Kiranga sio atheist ni non-believer

Kiranga sio atheist ni non-believer

Tatizo dini zimeonekana kama biashara inufaishayo jamii chache,sasa haya kwa MTU aliyefundishwa Barabara kumhusu mungu na akiangalia yatokeayo anaamua kuamini mungu in porojo.mfano ukiwa na akili timamu ukayaona kwa uchache ayafanyayo na kuyaamua mmarekani dhidi ya mataifa mengine,unapata picha kwamba mungu in bosheni
Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na uwezo wote angekuwepo hata mjadala wa kuwepo Mungu usingekuwepo.

Ungekuwa mjadala ambao hauyumkiniki kuliko mtu kufanya mjadala kama yeye mwenyewe yupo.
 
Tumeshndwa wangapi?

Swali lako halieleweki haujalifafanua zaidi ndyo maana umepgwa swali ktk kujibiwa muundo wa swali.

Ulichouliza haukijui kukielezea, utawezaje kuelewa hata jibu ukipewa?

Akili ni nini?
Una AKILI ama huna AKILI? Jibu
 
Ndiyo maana kiranga anauliza maana ya akili.Ili kama ni hii ya kuamini uwepo wa mungu aseme hana,au kama nyngine asema inavyostahiki.
Kiranga anauliza maana ya neno akili,sasa hata tukisema Kiranga hana akili kwa sababu haamini mungu bado swali lake la akili nini litakuwa bado halijajibiwa.

Maana yeye kataka kujua hiyo akili yenyewe hasa ni nini,au sijui sijamuelewa.
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na uwezo wote angekuwepo hata mjadala wa kuwepo Mungu usingekuwepo.

Ungekuwa mjadala ambao hauyumkiniki kuliko mtu kufanya mjadala kama yeye mwenyewe yupo.
Ana nguvu zote, ana uwezo wote ana kila kitu, lakini kila siku tunahubiriwa tumfate. Kwa nini tusimfuate "automatically", kwa nini tushurutishane kumfuata?

Mungu mwenye upendo lakini watu wake kila siku wanakufa, wengine kwa njaa na umasikini, wengine kwa vita na maradhi makubwa yenye kuumiza mwili.

Angekuwepo kweli wala tusingekuwa na arguments, tungemfata wote bila kujali.
 
Sasa"" mjinga atashinda vipi mkuu""!? maana wanaofuatilia mjadala watautambua ujinga wake kutokana " na uwezo wake mdogo wa kubishana bila logic/fact "" labda kama atapewa huo ushindi na wajinga wenzake ambao ndio "" wafuatiliaji wa huo mjadala"" ila kama mjadala unafuatiliwa na watu timamu wa akili sidhani kama huyo mjinga atashinda
Hata ukitambua ujinga wake ndiyo utafanya nini? hebu tizama huu mjadala na kinachobishaniwa.

Hivi neno akili ndiyo la kuleta ubishani wote huu wa kujaza uzi?
unataka kuniambia hivi neno akili lina mkanganyiko na ndiyo sababu ya huu ubishi humu? kwamba mtu ukimuuliza kama ana akili ashindwe kukuelewa?


Mpaka hapo haujaoni ni vp mjinga hauwezi kumshinda ubishi?na ukiangalia kuna mtu ameshapewa ushindi sasa utajua mwenyewe ni kwa lipi na hao watu ni kundi gani.
 
Unaweza kuuthibitisha huo uwezo wako unaodai unao mkubwa sana? Ulichokiongelea ni matokeo ya akili kwa mujibu wa tafsiri niliyoitoa awali.
Mbona huelewi?
Si umesema akili ni uwezo wa....?
Sasa ili ujue kuwa nina akili kwa tafsiri yako ni lazima nithibitishe uwezo huo kwa kutenda.
au kuna njia nyingine ya kuthibitisha 'uwezo'.Kwa mfano mtu mwenye uwezo wa kula maandazi 100 kwa wakati mmoja ana njia nyingine ya kuthibitisha uwezo wake zaidi ya kutenda kitendo cha 'kula' maandazi hayo?
 
Kuna mtu kasema juu hapo akili ni kutambua uwepo wa Mungu, nikasema kwa definition hiyo sina akili.

Sasa mtu kama huyo, ukitaka kujibu swali kichwa kichwa, unaweza kuwa huamini Mungu halafu ume solve Poincare's conjecture yako huko, ukasema mimi nina akili, kumbe kwake usipoamini Mungu huna akili.

Ndiyo maana ni muhimu tuanze na definitions kama tunaandika insha.

Ndiyo maana nikauliza.

Akili ni nini?

Sijajibiwa.
Hakuna aliyesema akili ni kutambua uwepo wa mungu,bali mwenye akili ni yule mwenye kuutambua uwepo wa mungu.

Kuna tofauti hapo,hapo neno akili limetumika tu ila halijatolewa maana yake hasa nini hadi huyo mwenye kuamini mungu ndiyo awe nayo hiyo akili.
 
Kushinda mabishano si kitu kibaya.

Aristotle alishinda mabishano. Socrates alishinda mabishano. Galileo alishinda mabishano. Tycho Brahe alishinda mabishano. Copernicus alishinda mabishano.Newton alishinda mabishano. Einstein alishinda mabishano. Niels Bohr alishinda mabishano

Pinga hoja kwa hoja, si kubwabwaja viroja.
Na hakuna niliposema kushinda mabishano ni kitu kibaya,ila nimesema Kiranga amejikita kushinda mabishano kwa hali yeyote. Sasa kama hao (manabii wako) nao walijikita kushinda mabishano kwa hali yeyote kama ufanyavyo wewe sawa.
 
Back
Top Bottom