Kiranga sio atheist ni non-believer

Kiranga sio atheist ni non-believer

Mazingira yake inaonekana amekulia katika jamii ya watu wa Pwani ya Tanganyika, ambayo ni jamii ya Kiislamu.
Baada ya kuanza na Imani ya Kiislam, aliweza pia kuvisoma kwa juu juu vitabu vya imani nyingine kama, Ubudha, Uyahudi, Ukristo nk, na bahati mbaya hakuvielewa vyote.
Kwani vyote vimeasisiwa na ama Mungu au miungu.
Yeye bado halijui hilo.
Angalia vizuri aina ya ujengaji hoja wake juu ya huyo mungu anayesema hayupo utaona ni wapi alipoelemea?
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na uwezo wote angekuwepo hata mjadala wa kuwepo Mungu usingekuwepo.

Ungekuwa mjadala ambao hauyumkiniki kuliko mtu kufanya mjadala kama yeye mwenyewe yupo.
aisee we mtu mimi nakukubali,sina namna ya kukuelezea ila kitu kilicho na nguvu kama mungu hakikupaswa kujifichaficha kama hivi.kingejieleza kujionesha kijipambanua na mengineyo mengi.labda kama kuna nguvu ingine watu wameamua kuificha baada ya kuijua na kuifahamu ambayo kwayo wanawatawala watu na kuwalisha wenye fikra fupi kwa kuiita mungu na kuificha iliyopaswa kuwa halisi.
 
Na hakuna niliposema kushinda mabishano ni kitu kibaya,ila nimesema Kiranga amejikita kushinda mabishano kwa hali yeyote. Sasa kama hao (manabii wako) nao walijikita kushinda mabishano kwa hali yeyote kama ufanyavyo wewe.
Kiranga ni delusional follower wa philosophers marehemu kina Socrates, Plato na wengineo.. Alisoma doctrines zao na zikam brainwash kwa kiwango cha juu mno... Ndio maana nje wa ubishi wake ukimbana mahali vizuri atatafuta pa kutokea kwa kuwa quote hao marehemu ambao maandishi yao bado yanaishi
Yani hakuna tofauti ya mtu anaye quote Bible na anaye quote mabandiko ya binadamu wengine
Nilipotea kidogo tulikuwa kwenye ibada site ya ma atheist katika uhalisia, hawajui kabisa Mungu ni kitu gani na hawana tatizo hata chembe kwa wewe unayemwabudu Mungu View attachment 784179
IMG_20180523_091023.jpg
 
Mbona huelewi?
Si umesema akili ni uwezo wa....?
Sasa ili ujue kuwa nina akili kwa tafsiri yako ni lazima nithibitishe uwezo huo kwa kutenda.
au kuna njia nyingine ya kuthibitisha 'uwezo'.Kwa mfano mtu mwenye uwezo wa kula maandazi 100 kwa wakati mmoja ana njia nyingine ya kuthibitisha uwezo wake zaidi ya kutenda kitendo cha 'kula' maandazi hayo?

Kwanini unasema sielewi, umejuaje kwamba sielewi?
 
Mbona huelewi?
Si umesema akili ni uwezo wa....?
Sasa ili ujue kuwa nina akili kwa tafsiri yako ni lazima nithibitishe uwezo huo kwa kutenda.
au kuna njia nyingine ya kuthibitisha 'uwezo'.Kwa mfano mtu mwenye uwezo wa kula maandazi 100 kwa wakati mmoja ana njia nyingine ya kuthibitisha uwezo wake zaidi ya kutenda kitendo cha 'kula' maandazi hayo?
Kwa hiyo mtu akitaka kuthibitisha kuwa ana uwezo wa kukuua inabidi akuue?
Hiyo ni sawa na kuijaribu sumu kwa kuionja!
 
