Mwanaukweli
JF-Expert Member
- May 18, 2007
- 4,789
- 1,732
Chanzo halisi cha Ugumu wa Kipindi:
Tumejadili mengi lakini tukumbushane pia kuwa Halmashauri ya Kinondoni inatengewa fedha na serikali kuu kwa ajili ya maendeleo. Lakini pia Halmashauri hiyo inakusanya ushuru ambao ni kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya Kinondoni (Kawe ikiwemo). Halmashauri hiyo inaongozwa na meya wa CCM na ina madiwani wengi wa CCM.
Mwaka wa fedha uliopita, Halmashauri ya Kinondoni ilikuwa na TShs. billioni 80 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na matumizi ya maendeleo. Mwezi July 2012 ilikuwa kifanyike kikao cha kujadili mapato na matumizi ya Halmashauri. Hata hivyo kikao kiliitishwa lakini hakukuwa na ajenda na kujadili mapato na matumizi badala yake kulikuwa na ajenda nyingine tu, ikiwemo ya uchaguzi wa Naibu Meya na wenyeviti wa kamati.
Madiwani wa Chadema na CUF walipinga uchaguzi huo kwa kuwa hizo kamati za zamani ndio zilisimamia matumizi, na ripoti yao ilifaa ijadiliwe kwanza kabla ya kuchagua kamati mpya. CCM kwa ubabe wao wa kawaida waliendelea na kumchagua Songolo Mnyonge kuwa naibu Meya na wakachagua viongozi wapya wa kamati.
Mwananchi wa Kawe unayelalamika kuwa kuna kipindi kigumu, hivi hizi TShs. Billioni 80 zilizo mikononi mwa CCM na nyingine za miaka yote tangu uhuru hazihusiki na utatuzi wa kero zako?
Hivi unashindwa kuona kuwa kuna wanaozuia maendeleo yako pale Halmashauri?
Unashindwa kuona kwa kuwa hujui au ndio ushabiki wa kisiasa?