Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 87,761
- 152,684
Kwangu mimi, tegemea usichotegemea, ambacho nacho kinaweza kuwa sicho, kwa sababu ushategemea.Ok sawa, ingawa nilitegemea ungetumia mbinu za swali kwa swali.
Bora usitegemee chochote!
Kwangu mimi, tegemea usichotegemea, ambacho nacho kinaweza kuwa sicho, kwa sababu ushategemea.Ok sawa, ingawa nilitegemea ungetumia mbinu za swali kwa swali.
Duh,Kiranga kashindikana kwa hoja mzito mshana hatoweza kwa uoga wake. Anajua ataumbuka kiranga ni jina kubwa jf kasha angusha mibuyu mikubwa kama Max shimba, Eiyer,Katalan, hawa ni manguli kwenye battle ya namna hii. Mshana una tujazia server jibu AKILI NI NINI? Ukijibu hili mjadala umekwisha tuna mpa kombe kiranga mara ya pili. Huo mtawi ulio shika shikilia hivyo hivyo ukiachia tu tunapata point 3 team kiranga
mkuu unaurejesha mjadala nyuma " haya maswali yote Tayari yameshajibiwa mbonaKwahiyo huamini uwepo wa Mungu? Nauliza tu mkuu!
Siku hizi ukiwa unapinga uwepo wa Mungu basi tayari wewe ni akili kubwa?
Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na uwezo wote hayupo.Akili ni mfumo wa ufahamu alionao binadamu ( kwa akili yangu inavofikiria )
Binadamu wengi ni wavivu wa kutumia akili. Jaribu kufikiria wewe ndio wa kwanza hapa duniani. Je ungewezaje kufahamu jinsi ya kuishi bila ya kutumia akili, vitabu ni vitu ambavyo viliandikwa na wanadamu kama wewe waliokua na akili uliyonayo wewe lakini je Akili yako inakupa jibu gani unapoacha nadharia ya kuamini vilivyopita na kutumia Akili ako inayokuongoza.
Mungu yupo na kuna ushahidi gani ya uwepo wake..!? (Tumia akili yako kufahamu hili usitumie nadharia ya watu wengine waliopita) NA Mungu hayupo na kuna ushahidi gani ya kutokuwepo kwake..!? (Tumia akili yako kufahamu hili usitumie nadharia ya watu waliopita)
Mwisho kila mtu atakuja na jibu lake analopata kutoka kwenye akili yake na huu mjadala hautakua na mwisho
NB: Tuwe tunatumia akili zetu kwanza. Kwani kwenye akil zetu kila mmoja ana jibu la uwepo wa mungu bila kutumia nadharia nyingine yoyote.
Mkuu we ni mkristo? kama siyo wazee wako walikuwa na dini gani?wenyew " wanasema malaika ni viumbe mkuu " yaani kama wasaidizi wanaoagizwa na Mungu katika kufanikisha mission zake "" ....mimi sitaki kufunga mana na hayo "" so sijui chochote kuhusu wao ""
mkuu kiimani mimi siamini chochote kwa sababu sioni kama kuna umuhimu au ulazima wa kuwa na imani ""
mkuu mimi sio mkristo "" ila wazee wangu wote imani yao ni waislam ""Mkuu we ni mkristo? kama siyo wazee wako walikuwa na dini gani?
unamjua kiranga vyema " kupitia Humu "" au umemjulia kupitia haya mabandiko ya imani tu " mkuu""......hebu jaribu kumfuatilia kwanza katika mijadala ambayo haihusiani na imani halafu ndio uje kutoa hiyo hoja yakoSiku hizi ukiwa unapinga uwepo wa Mungu basi tayari wewe ni akili kubwa?
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu bado unatumia nadharia ya watu waliopita kwa hali hiyo huwezi kufanya wengine waamini kutokuwepo kwa Mungu na bado unaacha kutumia akili yako kufahamu kutokuwepo au kuwepo kwa Mungu.Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na uwezo wote hayupo.
Hayupo kwa nini?kwa sababu dhana ya kuwepokwake, inajipinga yenyewe.
Ukiona dhana ya kuwepokitu inajipinga yenyewe, ujue hichokitu hakipo.
Mathalani, nikisema "pembe tatu duara katikaEuclidean geometry" kitu hichohakiwezikuwepo, kwa sababu, katikaEuclidean geometry pembetatu ni pembetatu,ina nyuzi 180, duara ni duara, lina nyuzi 360, hivyo, pembetatu haiwezikuwa duara hapo hapo.
Kwa hiyo tunajua pembetatu duara haiwezi kuwepo, kwa sababu dhana ya kuwepo pembetatu duara inajipinga, ina contradiction.
Vivyo hivyo, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote (pembetatu) ambaye alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauwezekani kuwa na mabaya, lakini hakuuumba huo, akauumba huu ambao mabaya yanawezekana (duara) , hayupo.
Kwa sababu dhana hizi mbilizinapingana zenyewe kama "pembetatu duara".
Mungu huyohayupo, kama vile "pembetatu duara" hiyo isivyokuwepo.
Hilo andiko unalozungumzia hapa is the bunch of contradictions na ni aibu hata kulitaja!mi n
Mi nilijua umeleta andiko kumbe unaleta porojo.....hahahaaaaa
Unapoandika "watu waliopita kwah ali hiyo" una maana gani? Na unawezaje kuthibitisha hilo?Mkuu bado unatumia nadharia ya watu waliopita kwa hali hiyo
huwezi kufanya wengine waamini kutokuwepo kwa Mungu
na bado unaacha kutumia akili yako kufahamu kutokuwepo au kuwepo kwa Mungu.
Kila mwenye Akili hapa duniani
anaamini uwepo wa Mungu
na akili yako
inabaki na swali la ushahidi wa uwepo wake
hapo ndipo panafanya uanze kutokuamini uwepo wake
lakini kwenye akili
yako kitu cha kwanza kinakwambia kuna uwepo wa Mungu.
Tatizo sio watu kumuamini tu,imani ni jambo la ajabu sana na ndiyo maana hadi leo kuna imani nyingi tofauti na maisha yanaendelea.Atamuamini kwa sababu ya slave mentality zake ktokan na kasumba iliyofanywa na walioasisi hilo neno la Mungu"" ndio maana nilikwambia...hujawahi kuona Jamii yenye mtazamo unao amini uwepo wa samaki mtu "" unadhani kwanini wanaamini hivyo ??
Kinara mbishi
Kipengele muhimu hawa watu wasio waaamini ni kule kutaka wanachokikwepa ni kile cha kutotaka kutambua kuwa ishu za kiroho, Kimungu hazina ithibati za kisayansi.
Wote tuna akili. Je, kuna ithibati? Na kama hatuna akili tuna ithibati? Lakini uhalisia unasemaje?
Kwahiyo Kiranga anataka umuoneshe Mungu as if ni kitu solid. Kiufupi hawa sio atheists bali non believers!!!
Mfano upi ambao sijaelewa?Hata huo mfano hujauelewa.
Hujathibitisha Mungu yupo, kwa sababu hayupo.
Mkuu we ni mkristo? kama siyo wazee wako walikuwa na dini gani?
Haujajibu swali,mie nataka nipate tofauti ya kujua na kuamini kupitia hilo swali nililokuuliza. Sasa matokeo yake badala ya kujibu swali unaniuliza mie unategemea mie nikujibu nini?Nikikwambia baba yangu simjui na wala siamini kwamba ni baba yangu, sijawahi kumjua wala kumuamini. Utanijibu vipi?
Unafahamu huo mfano wa "baba yako unamjua au unamuamini" ukiufuatilia sana utathibitisha Mungu hayupo?
Kwa sababu utalazimisha baba yangu, na mimi nitalazimisha baba yake Mungu, na kumfanya Mungu asiwe Mungu, kwa sababu atahitaji baba?
Kama sijachanganya ulishawahi kuniambia kuwa wewe ni muislamu,kwenye uzi unaozungumzia zanzibar wamepiga marufuku kula mchana hadharani.mkuu " kama umeisoma vyema ile comment " maneno yanayo patikana kwenye aya ya mwisho" nimajibu tosha..yatkayoweza kukufanya usipoteze nguvu za kuuliza hili swali...rejea kusoma vyema tafadhali ""
hili mbona nimeshalitolea ufafanuzi mkuu..hebu pitia post zangu za mwsho vyema ""Kama sijachanganya ulishawahi kuniambia kuwa wewe ni muislamu,kwenye uzi unaozungumzia zanzibar wamepiga marufuku kula mchana hadharani.