kingunge awashangaa wabunge wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kingunge awashangaa wabunge wa CCM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ochu, Aug 28, 2008.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  katika hali ya kushangaza Mbunge wa kuteuliwa Kingunge Ngombare mwiru amewashangaa wabunge wa CCM wanaoiponda serikali kwa madai ya maslahi ya taifa badala ya kukutetea na kukilinda chama chao. Amesema katika hali hii wabunge wa CCM wanasaidia wapinzani bila kujijua.
  alitoa kauli hiyo juzi wakati anapokea maandamano ya wanaCCM wa dodoma walioandamana kuunga mkono hotuba ya rais bungeni
   
 2. LESIRIAMU

  LESIRIAMU JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2008
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 4,006
  Likes Received: 2,223
  Trophy Points: 280
  Huyu babu kapitwa na wakati. Haelewi anachozungumza, kwani wabunge wako kwa maslahi ya chama au maslahi ya Wananchi??

  Sijui kwanini bado anaongea anatakiwa akapuzike ili angalau awekwe kwenye historia nzuri. Otherwise tutahitaji kupima ubongo wake ili ieleweke kama anaweza kutoa ushauri kwa Taifa muda huu.
   
 3. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kingunge alipuka

  na Rahel Chizoza


  “Tumegundua nia ya wapinzani ni kutaka kukidhoofisha chama chetu, hawawezi na sisi tumejipanga imara, si tu kwamba wakinawa hawatakula, bali pia hawatakiwi hata kunawa”

  MKONGWE wa siasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Kingunge Ngombale-Mwiru, amewashangaa viongozi wa chama hicho wanaoiponda serikali kwa madai ya kutetea masilahi ya taifa.

  Kingunge alitoa kauli hiyo juzi baada ya kupokea maandamano yaliyoandaliwa na CCM Mkoa wa Dodoma, kwa lengo la kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete kwa hotuba aliyoitoa bungeni mwishoni mwa wiki.

  Alisema kila kiongozi aliyepo ndani ya CCM, amepata umaarufu kupitia chama hicho na si kwa juhudi zake binafsi.

  “Wanaodhani umaarufu walionao umetokana na wao wenyewe, wanajidanganya, hebu wasimame peke yao tuwaone kama wataendelea kuwa maarufu, umaarufu huo ni kwa ajili ya chama chao na madaraka waliyonayo yametokana na chama,” alisema Kingunge mbele ya waandamanaji wachache waliojitokeza.

  Alisema viongozi wa CCM wanapaswa kuwa makini, vinginevyo watajikuta wakiwasaidia wapinzani katika kukivuruga chama na serikali kwa kisingizio cha kusimamia masilahi ya taifa.

  Ingawa hakutaja majina ya wana CCM aliokuwa akiwazungumzia, ni dhahiri mkongwe huyo alikuwa akiwalenga baadhi ya wabunge wa CCM wa aina ya Spika wa Bunge, Samuel Sitta (Urambo Magharibi), Anne Kilango (Same Mashariki), Harrison Mwakyembe (Kyela), Aloyce Kimaro (Vunjo) na Christopher ole Sendeka (Simanjiro), ambao wamekuwa mbele kuikosoa serikali, hasa katika masuala yanayohusu masilahi ya taifa, hususan vita dhidi ya ufisadi.

  Kingunge alisema hivi sasa kuna tabia iliyozuka kwa wabunge wa upinzani kuanzisha hoja na kudai si ya upinzani bali ya kitaifa, hali inayosababisha baadhi ya wabunge wa CCM kujiingiza katika kutetea hoja hizo bila kujua kwamba kwa kufanya hivyo, wanakidhoofisha chama chao.

  “Umezuka mtindo hivi sasa, wapinzani wanaibua hoja ili kuwakamata vizuri CCM, wanasema hoja hii ni ya kitaifa, kwa masilahi ya wananchi, hivyo viongozi wetu wa CCM nao wanajikuta wakiingia katika mijadala hiyo bila kujua kwamba wanachofanya ni kukidhoofisha chama,” alisema.

