Dkt. Maguha: Takwimu zinaonesha Saratani ya Mlango wa Kizazi inasumbua Wanawake wengi ikifuatiwa na Saratani ya Matiti

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Katika kuhakikisha elimu inawafikia watu wengi zaidi kuhusu Ugonjwa wa Saratani, Taasisi ya Ocean Road imeanza Kampeni ya kutembelea Hospitali za Rufaa za Mikoa ili kushirikiana na Wataalam mbalimbali.

Dkt. Maguha Stephano ambaye ni Meneja wa Huduma za Kinga anazungumzia kuhusu huduma hiyo ambapo kwa sasa wapo Mkoani Singida.

3e3de214-338f-45aa-8950-c41541f5eaf6.jpeg

Madaktari walipofika kujitambulisha kwa Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Victorina Ludovick (mwenye suti nyeusi), kulia ni Dkt. Maguha Stephano ambaye ni Meneja wa Huduma za Kinga wa Taasisi ya Saratani Ocean Road

Ameeleza kuwa huduma hiyo ya vipimo na elimu kuhusu ugonjwa huo ilianza kutolewa Alhamisi ya Septemba 21 2023 na inatarajiwa kumalizika Jumapili Septemba 24, 2023.

Akifafanua kuhusu huduma wanazotoa ambapo timu ya Wataalam 14 wa ubingwa tofautitofauti kutoka Ocean Road ambapo wanashirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Singida iliyopo Mandewa anasema:

“Kama tunavyofahamu kuwa Ugonjwa wa Saratani sio wa kuambukiza na kwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na changamoto katika Taifa letu, mfano katika Taasisi ya Ocean Road zaidi ya 75% ya Wagonjwa wa Saratani wanaofika kwa ajili ya matibabu au vipimo wanafika wakiwa katika hatua kubwa za ugonjwa huo, ndio maana Taasisi imeona kuna umuhimu wa kufanya kampeni hii.
1660d0e8-dd76-4d13-906c-d822a40f0936.jpeg

39056da7-f989-4f85-9b88-fa15dd2214d5.jpeg

Wataalam wakifanya vipimo vya Saratani

“Uamuzi huo umechagizwa na maelekezo ya Rais Samia Suluhu ambaye alitoa agizo kwa Hospitali za Kibingwa kufika kwenye Hospitali za Mkoa kutoa huduma hizi, lengo likiwa ni kuwafikia Wananchi wenye kipato cha chini ambao hawana uwezo wa kufika katika Taasisi kama Ocean Road kupata huduma.

“Huduma nyingine tunazotoa katika mchakato huu ni Elimu ya Saratani, jinsi ya kujikinga kwani uchunguzi wa Saratani unahitajika kufanyika hata kama hauna dalili.

“Pia tunatoa huduma za Saratani ambazo zinawakumba watu wengi na ni changamoto kwa asilimia kubwa ya Wagonjwa hapa Nchini.

“Upande wa kina mama Saratani ya Mlango wa Kizazi ndio inayoongoza, takwimu zetu zinaonesha zaida ya 43% ya wanasumbuliwa na changamoto hiyo ikifuatiwa na Saratani ya matiti.

"Ikumbukwe kuwa huduma hii tunayoitoa hapa ni bure kama ambavyo tunatekeleza maagizo ya Rais aliyotoa, hiyo pia inaambatana na huduma ya kumuona daktari bingwa, nawasisitia watu wa Singida wana nafasi ya kuja kupata huduma ya vipimo bila malipo kwa kuwa Jumapili ya Septemba ndio itakuwa mwisho kwa hapa Singida."
a99bb008-d657-4175-b49e-57154ef257c3.jpeg

Huduma ya vipimo ikiendelea
 
Back
Top Bottom