 
Ahsante sana.

Hivyo ulivyoandika khasa ndiyo ulikuwa mstakbali wa enzi zile.

Kuna mzee mmoja akiitwa Abdallah. Yeye alikuwa ndiyo messenger wa Abdulwahid pale sokoni Kariakoo
anasema yeye kwa mkono wake alikuwa anachinja kuku hadi 20 anapeleka nyumbani kwa Abdu kwa ajili
ya chakula cha waheshimiwa.

Anasema wakati ule wakubwa wengi katika siasa za kikoloni wakienda kwa Abdu kwa hili na lile. Watu kama
Chifu Kidaha Makwaia, Dunstan Omari, Stephen Mhando, Mangi Mkuu Thomas Marealle, Zuberi Mtemvu, Chifu Msabila Lugusha,
Chifu Abdallah Said Fundikira, Wilbard Mwanjisi, Dr. Vedasto Kyaruzi nk.

Ndiyo maana haikuwa ajabu kuwa Nyerere alipofika Dar es Salaam 1952 ilibidi na yeye aingie nyumba ile akatambulishwe
kwa Abdulwahid Sykes Rais wa TAA.

Ile nyumba ndiyo yalikuwa makazi ya Rais wa TAA. Ndiyo ilikuwa "Ikulu" yao kwa wakati ule.

Mimi nimeonyeshwa hadi chumba alichokuwa akilala Nyerere. Awali chumba kile kilikuwa cha Abbas Sykes lakini kaka yake
akamuhamisha kumpisha Nyerere. Abbas wakati ule ndiyo alikuwa kijana mdogo wa kutumwa dukani.

Nyumba hii ilijengwa na na baba yake Abdu Mzee Kleist mwaka 1942 baada ya kustaafu Tanganyika Railway na
kwa hadhi ya wakati ule ilikuwa nyumba ya kupendeza sana ina mabomba ya maji, umeme na sakafu ya sementi.

Hiki kipindi kina historia nzuri sana na kwa hakika tungelifaidi sana kama Nyerere mwenyewe angetulezea walichokuwa
wakijadili mle ndani wakati ule.

Hapa palikuwa pangu nyumba hii naingia mlango wa mbele Mtaa wa Aggrey natokea mlango wa uani Mtaa wa Sikukuu.

Nilipokwenda kwa Ally Sykes kuomba majalada na kumbukumbu za TAA na TANU niandike historia ya marehemu Abdu
kwangu haikuwa shida niliaminika wala sikutiliwa shaka labda nimetumwa na mashushushu.

Hii ndiyo "advantage" kubwa sana niliyonayo ukinifananisha mimi na watafiti wengine.

Nilikuwa na muamana.
 
Singependa kujadili sana kuhusu hilo hata hivyo nayaheshimu mawazo na fikra zako.
 
Nafikiri Mzee Nyerere alikua anaogopa zaidi udini kuliko dini ya Kiislamu.....nafikiri mawazo yake yalikua kwamba hichi kitabu kingeamsha waislamu kuwafanya wahisi wanahaki zaidi ya watu wengine (wakristu+dini nyengine/aethists) katika jamhuri kwani wao ndio waliochangia zaidi...hili sasa lingeleta mtafaruku na ndilo aliloogopa...vut=rugu za kidini!!

Nyerere hakuogopa dini ya ki islam hata kidogo.Aliogoga dhambi ya ubaguzi na kubaguana kwa kufuata dini,kabila,rangi,itikadi za kisiasa na uwezo wa kipato.Labda kuna points sijazipata vizuri.

Sijaelewa objective ya mjadala huu ni nini. Kitabu kama kitabu ni kizuri tu na kinatusaidia kuzidi kuelewa historia ya ukombozi wetu. Sidhani kama kuna mtu anabisha kwamba hao wazee wetu wa ki islam(pamoja na wale wa kikristo +kipagani nk) walichangia kwa kiasi kikubwa kuutoa ukoloni. Nachotafakali mimi,then what?.

Tunazitafakari juhudi zile positively or negatively? Kumbuka nchi ya America ki historia ni ya wahindi wekundu. Mbona leo hii anawatawala mtu mwenye asili ya kenya - Africa. Kwa wenzetu historia haihusiani sana na maendeleo ya mtu/nchi. Huwa wanamini uwezo wako wa kufanya kazi/kuongoza nio huleta maendeleo yako binafsi na nchi ki u jumla,si dini yako,rangi wala kabila lako.

Huyo nyerere anayesemwa mdini aliwahi kugombana na askofu wa kikristo pale askofu alipotaka kumtetea mgiriki mmoja(naye mkristo)aliyesema serikali yote kaiweka mfukoni. Nyerere huyohuyo alikuwa akienda mara kwa mara kuombewa dua na rehema kwa ma sheikh wa ki islam(fuatilia hotuba zake).
 
Mbogoni kitabu chake kiliruhusiwa kuingia nchini na maudhui ni hayo hayo lakini kitabu cha Hamza Njozi "Mwembechai Killings" kilipigwa marufuku ukikutwa nacho ni kosa la jinai na maudhui ni hayo hayo.