  Mkongwe huyo wa siasa alikwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa wapo wana CCM wanaorukia hoja za wapinzani kwamba wanazungumzia masilahi ya taifa bila kujua lengo la wapinzani ni kutaka kuwamaliza kisiasa.

  Aliwataka wana CCM kuwa na umoja na kuwataka wanaounga mkono hoja za wapinzani, kuacha kufanya hivyo mara moja.

  “Umaarufu wa magazetini haufai, ni wa kupita tu, na inapofikia kipindi fulani, hata hayo magazeti yanakusahau, wapo wengi tuliwaona, lakini wako wapi sasa?” alihoji Kingunge.

  Aliwataka wanaojiingiza kwenye hoja za wapinzani na kuzizungumzia kwa nguvu, watafakari kabla ya kukurupu na wajitahidi kuweka mbele masilahi ya chama chao.

  Kingunge aliwataka wana CCM kuwa makini na vyama vya upinzani, kwani si vya kuvibeza.

  “Wapinzani hawana hoja wala sera za kueleweka, ndiyo maana wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali za kuwarubuni wana CCM kwa kuwataka wachangie hoja zao baada ya kuzipa nguvu na kuziita hoja za kitaifa.

  “Tumegundua nia ya wapinzani ni kutaka kukidhoofisha chama chetu, hawawezi na sisi tumejipanga imara, si tu kwamba wakinawa hawatakula bali pia hawatakiwi hata kunawa,” alisisitiza.

  Kuhusu suala la Muungano ambalo limezua mjadala wa muda mrefu na kuhitimishwa na Rais Kikwete katika hotuba yake aliyoitoa bungeni, alisema walioanzisha mazungumzo hayo wana ajenda zao za siri.

  Aliwashangaa pia viongozi wa CCM walioingilia kati na kuanza kuzungumzia suala la muungano bila kujua kwamba wanajimaliza wenyewe.

  “Wanaozungumzia muungano hivi sasa, miaka yote walikuwa wapi kama si kutaka kusababisha vurugu na kutaka kuiyumbisha serikali?” alisema Kingunge.

  Kingunge anatoa kauli yake, siku chache tu baada ya Spika wa Bunge kutoa matamshi muda mfupi baada ya Rais Kikwete kulihutubia Bunge, ambayo baadhi ya wana CCM wameyatafsiri kuwa yaliyokuwa yakilenga kuikosoa serikali na rais mwenyewe.

  Aidha, kauli hiyo ya Kingunge inakuja wakati baadhi ya wabunge wa chama hicho tawala wakiwa mstari wa mbele kuikosoa serikali kwa namna inavyoshughulikia masuala mbalimbali, kama mikataba ya madini na ufisadi wa Richmond na EPA
   
 4. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2008
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Huyu babbu bila shaka anahitaji maombi.
   
 5. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  haka kababu kameshachanganyikiwa kanahitaji kukimbizwa Milembe!Sijui kanadhani bado kako Russia maana ni so conservative!Hakana ajenda kamekalia majungu tuu!
  Yaani kenywe kanadhani CCM ndiyo nchi?
  Mungu akasamehe!
   
 6. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2008
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  and we still wondering why we are moving so FAST backwards....huyu jamaa yuko bungeni, kijiwe cha kuwakilisha wananchi....do you want me to say more.?.
   
 7. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ....there we go again.... the unfortunate fact of life that we can have senility!! :(
   
 8. RR

  RR JF-Expert Member

  #8
  Aug 28, 2008
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Mzee Kinje tunahitaji busara zako (kama bado zipo), lakini katika hili tafuta wengine!
   
 9. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #9
  Aug 28, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ashauriwe kupunguza kuzungumza kwani tangu wakati wa EPA alijitokeza na kuisema kuwa ni uzushi sasa sijui anajisikiaje baada ya mambo kuwa hadharani sasa.