Hugo mtoto mchanga kwanini msimuache mpaka mungu mwenyewe amfunukie akamjulisha kwamba yeye mungu yupo,na badala yake mmemuandalia mavitabu na makaburasha kibao ya kumkaririsha
hahaa..kama Mungu ni muweza wa yote " kweli !!? alishindwa vipi kumfanya mtoto mdogo aweze kumtambua...mpaka asubiri uwezo wa wa binaadamu waweze kumsaidia ktika kumfanya mtoto mdogo aweze kumtambua yeye
 
hahaaa...kama Mungu ni muweza wa yote "". alishindwa kufanya jambo Dogo kama hilo kwa mtoto mchanga " mpaka asubiri uwezo wawatu ili wa msaidie kwenye kumkarilisha kuhusu yeye""....
nadhani umenielewa nawaambia wanaomtaja mungu kwamba wawaache watoto wadogo bila kuwagusia chochote kuhusu mungu mpaka yeye awafunulie mwenyewe kwa uweza wake.
 
Kwasababu umeshindwa kujifunza,kuelewa na kuchambua.

Unajua huu mzunguko woote umeanzia kwenye kujibu swali la akili ni nini?

Sijapenda hili jibu lako kwangu lakini hainisumbui kwa sababu sielewi kiwango cha uelewa wako wa mambo.

Kwa kuwa tu sijajibu unavyotaka wewe haimaanishi sijakuelewa au sina akili ambayo haujaielezea ni kitu gani.

Kwanza, naweka wazi msimamo wangu binafsi kuhusu uwepo wa Mungu, mimi ni muumini mzuri tu kwamba yupo.

Pili, vitabu vinavyomuongelea Mungu (namaanisha Biblia takatifu) vimeweka bayana kwamba hatua ya kwanza kabisa, lazima uwe na Imani. Nje ya hapo utakuwa sahihi kusema hayupo.

Biblia imeeleza kwa upande wake uweza, mamlaka na sifa za Mungu, leo anakuja mtu kusema hapana, anatakiwa athibitishwe kwa aina anayotaka yeye, haiendi hivyo. Nnaweza kuwa tajiri na nikatoa msaada kwa namna nnayotaka mimi au nisitoe kabisa, haitamaanisha mimi sio tajiri.

Mara nyingi sipendi kubishana sana kuhusu hili jambo kwa sababu kuu moja tu. Huyo Mungu mie sio kazi yangu kumthibitisha wala kuutetea uungu wake, atafanya hivyo kwa namna yake.

Mwisho, naheshimu maoni ya watu wote, nisichokipenda ni ile upande mmoja kuona wengine kama wamepungukiwa akili au wana tatizo flani kutokana na msimamo wao kiimani iwe uwepo wa Mungu au kutokuwepo. Wote mnaamini vitu tofauti, wote mnakufa, mna ubitaji wa mambo muhimu kama chakula, hewa maji n.k. wote mnasoma shule, mnahitimu mnaajiriwa nyadhifa tofautitofauti, kila mmoja anaendesha maisha yake. Sasa hapo dharau ya mtu wa imani nyingine inakuongezea au kukupunguzia nini?
Au kuna utafiti uliwahi kuonyesha kuhusu mafanikio ya maisha ya wanaoamini na wasioamini uwiano ukoje? Ntafurahi na ningependa niusome huo utafiti, kama upo na uliwahi kufanyika.
 
Kinara mbishi asiyekubali kuwa kuna Mungu. Mbishi kwa viwango vyote unavyojua ila mwepesi wa hoja.

Kiranga sio atheist, kwa tafsiri rahisi atheist ni mtu asiyejua lolote kuhusu Mungu ama miungu (Hana ABC zozote kuhusu hizo imani za Mungu na miungu)

Kiranga sio mmojawapo. Kiranga ni mmojawapo wa wale waliokengeuka imani, walizaliwa katika ukristo wakabatizwa na kuishi maisha ya ukristo... Lakini along the way wakabahatika kusoma doctrines za kikristo, Mungu nk.

Ni katika hizo doctrines wakashindwa kukubaliana na vifungu kadhaa hivyo wakakengeuka na kuwa wapinga Uwepo wa Mungu mkuu.

Ni watu wenye elimu kubwa kuhusu dini hasa ukristo halafu wakasoma na doctrines nyingine zinazopinga uwepo wa Mungu na kuchagua kuyaamini hayo.

Kipengele muhimu hawa watu wasio waaamini ni kule kutaka wanachokikwepa ni kile cha kutotaka kutambua kuwa ishu za kiroho, Kimungu hazina ithibati za kisayansi.

