What has Halima Mdee done for Kawe (2010-2015)?

What has Halima Mdee done for Kawe (2010-2015)?


Yaani hapa JF kuna katabia cha kuanzisha UZI ili mtu aonekane kuwa naye anajua kuanzisha Mada. Kuna mtindo wa baadhi yetu kuharibu mijadala ya hapa kwa kuchukua mada zilizojadiliwa siku ya nyuma na kuileta upya ili tu aonekane na yeye ameanza.

HII MADA ILIJADILIWA KWA KIREFU SANA WIKI hii KABLA JF HAIJAFUNGWA KWA MATENGENEZO. NA MH. HALIMA MDEE ALIICHANGIA kwa KIREFU SANA.

Sasa kama waungwana tumekosa mambo ya kuandika, ni kwanini tusichangie au kusoma tu kwa kuhabarika mada za wengine ambazo ni mpya, kuliko kuturudisha nyuma.

TAFAKARI KABLA YA KUWEKA uzi MPYA HAPA; MNATUCHOSHA NA KUTUHARIBIA UMAKINI WETU KATIKA KUFIKIRIA MAMBO YA KUCHANGIA KWA KUWA NA HOJA ZISIZOKUWA na MIGUU WALA MASIKIO.



MIZAMBWA
INANUMA SANA!!!
Mizambwa bwana! Cku zote huwa napenda sana comment zako! Ila unabii utarajiwa vipi? Siku hizi umekuja kivingine,inakuuma sana!
 
Siku moja nilitembelea maeneo ya madale nikapita kijiwe kimoja nikaweka kijiwe na mie kujua nini kinaendela vijana wanalalamika kuwa tangu Halima apate Ubunge hajaonekana huko ,Na mmoja akakazia wewe mwache tu tunasubiri 2015Halima please fanya fanya ziara kwa wapiga kura wako
Wananchi hawana jema Kazi Yao kulalama kila Siku. Majimbo karibu yote wanalalama. Ishu sio kutembelea suala ni kutatuliwa kero zao, I hope yupo Katibu wake anafanya Kazi hii.
 
Sidhani kama mhe.Mdee hatarudi tena hapa kurudia kueleza kile alichoeleza hapa...


Mtoa hoja nimegundua kuwa unajambo lako binafsi na mhe. Mdee ,juzi umeweka uzi kama huu na mhe.Mdee akaja hapa mwenyewe na kutoa ufafanuzi mzuri tu, leo tena umerudia yale yale unataka ujibiwe nini zaidi ya majibu uliyopewa?
 
Kama vipi amia Segerea au ukonga huku wanaonekana kila siku,tena kunamaendeleo kibao ,maji ya bomba masa24 na barabara nzuri pia shule zipo nzuri na umeme haukatikagi. Huku kawe na ubungo tuachie sisi.
 
unalalamika mno comrade mbona juzi kwenye harambee hukuonekana na mh alikuwepo? tafiti kwanza kisha uje humu huna data
 
Siku moja nilitembelea maeneo ya madale nikapita kijiwe kimoja nikaweka kijiwe na mie kujua nini kinaendela vijana wanalalamika kuwa tangu Halima apate Ubunge hajaonekana huko ,Na mmoja akakazia wewe mwache tu tunasubiri 2015
Halima please fanya fanya ziara kwa wapiga kura wako
kweli kabisa firstlady1, akidhani amesimama aangalie asianguku, awaangilie akina sugu, zito, mbowe, mnyika, na wengine, mbona tunawasikia majimboni mwao? au ndo kaisha uchoka ubunge?
unajua wakati mwingine hata kama umeshindwa kutimiza baadhi ya ahadi bora urudi kwa ulio waahidi ukatoe feedback vinginevyo hautaeleweka.
Pita pita jimboni mdee, hatupendi kuona haurudi mjengoni 2015
 
kwa nini hamkuchagua video kama mlitaka kuangalia?

na wewe mafilili acha kuhangaika na wanawake wenzio tafuta vidume kama sugu vikupe kitu mpaka ushangae.
 
unasema sisi wananchi umekaa na nani kujadiliana swala la halima kutokuleta maendeleo kwenye jimbo lake? acha unafiki ndugu jisemee mwenyewe lakini usijumuishe wakazi wa kawe wote unajuaje kama kuna maeneo mengine kama kaleta maendeleo ? Kuwa makini na unacho kiandika
 
Ni masikitiko kwa wana Kawe, Mbunge Halima Mdee umekuwa huonekani jimboni mwako hasa majira ya mchana. Umekuwa ni mtu wa kutoka alfajiri ili ukimbie kuonana na wapiga kura, unarudi usiku wa manane.
Kwa kweli waliokushauri uchukue ubunge wa jimbo walifanya makosa makubwa, uwezo wako ni kuwa MBUNGE wa Viti Maalum. Tunakushangaa zimebaki siku chache kwenda kikao cha BAJETI, Dodoma, HAUJATHUBUTU kupita kwa wapiga kura kukusanya maoni ili uyawakilishe BUNGENI. Kwa taarifa yako TUMEKUCHOKA SANA pamoja na chama chako!!

