TFF kemeeni na toeni adhabu Kali Kwa mashabiki na wachezaji wanaotoa mataulo na kufukua langoni Kwa timu pinzani.

man dunga

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
3,216
5,566
Ligi yetu inakua ila baadhi ya wachezaji na mashabiki bado Wana fikra za kipuuzi na za kizamani. Ni upuuzi kwenye ligi kuu ya nchi kuwa na wachezaji wanaoamini goli halipatikani sababu ya taulo la kipa au kuna vitu vimefukiwa.Hayo mambo ni ya timu za mtaani. Ajabu zaidi hata zinazojiita timu kubwa za Simba na yanga bado zina wachezaji wanaoamini ushindi unaweza kuzuiwa na taulo la kipa au vitu kufukiwa.

Toeni adhabu Kali sio hivyo vimilioni . Pia toeni adhabu Kwa klabu ambayo shabiki au mchezaji atafanya huo upuuzi.

Kuwa na wachezaji aina hii taifa haliwezi kusonga mbele maana hawawezi kujituma wakiamini ulozi ndio unawakosesha ushindi. Pia mashabiki wanaofanya huo upuuzi ni wale ambao ujinga bado haujawatoka yaani elimu ndogo sasa hao dawa yao ni kuwapeleka tu hata polisi tu walale hata wiki kwa kosa la kuingilia mchezo.
 
Naunga mkono hoja.
 
Mkuu sitetei ushirikana ila hawa wachezaji wanaonana kwenye nguvu za giza, wangeletwa wale waganga wa kujua uchawi na kukaguliwa kabla ya mechi ungeshangaa wachezaji wote 22 na benchi zao wasingeingia uwanjani.

Mtu kama siyo mchawi anajuaje kwenye taulo au golini imechimbwa kitu?
 
Nimeshangaa kwa nini hukukemea wanaoweka vitu, ambao wakiacha automatically wengine watakosa vya kutoa. Jana baada ya kutoa sindano tu langoni goli zikasoma. La sivyo ingekuwa droo.
Uchawi watu wanatumia sana kwenye soka. Niliwahi kuambiwa Yanga wakiwa na mechi mkoani basi wanaagiza waganga wa mkoa huo wafanyie kazi. Mechi ya Simba na Yanga zinachezwa sana kwa waganga, ndio maana utasikia Yanga kagoma kupita geti kuu.

Haiwezekani mkigoma tunamuoma kafukia kitu pale halafu tutulie tu wakati goli haliingii. Watu wasitumie uchawi, ila ukitega inabidi uteguliwe tu hakuna namna
 
Uanzishwe utaratibu mpya. Waamuzi wanapoingia uwanjani mwanzoni mwa mchezo kukagua uwanja wanapokagua sehemu ya magoli, waangalie dalili zozote za udongo au nyasi kutifuliwa na ikibidi wafukue kuona kama kuna mavitu yamefukiwa. Wafanye hivyo pia kabla kipindi cha pili hakijaanza.

Pia camera ikinasa tukio lolote la kufukiwa au kufichwa kitu, mwamuzi asimamishe mchezo, akatoe kilichofukiwa na adhabu apewe huyo aliyefukia.
 
Nimeshangaa kwa nini hukukemea wanaoweka vitu, ambao wakiacha automatically wengine watakosa vya kutoa. Jana baada ya kutoa sindano tu langoni goli zikasoma. La sivyo ingekuwa droo.
Uchawi watu wanatumia sana kwenye soka. Niliwahi kuambiwa Yanga wakiwa na mechi mkoani basi wanaagiza waganga wa mkoa huo wafanyie kazi. Mechi ya Simba na Yanga zinachezwa sana kwa waganga, ndio maana utasikia Yanga kagoma kupita geti kuu.

Haiwezekani mkigoma tunamuoma kafukia kitu pale halafu tutulie tu wakati goli haliingii. Watu wasitumie uchawi, ila ukitega inabidi uteguliwe tu hakuna namna
Hivi vitu kama sindano,pete ,cheni si haviruhusiwi uwanjani?pete mtu anaweza kusahau,sindano anapeleka wapi uwanjani,alifaa kupewa kadi
 
Nimeshangaa kwa nini hukukemea wanaoweka vitu, ambao wakiacha automatically wengine watakosa vya kutoa. Jana baada ya kutoa sindano tu langoni goli zikasoma. La sivyo ingekuwa droo.
Uchawi watu wanatumia sana kwenye soka. Niliwahi kuambiwa Yanga wakiwa na mechi mkoani basi wanaagiza waganga wa mkoa huo wafanyie kazi. Mechi ya Simba na Yanga zinachezwa sana kwa waganga, ndio maana utasikia Yanga kagoma kupita geti kuu.

Haiwezekani mkigoma tunamuoma kafukia kitu pale halafu tutulie tu wakati goli haliingii. Watu wasitumie uchawi, ila ukitega inabidi uteguliwe tu hakuna namna
Wanaofukia pia sio wa kuwakalia kimya , wakikamatwa pia adhabu kali iwahusu lakini kuhalalisha kufukua kisa umemuona anaefukia sio Sawa sababu hakuna ushahidi kuwa kufukua ndio kumeleta goli. Timu gani haistahili kupata sare ya 0-0? Nani anajua muda gani goli linapatikana ndani ya DK 90? Atakaeonwa anafukia suluhisho sio kwenda kufukua bali ni mamlaka kuchukua hatua Kali. Uchawi WA Simba na yanga kama upo mbona dhidi ya akina Al Ahly haufanyi kazi tangu enzi za akina Lunyamila?
 
Back
Top Bottom