Wote tuna akili. Je, kuna ithibati? Na kama hatuna akili tuna ithibati? Lakini uhalisia unasemaje?

Kwahiyo Kiranga anataka umuoneshe Mungu as if ni kitu solid. Kiufupi hawa sio atheists bali non believers!!!
Asante kwa taarifa kuhusu Kiranga.Watu wa aina yake JF wako wengi.Ila sasa na wewe Mshana ndugu yanguu,ni atheist au nonbeliever?
 
Akili ni nini?
Ulivouliza akili ni nini, umetoa nafasi ya mjadala kua mkubwa na kumfanya Mshana aonekane bado ana hoja.

Akili - neno linalohusisha namna mtu anavyofikiri, anavyotafuta majawabu, anavyotafsiri muonekano wa vitu, anavyokubaliana na mambo na jinsi anavyohisi.

Kwa maana hii akili sio umbo bali neno, kwahio swali la kwamba mtu ana akili au lah ni batili. Kwakua kazi nyingi za akili zinahusiana na ubongo ndio maana waswahili hua tunauliza kama mtu ana akili lakini si sahihi .
Akili kwa kiingereza ni mind . Kwa mtu anaeongea kiingereza hawezi kukuuliza kama una akili, yani " the question as to whether one has a mind or not is either invalid or futile "
Ila unaweza kuulizwa kama una ubongo au lah .

Ref;
Mind - Wikipedia https/en.m.wikipedia.org/wiki/Mind?iorg_service_id_internal=803478443041409%3BAfonYAdB1BsjBypX
 
Are you out of your mind? Nimependa ufafanuzi wako wa neno akili mkuu.
 
Unajua huu mzunguko woote umeanzia kwenye kujibu swali la akili ni nini?

Sijapenda hili jibu lako kwangu lakini hainisumbui kwa sababu sielewi kiwango cha uelewa wako wa mambo.

Kwa kuwa tu sijajibu unavyotaka wewe haimaanishi sijakuelewa au sina akili ambayo haujaielezea ni kitu gani.

Kwanza, naweka wazi msimamo wangu binafsi kuhusu uwepo wa Mungu, mimi ni muumini mzuri tu kwamba yupo.

Pili, vitabu vinavyomuongelea Mungu (namaanisha Biblia takatifu) vimeweka bayana kwamba hatua ya kwanza kabisa, lazima uwe na Imani.

Biblia imeeleza kwa upande wake uweza, mamlaka na sifa za Mungu, leo anakuja mtu kusema hapana, anatakiwa athibitishwe kwa aina anayotaka yeye, haiendi hivyo.
Usipoamini uwepo wa Mungu ni kosa?
 
Usipoamini uwepo wa Mungu ni kosa?

Kosa litoke wapi tena? Nimeeleza hapo juu, ni jukumu la Mungu kujidhihirisha kwa watu, mimi nimesisitiza tu kwamba, bila imani hauwezi kumpendeza Mungu.

Thomas mwenyewe mwanafunzi wa Yesu alipoambiwa amefufuka alikomaa kwamba nisipo muona sisadiki hizo mambo jumbo, ndio Yesu akamwambia aende aguse makovu ya misumari athibitishe, hakumwambia amefanya kosa. Alisema heri wale watakao amini bila kuniona.
 
hahaa..kama Mungu ni muweza wa yote " kweli !!? alishindwa vipi kumfanya mtoto mdogo aweze kumtambua...mpaka asubiri uwezo wa wa binaadamu waweze kumsaidia ktika kumfanya mtoto mdogo aweze kumtambua yeye
Nishauliza sana bila majibu mkuu.
 
Kosa litoke wapi tena? Nimeeleza hapo juu, ni jukumu la Mungu kujidhihirisha kwa watu, mimi nimesisitiza tu kwamba, bila imani hauwezi kumpendeza Mungu.

Thomas mwenyewe mwanafunzi wa Yesu alipoambiwa amefufuka alikomaa kwamba nisipo muona sisadiki hizo mambo jumbo, ndio Yesu akamwambia aende aguse makovu ya misumari athibitishe, hakumwambia amefanya kosa. Alisema heri wale watakao amini bila kuniona.
Na wasioamini itakuwaje?
 
Back
Top Bottom