  Akiendelea kuzungumza heshima yake itaendelea kupotea mbele ya jamii kila siku ,kwanini asiwe kimya kama wazee wengine?ama anafikiri kuwa yeye anajua zaidi?
   
 10. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #10
  Aug 28, 2008
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Sijui kwa nini hakafi haka kababu kajinga? Hata meno mdomoni hakana bado kanazungumza. Kalaaniwe kwa Jina la Yesu kwa kauli zake zisizo na hoja na mema kwa nchi hii.
   
 11. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #11
  Aug 28, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  he he he ... kazinduka ... nasikia buguruni kulikuwa na babu mmoja akilala basi mpaka mwezi ukatike ndo anaamka ... halafu anaanza kuhadisiwa kila kitu kimoja badala ya kiingine ... kwa walokufa hujikuta akilia pekeyake huku wengine wameshasahau , mtoto alokosa anataka amwaadhibu ilhali jambo limeshapita .... mhhh!
   
 12. Geeque

  Geeque JF-Expert Member

  #12
  Aug 28, 2008
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 848
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Is Kingunge still alive? Duh mimi nilidhani ameshakatika long time, just imagine huyu mtu alipigana kwenye vita vya MajiMaji na kina Kinjeketile Ngwale mwaka 1905 lakini mpaka leo anadunda. Au ni clone wake ndio anaongea hizi pumba.
   
 13. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #13
  Aug 28, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mijitu mingine haina hata aibu!
   
 14. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #14
  Aug 28, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Why would anyone accomodate the garbage coming out of this corrupt and obselete leader?

  But on the other hand, I am glad he came out in public and clarified the Ibara ya 15.1 the one I spoke months ago about CCM putting self interest in forefront and not Nations well being!
   
 15. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #15
  Aug 28, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Masikini Kingunge, mwachie Kinjeketile tujibizane naye kwani umepitwa na wakati. Wote wale uliowafunda siasa pale chuo cha TANU Kivukoni kwenye miaka ya sitini na sabini tayari wamestaafu siasa na wanatumbua kwa kutumia mbinu ulizowafunulia. Hawa wa sasa ni wa kizazi kipya, kalagabaho.......
   
 16. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #16
  Aug 28, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kingunge kasema kuwa kumbe wao kuwa madarakani, yaani CCM ni kula ndio maana anasema hata wakinawa hawatakula na pia hawatawaruhusu kunawa.

  Kuna mpango wa kuwauwa?
   
 17. F

  Fataki Senior Member

  #17
  Aug 28, 2008
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tofauti ya Kingunge na wabunge aliowataja ni kuwa yeye ni viti maalum!
   
 18. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #18
  Aug 28, 2008
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Source:http://www.chadema.net/blogu/mnyika/2008/03/kingunge-alijivunjia-mwenyewe-heshima.html


