Kinachopingwa na TEC na Watanzania walio wengi siyo Uarabu wala Uislamu; ushahidi ni miradi ya SGR na JNHPP

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,893
3,200
Habari wana Jamii Forums,

Pasipo kupoteza muda, naomba niende kwenye mada tajwa hapo juu.

Kumekuwa na mjadala mkubwa sana kuhusiana na baadhi ya watu walioishiwa hoja za kuunga mkono mkataba tata wa DPW. Hivyo baadhi wamejikuta wakitumia hoja ya udini na uarabu.

Wanaopinga mkataba wanaorodhesha hoja za msingi na zinazoeleweka vizuri kabisa pasipo hata kutumia nguvu ya kufikiria.

Wanaouunga mkono mkataba huo wenye masharti ya hovyo, wanatumia nguvu nyingi sana kuwapinga wanaoupinga mkataba bila hata ya kugusia mkataba wenyewe. Ingekuwa busara kama wangezijibu hoja zinazotolewa.

Zaidi ya hayo, wanaoupinga mkataba wamesema wazi kasoro za mkataba, na si kumkataa mwekezaji aliyetambuliwa kwenye mkataba. Wanasingizia kuingiza mambo ya udini ambayo wala hawakuyagusia kwenye hoja zao.

Kama ingekuwa ni masuala ya dini, kwa nini hakukuwa na upinzani kwa Uturuki, nchi ya Kiislamu, kujenga SGR?

Au kwa nini hakukuwa na upinzani kwa Stieglers Gorge (MRADI WA JNHPP) kujengwa na Misri, nchi ya Kiarabu na Kiislamu?

Bila shaka hakuna udini katika kupinga mradi.

Kwa mambo yalipofikia hivi sasa, suluhisho ni kuitisha kura ya maoni (referendum) ili maoni ya wengi ndiyo yachukuliwe. Kuna Mkatoliki mwenzangu anayeupinga waraka wa TEC kwa hoja kwamba hakuulizwa atoe maoni yake na kwamba inabidi tuukubali mkataba kwa kuwa Bunge limeridhia. Hoja hii si sahihi. Kuhusiu TEC kutomhusisha na kwamba Bunge limeridhia, jee Mbunge wake alikwenda kumuuliza maoni yake kabla ya Bunge kuridhia? Kwa nini adai kuulizwa na TEC tu na siyo Mbunge wake? Hoja hii haina mshiko.

Aidha, TEC haijasema iwe wanavyotaka wao. Wanachosema ni kwamba Serikali isikilize wananchi. Hao wananchi waelezwe kiuwazi mkataba ulivyo na wao ndio waamue. Serikali haitaki kuweka mambo wazi, na ndiyo maana Waziri Nnauye akakataza vyombo vya habari kuutangaza waraka wa TEC. Ni siri ipi hiyo inayolindwa hivyo na Serikali?

Katika miaka michache iliyopita kumekuwa na kesi si chini ya kumi kati ya DP World na inchi mbalimbali ulimwenguni ambazo DP World ilishindwa. Hii ni sababu tosha kwamba tuwe makini kwenye mikataba tunayoingia. Aidha Tanzania imefikishwa mahakamani mara kadhaa sasa na kutozwa faini kwa sababu ya kuvunja mkataba ambao tumekuja kugundua baadaye kwamba mkataba tulioingia una kasoro. Nashindwa kuelewa kwa nini mtu apinge kuchunguzwa kwa mkataba huu ili kuondoa uwezekano wa kuishia mahakamani kama ilivyotokea hivi sasa, maadam tumegutuka kwamba kuna kasoro.

Hivi Serikali ilikuwa 'serious' kweli kupeleka Dubai wasanii kama Steve Nyerere kwenye majadiliano ya mkataba? Aidha, Bunge lilitoa saa 24 tu kwa watu kutoa maoni na watu 72 wakafikisha maoni ndani ya muda huo. Kuna namna mbili za kuangalia idadi hiyo. Moja, hao watu 72 ni wachache mno kati ya milioni zaidi ya 60 ya Watanzania kusema kwamba tulipata mawazo ya wananchi.

