Kiranga sio atheist ni non-believer

Kiranga sio atheist ni non-believer

Hata wewe ukisema "nadharia ya watu waliopita"umetumia nadharia ya watu waliopita.

Tumia akili yako acha kufuata nadharia ya watu waliopita.

Unajichanganya mwenyewe.

Ubora wa nadharia hautokani na kwamba ni ya watu waliopita au ni yako mpya.

Unajuaje ninaposema nadharia fulani natumiailiyoandikwa na watu waliopita au niliyoichunguza na kuikubali mwenyewe kivyangu?

Nadharia bora na ya kweli hata kama imetumiwa na watu waliopita, kama ni ya kweli na ina ubora, itatumiwa tu na watu wanaofuata.

This is why people do not reinvent the wheel, calculus, fire, the internal combustion engine, the rules of soccer, etc from scratch everyday.

Somehow you have this nonsensicalidea that everything has to be reinvented from scratch everytime.

Ukipinga nadharia za watu waliopita kwa sababu niza watu waliopita,utapinga kuwepokwa Mungu aliyeandikwa na manabii wote kwenye vitabu.

Kwa sababu nazo ni nadharia za watu waliopita.

Sasa unapinga maandiko yote ya watu waliopita?
Mimi naongelea nadharia zilizopita kwenye kuhusu kuamini uwepo wa mungu si mahala pengine ulipogusia wewe sijasema kwenye kila kitu bali kwenye kuamini kwa uwepo wa mungu....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwangu mimi, tegemea usichotegemea, ambacho nacho kinaweza kuwa sicho, kwa sababu ushategemea.

Bora usitegemee chochote!
Ok, ni sawa binadamu hubadilija kama kivuli. Ni kwamba si kila swali unalijibu kwa swali. Yapo unayoyajibu moja kwa moja kwa kuwa unakuwa huna wasiwasi na majibu yako, au unahisi huwezi kuwa katika mtego.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi naongelea nadharia zilizopita kwenye kuhusu kuamini uwepo wa mungu si mahala pengine ulipogusia wewe sijasema kwenye kila kitu bali kwenye kuamini kwa uwepo wa mungu....

Sent using Jamii Forums mobile app
Hutaki tukubali nadharia za watu waliopita kuhusu uwepo wa Mungu.

Hutaki tuikubali Biblia, na Quran na maneno yaliyoandikwa humo, kuhusu uwepo wa Mungu, kwa sababu nazo ziliandikwa na watu waliopita.

Ndicho unachomaanisha hicho?
 
Kama akili ni mfumo/ uwezo wa kufahamu, nina akili.

Kwa sababu nimeweza kukusoma na kukuelewa swali lako, nikatumia mfumo wa kuelewa/kufahamu (akili, kwa mujibu wako), nikaweza kulijibu.

Nina akili, ningekuwa sina akili (mfumo wa kuelewa/kufahamu) nisingeelewa swali lako na kuweza kukujibu kwamba nina akili au sina akili.

Nimekuthibitishia akili ninayo hapo, kwa kuzingatia definition yako.
Mkuu mshana Jr ameshajibiwa swali lake kwa kupitia dhana ya akili ni uwezo wa kufahamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ok, ni sawa binadamu hubadilija kama kivuli. Ni kwamba si kila swali unalijibu kwa swali. Yapo unayoyajibu moja kwa moja kwa kuwa unakuwa huna wasiwasi na majibu yako, au unahisi huwezi kuwa katika mtego.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana.

Ninapojibu kwa maswali, huwa natumia kitu kinaitwa "Socratic Method" si kwa sababu ya kuogopa mtego.

Socratic method - Wikipedia

Hata Yesu, tunaambiwa kwenye maandiko, alipoulizwa na watu kama walipe kodi kwa Kaizari au wasilipe, aliwaonesha sarafu na kuwajibu kwa swali, akiwauliza sarafu hii ina picha ya nani?

Lengo lake lilikuwa si kuepuka mtego.

Lengo lake lilikuwa kwafanya waliouliza swali wapate jibu kwa mwanga mzuri zaidi wa kuona kwamba kama sarafu ina picha ya Kaisari, basi ni mali halali kumlipa Kaisari.

Sasa angekuwepo Yesu anajibu watu kwa maswali hivyo, ili wapate mwanga mzuri zaidi, ungesema anakwepa maswali anaogopa mtego?
 
Hutaki tukubali nadharia za watu waliopita kuhusu uwepo wa Mungu.

Hutaki tuikubali Biblia, na Quran na maneno yaliyoandikwa humo, kuhusu uwepo wa Mungu, kwa sababu nazo ziliandikwa na watu waliopita.

Ndicho unachomaanisha hicho?
Exactly...tumia akili yako kufahamu kwa sababu kuamini uwepo wa Mungu upo katika akili yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Exactly...tumia akili yako kufahamu kwa sababu kuamini uwepo wa Mungu upo katika akili yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
No wonder Kiranga amekwepa kiunzi, kumbe kama haumini uwepo wa mungu hauna akili!

No wonder Mshana cannot answer a simple question!

Kitu ambacho kuna wengine wanadaiwa kuwa nacho less than kuku? Hata ukiwa na uwezo tu wa kuvuka barabara utaambiwa una akili!😱

Akili ni nini is a good question from Kiranga

Mshana Jr jibu swali. 60 something pages yet you cant answer it? Or is it you're busted?
 
Exactly...tumia akili yako kufahamu kwa sababu kuamini uwepo wa Mungu upo katika akili yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimetumia akili yangu nimefahamu Mungu hayupo, ni hadithi tu.

Kwa sababu ana contradictions nyingi sana.

Unaambiwa eti Mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.Ana haki ya juu kabisa.

Halafu unaambiwa eti kahukumu wanyama katika gharika, wamekufa sana kwa mafuriko, kwa makosa waliyoyafanya watu.

Sasa Mungu gani wa haki anahukumu wanyama kwa makosa ya watu?

Tunaambiwa Mungu ni wa haki, lakini anahukumu vitukuu na vitukuu vya vitukuu kwa makosa ambayo hata havijafanya, yamefanywa na wazee wao zamani sana huko.

Sasa huyu Mungu wa haki kwa nini anahukumu vitukuu hivi kwa makosa ambayo havijafanya? Mungu anashindwa kwa haki na hakimu ambaye sheria inamkataza kumhukumu mtoto kwa kosa la baba?

Tunaambiwa eti Mungu anapata hasira. Hasira ni udhaifu ambao unaonesha kukosa control, kukosa kujua mambo vizuri, kupata matokeo ambayo hukutegemea, ni udhaifu. Sasa huyu Mungu aliyekamilika kila kitu hasira anaanzaje kuipata?

Tunaambiwa Mungu anapanga mpango, halafu unaenda tofauti na alivyotaka, anataka kughairi.

Sasa huyu Mungu anayejua kila kitu inakuwaje hakujua mpango huu utaenda hivi, mpaka anataka kughairi?

Tunaambiwa Mungu ana taifa lake teule, sasa Mungu mwenye upendo wote inakuwaje atoe upendeleo kwa taifa lake teule?

Tunaambiwa kuna watu Mungu atawaziba mioyo, masikio na macho, hata wajitahidi vipi kumjua hawatamjua, hao msihangaike nao. Sasa inakuwaje Mungu awazibe masikio, macho na mioyo watu wasimjue? Na hawa nao atawahukumu kwa kutomjua?Au atawasamehe tu kwa sababu ni yeye mwenyewe aliwaziba mioyo, masikio na macho na hivyo anajua wasingeweza kumjua?

Tunaambiwa Mungu yeye ndiye anatoa neema ya kumjua, sasa wale ambao hajawapa neema ya kumjua atawahukumu kwa kutomjua au atawachia tu kwa sababu ni yeye mwenyewe hakuamua kuwapa neema ya kumjua?

Tunaambiwa mti ambao hauzai matunda utakatwa na kuchomwa moto kama adhabu ya kutotoa matunda, sasa Mungu mbona anauhukumu mti kwa sababu haujazaa matunda, wakati yeye ndiye anatoa rehema ya kuzaa matunda?

Contradictions allover the place.

Ukichunguza unaona huyu Mungu katungwa na watu tu, ndiyo maana kapewa tabia za watu.
 
A: Una akili?
B: Akili ni nini?

Maswali mawili, hayajapata majibu hadi posts zaidi ya 1000.

Sent from my TA-1032 using Tapatalk
 
A: Una akili?
B: Akili ni nini?

Maswali mawili, hayajapata majibu hadi posts zaidi ya 1000.

Sent from my TA-1032 using Tapatalk
Swali la kwamba nina akili nimelijibu kutoka kwa angalau watu watatu (sio Mshana), kwa mujibu wa definitions zao za akili.

Kwa hiyo, kwa upande wangu,swali hilo nimelijibu angalau mara tatu, kwa watu watatu tofauti.

Fuatilia mjadala.

Ila Mshana sijamjibu, kwa sababu hajaniambia akili ni nini.

Kati yangu na Mshana, mimi nimejibu swali mara tatu, Mshana hajajibu hata mara moja.
 
Nimetumiaakili yangu nimefahamu Mungu hayupo, nihadithi tu.

Kwa sababu ana contradictions nyingi sana.

Unaambiwa eti Mungu ana uwezowote, ujuzi wote na upendo wote.Ana haki ya juu kabisa.

Halafu unaambiwa eti kwahukumuwanyamakatika gharika, wamekufa sana kwa mafuriko, kwa makosa waliyoyafanya watu.

Sasa Mungu gani wa haki anahukumuwanyama kwamakosa ya watu?

Tunaambiwa Mungu ni wa haki, lakini anahukumu vitukuu na vitukuu vya vitukuu kwa makosa ambayo hata havijafanya, yamefanywa na wazee wao zamani sana huko.

Sasahuyu Mungu wa haki kwa nini anahukumuvitukuu hivi kwa makosa ambayo havijafanya? Mungu anashindwa kwa haki na hakimu ambaye sheria inamkataza kumhukumu mtoto kwa kosa la baba?

Tunaambiwa eti Mungu anapata hasira. Hasira ni udhaifu ambaounaonesha kukosa control, kukosa kujua mambo vizuri, kupata matokeo ambayo hukutegemea, niudhaifu. Sasa huyu Mungu aliyekamilika kila kitu hasira anaanzaje kuipata?

Tunaambiwa Mungu anapanga mpango, halafu unaenda tofauti na alivyotaka, anataka kughairi.

Sasa huyu Mungu anayejua kila kitu inakuwaje hakujua mpango huu utaenda hivi, mpakaanataka kughairi?

Tunaambiwa Mungu ana taifa lake teule, sasa Mungu mwenye upendo wote inakuwaje atoe upendeloe kwa taifa lake teule?

Tunaambiwa kuna watu Mungu atawaziba mioyo, masikio na macho, hata wajitahidi vipi kumjua hawatamjua, hao msihangaike nao. Sasa inakuwaje Mungu awazibe masikio, machona mioyo watu wasimjue? Na hawa nao atawahukumu kwa kutomjua?Au atawasamehe tu kwa sababu ni yeye mwenyewe aliwaziba mioyo, masikio na macho na hivyo anajua wasingeweza kumjua?

Tunaambiwa Mungu yeye ndiye anatoa neema ya kumjua, sasa wale ambao hajawapaneema ya kumjua atawahukumu kwakutomjua au atawachia tu kwa sababu ni yeye mwenyewe hakuamuakuwapa neema ya kumjua?

Tunaambiwa mti ambao hauzai matunda utakatwa na kuchomwa moto kama adhabu ya kutotoa matunda, sasa Mungu mbona anauhukumu mti kwa sababu haujazaa matunda, wakati yeye ndiye anatoa rehema ya kuzaa matunda?

Contradictions allover the place.

Ukichunguza unaona huyu Mungu katungwa na watu tu, ndiyo maana kapewa tabia za watu.
Hapa umegalagaza!
 
Hizo contraditions bado unasema unaambiwa yani bado unatumia nadharia ya watu wengine. Hapo umetumia akili kufahamu au kujua yale yaliyojadiliwa na watu waliopita kwa hali hiyo hutaki kuamini kile kilicho ndani ya akili yako.

Narudia tena mkuu uwepo wa Mungu upo katika akili yako na sio kutumia akili yako kujua uwepo wa Mungu

Unaelewa kwamba hakuna utakachofikiri wewe leo ambacho hakijawahi kuwa nadharia ya wengine hapo kabla?
 
Natamani nawe ungenielewa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama hajakuelewa ni kwa sababu tunaishi kwenye ulimwengu ambao haujaumbwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.

Angekuwepo, kika ntu angemuelewa kila mwingine bila tatizo.

Mtu kutokukuelewa ni ushahidi Mungu huyo hayupo.
 
Back
Top Bottom