Kisutu: Kesi ya Erick Kabendera yaendelea. Jamhuri yaweka kisiki Erick kushiriki msiba wa mama yake mzazi

Kwani alizaliwa peke yake? Lini mshitakiwa aliwahi ruhusiwa kwenda kwenye mazishi? Au hii iwe special kwa huyu, mwandishi habari? Wakulima je? Wafugaji je?
Tusiishie kusikitika, tuepuke kujiingiza kwenye mambo ya kujitakia. Kulikuwa na kila njia ya kuachana na hayo lakini naona alijivunia ushujaa.
Tusiwe kama uncivilized society in a modern world kwani akiruhusiwa kumzika mama yake itaipunguzia nn jamhuri?
 
Mkuu tetea uovu maana uko mezani kwa mfalme na sahani yako imejaa mlo wa kutosha, na namna nzuri ya huo mlo ili uweze kushuka utakavyo ni pamoja na kujenga hoja ya kuutetea huo uovu. Hata akina Mwigulu, Nape, Januari nk walikuwa wanatetea uovu enzi za JK wakiwa mezani kwenye mlo kama ww. Ila hiyo warmup inayowakuta hivi sasa akili imewarudia.
Huyo ni anasapoti lolote linalofanywa na serikali' huyo huyo kabendera akiteuliwa atasifia. Usijichoshe
 
Kwani alizaliwa peke yake? Lini mshitakiwa aliwahi ruhusiwa kwenda kwenye mazishi? Au hii iwe special kwa huyu, mwandishi habari? Wakulima je? Wafugaji je?
Tusiishie kusikitika, tuepuke kujiingiza kwenye mambo ya kujitakia. Kulikuwa na kila njia ya kuachana na hayo lakini naona alijivunia ushujaa.
Mahakama Bado Haijathibitisha Kama Jamaa Alifanya Hayo Wewe Tayari Ushaweka Conclusion.

Alijiona Shujaa Akifanya Hayo, Nan Kahakikisha Kama Kafanya Maana Hata Wanaomtuhumu Bado Wanachunguza,

WEWE UMEJUAJE KAMA KAFANYA NA ALIJIONA SHUJAA??

Jifunze Kuweka Akiba Ya Maneno, Yaliyomkuta Huyo Jamaa Hata Wew Yanaweza Kukukuta Hapo Ukachukuliwa Ukakaa Ndan Baadae Wakakwambia Hauna Kesi.

Inawezekana Umelelewa Kwenye Maisha Ya Pilau Sisi Wa Mtaani Tunajua Kadhia Ya Kubambikiwa Vitu Ili Ukomolewe.

Yangu Ni Hayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama huyu amekufa kutokana uonevu na kubambikiwa kesi kwa mwanaye. Hata hivyo bado na mambo hayo mabaya kutendeka, bado hata huruma kwa Kabendera haipatikani busara ya kwenda kumuaga mama yake mzazi. Huruma ipo kwa wabakaji, watuhumiwa wa uhujumu uchumi, majangili, wauwaji na wala si wabambikiwaji wa kesi za kisiasa kwa sura ya utakatishaji wa fedha.

Watesi na wadhulumaji wa haki za msingi wapo katika mikono salama ya Ibilisi. Kwa kuwa;
1. They are used already
2. They are misused by evil powers
3. They start to be abused
4. Indeed, they will end up be confused and perish to hell.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani alizaliwa peke yake? Lini mshitakiwa aliwahi ruhusiwa kwenda kwenye mazishi? Au hii iwe special kwa huyu, mwandishi habari? Wakulima je? Wafugaji je?
Tusiishie kusikitika, tuepuke kujiingiza kwenye mambo ya kujitakia. Kulikuwa na kila njia ya kuachana na hayo lakini naona alijivunia ushujaa.
Anaweza ruhusiwa au kutoruhusiwa,maana huyo si'mfungwa bali ni mshtakiwa aliyeko mahabusu.

Please just give yourself a minute and think twice. " Where Shall I be by this TIME Tomorrow???????"
 
Mahakama imempa pole Mwandishi wa Habari za uchunguzi, Erick Kabendela kwa kufiwa na Mama yake mzazi, Verdiana Mujwahuzi huku ikiyapinga maombi yake ya kutaka kwenda kushiriki Ibada ya mazishi ya mama yake.

Hiyo imebainika leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati Kabendera anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha alipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kesi yake kutajwa.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amemueleza Hakimu Mkazi, Janeth Mtega kwamba Jamhuri inampa pole Kabendera kwa kufiwa na Mama yake mzazi.

Wankyo amedai kuwa maombi ya Kabendela kupitia mawakili wake yamewasilishwa wakati ambao si sahihi kwa sababu mahakama haina mamlaka na pia Mkurugenzi wa Mashitaka hajaipa kibali ya kusikiliza kesi hiyo.

Kukataliwa kwa Kabendera kushiriki mazishi ya Mama yake, kumeibuka kutokana na maombi aliyoyatoa Kabendera kupitia Mawakili wake akiwemo Jebra Kambole.

Wakili Kambole amedai wanaiomba mahakama hiyo imruhusu Kabendera akashiriki Ibada ya Mazishi ya Mama yake mzazi katika Kanisa la Roman Katoliki lilipo Changombe majira ya mchana.

Kambole ameieleza mahakama kuwa suala la kushiriki sala ya mwisho ya msiba ni haki ya Binadamu, suala la faragha. "Kushindwa kuudhuria maziko ya Mama yake tutakuwa tumemuadhibu adhabu kubwa tena kwa kuangalia uhusiano wa mshitakiwa na mama yake mzazi kwani alikuwa akimuuguza na ni vizuri akatoa heshima ya mwisho,"ameeleza.

Wakili Jebra amedai kuwa ni muhimu kwa Kabendera kushiriki kwa sababu Mama mzazi ni mmoja, akifa anaagwa mara moja.

Baada ya kutoa hoja hizo, Hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi saa 8:45 mchana kwa ajili ya kutoa uamuzi kama Kabendera ashiriki Ibada ya mazishi ya Mama yake mzazi ama lah.

Mama Kabendera alifariki dunia Desemba 31, 2019 ikiwa ni wiki kadhaa baada ya kumuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amsamehe mtoto wake.

Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu ikiwemo la utakatishaji wa Sh.Mil 173.
 
Kwani alizaliwa peke yake? Lini mshitakiwa aliwahi ruhusiwa kwenda kwenye mazishi? Au hii iwe special kwa huyu, mwandishi habari? Wakulima je? Wafugaji je?
Tusiishie kusikitika, tuepuke kujiingiza kwenye mambo ya kujitakia. Kulikuwa na kila njia ya kuachana na hayo lakini naona alijivunia ushujaa.
Vipi hao washtaki wakiwa kwenye hali hio mara pa wamepigiwa Simu mama zao wako mochwari wamepata ajali vipi wataendelea na kesi ?
 
Mungu ndiye aliyesema tiini sheria za wanadamu na tiini wenye mamlaka! Huyu kavunja sheria ina maana kavunja amri ya Mungu na wanadamu. Sasa unaposema Mungu atakulipia mi sikuelewi.
 
Kila mtu angependa Erick akahudhulie msiba wa Mama yake......bila kujali kuwa tuhuma anazotuhumiwa ni kweli au siyo kweli.

Je kuna sheria yoyote au kifungu kinaweza kumpa mahabusu nafasi ya kwenda kumzika mpendwa wake?
 
Kwani alizaliwa peke yake? Lini mshitakiwa aliwahi ruhusiwa kwenda kwenye mazishi? Au hii iwe special kwa huyu, mwandishi habari? Wakulima je? Wafugaji je?
Tusiishie kusikitika, tuepuke kujiingiza kwenye mambo ya kujitakia. Kulikuwa na kila njia ya kuachana na hayo lakini naona alijivunia ushujaa.

Kwani ameisha patikana na hatia ya hayo unayomshutumu? Au unataka kutuambia kuwa hayo yanayoendelea mahakamani ni maigizo tu maana tayari alishapatikana na hatia na kinachosubiriwa ni hukumu tu?

Amandla......
 
Please just give yourself a minute and think twice. " Where Shall I be by this TIME Tomorrow???????"
It doesn’t matter legality is already reasonable to take care of such thinking!
Anaweza ruhusiwa au kutoruhusiwa,maana huyo si'mfungwa bali ni mshtakiwa aliyeko mahabusu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeuliza. Huwainaruhusiwa? Je, imewahi tokea? Au tuanze na huyu anayeonekana ni mtu mashuhuri?
 
Kwani alizaliwa peke yake? Lini mshitakiwa aliwahi ruhusiwa kwenda kwenye mazishi? Au hii iwe special kwa huyu, mwandishi habari? Wakulima je? Wafugaji je?
Tusiishie kusikitika, tuepuke kujiingiza kwenye mambo ya kujitakia. Kulikuwa na kila njia ya kuachana na hayo lakini naona alijivunia ushujaa.
Bado sijajua sheria zetu tz zinasemaje kuhusu hili, nadhani DPP atakuwa ana play part kubwa hapa, na hata kama ikimuhusisha DPP still itachukua muda mrefu zaidi kumuandikia DPP kuhusu hiyo issue, but kwa humanitarian reasons nadhani itawezekana. Hii issue inanikumbusha tukio lililotea Kenya last yr mwanamke aliyetuhumiwa kumuua mume wake (marehemu alikuwa raia wa nje), aliruhusiwa kwenda kwenye mazishi na mahakama licha alikuwa mtuhumiwa mahabusu.

Saa 14:45pm mahakama itakutana tena kutoa maamuzi kuhusu hili, ngoja tusubiri tuone.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom