kingunge awashangaa wabunge wa CCM

Anne Kilango Malecela na Mbunge wa Vunjo Aloyce Kimaro wameibuka na kumwamwambia Kingunge kuwa ni nabii wa mafisadi. wamemtaka atofatishe CCM ya mwaka 1977 na sasa. wamesema Nyerere angefufuka angemzaba kibao kwa maneno anayoyaongea kuhusu mafisadi
 
Ochu,

pinda_kingunge.jpg

Jamani hiyo sura na hayo macho!! Angekuwa Shinyanga saa hizi angebakia historia - mapanga mtindo moja. Halafu huyo Pinda angalia alivyopinda - kweli hawezi kufurukuta.
 
na kama huyu ndie mshauri mkuu wa rais katika siasa tutegemee nini?

Tutegemee kikwete kulinda masilahi ya ccm no matter CCM watachemka kiasi gani, Tanzania inabidi tusali sana maana hii ni ishara tosha kuwa haki haitakaa itendeke especial pale Mtu wa ccm atakapokuwa anahusika.
HIVI KIKWETE NI RAISI WA CCM AU? MAANA ANANICHANG'ANYA SOMETIME
LABDA TUMKUMbUSHE YEYE NI raisi wa nchi, MAMBO MENGINE ANATAKIWA AMWACHIE MAKAMBA,
EEH MUNGU KWANINI ULIMCHUKUA BALALI ALIYEKUWA NA USHAIDI WOTE WA EPA UKAMWACHA KING'UNGE ANAYETAKA KUTUMALIZA WATANZANIA KWA MASLAI YA CCM.TUEPUSHILIE HILI BALAH EE BABA TWAKUOMBA, USIACHE MWAKA HUU UPITE KABLA YA KUTENDA MIUJIZA SISI WANAO WANYONGE TUNALIA KWANI hatuna kimbilio tena kwani serikali yetu ndio hiyo inalinda maslai ya ccm, asante baba kwa kuwa utawachukua wote waliohusika na ufisadi na kwenda kuwaadhibu ipasavyo, kwani tunaamini machozi yetu yanayotiririka kutokana na ufisadi hayatamwagika yote bila wewe kutujibu.
 
unafiki na kutokutambua maslahi ya taifa ndio kinachotumaliza.
usishangae rais au waziri yuko kwenye ziara ya kitaifa lakini utakuta wapambe wake wamevaa sare za CCM... hii siyo sahihi. kampeni zikishaisha hakuna cha chama wala nini bali utaifa
 
Kilango amvaa Kingunge

2008-08-29 09:34:01
Na Simon Mhina

Wabunge wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bi. Anne Kilango Malecela (Same Mashariki) na Alloyce Kimaro (Vunjo) wamesema mwanasiasa mkongwe nchini, Bw. Kingunge Ngombale Mwiru ana mawazo mgando na kumtaka atofautishe CCM ya mwaka 77 na hii ya sasa.

Aidha wamesema kauli ambazo Bw. Kingunge ametoa jana, zinaashiria kwamba anazeeka vibaya na atamaliza vibaya.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Nipashe kwa njia ya Simu jana, wabunge hao ambao wapo mstari wa mbele kupambana na ufisadi, walisema wameshangazwa na kauli za Bw. Kingunge kwamba wanachokifanya ni kujitafutia umaarufu.

Jana Mzee Kingunge alikaririwa na vyombo vya habari akidai kuwa anawashangaa baadhi ya wabunge wa CCM wanaokiponda chama chao kwa kujifanya kutetea maslahi ya umma.

Bw. Kingunge alitoa kauli hiyo mjini Dodoma wakati anapokea maandamano ya wananchi waliokuwa wanapongeza hutuba ya Rais aliyoitoa Bungeni hivi karibuni.

Kingunge alikaririwa akiwaonya wabunge hao waachane na umaarufu wa `kwenye magazeti` kwa vile umaarufu wao umetokana na CCM.

Bi. Kilango, alisema Mzee Kingunge asingetoa kauli hizo kama hana anachofaidi kwa mafisadi.

Alimuomba Bw. Kingunge awataje hao wabunge wanaodhoofisha CCM kwa tabia yao ya kupinga ufisadi.

``Yaani Mzee Kingunge haoni madhara ya wabunge wa CCM kuwaachia wapinzani kutetea maslahi ya taifa peke yao? Mzee wetu huyu sio tu anaua chama, lakini hatua yake yakutetea mafisadi kinyume kabisa na msimamo wa Mheshimiwa Rais unatuachia maswali mengi kuliko majibu. Kingunge hawezi kuwatetea mafisadi, kama asingekuwa anafaidi matunda ya ufisadi,`` alisema.

Bi. Anne alimtaka Mkongwe huyo awaache wabunge watekeleze wajibu wao waliotumwa na wananchi.

``Nyerere angefufuka akamsikia Kingunge akiwakemea watu wanaopinga uovu, angemnasa kibao,`` alisema.

Hata hivyo, Mbunge huyo alisisitiza kwamba kauli za Bw. Kingunge hazitawakatisha tamaa na wataendeleza mapambano kwa lengo la kuifanya CCM iendelee kuheshimika nchini.

Alisema watu wenye mawazo mgando kama Kingunge ndio wanakuwa vyanzo vya kuanguka vyama tawala kwenye nchi za Kiafria.

``Huyu Mzee (Kingunge) ana lake jambo, kwanza inaonekana haitakii mema serikali ya Rais Kikwete ambayo imetumia muda mwingi kupamba na ufisadi kwa kuunda tume nyingi,``alisema.

Kuhusu kuweka mbele maslahi ya CCM, Bi. Malecela alisema maslahi ya chama hicho yameongezeka baada ya baadhi ya wabunge kupinga ufisadi.

Naye Mbunge Kimaro, alimtaka Bw. Kingunge apumzike kwa amani na asidandie magari ya kasi.

``Mimi nampenda Kingunge, nawapenda wazee kama yeye. Tunawaenzi na tunawahitaji, lakini wanapofikia mahali pa kutetea dhuluma, tunawaomba wakae pembeni,`` alisema.

Bw. Kimaro alisema madai ya Kingunge ni matokeo ya watu kung\'angania madaraka na kulewa nyadhifa katika sehemu moja muda mrefu.

``Mwambieni Kingunge maneno yake sio ya kweli, hakuna Mbunge wa CCM mwenye nia ya kukidhoofisha chama chake, wanaodhoofisha ni mafisadi pamoja na yeyote anayetaka kuwakingia kifua kama anavyofanya... Maneno na kejeli zake hazitatuvunja moyo tunaendelea. Habari ndiyo hiyo,`` alisema.

Mbunge huyo alisema Kingunge amechoka na wala hana jipya, hivyo ameshindwa kutambua alama za nyakati kuwa CCM ya mwaka 77 si hii ya sasa.

Alisema ndani ya CCM kuna watu ambao wamejiunga nayo kwa nia ya kujitajirisha, hivyo watu pekee wa kukemea hali hiyo ni wabunge.

``Kingunge hataki mabadiliko kwa vile hana jipya, mimi namheshimu ndio maana namuomba akae pembeni ale pensheni yake,`` alisema.

Bw. Kimaro alisema nia ya wabunge wanaochachafya mafisadi ni kukitetea chama chao na kuifanya CCM irejee kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi (wanyonge) kama yalivyo madhumuni ya kuanzishwa kwake.

Alisema inasikitisha kuona kwamba Kingunge haoni tatizo la ufisadi nchini, badala yake anaona wabunge wanaopinga ufisadi ndio maadui.

Alisema kwa vyovyote mafisadi wameishiwa nguvu, sasa wameamua kumfanya Bw. Kingunge kuwa nabii wao wa kuwasemea, baada ya wao kubanwa pande zote.

``Ukweli ndio unaojenga siku zote. Rais amezungumzia tatizo la ufisadi katika EPA, Waziri Mkuu naye amekiri ufisadi ndani ya Richmond, yote hayo Kingunge hayaoni? Tunadhani anayaona, ila huenda kuna faida anayoipata kwa hao mafisadi,`` alisema.

* SOURCE: Nipashe
 
Ochu,

View attachment 2158

Jamani hiyo sura na hayo macho!! Angekuwa Shinyanga saa hizi angebakia historia - mapanga mtindo moja. Halafu huyo Pinda angalia alivyopinda - kweli hawezi kufurukuta.

mimi huyu kingunge ameniudhi kuliko wakati wote niliowahi kuudhika kwa kipindi cha mwaka mzima,na laiti kama mwalimu angekuwa hai huyu ingekuwa ni jela moja kwa moja bila kesi 'DEAD MAN'
 
mimi huyu kingunge ameniudhi kuliko wakati wote niliowahi kuudhika kwa kipindi cha mwaka mzima,na laiti kama mwalimu angekuwa hai huyu ingekuwa ni jela moja kwa moja bila kesi 'DEAD MAN'

