Waziri Makamba avutia kampuni ya Ufaransa nchini

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
478
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) amekutana na wafanyabiashara wa Ufaransa jijini Paris katika kikao kilichofanyika Novemba 16, 2023.

Akizungumza katika mkutano huo Mhe. Makamba amesisitiza kuwa Tanzania inaendelea kutekeleza yale yote yaliyokubaliwa na mataifa hayo mawili wakati Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipotembelea Ufaransa mwaka 2022.

Pia amewahakikishia wafanyabiashara hao juu ya dhamira ya dhati ya Tanzania ya kuendelea kuwa sehemu salama ya biashara na uwekezaji kupitia ushirikiano wake wa kidiplomasia kikanda na kimataifa.

“Najua miongoni mwenu kuna ambao tayari wamewekeza na wanafanyabiashara nchini Tanzania hivyo kupitia mkutano huu tutapata fursa ya kufafanua masuala mbalimbali ambayo Serikali yetu imeboresha ili kukuza sekta hii muhimu". alisema Mhe. Makamba.

Katika mkutano huo wafanyabiashara hao waliuliza maswali juu ya fursa za biashara na uwekezaji zilizopo chini na kujibiwa na watalaam waliombatana na Mhe. Waziri kutoka katika sekta husika.

Kupitia mkutano huo, Mhe. Makamba amewashawishi wafanyabiashara hao na kuweka bayana maeneo ya kipaumbele ya uwekezaji unaotarajiwa nchini ili kuwezesha utekelezaji wake.

Maeneo matatu yaliyopitishwa kama maeneo ya kipaumbele kwa pande zote mbili ni miundombinu, madini, nishati na utalii.

Mkutano huo ulioandaliwa na Shirikisho la Wafanyabiashara wa Ufaransa (Mouvement Des Entreprises De France - International/MEDEF kwa kushirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa ulilenga kuwashawishi wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchini humo.

Mheshimiwa Makamba anatarajiwa kufanya mikutano mingine ya uwili na wafanyabishara wakubwa wanaoendesha shughuli zao nchini Tanzania ambao ni Total Energies (bomba la mafuta Tanga-Hoima) na Africa Global Logistics (bandari ya Malindi Zanzibar).

Mheshimiwa Makamba yupo Jijini Paris, Ufaransa kwa ziara ya siku tatu kwa lengo la kushawishi wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ufaransa kuangalia Tanzania kama chi sahihi ya kuwekeza na kukuza biashara.
20231117_053720.jpg
20231117_053733.jpg
20231117_053730.jpg
20231117_053714.jpg
20231117_053716.jpg
 

Attachments

  • 20231117_053730.jpg
    20231117_053730.jpg
    81.2 KB · Views: 2
Ni vema zaidi akawavutia wawekezaji wa Israel, Russia au Ukrainia wengi zaidi kwenye kilimo, hii inaweza kuchochea na kuleta tija zaidi.
Na Australian akawavutia kuwekeza kwenye Ufugaji...
 
Wafaransa wanakuja na mikataba ya michongo halafu wakati wa kusaini mtia saini wa kitanzania analeweshwa wine, mkija kustuka wafaransa wanawahi kwenye tribunal na kudai hela ndefu bila hata kukanyaga eneo la mradi.
Mnakumbuka Makamba alipopewa uwaziri wa mafuta alitembelea nchi za Africa kaskazn ili tuuziwe mafuta kwa Bei ya kiwandani, ajabu Ni kwamba mafuta yalipanda Bei Sana huyu mwamba alipokua kwenye usukani kuliko kipindi Cha waziri yoyote. Juzi kaondoka na wenyewe mmeshuhudia Bei ya mafuta.
 
Back
Top Bottom