Wale jamaa wakikuamulia hutoboi, kipindi nakua kuna familia moja nlishuhudia wanakufa mmoja mmoja wakaisha wote akabaki Baba,
Issue ilikua hivi, mwana familia mmoja alitaka kujenga kwenye kiwanja ambacho sio chake, Mmiliki alivopata hizi habari akaenda kiustarabu na kumwambia yule mwanafamilia asijenge pale yule mwana familia akataka kumshawishi mmiliki wa kile kiwanja kwa kumnunulia kiwanja kingine sehemu nyingine, mmiliki akagoma akasema anaomba kiwanja chake kisiguswe kiachwe, Yule mwana familia kwakua alikua ametoka familia tajiri kwa kiburi akaona mmiliki wa kiwanja hawezi kumfanya kitu, akaendelea na ujenzi, yule mmiliki akasema "jengeni kwenye hiko kiwanja mtaona"
Kilichotokea baada ya miaka kama miwili hivi, ikawa kila ikifika mwez fulani wa kila mwaka anakufa mwanafamilia mmoja kwa kifo cha utata, ile familia walikufa wote akabaki Baba yao tuu na kipindi hiko alikua ameshakua mzee sana, ndo wakaamua kama kwenda kuomba msamaha kwa yule aliyekua mmiliki halali