Labani og
JF-Expert Member
- Sep 15, 2020
- 15,776
- 24,211
Klabu ya Simba imetozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la mashabiki wake pamoja na walinzi wake wa uwanjani (stewards)kupanga njama na kufanikisha azma ya kuingia uwanjani na kufanya vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina wakati mchezo dhidi ya Mashujaa Fc ukiendelea kwenye uwanja wa Azam Complex Machi 15, 2024.
Walinzi wa uwanjani (stewards) wa klabu ya Simba, Kessy Mohamed, Mrisho Mindu Pamoja na Mohamed Salmin pamoja na shabiki aliyefahamika kwa jina la Mohamed Saleh, wamefungiwa kuingia viwanjani kwa kipindi cha miezi 12 (kumi na miwili) kwa kosa la kushiriki katika tukio la mashabiki kuingia uwanjani wakati mchezo tajwa hapo juu ukiendelea.
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inaendelea na uchunguzi wenye lengo la kufahamu wahusika wengine wa tukio hilo ambao hawakutambulika mara moja ili wachukuliwe hatua kali za kikanuni.
Klabu ya Simba inawajibika kuhakikisha mashabiki na viongozi walioadhibiwa wanatii adhabu zao na kuzitekeleza kikamilifu ili kuepuka adhabu zaidi kwa klabu.
#NBCPL