Pili, hao watu 72 ni wengi mno kuweza kujitokeza kwa kushtukizwa tu ndani ya saa 24. Ina maana kwamba kama muda ungekuwa mrefu zaidi, bila shaka watu lukuki wangejitokeza. Hivi ndivyo TEC wanavyoomba: wananchi wasikilwe: Mkataba uchunguzwe upya; kasoro zitakazobainishwa zirekebishwe; Mwekezaji huyo huyo apewe tenda kama amekubali kurekebisha dosari; na mambo yaendelee.

Credit zimwendee Ng'wanamalundi kwa kuwa sehemu kubwa ya uzi huu ni mchango wake katika moja ya nyuzi zangu. Nimeona ni mchango makini unaojitosheleza kuanzishiwa uzi kabisa.
 
Kweli

Labda nikusaidie kidogo

Misri ndiko Yesu alikofichwa baada ya Herode kutaka kumuua na Mamajusi wakamuingiza Chaka, hivyo Wagalatia wanaiheshimu sana Misri

Uturuki ndipo lilipotimia Neno la pili la Yesu pale Msalabani "Mama Tazama mwanao, Yohana Tazama mama Yako"
Basi kutoka pale Yohana mtume alimchukua Mariamu na kwenda kumtunza kwao Uturuki

Ahsanteni 😀😀🌟
 
Wapo ibada ngoja wamalize wapitie na kula biriani chakula kikuu cha mwekezaji then wanakuja hapa kwenye uzi wako.

Mimi mpaka nimeshachoka kufungua post zinazohusu hili jambo,unakuta mtu unamjua kabisa kupitia maandishi yake humu kwamba siyo kichwa maji Ila unakuta comment anayoshusha kuwapinga wasiowataka hao DP World unatamani umpe tusi moja ila ukiwaza utatukana kivuli unaachana nae.
 
Kwa hili swala linavyoenda, ukiacha madudu ya viongozi wetu, mataifa makubwa, USA, UK, nk kama yananufaika na uwekezaji wa DPworld, popote duniani, hayapo tayari kuona kuna kuwa na mkataba wa kuinufaisha nchi na wananchi wa kawaida. Kama wao, wa kubwa watanufaika, wananchi hata wakifa, poa tu, na watawatumia viongozi wetu majizi kama kikwete, samia na wengine, kuona rasilimali zetu zinaneemesha wageni.
 
Viongozi wa Tanzania ni hovyo kabisa, wanajua wanachokifanya wanatumia kete ya udini ndio kama njia ya kujibu hoja.

Hii ni hatari maana linaweza tokea jambo baya huko mbeleni, lakini viongozi wanafanya haya ili jambo lao lipite kwa nguvu yoyote.

Lakini sisi ngozi nyeusi sijui tuna shida gani ? hivi inakuwaje mtu unakosa uzalendo wa kuweka maslahi ya taifa mbele, unakubali kupokea pesa kutetea ujinga !!!
 
Kweli

Labda nikusaidie kidogo

Misri ndiko Yesu alikofichwa baada ya Herode kutaka kumuua na Mamajusi wakamuingiza Chaka, hivyo Wagalatia wanaiheshimu sana Misri

Uturuki ndipo lilipotimia Neno la pili la Yesu pale Msalabani "Mama Tazama mwanao, Yohana Tazama mama Yako"
Basi kutoka pale Yohana mtume alimchukua Mariamu na kwenda kumtunza kwao Uturuki

Ahsanteni 😀😀🌟
Ila Yohana Mbatizaji bhana wakati mwingine unaletaga utani hata kwa masuala serious ya nchi!!
 
Viongozi wa Tanzania ni hovyo kabisa, wanajua wanachokifanya wanatumia kete ya udini ndio kama njia ya kujibu hoja.

Hii ni hatari maana linaweza tokea jambo baya huko mbeleni, lakini viongozi wanafanya haya ili jambo lao lipite kwa nguvu yoyote.

Lakini sisi ngozi nyeusi sijui tuna shida gani ? hivi inakuwaje mtu unakosa uzalendo wa kuweka maslahi ya taifa mbele, unakubali kupokea pesa kutetea ujinga !!!
Inauma sana lakini huo ndo ukweli Mkuu
 
Habari wana Jamii Forum,
Pasipo kupoteza muda, naomba niende kwenye mada tajwa hapo juu.

Kumekuwa na mjadala mkubwa sana kuhusiana na baadhi ya watu walioishiwa hoja za kuunga mkono mkataba tata wa DPW. Hivyo baadhi wamejikuta wakitumia hoja ya udini na uarabu!

