Kibu na Mzamiru watozwa faini ya Sh. 1,000,000 kwa Ulozi

Boss la DP World

JF-Expert Member
Dec 12, 2021
1,997
7,552
Wachezaji wa klabu ya Simba, Kibu Denis na Mzamiru Yassin wametozwa faini ya Sh. 1,000,000 kila mmoja kwa kosa la kuondoa taulo la mlinda mlango wa Coastal Union litilokuwa limewekwa pembeni ya lango wakati mchezo ukiendelea, jambo lililoashiria imani za kishirikina.

FB_IMG_1710416107645.jpg
 
View attachment 2934330
Ni kosa la ulozi au utovu wa nidhamu? Sasa wao wanajuaje kama kufanya hivyo ni ulozi ? au kamati inatumia kigezo kujua kuwa mchezaji akitoa taulo golini ni ulozi ?
 
Wachezaji wa klabu ya Simba, Kibu Denis na Mzamiru Yassin wametozwa faini ya Sh. 1,000,000 kila mmoja kwa kosa la kuondoa taulo la mlinda mlango wa Coastal Union litilokuwa limewekwa pembeni ya lango wakati mchezo ukiendelea, jambo lililoashiria imani za kishirikina.

View attachment 2934330
Shida 🦁 hawa na ulozi damu damu,na imani na sayansi ya michezo imewapitia kando.😁
 
Hivi Feisal Salum juzi juzi naye si alimzinga kipa sikumbuki wa timu gani kuhusu taulo? Na yeye adhabu yake iko wapi?
 
Hiyo timu na wachezaji wake wana historia ya kipekee kwenye suala zima la imani za kishirikina. Kwenye mechi yao dhidi ya Platinum ya Zimbabwe kuna shabiki wao aliingia uwanjani na paka kubwa jeusi kwa ajili ya kuwaroga wapinzani.

Mechi dhidi ya Wasauzi kule Bondeni walitaka kuuchoma moto uwanja wa watu, kisa tu uchawi! Na mwisho wa siku CAF wakawapiga faini ya dola elfu 10!

Mechi yao dhidi ya Raja Casablanca msimu uliopita, dereva wa timu akiwa amewabeba wachezaji kwenye basi la timu alirudi kinyume nyume kwa umbali mrefu; huku akihatarisha usalama wa wachezaji! Kisa tu imani za kishirikina.
 
Sasa mnacheka nini kuhusu simba hivi nyie mna akili kweli? Mmewasahau wachezaji wenu kina mzize na Job?? Ila ukiwa utopolo na akili inaisha kabisa...
Yani wanajifanya wao sio makonkodi kwa mechi 2 mfululizo...
 
Utopolo aisee yani nimecheka sanaaa kweli nyie na majini yenu ni wa kutoa maneno kuhusu Simba haha wazee na waanzilishi wa vitaulo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom