BADILI TABIA
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 32,772
- 23,163
Kuna mengi ambayo ameyafanya huyu mbunge:
1. Barabara toka Millenium Tower, kupitia Chekechea ya Hindu Mandal hadi Shoppers Plaza inawekwa lami.
2. Daraja la njia fupi toka Rose Garden kwenda School of Journalism Mikocheni limejengwa.
3. Amesaidia kuhamisha soko la Tegeta na Stendi ya Daladala Tegeta toka barabarani kwenda sehemu nzuri zaidi.
4. Amesimamia vema ujenzi wa barabara toka Tegeta Nyuki hadi Bahari Beach kiwango cha lami. Ujenzi umekamilika.
5. Amesimamia vema ujenzi wa New Bagamoyo road na upgrade ya Old Bagamoyo Road.
6. Amepambana sana na uvamizi na ubadilishaji holela wa matumizi ya ardhi iliyotengwa kwa matumizi ya kijamii (KUNDUCHI, WAZO, MADALE n.k.) na kubatilishwa na kupewa watu wenye pesa. Katika hili kikwazo ni madiwani (wa CCM), ambao ndio wawakilishi wa maeneo husika kwenye vikao vya halmashauri pamoja na maafisa wa Halmashauri (inaongozwa na CCM) ambao ndio watekelezaji na ambao hawampi ushirikiano. Hapa ushirikiano wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ulihitajika sana.
7. Amekusanya data za viwanda na mahoteli yote ya jimboni kwake ili kuhakikisha wanalipa kod inayoongeza pato kwa shughuli za maendeleo ya jimbo la Kawe.
8. Amekuwa anakutana na wananchi na kusikiliza kero zao na kupata maoni yao. Angalia video hii
9.Amepigania chuo cha IMTU Kilikuwa kinatoza ada kwa dola za marekani sasa kinatoza kwa fedha za TZ, pia ada ya imeshuka na kuwa fixed.
10. Eneo la Tegeta amesimamia ujenzi wa Shopping mall ya kisasa. Imekamilika.
11. Amehamasisha na kuamsha ari ya vijana na kina mama katika kushiriki kwenye siasa na ameonyesha umahiri na kujiamini kwa hali ya juu jambo ambalo lemesaidia sana kubadili mtazamo wa wamama na wasichana walio wengi kwamba wakina dada nao wanaweza.
12. Ameshiriki unanzishaji na uendelezaji wa vikundi vya kina mama Kawe.
13. Amekuwa na mchango mzuri sana katika kujadili miswada bungeni, na katika kuibua hoja za kitaifa.
Na mengine mengi sana mnisaidie kuongeza.
Ameyafanya yote haya licha ya juhudi za makusudi za Halmashauri (ambao ndio wanapokea fedha za maendeleo za jimbo) na madiwani (ambao ndio wawakilishi wa wananchi wa kata zao kwenye halmashauri) kumkwamisha.
Nahisi nyuzi nyingi zinaletwa hapa kwa sababu wanataka kuona juhudi za makusudi za kumkwamisha zimefanikiwaje.
By the way, kati ya wabunge wote wa Dar hakuna ambaye amezorota kama Abas Mtemvu. Mbona haanzishiwi threads nyingi kama Mdee? Na kuna thread ipo nimejaribu kwa makusudi kupost ili iwe juu tuone kama kweli watu wako objective lakini hakuna anayepost kitu kule.
Fikiria vema!
hivi Dr. Ndungulile nae ana cha kujivunia?
Last edited by a moderator: