Kwenye Uongo Ukweli Utatafutwa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,268
KAMARA KUSUPA: PENYE UONGO UKWELI UTATAFUTWA

Kitabu cha Abdul Sykes.

Ukweli ni kuwa katika vitabu vyote vilivyoandikwa kuhusu historia ya TANU hakuna hata kitabu kimoja unachoweza kufananisha na kitabu hiki.

Vitabu hivyo vyote vimekufa vikiwa na umri mchanga na hakuna kilichochapwa toleo la pili.

Vyote vimechapwa mara moja kisha vikajifia.

Katika vitabu hivyo waandishi hawakuwa na ujasiri wa kumkabili Ally Sykes kumhoji kuhusu historia ya TANU lau hakuna ambaye hakuwa anajua kuwa chama cha African Association kiliasisiwa na baba yake na yeye Ally Sykes na marehemu kaka yake ndiyo waliompokea Julius Nyerere 1952 na wakawanae ndani ya TAA na kuasisi TANU mwaka wa 1954.

Kitabu cha Abdul Sykes ndicho kilichoeleza kuwa baada ya kuundwa kwa African Association kikaundwa chama kingine kuitia nguvu African Association - Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933.

Kitabu cha Abdul Sykes ndicho kilichowataja waasisi wa vyama hivi kwa majina moja baada ya lingine wakafahamika.

Kuanzia siku ile kitabu hiki kilipoingia Tanzania mwaka wa 1998 historia ya uhuru wa Tanganyika ikabadilika.

Kitabu hiki kinazungumzwa hadi leo huu mwaka wa 25.

Kitabu cha Abdul Sykes hakijakufa sasa kinakwenda toleo la tano kwa Kiingereza na Kiswahili.

Haingii msomaji ndani ya kitabu cha Abdul Sykes akatoka kama alivyoingia.

Baada ya kuchapwa kitabu hiki Kleist Sykes akaingizwa katika Dictionary of African Biography (DAB) pamoja na wanae wote watatu - Abdulwahid, Ally na Abbas wakawa sehemu ya historia ya Tanzania na historia ya Afrika.

Hizi ni volume 6 zilizochapwa na Oxford University Press, New York (2011).

Mwaka wa 2011 katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika Abdulwahid na Ally Sykes wakatunukiwa Medali ya Mwenge wa Uhuru.

1697517519214.png

1697517566115.png

1697517592510.png

1697517658521.png
 
Back
Top Bottom