Kisa cha usaliti baina ya Lowasa na rafikiake kinasisimua Sana. Miaka ijayo kitaigizwa kwenye filamu. Ni kisa cha Maisha

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,895
Kwema Wakuu!

Kisa cha Lowasa na Rafikiake na usaliti mkubwa uliotokea ni kisa kitakachoishi kwenye taifa hili kwa karne na karne.
Huwaga visa vya usaliti na mapenzi vinadumu sana. Historia na Historia zitapita lakini visa vya usaliti havipiti kwani ni visa vya maisha.

Kisa cha Yesu na Yuda ni maarufu na kitaendelea kudumu miaka na miaka kwa sababu kinahusisha. Usaliti.
Kisa cha Adamu na Hawa dhidi ya kumsaliti Mungu kipo mpaka hivi Leo.
Kisa cha Samsoni na Delilah halikadhalika.

Legacy pekee ambayo mwanadamu ataacha ni kuishi kwa wema na Upendo na watu.

Madaraja, mahospitali, viwanda, na miundombinu yoyote unayoiona hivi leo haijawahi na haitakuja kuwa Legacy na kumbukumbu ya maana kwa sababu miaka miambili ijayo vyote vitakuwa vimepitwa na wakati. Vitabomolewa na kujengwa upya na vitaitwa kwa majina mengine na kutumiwa na wahusika wengine.

Visa vya usaliti vinadumu sana kwa sababu vinahusu nafsi na maumivu ya mwanadamu.
Unapofanya usaliti mkubwa sio tuu utamuumiza yule uliyemsaliti bali utaumiza mioyo ya wanadamu wengine ambao hata ambao hawajawahi kukuona. Vile kusikia stori ya usaliti wenu jina lako linakuwa limeharibika.

Utakuwa na jina moja tuu, alikuwa mtu mbaya, msaliti.

Miaka ijayo tukiwa hatupo, kisa hiki cha Lowasa na Rafikiake kitaigizwa na vijana na zama hizo. Sio ajabu hata majina ya waigizaji yatakayotumika yakawa majina ya wahusika wa sasa waliokatika maisha yetu.

Ukishakuwa msaliti tayari wewe ni mtu aliyepata hasara kubwa ya maisha. Hasa unapomsaliti mtu wako wa karibu aliyekuamini na aliyekupenda.

Tatizo la usaliti Mkubwa ni ngumu sana kuomba msamaha.
Ni kama shetani na Mungu. Usaliti Mkubwa unajikuta unaamua tuu kuwa msaliti na kiburi cha kushindwa kuomba toba kinakuwa ndio maisha yako.

Jumapili njema
 
Usaliti hufuta mema yote.
Msaliti hanaga msamaha popote pale zaidi ya yule aliyemkosea.
Hasa usaliti Mkubwa
Jakaya hakuwa rafiki wa lowasa na genge lake la wafanyabiashara nyuma yake,Bali baada ya laana ya Nyerere kwa lowasa wakaona wamtumie jakaya kwa malengo yao ya baadae,jakaya ni mtu wa Dola, Nyerere alimtaka achukue form ya urais ili kumdhibiti profesa malima aliyekua islamist,maana wajumbe nec kule CCM wanatoka idadi sawa bara na visiwani,na wakati huo vuguvugu la uislam lilipamba moto
Lowasa tamaa zake ndizo zilimkaanga,hakutaka fursa ya kufua umeme impite,japo hata Kama Richmond isingetokea lowasa asingepewa fursa ya kuwakilisha CCM Wala kutangazwa mshindi wa uchaguzi
 
Hakuna sehemu nimesema au kumtaja huyo Rafiki wa Lowasa. Sijajua nini kimekushawishi kudhani jakaya anahusika kwenye huu uzi
 
Kwema Wakuu!

Kisa cha Lowasa na Rafikiake na usaliti mkubwa uliotokea ni kisa kitakachoishi kwenye taifa hili kwa karne na karne.
Huwaga visa vya usaliti na mapenzi vinadumu sana. Historia na Historia zitapita lakini visa vya usaliti havipiti kwani ni visa vya maisha.