  Kingunge alijivunjia mwenyewe heshima


  Hebu nikukumbushe kauli zake kidoooooooooogo---

  TAMKO KUHUSU KAULI ZA KINGUNGESisi, viongozi wa vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzina TLP tuliokutana Equator Hotel tarehe 20 Septemba2007 hapa Arusha tumeitafakari “Orodha yaMafisadi”(List of Shame) na tumejadili kauli za Waziriwa Nchi, Ofisi ya Rais, Siasa na Uhusiano waJamii-Mheshimiwa Kingunge Ngombale-Mwiru alizozitoa 18Septemba 2007 na kunukuliwa na vyombo mbalimbali vyahabari Jumatano 19 Septemba 2007 na kwa pamojatumeazimia kutoa tamko lifuatalo:Kingunge anapotosha umma, apuuzwe; wapinzani wanateteataifaTunaunga mkono uamuzi wa viongozi wetu wa kitaifakuanika wazi kwa umma orodha ya mafisadi; hii ni kwasababu rasilimali zinazofujwa ni za wananchiwatanzania, wanaoathirika kutokana na ufisadi ni ummawa watanzania na wenye uamuzi wa mwisho wakuwawajibisha viongozi mafisadi ni umma wa watanzania.Kwa kuzunguka nchini kueleza yaliyotokea bungeni(hususani kusimamishwa kwa Mbunge Zitto Kabwe nakupigwa danadana kwa hoja ya kashfa ya ufisadi ndaniya Benki Kuu iliyokuwa iwasilishwe na Dr WilbroadSlaa) wakati wa Mkutano wa Bunge la Bajetiuliomalizika hivi karibuni, wabunge wa upinzaniwanatimiza wajibu wao kama wawakilishi wa kweli wawananchi. Kwa kuzunguka nchini kueleza kuhusu ufisadiunaendelea nchini, viongozi wa upinzani wanatekelezawajibu wao wa kisiasa wa kuwazungumzia wananchi wotewa Tanzania wanaoguswa na ufisadi bila kujali itikadiama uanachama; ikumbukwe kuwa vyama vya siasa siovyombo vya uchaguzi tu bali ni taasisi muhimu katikajamii katika kuchochea uwajibikaji na maendeleo. Kwamantiki hiyo basi Waziri Kingunge anaupotosha ummaanaposema kwamba ziara za viongozi wa upinzanizinatokana na ‘hasira ya kushindwa uchaguzi mkuu 2005,kambi ya upinzani kushindwa kumtetea Zitto bungeni,wivu wa kuona CCM inatekeleza ilani yake vizuri, nakwamba wanautumia vibaya mfumo wa vyama vingi’.Tunapenda kusisitiza kuwa Viongozi wa umma wanaokiukana/au kuvunja masharti ya katiba ya Jamhuri yaMuungano na Sheria za Maadili ya Viongozi wa ummalazima waanikwe hadharani na kuwajibishwa na yoyoteanayetoka kauli ya kubeza jitahada hizi ni vyemawatanzania wakampuuza. Kama viongozi wa upinzaniwanavunja sheria kwa kutoa uzushi na kufanya uchochezikama Waziri Kingunge anavyodai kwa nini serikalihaiwakamati na kuwapeleka mahakamani badala ya kutoamatamko ya kulalamika?Kauli za Kingunge ni msimamo wa Serikali?; Ikulu itoetamko!Tumezijadili kauli za Waziri Kingunge na katika hatuaya sasa tusingependa kuamini kama zinawakilishamsimamo wa serikali kwa ujumla wake; hatutaki kuaminikwamba kauli hizo ni msimamo wa pamoja wa Serikalichini ya Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekitiwa Baraza la Mawaziri. Katika hatua ya sasatunazichukulia kauli hizo kuwa ni maoni binafsi yaBwana Kingunge mpaka hapo Ikulu itakapothibitishavinginevyo; hivyo kwa tamko hili tungependa ikulu itoeufafanuzi kuhusu kauli hizo. Lakini tunapenda piakutoa tahadhari kwamba inawezekana kauli hizi za BwanaKingunge amezitoa kwa nia ya kupoteza lengo tuanzekuzijadili kauli zake badala ya kujadili orodha yamafisadi na hatma ya rasilimali za nchi yetu. Hivyotungependa kusisitiza kuwa ikulu ijibu hojazilizotolewa na viongozi wa upinzani ambazo zimemgusamoja kwa moja Rais na serikali.Anayelinda ufisadi ndiye anayekwamisha maendeleo nahuduma za kijamiiTunashangazwa na uamuzi kauli ya Kingunge kwambauamuzi wa Viongozi wa Vyama na Wabunge wa Upinzanikuzunguka nchini ni mkakati wa kisiasa wa kuitoaserikali kwenye mstari wa kushughulikia maji, afya nabarabara. Tunapenda kumbukusha Waziri Kingunge kuwakatika orodha hii ya mafisadi pekee zaidi ya shilingitrilioni 1.3(1,300,000,000,000) ambazo kamazingetumika vizuri ni wazi zingeweza kutumikakuboresha maji, umeme na barabara bila kuendeleakuwakamua zaidi wananchi masikini. Ukweli ni kuwa kwakuendelea kulea ufisadi serikali inajitoa yenyewekwenye mstari wa kutumia vyema kodi za wananchi narasilimali za taifa katika kushughulikia shughuli zamaendeleo na huduma za kijamii ikiwemo maji, afya nabarabara. Ni ukweli pia kwamba kwa kuwawajibishamafisadi viongozi wa upinzani wanatimiza wajibu wao wakuhakikisha rasilimali za taifa zinatumika kwa ustawiwa wananchi walio wengi.Vyombo vya dola tayari vinayo orodha ya mafisadi;vichukue hatuaTunashangazwa na kauli ya Waziri Kingunge ya kuhojisababu za Viongozi wa Upinzani kushindwa kuziwasilishakwenye vyombo vya dola tuhuma walizozitoa dhidi yavigogo hao iwapo kweli wanao ushahidi wakuzithibitisha. Tunashangazwa na kauli hii kwa kuwatunaamini kabisa Waziri Kingunge anafahamu kabisa kuwasehemu kubwa ya tuhuma hizi zipo katika Ripoti zaMkaguzi wa Serikali ikiwemo ile ya mwaka 2005/06 nakwamba vyombo vya dola vinafahamu uwepo wa tuhuma hizilakini kwa zaidi ya miaka miwili vyombo hivyohavijachukua hatua dhidi ya vigogo waliotajwa.Tunaamini kwamba viongozi wa upinzani walichofanya nikuamua kushtaki kwa wenye mali walioibiwa ambao niwananchi wote wa Tanzania ili kwa pamoja tuwezekuvitaka vyombo vya dola viweze kuchukua hatua.Tunashangazwa na kauli hii ya Waziri Kingunge ya‘kuwahukumu’ viongozi wa upinzani kwa kushindwakupeleka ushahidi kwa kuwa kauli hii inapingana nakauli zingine ambazo zimewahi kutolewa na viongozi waserikali kuhusu tuhuma hizo hizo. Tunapendakumkumbusha Waziri Kingunge kwamba tayari Spika WaBunge-Samuel Sitta alishasema kwamba anavipelekapolisi vielelezo vyote vya ushahidi alivyotoa Dr Slaaili vichunguzwe. Pengine Kingunge angetoa hukumu hiyokwa Spika kwa kushindwa kupeleka vielelezo. Piaikumbukwe kwamba ni serikali hiyo hiyo iliyowahi kutoataarifa kwa umma kwamba tuhuma za ufisadi ikiwemo zaBOT zinachunguzwa na TAKUKURU. Kadhalika WaziriMkuu-Edward Lowasa alitoa kauli baadaye kwambaSerikali iliyafahamu madai ya Kashfa ya ufisadi BenkiKuu(BOT) kabla ya upinzani. Kwa upande mwingine, madaiya kutaka kushughulikia rushwa kubwa kubwa ikiwemo zakwenye mikataba yalianza kutolewa na Rais Kikwetewakati akifungua Mkutano wa Kwanza kabisa wa Bungemwaka 2005. Lakini baadaye ni Rais Kikwete alinukuliwana vyombo vya habari akisema kwamba anawafahamu walarushwa na anawapa muda wajirekebishe; tulitarajiaWaziri Kingunge kama mshauri wa Rais wa masuala yasiasa angemshauri apeleke ushahidi