CUF walikwisha mtangaza huyu mzee kuwa akili yake sio timamu ,mkawaona wapinzani wamechemsha ,sasa CUF wametulia kizee hakina cha kupingana nae kimevamia Chama chake na kukicharanga ,mi naona iwe hawampi mic au japo wakimpa waizime yeye atakuwa anazungumza tu ,na wale controller wa ukumbi wawe wanamwangalia akitaka kuigonga gonga mic ,waiwashe ili awe anasikia ile ko ,ko,ko akianza kuzungumza wanamzimia mpaka anaaga na kukaa.Atakuwa haelewi kumepita nini,ila akijua anaweza akamwaga razi kabisa ,unajua vizee vinapokuwa vinaona vinazarauliwa basi huwa vinazidi kupoteza akili na hutoa ukali sana ,anaweza akapata wazimu na kwa hiyo picha ilivyo kama watamchokola chokola kwa vijineno basi bila ya shaka yeyote atapata wazimu.
yaani hata ukimuangalia Mh.Pinda utaoana amekaa kama mganga wa kutibu wagonjwa wa akili ,na zile action za Kingunge zinamfanya Mheshimiwe ashike tama ,hajui kizee hiki akifanye nini
 
Anna kilango and kimalo ninyo habali njema msijali uyo mzee ana cancer kwenye asshole so uchaguzi ujao hatakuwapo is dieng now, wewe tizana kinje ndiyo uzao wake like father like son watu wana mlaumu kine is bogasi no amerithi kigunge maisha yake yote amekuwa omogulumkwee-kuwadi wa vigogo toka julius hadi abunuasi, wewe ona wakati wa ujamaa was close to chairman nyerere, wakati wa sheihk ruksa oooh he was dear to him,wakati wa don corleone alikuwa hit man if not posta boy , sasa wakati wa abunuasi aliailikwa kuceka pale, poa kalibu atalala na samaki
 
Babu umechoka si upumnzike kama mwenzio Kawawa?unatuletea mambo ya kizamani nidhamu za woga miaka hii???pumnzika mzee Kingunge umesha jichokea wewe....huna jipya ume-expire.
 
CUF walikwisha mtangaza huyu mzee kuwa akili yake sio timamu ,mkawaona wapinzani wamechemsha ,sasa CUF wametulia kizee hakina cha kupingana nae kimevamia Chama chake na kukicharanga ,mi naona iwe hawampi mic au japo wakimpa waizime yeye atakuwa anazungumza tu ,na wale controller wa ukumbi wawe wanamwangalia akitaka kuigonga gonga mic ,waiwashe ili awe anasikia ile ko ,ko,ko akianza kuzungumza wanamzimia mpaka anaaga na kukaa.Atakuwa haelewi kumepita nini,ila akijua anaweza akamwaga razi kabisa ,unajua vizee vinapokuwa vinaona vinazarauliwa basi huwa vinazidi kupoteza akili na hutoa ukali sana ,anaweza akapata wazimu na kwa hiyo picha ilivyo kama watamchokola chokola kwa vijineno basi bila ya shaka yeyote atapata wazimu.
yaani hata ukimuangalia Mh.Pinda utaoana amekaa kama mganga wa kutibu wagonjwa wa akili ,na zile action za Kingunge zinamfanya Mheshimiwe ashike tama ,hajui kizee hiki akifanye nini

Mwiba,

Hakika leo ndiyo nimeelewa nini maana ya jina lako Mkuu(mwiba), kweli umenimaliza mkuu,sina mbavu mkuu, da......., sijui kama huyu mzee akiyasoma haya uliyoyasema hapa si ndiyo anajiudhuru UCCM wenyewe huo, ndugu yangu una maneno makali sana Mkuu.

Ila tambua kuwa binadamu yoyote anapofikisha miaka 80' hivi upeo wake wa kufikiri hupungua kila kukicha, hivyo tusishangae yale anayoyatamka mzee wetu.

Mlinganisheni na mtoto wa miaka 3 - 5, fikra zake zinawaza chakula na pia kama mzee huyu ataendelea kuwa ndani ya ccm mengi tutayasikia.
 
Mzee Kinje tunahitaji busara zako (kama bado zipo), lakini katika hili tafuta wengine!

Umri huo siyo wa busara tena. hapo alipo ni senility. Hayuko tena sensitive na eti tunajidai kusema busara imeongezeka. No way!

Au kweli anafaidika na ufisadi? maana nasikia ndiye anayeendesha ushuru wa Ubungo.
 
Back
Top Bottom