Kisutu: Kesi ya Erick Kabendera yaendelea. Jamhuri yaweka kisiki Erick kushiriki msiba wa mama yake mzazi

Tunatawaliwa na serikali ya kibabe na katili sana. Ukitaka uthibitisho, liangalie suala la Kabendera, ombi la mama yake kwa Rais, na sasa msimamo wa serikali kupitia mawakili wake baada ya kifo cha mama. Ni ukatili wa kutisha, Yaani ni kama tuko kwa akina Pinotchet wa Amerika ya Kusini!!!
 
Kwani alizaliwa peke yake? Lini mshitakiwa aliwahi ruhusiwa kwenda kwenye mazishi? Au hii iwe special kwa huyu, mwandishi habari? Wakulima je? Wafugaji je?
Tusiishie kusikitika, tuepuke kujiingiza kwenye mambo ya kujitakia. Kulikuwa na kila njia ya kuachana na hayo lakini naona alijivunia ushujaa.
Hujui ulisemalo
 
Mkuu tetea uovu maana uko mezani kwa mfalme na sahani yako imejaa mlo wa kutosha, na namna nzuri ya huo mlo ili uweze kushuka utakavyo ni pamoja na kujenga hoja ya kuutetea huo uovu. Hata akina Mwigulu, Nape, Januari nk walikuwa wanatetea uovu enzi za JK wakiwa mezani kwenye mlo kama ww. Ila hiyo warmup inayowakuta hivi sasa akili imewarudia.
Hakuna sababu ya kuwasha waliolala kwa kuvimbiwa.. Subiri kidogo.. Mwisho wao njiani.
 
Tatizo kina watu wanadhani serikali inaendeshwa kwa huruma na kuombewa na kusaidiana. Ikiwa ni hivyo nani angekuwa gerezani?
Kwa civilized society sheria ubadilika kulingana na wakati pia kulingana na mazingira.Possible mfungwa au mtuhumiwa kuwezapewa mda wa kumzika mpendwa wake,jela ni ya wote,yeyeto kuanzia raisi hadi mpiga debe anawezaingia.
 
Tatizo kina watu wanadhani serikali inaendeshwa kwa huruma na kuombewa na kusaidiana. Ikiwa ni hivyo nani angekuwa gerezani?
Ukiongea hivyo msamaha wa magufuli wa walioba hela wakiri wenyewe waachiwe sio huruma?
 
Atleast jamhuri na mahakama wamfute Kabendera hayo machozi anayojifuta hapo, show that you care for a second guys, mruhusuni huyu mtu akamuage mama yake, anaumia vibaya sana hapo alipo, itakuwaje mkimnyima ruhusa halafu mwisho wa siku msimkute na hatia? mtaweza kumrudisha mama yake akamuage?...

Hebu onesheni ubinadamu wenu kwenye hili, sisi binadamu tunatofautishwa na wanyama kwa sababu hiyo, tuna huruma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeshasema mshtakiwa kwa maana bado hajakutwa na hatia.
Vipi ikitokea akaachiwa huru kwa kukosekana ushahidi wa kumtia hatiani.
Usiwe unajitoa ufaham tu mwenzio amefiwa na bi mkubwa wake!

Sent using Jamii Forums mobile app

ha ha unavyosema na kubishana na hawa wasio na majina halisi, ni kama wanaweza kusaidia kitu??

yaani ubishi wako ukifikia ukashinda au JF woote wakakubaliana kuwa Erick aende msibani, NDIO inakuwa hivyo??

tunapenda sana ubishi usio na tija wala matokeo
 
Kwani alizaliwa peke yake? Lini mshitakiwa aliwahi ruhusiwa kwenda kwenye mazishi? Au hii iwe special kwa huyu, mwandishi habari? Wakulima je? Wafugaji je?
Tusiishie kusikitika, tuepuke kujiingiza kwenye mambo ya kujitakia. Kulikuwa na kila njia ya kuachana na hayo lakini naona alijivunia ushujaa.
Ushahidi uko wapi unaoonesha yule jamaa alitenda hayo? Umesoma wapi yule mwandishi ni mfungwa kahukumiwa?
 
Hamna kesi hapo bali kinachofanyika ni kumkomoa kisa ni mkosoaji wa rais. Mahakama inatumika kama sehemu ya kukomoa watu wanaoikosoa mamlaka
Noma sana
IMG_20200101_073028.jpeg
 
Back
Top Bottom