Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 5,897
- 10,358
Awali:
Erick Kabendera mwandishi wa Kujitegemea wa Habari za uchunguzi inaendelea leo Mahakama ya Kisutu.
Kabendera anashtakiwa kwa Makosa matatu ikiwemo kukwepa Kodi, Utakatishaji Fedha na kujihusisha na genge la uhalifu.
UPDATES
MAHAKAMA YAOMBWA KABENDERA KUMUAGA MAMAKE
HOJA SITA ZA UPANDE WA UTETEZI KWANINI KABENDERA APEWE RUHUSA KUSHIRIKI MAZIKO YA MAMA YAKE
Jopo la mawakili wa Mwandishi wa habari wa kujitegemea Erick Kabendera, wakiongozwa na Wakili Jebra Kambole wamewasilisha hoja sita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Janet Mtega kwa mshitakiwa kupatiwa ruhusa chini ya ulinzi ili aweze kushiriki Katika maziko au kutoa heshima za mwisho kwa mama yake aliyefariki hivi karibuni.
1. Kutoa heshima za mwisho ni haki ya msingi ya binadamu. Wakili ameeleza kuwa Kabendera ana haki ya kuwa na kuheshimu familia pamoja na haki ya faragha hivyo kuna umuhimu kwa Kabendera kushiriki Katika kutoa heshima za mwisho kwa mama yake.
2. Erick Kabendera anatakiwa adhaniwe kuwa hajatenda kosa mpaka pale mahakama itakapothibitisha kuwa ametenda kosa na kumzuia kushiriki mazishi itakuwa ni adhabu ya Kinyama kwa Kabendera.
3. Tangu Mshitakiwa amekamatwa hajaonesha nia ya kutoroka au kutaka kufanya vurugu hivyo hakuna uwezekano wa mtuhumiwa kutoroka Kama atapatiwa ruhusa
4. Mashitaka anayokabiliwa nayo mshitakiwa hayahusiani na uvunjifu wa amani hivyo Mahakama itilie maanani ombi Hilo
5. Kama Mahakama ilitoa amri aende mahabusu hivyo Mahakama Ina uwezo wa kuamua ombi hilo kwani kama mshitakiwa pia aliweza kupelekwa mahakamani haitashindikana kumpeleka kanisani kumuaga mama yake.
6. Ruhusa ya Kabendera kuhudhuria mazishi Jamhuri haiwezi kuathirika
MAJIBU YA UPANDE WA SERIKALI
Jamhuri yampa pole nyingi kwa msiba wa mama yake mzazi, Bibi Verdiana Mjwahuzi. Pia Jamhuri imepinga hoja za utetezi wakidai Mahakama haina Mamlaka wala DPP hajaipa mamlaka ya kutoa maamuzi hayo.
Wakili wa Serikali, Simon Wankyo amesema...
"Hata sisi tuna masikitiko makubwa na tunampa pole nyingi Kabendera kwa kufiwa na mama yake mzazi, lakini mahakama isifungwe mikono kwa maombi yaliyowasilishwa ya kutaka mshtakiwa kushiriki Msiba.”
Mheshimiwa Hakimu katika macho ya kisheria mahakama yako haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo kwa sababu kesi hii ni ya uhujumu uchumi, licha ya kuwa hata sisi tuna masikitiko makubwa lakini tunaiomba Mahakama yako isifungwe mikono.”
Soma:
Tanzia: Mama mzazi wa Mwandishi Erick Kabendera, Verdiana Mjwahuzi amefariki dunia leo Jumanne Desemba 31, 2019
Mama mzazi wa mwandishi Erick Kabendera, Verdiana Mjwahuzi amefariki dunia leo Jumanne Desemba 31, 2019. Amefariki akiwa Hospitali ya Amana alikokuwa akip Soma pia: Mama Mzazi wa Erick Kabendera amuomba Rais Magufuli kumsamehe mwanae
www.jamiiforums.com