katika vyombo vyadola na si kuwahukumu viongozi wa upinzani ambaowametoa orodha ya mafisadi na ushahidi kutoka kwenyetaasisi za serikali yenyewe!. Na ni jukumu la vyombovya dola kuchukua hatua za kufuatilia baada ya orodhaya mafisadi kuwekwa hadharani.TAKUKURU inajipotezea imani yenyewe!Tumeshangazwa pia na kauli ya Waziri Kingunge yakuwalaumu viongozi wa upinzani kwa kutokuwa na imanina TAKUKURU. Kwa misingi ya kauli zao ambazo wamezitoakatika nyakati mbalimbali, viongozi wa upinzaniwamekuwa wakikisisitiza kuwa TAKUKURU inajipotezeayenyewe imani kwa wananchi kutokana na taarifa zake nakwamba wamekuwa wakiipa changamoto TAKUKURU kuchukuahatua. Mathalani TAKURU kuisafisha kampuni yaRICHMOND. “….hakuna ushahidi wowote uliopatikanakuthibitisha vitendo vya rushwa, uzembe na upokeaji wakamisheni watendaji wa serikali….uchunguzi huoumethibitisha udhaifu wa kawaida katika utendaji naambao haukuhusisha rushwa au manufaa ya aina yoyoteile kwa upande wa watendaji na hakuna hasarailiyosababishwa na udhaifu huo”(Mwananchi 12/5/2007).“….baada ya kuona hivyo, Richmond ilionekana kufahamumwenendo wa mambo serikalini…”(Tanzania Daima12/5/2007). Maswali yaliyobaki mpaka hivi sasa ambayosi TAKURU wala TAKUKURU ya sasa hawajayajibu ni pamojana: Ni kwanini Kamati ya Waziri Mkuu iliipa tendaRichmond baada ya Bodi ya Wakurugenzi ya Tanescokuitaka bodi yake ya sabuni kutangaza upya zabuni hiyokwa kutimia zabuni za kimataifa? Richmond kuwezakufahamu mwenendo wa mambo ya ndani serikalini sioishara ya rushwa ya kimadaraka? Ni kweli kama hakunahasara iliyosababishwa na uamuzi huu wakati ambapowatanzania wamekaa bila umeme kwa miezi mingi bilakupata umeme wa dharura waliotarajia wakati wadharura, Rais amekiri kwamba umeme ulichangia kushukakwa kasi ya ukuaji wa uchumi na hata kuongeza mfumukowa bei na mpaka leo bado megawatts 100 hazijatimizwana Richmond/Dowans? Tunapenda kumkumbusha WaziriKingunge kwamba Mkataba wa Richmond/Dowans pekeeumeligharimu taifa zaidi ya Bilioni 200 mpaka sasaambazo zingeweza kuelekezwa kwenye elimu, afya nabarabara. Viongozi wa upinzani wanapohoji utendaji waTAKUKURU wanataka ichukue hatua za harakakushughulikia mafisadi na kuendelea kuwa Taasisi yaKuzuia na Kudhibiti Rushwa na si Taasisi ya Kulinda,Kusafisha ama Kutetea Rushwa !Wasomi na asasi za kijamii wako sahihi; Kingungeamelewa madarakaTumefadhaishwa na kauli ya Waziri Kingunge kwambawasomi nchini wametathimini uamuzi wa Bunge wakumsimamisha Mbunge Zitto Kabwe kwa kutanguliza jazbabadala ya busara na kutilia wasiwasi uelewa wa makundiya kijamii kuhusu mantiki ya uzalendo. Hatutakikuamini katika hatua ya sasa kwamba huu ni msimamo waserikali kwamba wasomi na makundi ya kijamiiwametanguliza jazba na kukosa busara na uelewa katikakuijadili adhabu aliyopewa Mbunge Zitto Kabwe na hojayake ya kutetea Rasilimali za nchi yetu hususanimadini. Tunaamini kwamba kauli hii ni maoni binafsi yaBwana Kingunge ambayo ni ishara ya kulewa madarakakutokana kung’ang’ania serikalini toka wakati nchi hiiinapata uhuru kwani hii si mara ya kwanza kutoa kauliza kubeza-aliwahi kuibeza CHADEMA kwa kumtaja Nyererekwenye kampeni 2005 