Kiranga sio atheist ni non-believer

Kiranga sio atheist ni non-believer

Wasema atheist ni yule asiyejua lolote kumhusu Mungu ama miunngu. Lakini ili tupate tofauti halisi ya nonbeliever na atheist ni lazima tuangalie engo mbalimbali, kama vile; Elimu ya mtu, jamii alimozaliwa, uwezo wa kiuchumi wa mtu au taifa atakapo, upatikanaji wa machapisho ya kidini n.k.

Sasa ukija kuangalia vigezo hivyo utagundua kua kuna watu wanaamini uwepo wa Mungu pasipo kuwa na elimu yoyote kumhusu Mungu na hawana hoja imara za kutetea uwepo wa Mungu.

Hawa ni wale wanaoishi chini ya umaskini mkubwa katika maeneo maskini ambayo wakati fulani yaliwahi kufikiwa na waeneza dini ambao walipata wafuasi fulani lakini baadaye mawasiliano yale yakakata hivyo wafuasi waandamizi wakakosa elimu ya kile walichoridhi toka kwa wazazi wao, na wao kubaki tu na majina yanayoashiria dini ile hivyo kuendelea kuitwa waamini.

Vilevile utaona pia kuna watu wamezaliwa kwenye mataifa ya kidini ambamo dini ni sehemu ya maisha katika jamii husika, lakini wao hawaamini katika hizo dini bila kujali kama walipata elimu ya dini ama la na hawapingani na yeyote kumhusu Mungu. Hivyo wanasalia kuitwa waamini pasipo wao kuamini.

Pia kuna wengine wamesoma kanuni na miongozo mbalimbali ya kidini, lakini wao wakaichukulia kama vitabu na machapisho mengine ya kutoa elimu wakashika maarifa yaliyomo na wasifuate njia za kuabudu za kundi lile. Mfano mzuri ni Japan nchi inayoongoza kuwa na maatheist wengi lakini bado hua wanasoma authoritative books ambazo zimeandaliwa na watu wa dini kwa lengo la kuwaelimisha waamini wao.
Mtazamo mwingine dhidi ya nonbeliever na atheist waweza kuangaliwa kupitia wale wanaojiita waamini ama wenye dini. Kwa miaka mingi kumekua na matamshi kutoka kundi fulani la wanaojiita wenye dini kuwaita wafuasi wa kundi jingine kama wasioamini (nonbelievers) kwa sababu tu, wanatofautiana katika imani zao kumwelekea Mungu. Na hii inatokana na ubinafsi wa kila mwenye dini kuamini kuwa dini yake ni sahihi kiliko mwingine.

Hitimisho, kwa hayo machache waweza kuona namna ilivyo vigumu kupata kategoria rahisi za kuwatofautisha nonbelievers na maaatheists. Kwa sababu dunia ya sasa yenye teknologia bora kabisa ya kewezesha watu kipata machapisho mbalimbali yahusuyo dini na miongozo yake imekua ikishuhudia kuongezeka kwa kasi kwa kundi la wale wanaoitwa wakana Mungu.
nimeshangaa mnooo baada ya kuona umepata like moja...wakati umetoa hoja yenye mashiko mnooo"" aisee..kweli maisha bila ya unafiki hayaendi ""
 
target ya swali lake nimeielewa vizur,ukisema ndio una akili atakuuliza uthibitishe akili ilivyo hahahaha ukisema aionekan ilo jibu litaamia kwa mungu kua nae aonekan umewezaje kuamini akili unayo wakati aionekan,,,,,, picha tamu ili nisiharibu mitego
hapa kakimbia
 
Hawa ni wale waliosema 'Tumesikia, tumeelewa na HATUTAKI'. Nafsi zao zimepigwa muhuri wa kukanusha uwepo wa Mungu Muumba eti kwa vile sayansi haiwezi ku prove wakati ziko dalili nyingi sana ikiwepo complexity ya mfumo wa ufanyaji kazi wa mwili wake mwenyewe ambao atheists na non believers ignorantly wanapinga uwepo wa aliyeusuka mfumo huo na kwamba eti umetokea by chance!(wanaamini all creatures wapo by chance)
Wewe ndo upo sawa..! Sio Mshana Jr analeta porojo zake hapa..!
 
Kabla ya kufika mbali kote huko, inabidi mtu a define akili ni nini.

Mtu anaweza kuniuliza "Wewe ni Mkristo?".

Swali hilo likawa gumu kwangu kujibu.

Nimebatizwa kwenye Ukristo na hakuna siku nilikoenda kanisani kusema najitoa Ukristo - kwa hiyo kwa definition ya watu waliobatizwa Ukristoni, waliolelewa familia ya Ukristo ,wenye majina ya Kikristo, mimi ni Mkristo.

Lakini pia, Mkristo ina tafsiri nyingine, kwamba mtu anayemuamini Yesu Kristo na kumfanya kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kwa tafsiri hiyo mimi si Mkristo.

Sasa mtu akiniuliza "Wewe Mkristo?", kabla sijamjibu, inabidi nimuulize, unaposema "Mkristo" una maana gani? Hilo neno lina tafsiri nyingi sana.

Ndicho ninachojaribu kufanya kwa Mshana hapa.

Kaniuliza kama nina "akili".

Neno "akili" lina tafsiri nyingi sana. Sasa, ili kuondoa mkanganyiko, namuomba anipe tafsiri ya neno hilo anayoitumia, anaposema "akili" ana maana gani?

Kusudi nikimjibu nijikite kwenye tafsiri aliyoisema.

Sasa hata mtu aliyeuliza swali hajui anauliza nini.

Mimi nitawezaje kumjibu?
akili nyingi sana nae kwa kugundua hilo anaona akikujivu maana ya akili anayokusudia atakuwa kakurahisishia kujibu swali lake na yeye kushindwa kukupata kweny mtego wake,,,kwa kifupi huu mjadara hauwezi kuisha had mmoja kati yenu akubali kuingia king
 
Back
Top Bottom