Kisa cha Yesu na Yuda ni maarufu na kitaendelea kudumu miaka na miaka kwa sababu kinahusisha. Usaliti.
Kisa cha Adamu na Hawa dhidi ya kumsaliti Mungu kipo mpaka hivi Leo.
Kisa cha Samsoni na Delilah halikadhalika.

Legacy pekee ambayo mwanadamu ataacha ni kuishi kwa wema na Upendo na watu.

Madaraja, mahospitali, viwanda, na miundombinu yoyote unayoiona hivi leo haijawahi na haitakuja kuwa Legacy na kumbukumbu ya maana kwa sababu miaka miambili ijayo vyote vitakuwa vimepitwa na wakati. Vitabomolewa na kujengwa upya na vitaitwa kwa majina mengine na kutumiwa na wahusika wengine.

Visa vya usaliti vinadumu sana kwa sababu vinahusu nafsi na maumivu ya mwanadamu.
Unapofanya usaliti mkubwa sio tuu utamuumiza yule uliyemsaliti bali utaumiza mioyo ya wanadamu wengine ambao hata ambao hawajawahi kukuona. Vile kusikia stori ya usaliti wenu jina lako linakuwa limeharibika.

Utakuwa na jina moja tuu, alikuwa mtu mbaya, msaliti.

Miaka ijayo tukiwa hatupo, kisa hiki cha Lowasa na Rafikiake kitaigizwa na vijana na zama hizo. Sio ajabu hata majina ya waigizaji yatakayotumika yakawa majina ya wahusika wa sasa waliokatika maisha yetu.

Ukishakuwa msaliti tayari wewe ni mtu aliyepata hasara kubwa ya maisha. Hasa unapomsaliti mtu wako wa karibu aliyekuamini na aliyekupenda.

Tatizo la usaliti Mkubwa ni ngumu sana kuomba msamaha.
Ni kama shetani na Mungu. Usaliti Mkubwa unajikuta unaamua tuu kuwa msaliti na kiburi cha kushindwa kuomba toba kinakuwa ndio maisha yako.

Jumapili njema
Dhambi ya usaliti imeitafuna hadi familia yake. Nina hakika watoto wao wanafahamiana kutokana na uhusiano mkubwa walikuwanao wazazi wao. Je, msibani walienda? Kwa mtu mzima mwenye Kariba yake haipendezi kusutwasutwa kila wakati. Nilimuona akijitetea kwenye msiba wa JPM, nadhani kwa Lowassa hakupewa nafasi.
 
Hakuna sehemu nimesema au kumtaja huyo Rafiki wa Lowasa. Sijajua nini kimekushawishi kudhani jakaya anahusika kwenye huu uzi
na wewe pia wacha unafki kwani wasaliti na wanafki ni watu wa aina moja tanuri lao la moto ni moja...rafiki yake lowassa ni jakaya why uwe mnafki kwenye hilo!!!
hufanani na unafki mzee
 
Mimi sijaona usaliti wowote hapo.

Urais haugaiwi Kwa vigezo vya urafiki,

Na Rais aliyepo madarakani,Hana final say kuhusu nani awe Rais baada yake Nchi hii.

Ni sawa tu na watu walioanza compaign za Urais kabla ya vikao vikuu vya wenye maamuzi ya nchi, ni nadra kutoboa,

Tusubiri.
 
Kwahiyo mlitaka wagawane vyeo? Msiaze kulialia wakiwa wanagawana vyeo
 
Unaweza fikiri mtu ana akili na busara ...wait till aguswe mtu wake alie na mahaba nae...
Kumbe Sukuma gang Wana nafuu kuliko chawa wa Lowassa....
Au ni same gang?..

Ghafla mtu wao kageuka 'mwenye haki ya Urais" kutoka mbinguni na waliomzuia wamekuwa"wasaliti,"
 
Back
Top Bottom