na hivi karibuni Julai 3, 2007aliripotiwa na vyombo vya habari akitetea msimamo waRais Kikwete wa kutumia nafasi yake kama raiskudhoofisha upinzani kwa kufanya kampeni za CCM katikamikutano ya kiserikali. Tunapenda kumbukusha WaziriKingunge maneno ya Shaban Robert kwamba “ elimuilipokuwa bado kujulikana mvi zilihesabika kuwa alamaya hekima lakini fikra hizo wakati wake umeshapitahaupo na wala hauji tena. Kisichobadilika ni kwambamtu mzima bado anastahili heshima kutoka kwa mdogo” .Ni vyema Waziri Kingunge akafahamu kwamba wasomi kamaProfesa Issa Shivji na makundi ya Kijamii mathalaniMtandano wa Jinsia(TGNP), Chama cha Wanasheria waMazingira(LEAT), Kituo cha Sheria na Haki zaBinadamu(LHRC) walifanya tathmini yao kwa lengo lakulinda maslahi ya taifa bila kujali itikadi.Mafisadi zaidi waendelee kutajwa; serikali ijibu hojaHivyo tunapongeza na tutaendelea kuunga mkono jitahadazote za vyama vya siasa, asasi za kijamii na hata watubinafsi waliowataja na watakaoendelea kuwatajaviongozi na/au maafisa wa umma na/au mawakala na/auwashirika wao katika sekta binafsi ambao kwa namnambali mbali wameshiriki katika kupora utajiri na/aufedha za umma na hivyo kulisababishia taifa na umma waWatanzania ufukara na/au umaskini mkubwa. Kadhalikatunaunga mkono na kutoa mwito kwa vyama vya siasa,asasi za kijamii na hata watu binafsi kuendeleakuwawajibisha viongozi wa umma ambao kwa kutumianyadhifa na/au vyeo vyao katika utumishi wa ummawamefanya maamuzi ambayo yamesababisha taifalimepoteza mapato na/au utajiri na rasilmali zake nakuwaneemesha raia na/au taasisi za kiuchumi na/au zakibiashara za kigeni. Kwa mfano, viongozi wa ummawalioshiriki katika kusaini mikataba mibovu katikasekta za madini na/au nishati na/au maeneo mengineyenye umuhimu mkubwa kwa maisha ya taifa na jamii yaWatanzania. Na katika haya tunataka serikali ijibuhoja na si kupuuzia na kutoa kauli za kejeli kama "haoni wapinzani hawana jingine la kufanya", "wana haki yakutoa maoni yao na huo ndio uzuri wa demokrasia" .Waziri Kingunge na serikali kumbukeni kuwa watuwachache wanaweza kudanganyika katika muda mchachelakini watu wote hawewezi kudanganywa wakati wote.Watanzania wa leo na kesho si watanzania wa jana najuzi.John MnyikaMkurugenzi wa Vijana Taifa (CHADEMA)Na Mwenyekiti wa KikaoGodbless LemaKatibu Mwenezi Mkoa-Arusha(TLP)Na Msemaji wa Ushirikiano wa Vyama vya Upinzani-ArushaMohamed MaabadMwenyekiti wa Wilaya-Arusha Mjini(CUF)Na Mwenyekiti wa Ushirikiano wa Vyama vyaUpinzani-ArushaEned MuroMwakilishi-Arusha(NCCR-Mageuzi)Amos KibandaKatibu Mkoa-Arusha(CHADEMA)Calist LazaroMwenyekiti wa wilaya-Arusha Mjini (TLP)

  posted by John Mnyika at 12:58 PM
   
 19. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #19
  Aug 28, 2008
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,213
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu Kingunge angekuwa kiongozi mkuu wa nchi, angekuwa na tofauti gani na Mugabe?
   
 20. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #20
  Aug 29, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  na kama huyu ndie mshauri mkuu wa rais katika siasa tutegemee nini?
   
Loading...