Labda nikuulize serikali inaogopa nini?

Sasa hizo nukuu za Mbogoni hazina maana yoyote ikiwa yeye ataruhusiwa kusema peke yake.

Waislam tunakijua kinachoogopewa.

Hujajibu hoja. Hoja ni madai yako kwamba EAMWS ilipigwa marufuku kwa shinikizo ya kanisa Katoliki. Hapa unaruka na kusema kitabu cha Mbogoni kiliruhusiwa kuingia lakini cha Njozi kilipigwa marufuku. Nimevisoma vyote. Kitabu cha Mbogoni ni more rational wakati kitabu cha Njozi kina ushabiki wa Kiislamu zaidi.

Maudhui ni tofauti. Na kuhusu wapagani ni kweli idadi yao imekuwa inapungua kutokana na kazi zinazofanywa na shule, makanisa na misikiti.

Niliposoma shule kule Musoma, miaka ya 60 nusu ya wanafunzi walikuwa wapagani, lakini leo wengi ni Wakristo au waislamu baada ya kwenda shuleni. Lakini jibu hoja kuhusu kanisa Katoliki na EAMWS.
 
Naona watu mmeanza kuhariri kazi ya mtu...........kazi nzuri so far
 
Hujajibu hoja. Hoja ni madai yako kwamba EAMWS ilipigwa marufuku kwa shinikizo ya kanisa Katoliki. Hapa unaruka na kusema kitabu cha Mbogoni kiliruhusiwa kuingia lakini cha Njozi kilipigwa marufuku. Nimevisoma vyote. Kitabu cha Mbogoni ni more rational wakati kitabu cha Njozi kina ushabiki wa Kiislamu zaidi. Maudhui ni tofauti. Na kuhusu wapagani ni kweli idadi yao imekuwa inapungua kutokana na kazi zinazofanywa na shule, makanisa na misikiti. Niliposoma shule kule Musoma, miaka ya 60 nusu ya wanafunzi walikuwa wapagani, lakini leo wengi ni Wakristo au waislamu baada ya kwenda shuleni. Lakini jibu hoja kuhusu kanisa Katoliki na EAMWS.

Jee, umekisoma kitabu tajwa kwenye hii mada?
 
Umekisoma hicho kitabu hata ukatoa comments hizo hapo juu? Soma halafu ueleze ni page gani na gani mwandishi amemaanisha udini.

Naanza kuona kwamba muandishi wa kitabu ha shabikii udini bali ana very scientific marketing strategy ya kuuza kitabu chake. Hii si mbaya sana kwenye mbinu za utafutaji masoko!
 
Jee, umekisoma kitabu tajwa kwenye hii mada?

Itakuwa bora kama utasoma kitabu kwanza na kisha ndiyo utoe maoni. Nimeeleza matatizo yalianza toka 1963 na hapa ukienda katika kitabu utakutana na Sheikh Hassan bin Amir akieleza njama zilivyoanza na jinsi na yeye alivyojaribu kupambananazo. Elewa kuwa huyu ndie alikuwa Mufti wa Tanganyika na Zanzibar na mchango wake kwa Nyerere na TANU hauna kifano.

Utamkuta Bilal Rehani Waikela (yu hai na Allah ampe umri mrefu. Amin) anaeleza mipango waliyopanga ndani ya EAMWS kupambana na fitna za Kanisa Katoliki dhidi ya kujengwa kwa Chuo Kikuu cha Waislam.

Utasoma maungamo ya Shaban Kayugwa (State Intelligence 1960s) aliyuhusika katika kukamilisha fitna ile. Nini aliwaeleza Waislam kabla mauti hayajamfika.

Mwisho utamkuta Bibi Titi Mohamed ndani ya Kamati Kuu ya TANU alivyotoleana maneno na Nyerere na Titi akamwambia Nyerere "Mimi namuogopa Allah simwogopi yoyote." Ugomvi wao ni kuwa Titi alikuwa anapinga kufungiwa kwa EAMWS akisema imekuwapo kabla ya TANU na ina manufaa makubwa kwa Waislam na Uislam na Nyerere akishinikiza EAMWS ivunjwe.

Mwisho utamsikiza mrehemu Hamza Azizi aliyekuwa IGP wakati ule nini alinambia mimi na wengine ili aende kwa Mola wake akiwa ana radhi ya Allah.

Utamsoma Godfrey Sawaya aliyekuwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai alivyokuwa akitisha Waislam viongozi wa EAMWS.

Ukisoma haya yote kwa ukamilifu wake utakuwa katika nafasi ya kuzungumza utakacho.
 
Jee, umekisoma kitabu tajwa kwenye hii mada?
Ndiyo nimeshakisoma hicho kitabu hata ninayo nakala hapa nyumbani kama nilivyo na nakala ya kitabu cha Mbogoni na Judith Listowell. Lakini jibuni hoja. Onyesheni ni wapi kanisa Katoliki lilihusika katika kufutwa kwa EAMWS.
 
Itakuwa bora kama utasoma kitabu kwanza na kisha ndiyo utoe maoni. Nimeeleza matatizo yalianza toka 1963 na hapa ukienda katika kitabu utakutana na Sheikh Hassan bin Amir akieleza njama zilivyoanza na jinsi na yeye alivyojaribu kupambananazo. Elewa kuwa huyu ndie alikuwa Mufti wa Tanganyika na Zanzibar na mchango wake kwa Nyerere na TANU hauna kifano.

Utamkuta Bilal Rehani Waikela (yu hai na Allah ampe umri mrefu. Amin) anaeleza mipango waliyopanga ndani ya EAMWS kupambana na fitna za Kanisa Katoliki dhidi ya kujengwa kwa Chuo Kikuu cha Waislam.

Utasoma maungamo ya Shaban Kayugwa (State Intelligence 1960s) aliyuhusika katika kukamilisha fitna ile. Nini aliwaeleza Waislam kabla mauti hayajamfika.

Mwisho utamkuta Bibi Titi Mohamed ndani ya Kamati Kuu ya TANU alivyotoleana maneno na Nyerere na Titi akamwambia Nyerere "Mimi namuogopa Allah simwogopi yoyote." Ugomvi wao ni kuwa Titi alikuwa anapinga kufungiwa kwa EAMWS akisema imekuwapo kabla ya TANU na ina manufaa makubwa kwa Waislam na Uislam na Nyerere akishinikiza EAMWS ivunjwe.

Mwisho utamsikiza mrehemu Hamza Azizi aliyekuwa IGP wakati ule nini alinambia mimi na wengine ili aende kwa Mola wake akiwa ana radhi ya Allah.

Utamsoma Godfrey Sawaya aliyekuwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai alivyokuwa akitisha Waislam viongozi wa EAMWS.

Ukisoma haya yote kwa ukamilifu wake utakuwa katika nafasi ya kuzungumza utakacho.
Yote hayo tisa. Mimi nimeuliza swali moja tu. Ushahidi uko wapi kwamba kanisa Katoliki lilihusika katika kupigwa marufuku kwa EAMWS? Kumbuka kitabu chako ni rekodi.

Na kama rekodi imekosewa vizazi vijavyo vitayachukulia hayo makosa kama ni ukweli isipokuwa kama kuna mtu atajitokeza kuyasahihisha makosa hayo hivi sasa. Kubali kuwa ni dhana yako tu kwamba kanisa Katoliki lilihusika katika upigaji marufuku wa EAMWS na siyo fact.
 
Sina ugomvi na fikra yako na unavyoamini. Mimi nimendika kama nilivyoona katika utafiti.
Nyerere amesoma kitabu na akaombwa atoe maelezo yake.

Kwa nini hakufanya hivyo mimi siwezi kujua. Padri Sivalon kaandika kitabu

"Kanisa Katoliki na Siasa Tanzania Bara..." kaeleza yale niliyoeleza na mengine
makubwa na mazito.

Waislam tumeyasoma na imetuthibitishia dhana yetu.

Si Kanisa Katoliki wala Nyerere wametoa majibu.

Ikiwa wewe unataka kumjibia Nyerere na Kanisa Katoliki uhuru
huo unao na nitakusikiliza kwa makini.
 
Ikiwa unahitaji ushahidi wa mahakama itabidi Waislam waende mahakamani.

Iwe iwavyo historia imeandikwa na Waislam leo wanajua.

Ingekuwa vizuri endapo Nyerere na Kanisa Katoliki lenyewe wangejibu maana ndiyo watuhumiwa
mimi sijakutuhumu wewe.

Ndiyo maana Prof. Haroub Othman alimuomba Nyerere ajibu shutuma kwenye kitabu changu ili Waislam
wajue ni kwa nini aliipiga marufuku EAMWS ni kwa woga, husda na fitna ya kuwa Waislam wakiwa na
Chuo Kikuu na zile shule walizokuwa wakijenga nchi nzima kwa msaada wa Aga Khan watatoa changamoto
kwa kanisa au palikuwapo na jingine?

Hofu kuwa Waislam wakisoma watachukua uongozi wa nchi?
 
Yote hayo tisa. Mimi nimeuliza swali moja tu. Ushahidi uko wapi kwamba kanisa Katoliki lilihusika katika kupigwa marufuku kwa EAMWS? Kumbuka kitabu chako ni rekodi. Na kama rekodi imekosewa vizazi vijavyo vitayachukulia hayo makosa kama ni ukweli isipokuwa kama kuna mtu atajitokeza kuyasahihisha makosa hayo hivi sasa. Kubali kuwa ni dhana yako tu kwamba kanisa Katoliki lilihusika katika upigaji marufuku wa EAMWS na siyo fact.

Hivi katika fikra zako, Nyerere kwa jema lipi alilofanya atake kupewa u Saint? ukilieleza hilo utapata jibu, na ukishindwa kulieleza tutakupa jibu.
 
Similar Discussions

12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom