Kiranga sio atheist ni non-believer

Kiranga sio atheist ni non-believer

Usitafute sympathy.... Twende kwa mjadala na hoja.... N prove your abilities!
Nakwendakwa hoja.

Moja ya kanuni za msingi kabisa za insha, mijadala, utafiti etc ni ku define vitu mwanzo kabisa.

Umeuliza swali, umetumia neno, neno tata, swali halipo clear.

Umeulizwa kufafanua swali lako.

Wewe unayeuliza swali huwezikufafanua swali lako, huwezi kuniambia akili ni nini.

Unategemeaje mimi niweze kukujibu?

Unaniambia nikutafsirie ndoto.

Nakwambia sawa, niambie hiyo ndoto, unaniambia ndoto yenyewe nayo sikwambii, wewe niambie ndoto yangu niliyoota kisha itafsiri.

Kama Nebuchadnezzer.

Sawawa hiyoo?

Hataaaaa.

Hiyo si sawa Mshana, acha vituko!
 
Nimekuuliza mimi in the first place! Jibu
Wewe umeniuliza kama nina akili, hukuniuliza akili ni nini.

Mimi ili nikujibu vizuri, nataka unipe definition yako ya akili ili nisikujibu kitu tofauti na unachotaka wewe.

Kumbe, wewe unayeniuliza hujui unauliza nini.

Sasa mimi nitakujibu vipi ikiwa wewe unayeuliza hujui unauliza nini?
 
Huyo anauliza kitu ambacho hata yeye mwenyewe swali lake hawezi kulifafanua lieleweke vizuri, halafu anataka jibu.
target ya swali lake nimeielewa vizur,ukisema ndio una akili atakuuliza uthibitishe akili ilivyo hahahaha ukisema aionekan ilo jibu litaamia kwa mungu kua nae aonekan umewezaje kuamini akili unayo wakati aionekan,,,,,, picha tamu ili nisiharibu mitego[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kinara mbishi asiyekubali kuwa kuna Mungu. Mbishi kwa viwango vyote unavyojua ila mwepesi wa hoja.

Kiranga sio atheist, kwa tafsiri rahisi atheist ni mtu asiyejua lolote kuhusu Mungu ama miungu (Hana ABC zozote kuhusu hizo imani za Mungu na miungu)

Kiranga sio mmojawapo. Kiranga ni mmojawapo wa wale waliokengeuka imani, walizaliwa katika ukristo wakabatizwa na kuishi maisha ya ukristo... Lakini along the way wakabahatika kusoma doctrines za kikristo, Mungu nk.

Ni katika hizo doctrines wakashindwa kukubaliana na vifungu kadhaa hivyo wakakengeuka na kuwa wapinga Uwepo wa Mungu mkuu.

Ni watu wenye elimu kubwa kuhusu dini hasa ukristo halafu wakasoma na doctrines nyingine zinazopinga uwepo wa Mungu na kuchagua kuyaamini hayo.

Kipengele muhimu hawa watu wasio waaamini ni kule kutaka wanachokikwepa ni kile cha kutotaka kutambua kuwa ishu za kiroho, Kimungu hazina ithibati za kisayansi.

Wote tuna akili. Je, kuna ithibati? Na kama hatuna akili tuna ithibati? Lakini uhalisia unasemaje?

Kwahiyo Kiranga anataka umuoneshe Mungu as if ni kitu solid. Kiufupi hawa sio atheists bali non believers!!!
@mshana jr naomba uachane na hizi habari maana huna unachokielewa..! Kuanzia kwenye definition ya atheist umeingia chaka mpaka kwenye kujaribu kumuelezea Kiranga pole mkuu endelea na madogoli tu..! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
target ya swali lake nimeielewa vizur,ukisema ndio una akili atakuuliza uthibitishe akili ilivyo hahahaha ukisema aionekan ilo jibu litaamia kwa mungu kua nae aonekan umewezaje kuamini akili unayo wakati aionekan,,,,,, picha tamu ili nisiharibu mitego[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Kabla ya kufika mbali kote huko, inabidi mtu a define akili ni nini.

Mtu anaweza kuniuliza "Wewe ni Mkristo?".

Swali hilo likawa gumu kwangu kujibu.

Nimebatizwa kwenye Ukristo na hakuna siku nilikoenda kanisani kusema najitoa Ukristo - kwa hiyo kwa definition ya watu waliobatizwa Ukristoni, waliolelewa familia ya Ukristo ,wenye majina ya Kikristo, mimi ni Mkristo.

Lakini pia, Mkristo ina tafsiri nyingine, kwamba mtu anayemuamini Yesu Kristo na kumfanya kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yake. Kwa tafsiri hiyo mimi si Mkristo.

Sasa mtu akiniuliza "Wewe Mkristo?", kabla sijamjibu, inabidi nimuulize, unaposema "Mkristo" una maana gani? Hilo neno lina tafsiri nyingi sana.

Ndicho ninachojaribu kufanya kwa Mshana hapa.

Kaniuliza kama nina "akili".

Neno "akili" lina tafsiri nyingi sana. Sasa, ili kuondoa mkanganyiko, namuomba anipe tafsiri ya neno hilo anayoitumia, anaposema "akili" ana maana gani?

Kusudi nikimjibu nijikite kwenye tafsiri aliyoisema.

Sasa hata mtu aliyeuliza swali hajui anauliza nini.

Mimi nitawezaje kumjibu?
 
Back
Top Bottom