Kisa cha binti aliyebakwa na Wazungu wanne na mbwa wao

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,891
155,895
Hiki ni kisa cha miaka mingi kidogo, kuna baadhi ya members wa JamiiForums walikuwa hawajazaliwa, na wengine walikuwa ni wadogo sana, na wengine walikuwepo ila walikisahau.

Ninakiweka kisa hiki ili kuwakumbusha mabinti wa kizazi hiki ambao wanadhani mabwana wa kizungu na maisha ya kudanga ndio msingi wa maendeleo yao.

SIKU ya Jumatatu Aprili mosi, 1991 ilikuwa mbaya sana kwa Sara (jina halisi linahifadhiwa), msichana kutoka Mkoa wa Iringa aliyekuwa anaishi na dada yake eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam. Siku hiyo ilikuwa ni ya pili ya Pasaka, yaani Easter Monday kwa Kiingereza, na Sara (aliyekuwa na umri wa miaka 20 wakati huo) aliamua kufanya matembezi katikati ya jiji.

Ilikuwa majira ya saa nne usiku alipoingia katika Hoteli ya Kilimanjaro kwenye ukumbi wa burudani, ilipokuwa inatumbuiza bendi maarufu ya The Tanzanite's. Akiwa ukumbini hapo, alijikuta akifahamiana na Wazungu wanne waliomkaribisha kinywaji aina ya Vodka.

Ilipotimia majira ya saa sita usiku, Wazungu wale walimshawishi Sara afuatane nao kwenda kwenye nyumba ya mmoja wao eneo la Mlalakuwa. Sara alifikiri Wazungu wale walikuwa watu waungwana kwa kuwa walionyesha ukarimu kwake. Walimchukua katika gari lao hadi katika nyumba hiyo na kumkaribisha sebuleni kwa vinywaji zaidi. Kwa vile Sara alikuwa si mwenyeji sana katika Jiji la Dar es Salaam hakujua ramani ya eneo alilokuwa huko Mlalakuwa.

Baada ya kutosheka na vinywaji, Wazungu wale walimwacha Sara peke yake sebuleni na kwenda zao kulala vyumbani. Usiku wa manane ulipowadia, Wazungu waliamka na kumtoa Sara sebuleni hadi baraza ya kando ya nyumba. Walimshika kwa nguvu, wakamvua nguo zake na kubakia kama alivyozaliwa.

Baada ya hapo walimchukua mbwa wao na kumgeuza 'mume' wa Sara! Kitendo hicho kilifanywa kwa nguvu bila Sara kuridhia wala kuweza kujitetea. Mmoja wa Wazungu wale alikuwa anapiga picha kwa kamera yake ndogo wakati mbwa akifanyishwa ngono na Sara.

Baada ya ya unyama huo, Sara alipakiwa katika gari na kurudishwa katikati ya jiji na kuachwa kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Hospitali ya Ocean Road. Maskini Sara alikuwa amedhalilishwa kiasi cha kuona hana tena thamani katika dunia, hivyo alitaka kujiua kwa kujitosa baharini.

Wakati akihangaika hovyo karibu na alfajiri, askari polisi wa ulinzi baharini walimwona na kumwokoa. Baadaye aliwasimulia yaliyomkuta, wakaamua kumpeleka Hospitali ya Rufaa Muhimbili (wakati huo) kupima afya yake.

Madaktari walithibitisha kwamba ni kweli alikuwa ameingiliwa kimwili na mnyama. Uthibitisho huo uliwapa fursa polisi kuanza uchunguzi. Wakati polisi wanafanya uchunguzi, habari hizi zilifika Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA) wakati huo na kuandikwa katika gazeti la serikali la Sunday News la Aprili 7, 1991. Siku chache baadaye, polisi walifanikiwa kujua nyumba ambayo Sara alifanyiwa unyama na kuwatia mbaroni Wazungu wale.

Polisi hawakuchelewa kufungua mashtaka mahakamani (wakati huo Kivukoni). Wazungu walipelekwa kusomewa mashtaka na kunyimwa dhamana. Siku walipofikishwa mahakamani, watu wengi walifika kutaka kuona Wazungu hao walikuwa watu wa aina gani.

Pale Kivukoni ilipo Mahakama Kuu, Kitengo cha Biashara hivi sasa, palifurika watu ambao hawajawahi kuonekana tena eneo hilo. Dk. Masumbuko Lamwai ndiye alikuwa wakili wa utetezi na hoja zake za kuomba dhamana kwa washtakiwa zilishindwa, kwani hakimu alisema wakiachiwa wanaweza kudhuriwa vibaya na jamii iliyokuwa imekasirishwa sana na habari za unyama waliofanya.

Baada ya mwezi mzima wa kesi, serikali ilitoa hati ya kuwafukuza nchini Wazungu wale, kama watu wasiotakiwa kufika tena hapa Tanzania. Ilibainika baadaye kwamba walikuwa ni raia wa Ujerumani na walikuwa nchini kama wataalamu wa kigeni (expatriates) wakati huo maarufu kama'.

Serikali ilichukua hatua hiyo baada ya kuona kesi hiyo inaweza kujenga hisia za kibaguzi katika jamii, kwani tayari watu wengi walianza kuonyesha chuki mbaya kwa Wazungu wote, wakiwamo watalii, wawekezaji na mabalozi. Ulikuwa ni uamuzi wa busara sana wa Serikali ya Awamu ya Pili chini ya Alhaji Ali Hassan Mwinyi.

Lakini busara hizo hazikuzingatiwa sana, kwani habari za uchunguzi zinasema Wazungu wawili miongoni mwa wale wanne, walirudi tena nchini kinyemela. Inasadikiwa walirudi chini ya mwavuli wa dhehebu moja la dini. Hadi sasa haifahamiki kama walitumia majina mengine ya bandia na kama bado wapo nchini, lakini habari za kuonekana kwao tena Dar es Salaam zilifahamika tangu 1997
 
Hicho ni kisa ambacho kweli kiliripotiwa miaka hiyo ya tisini mwanzoni.

Lakini kiuhalisia inavyoonekana huyo binti alikuwa ni wale malaya wanaojiuza, na alichukuliwa na wazungu kama malaya wa kwenda kufanya ngono na kulipwa, tatizo nadhani liko hapa....
1. Hakukusudia kufanyishwa ngono na mbwa bali na binadamu.
2. Kurekodiwa akifanya ngono.
3. Kupunjwa malipo yake.
 
Yaani watu wafanye ukatili hivyo halafu wakaachiwa kirahisi hivyo..kma ni kweli nchi zetu za kimaskini hazitakaa tuendelee. Piga picha mtz angekuwa amefanya Ukatil dizain hyo huko ujeruman, USA ingekuwa vipi? Je wangejali chochotee...
Enzi za Mwinyi mtu ulikuwa unaweza kufanya chochote ili mradi tu, wewe una pesa. Ndio maana akaitwa Mzee Ruksa
 
Yaani watu wafanye ukatili hivyo halafu wakaachiwa kirahisi hivyo..kma ni kweli nchi zetu za kimaskini hazitakaa tuendelee. Piga picha mtz angekuwa amefanya Ukatil dizain hyo huko ujeruman, USA ingekuwa vipi? Je wangejali chochotee...
Mkishikwa na bangi wewe na mzungu hapa bongo ujue wewe Keko inakuhusu na mzungu atajidhamini mwenyewe.
 
MAmbo yote ya hovyo na ya kipuuzi yalianza enzi za utawala wa Mwinyi. Mambo ya mashoga kujiita auntie, madawa ya kulevya, kuuzwa kwa rasilimali za taifa kama alivyouza Loliondo (Loliondo Gate Scandal) na kadhalika.
Mwinyi hakupendwa hata na Waislam wenzake, alikuwa ni kibaraka wa wazungu.


hivvyo unavyosema siyo fair kwani hii issue haikuwahi kutokea au kuripotiwa kabla. Unafanya generalisation.
 
Back
Top Bottom