Angalau wewe Mkuu
Mwita Maranya umejibu bila jazba lakini jawabu zako hazitoshelezi. Ingefaa ungeweka angalau data kidogo na/au ratiba kuhusu mikutano hiyo.
Ikiwa hoja ya mleta mada tunaona ni ya kipuuzi, ingekuwa busara na pigo kwa propaganda za Magwanda kuzizima kwa matokeo halisi na data, kuliko kulinganisha kwa kauli kavu na yaliyofanywa na Mkuu wa Wilaya/serikali, vyenginevyo kusingekuwa na haja ya kuwa na wabunge.
Kwa kuwa Mhe. Mdee huwa anaingia humu nahisi ni busara na yeye pia kufanya kama vile alivyofanya Marahemu Regia (R.I.P) au anavyofanya Mhe. Mnyika, aweke orodha ya ahadi zake jimboni na aliyofanya huko au pengine nchini, kulikoni sisi wapambe, wafuasi, wapenzi na wanachama wa CDM kuvurumisha makombora tu.
Mara kadhaa kuna watu humu wamesema kuwa udhaifu mmoja wa wapambe wa vyama vyetu vya upinzani hawapendi kukosolewa wala kupokea ushauri. Ni vizuri basi, haya yanayosemwa kuchukuliwa kama ni changamoto, ikiwa ni kweli zifanyiwe kazi na kama ni uongo zizimwe kwa nguvu ya hoja.