Kipindi kigumu jimboni Kawe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipindi kigumu jimboni Kawe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAFILILI, Sep 15, 2012.

 1. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wananchi wa jimbo la Kawe tupo katika kipindi kigumu cha kukosa mwakilishi aliye makini bungeni katika kipndi cha mwaka 2010 kuelekea 2015. Mbunge aliyeingia kwa mbwembwe nyingi Halima Mdee amekuwa ni zigo lisilosaidia wapiga kura badala yake anajisaidia mwenyewe.

  Tangu amechaguliwa:
  1. Hapendi kuitisha mikutano ili kupata mawazo ya wananchi
  2. Wananchi wa Madale waliopatwa na mashambulizi ya polisi wamekosa pole na msaada wake
  3. Wakazi wa Majipwande wanamlilia kwa kutopata msaada wa mali na faraja toka kwake
  4. Mfuko wa Jimbo haujatolewa maelelezo kwa wananchi
  5. Kushindwa kutekeleza ahadi zake za kuinua kiuchumi vikundi vya vijana na wanawake
  6. Kushindwa kutatua matatizo wanayoyapata vijana wa bodaboda na bajaji

  Hizo ni kero chache ambazo zilitakiwa zifanyiwe kazi na mbunge wetu.

  Kwa kweli wakazi wa jimbo la Kawe tupo katika kipindi tete tunamkumbuka RITA Mlaki ambaye alikuwa karibu na wapiga kura.
   
 2. fugees

  fugees JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 2,587
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Ww c cuf na ccm hata kula hukumpa mdee. kaa pembeni then kula G.
   
 3. fugees

  fugees JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 2,587
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Zigo kushinda jk?
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,731
  Trophy Points: 280
  ...We kweli akili magamba!!!....unamuona Halima Mdee zigo lisilosaidia wapiga kura badala yake anajisaidia mwenyewe...lakini wakati huo huo humuoni DHAIFU alivyo zigo kwa wapiga kura na kujisaidia mwenyewe, mafisadi wenzake, wageni wanaojifanya wawekezaji na familia yake!!!! Ama kweli Nyani haoni......

   
 5. Madame B

  Madame B JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 24,128
  Likes Received: 4,995
  Trophy Points: 280
  Anatunisha kwanza mfuko wake nyumbani.
  Msijali atakuja tu.
   
 6. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,636
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Tunasubiri 2015 tumkabidhi jimbo KIPE,ni wendawazimu anachokifanya huyu dada tena hana adabu anafanya utumbo kwenye jimbo analoishi katibu mkuu wake.
   
 7. ijoz

  ijoz JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 671
  Likes Received: 375
  Trophy Points: 80
  sasa kwanini tunapenda kujustfy udhaifu wa mtu kwa kulinganisha na udhaifu wa Jk? Nafikiri mleta mada kaeleweka,tatizo hapa baadhi tunapenda au kuchukia mada bila kuwa na sababu.
  "sikiliza shauri na kupokea mafundisho upate hekima ya kukufaa siku zijazo" (Meth 19:20)
   
 8. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  dah.... kumbe wabunge wana kazi nyingi sana....
   
 9. T 2015 CDM

  T 2015 CDM Member

  #9
  Sep 15, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Gombea basi wewe tukupe. We unataka mbunge ashugulikie kila kitu? hao wabunge wengine wamefanya nini? Magamba mna shida sana,, hizo pesa za jimbo waulize magamba wenzio maana wao ndo wanajua ziko wapi,,, wala usimlaumu Mdee. Na aliyekutuma mwambie huku JF tuko vizuri magorofani hatujadili hoja zisizo na mshiko. Huwezi anza kumlaumu mbunge wakati bado ana miaka miwili na ushee. Haya zile ahada 77 za mheshimiwa sana mbona huuliziii? kuna meli ngapi zimeshatengenezwa? Je kigoma imekuwa kama Dubai? Reli je? Nakushauri ukiwa bored badala ya kupost vitu kama hivi ingia hapa www.theudaku.blogspot.com:A S-coffee:
   
 10. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Punguza JAZBA hoja ni kuhusu mbunge wetu usipende kuficha udhaifu wake kwa kuleta hoja isiyo na tija. Msaada kwake ni kupokea mawazo na kuyafanyia kazi kwa manufaa ya wakazi wa Kawe
   
 11. I

  Inaniuma Sana Member

  #11
  Sep 15, 2012
  Joined: Sep 14, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hamia mchinga
   
 12. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hoja zinahitaji utekelezaji lakini sio kumlaumu maana aliyeshika kila kitu ni ccm sasa utakapo lalamika hatutakuwa tunamtendea haki yeye anapiga kelele ccm ndio wanafanya ingekuwa serikali iko chini ya chama chake hapo kila lawama zilitakiwa kuelekezwa kwake
   
 13. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #13
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,636
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Hivi kukutana na wanachi na kuwajulia shida zao nalo linahitaji jitihada za serikali ya ccm? mbona katika muda mfupi wa uchaguzi aliweza kuzungukia kata,kaya,mitaa yote ya jimbo lake na kutoa ahadi lukuki zenye matumaini.Any way tutakachokifanya hatoamini majicho yake atabakia kulalamika kuibiwa kula baada ya wananchi kughairi 2015.

   
 14. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #14
  Sep 15, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hapana mkuu ni bora ange kuwa anafanya hata mikutano ya hadhara jimboni mwake kama wenzake wanapotoka bungeni tu inasaidia sana kuepusha maneno kama haya
   
 15. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #15
  Sep 15, 2012
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Hahahah
   
 16. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #16
  Sep 15, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hakuna tofauti yoyote ya kimaendeleo jimbo la kawe tangu aingie halima.labda anajipanga kwa 2015 ndio ataleta maendeleo
   
 17. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #17
  Sep 15, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  hapo manake hatoshi.inabidi uchaguzi ujao tumpe mbunge wa chama kilichopo madarakani ili aweze kutekeleza
   
 18. PROSPER MALLYA

  PROSPER MALLYA Member

  #18
  Sep 15, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Watu makini wanaona anayoyafanya,hatummiss MLAKI
   
 19. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #19
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,029
  Trophy Points: 280
  Mkuu wa Wilaya amefanya nini?
   
 20. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #20
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ni afadhali na bora ww umesema, mie niliisha andika humu zaidi ya mara 10 ahadi na ulaghai wa HM kwa wananchi wa kawe, mpaka sasa hajafanya chochote, yeye ni kwenye kumbi za starehe tu ndio utamuona, halafu tukisema mnasema anaonewa. HM ni janga la sie wana kawe, nadhani katika katiba ijayo kuwe na kipengele cha mbunge akishindwa kazi basi , mtu mwingine atoke kwenye chama chake aje achukue hiyo nafasi. Mie sina shida eti kwa kuwa ametoka cdm , ila cdm next election wamlete mtu makini sio HM hawezi kitu

   
Loading...