Umetumwa wewe, si bure, kwani mnaishi mtaa mmoja? nnavojua kawe ni kubwa au we ni mzee wa kuweka jungu barazani?
 
BIFU LA VIWANJA TEGETA WAZO KISANGA
Kweli Zaleo ameongea kuhusu magomvi ya viwanja kule Tegeta Kisanga. Nakubali Mh. Halima Mdee unajua sana suala hilo. Mbona mmenyamaza? Au utaenda kule tena ukikaribia uchaguzi 2015? Fuatila vilio vya watu tusijedhani nawe umewekwa mfukoni mwa wajanja wa jiji. Malalamiko rasmi yako Wizara ya Ardhi nawe unazo nakala. Sasa mtanzania wa kawaida unaelewa hawezi kupenya kila mahali hasa ambako wakubwa ndio macho yao ya husda yamekaa, lakini mbunge wetu unaweza na tunakuaminia. Maliza uozo, wenye hela wanatesa sana kunyang'anya viwanja vya watu dhaifu kipesa. Wengine walishajipanga kujenga lakini wamezuiwa na haieleweki nini kinaendelea. Madalali kina Chinga wamewashinda?
 
Je, ndugu yangu hili swali ulishamuuliza Waziri wa Ardhi??

Na alikujibu vipi,



MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
tafuta barua ya Halima aliyomuandikia waziri wa ardhi baada ya jk kurecycle baraza la mawaziri, ipo humu humu na majibu yako yote utayakuta huko
 
Duh...huyu Mdee mbona wakazi wa jimbo la Kawe wamemkalia kooni hivi...inawezekana kweli akawa hafanyi kazi aliyoahidi eenh?!
 
Halima Mdee + John Mnyika = Hodari wa kupiga maneno, UFUATILIAJI ni ZERO. Wabunge hawa wameshajijua 2015 hawarudi mjengoni hivyo wanashughulika na mambo yao binafsi kuliko kusikiliza na kufanyia kazi kero za wananchi.

Wananachi wa ubungo wanajuta kumpa kura Mnyika, wa Kawe wanasema afadhali enzi za Rita Mlaki alikuwa msikivu na mfuatiliaji
 
Halima Mdee + John Mnyika = Hodari wa kupiga maneno, UFUATILIAJI ni ZERO. Wabunge hawa wameshajijua 2015 hawarudi mjengoni hivyo wanashughulika na mambo yao binafsi kuliko kusikiliza na kufanyia kazi kero za wananchi.

Wananachi wa ubungo wanajuta kumpa kura Mnyika, wa Kawe wanasema afadhali enzi za Rita Mlaki alikuwa msikivu na mfuatiliaji
Hapo kwenye bold ya mwanzo ndio wadudu gani hao? Na hapo kwenye bold ya pili:Kama huyo hawara wa Mkwerre alikuwa msikivu na mfuatiliaji je, Halima Mdee angekuta kero hizi zinazotamkwa? Kwa Tz lolote linawezekana, kwani kama Mkwerre hakuwahi kuwa msikivu na bado "alishinda" kimagumashi kwenye uchaguzi mkuu uliopita, ishindikane vipi kwa hawa wateule wa wananchi?
 
tafuta barua ya Halima aliyomuandikia waziri wa ardhi baada ya jk kurecycle baraza la mawaziri, ipo humu humu na majibu yako yote utayakuta huko

Sasa ndugu yangu, wewe kama unakumbuka ilikuwa rahisi kuipata. Sasa mimi sijawahi hata kusikia au kuona thread ya aina hiyo nitawezaje kuipata? Labda moderator akumbuke. Au aliyeileta atakuwa na nakala labda ailete tena tupate majibu hayo. Maana kweli wenye hela wanasumbua sana kunyanyasa watu kwenye viwanja vyao, hasa kwa sababu wanatumia mbinu ya "tunashughulikia mtua aiendeleze hadi tutakapompa kibali", lakini wenye hela wanachimba msingi na kupandisha kuta wewe unaona, ukienda pale unakuta FFU kabisa na ndusu zao wanasimamia ujenzi wa mporaji!!!!!!! Kwa macho yangu nimeona. Mahakamani jamaa haliendi hata mara moja wala anayemwakilisha, kesi zinasomwa weeee, nenda rudi nenda rudi lakini mwishoni wanaishia kusema lijamaa liporaji limeshinda kesi na makaratasi feki feki kabisa! Uuuuuwiii!
 
Back
Top Bottom