Wanaopinga mkataba wanaorodhesha hoja za msingi na zinazoeleweka vizuri kabisa pasipo hata kutumia nguvu ya kufikiria.

Wanaouunga mkono mkataba huo wenye masharti ya hovyo, wanatumia nguvu nyingi sana kuwapinga wanaoupinga mkataba bila hata ya kugusia mkataba wenyewe.

Ingekuwa busara kama wangezijibu hoja zinazotolewa.

Zaidi ya hayo, wanaoupinga mkataba wamesema wazi kasoro za mkataba, na si kumkataa mwekezaji aliyetambuliwa kwenye mkataba.

Wanasingizia kuingiza mambo ya udini ambayo wala hawakuyagusia kwenye hoja zao.

Kama ingekuwa ni masuala ya dini, kwa nini hakukuwa na upinzani kwa Uturuki, nchi ya Kiislamu, kujenga SGR?

Au kwa nini hakukuwa na upinzani kwa Stieglers Gorge (MRADI WA JNHPP) kujengwa na Misri, nchi ya Kiarabu na Kiislamu?

Bila shaka hakuna udini katika kupinga mradi.

Kwa mambo yalipofikia hivi sasa, suluhisho ni kuitisha kura ya maoni (referendum) ili maoni ya wengi ndiyo yachukuliwe. Kuna Mkatoliki mwenzangu anayeupinga waraka wa TEC kwa hoja kwamba hakuulizwa atoe maoni yake na kwamba inabidi tuukubali mkataba kwa kuwa Bunge limeridhia. Hoja hii si sahihi. Kuhusiu TEC kutomhusisha na kwamba Bunge limeridhia, jee Mbunge wake alikwenda kumuuliza maoni yake kabla ya Bunge kuridhia? Kwa nini adai kuulizwa na TEC tu na siyo Mbunge wake? Hoja hii haina mshiko. Aidha, TEC haijasema iwe wanavyotaka wao. Wanachosema ni kwamba Serikali isikilize wananchi. Hao wananchi waelezwe kiuwazi mkataba ulivyo na wao ndio waamue. Serikali haitaki kuweka mambo wazi, na ndiyo maana Waziri Nnauye akakataza vyombo vya habari kuutangaza waraka wa TEC. Ni siri ipi hiyo inayolindwa hivyo na Serikali?
Katika miaka michache iliyopita kumekuwa na kesi si chini ya kumi kati ya DP World na inchi mbalimbali ulimwenguni ambazo DP World ilishindwa. Hii ni sababu tosha kwamba tuwe makini kwenye mikataba tunayoingia. Aidha Tanzania imefikishwa mahakamani mara kadhaa sasa na kutozwa faini kwa sababu ya kuvunja mkataba ambao tumekuja kugundua baadaye kwamba mkataba tulioingia una kasoro. Nashindwa kuelewa kwa nini mtu apinge kuchunguzwa kwa mkataba huu ili kuondoa uwezekano wa kuishia mahakamani kama ilivyotokea hivi sasa, maadam tumegutuka kwamba kuna kasoro. Hivi Serikali ilikuwa 'serious' kweli kupeleka Dubai wasanii kama Steve Nyerere kwenye majadiliano ya mkataba? Aidha, Bunge lilitoa saa 24 tu kwa watu kutoa maoni na watu 72 wakafikisha maoni ndani ya muda huo. Kuna namna mbili za kuangalia idadi hiyo. Moja, hao watu 72 ni wachache mno kati ya milioni zaidi ya 60 ya Watanzania kusema kwamba tulipata mawazo ya wananchi. Pili, hao watu 72 ni wengi mno kuweza kujitokeza kwa kushtukizwa tu ndani ya saa 24. Ina maana kwamba kama muda ungekuwa mrefu zaidi, bila shaka watu lukuki wangejitokeza. Hivi ndivyo TEC wanavyoomba: wananchi wasikilwe: Mkataba uchunguzwe upya; kasoro zitakazobainishwa zirekebishwe; Mwekezaji huyo huyo apewe tenda kama amekubali kurekebisha dosari; na mambo yaendelee.

Credit zimwendee Ng'wanamalundi kwa kuwa sehemu kubwa ya uzi huu ni mchango wake katika moja ya nyuzi zangu. Nimeona ni mchango makini unaojitosheleza kuanzishiwa uzi kabisa..
Suala limeshakwisha hili.
 
Back
Top Bottom