Kina nani walimpigia JK kura ya Hapana?

Nasikia harufu ya nyundonzito, coming back na jina jipya kwenye hii topic, just me! Lakini it sad as a nation tunapoanza kujadili nani alipigaje kura yake, that is very low in my opinioni, na viongozi etu watafurahi sana kuona mjadala wa aina hii! kutoka kwetu smart wananchi
 
Kama mimi ni Mwandosya, naamua kujiuzulu kwa sababu binafsi...~

fukuto lilishaanza,Hata mie nakuunga mkono Mwanakijiji..itakuwa kama kumshushia hadhi Prof.,Mramba alishajua hatakiwi anachokifanya sasa ni kuhakisha anajijenga pembeni (anaiba)na aondoke kwa amani..Mungwana anaendeleaza siasa zake za kijiweni,Yeye hakai nchini anajuaje kama Mawaziri hawafanyi kazi?
 
Inawezakana mtu aliyewahi kuwa Waziri Mkuu kuwa waziri wa kawaida?

Hebu nifahamisheni!

KAKA MASAKI ..KATIKA HISTORIA YA TANZANIA MAWAZIRI WAKUU WOTE WAMEWAHI KUWA MAWAZIRI WA KAWAIDA HATA BAADA YA KUWA MAWAZIRI WAKUU...EXCEPT SOKOINE..na malecela

1.RASHID MFAUME KAWAWA [amewahi kuwa makamu wa rais.,waziri mkuu ..waziri asiye na wizara maalum,waziri wa ulinzi ...waziri asiye na wizara maalum]

2.CLEOPA DAVID MSUYA[waziri wa biashara, waziri mkuu na makamu wa pili wa rais ,waziri wa fedha, waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais, na waziri wa biashara na masoko]

3.SALIM AHMED SALIM[waziri wa mambo ya nje,waziri mkuu na makamu wa pili wa rais,naibu waziri mkuu na waziri wa ulinzi..]

4.JOSEPH SINDE WARIOBA[mwanasheria mkuu,waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais,waziri wa tawala za mikoa na serikali za mitaa]

5.CYGEMWISI JOHN SAMWEL MALECELA[WAIRI wa mambo ya nje,waziri wa mawasiliano na uchukuzi,mkuu wa mkoa iringa,balozi london,waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais,..nadhani after that akarudi chamani tu...

so sioni ajabu kwa FREDERICK TLUWAY SUMAYE kama rais atamteua kuwa mbunge na baadaye waziri na yeye akaukubali uteuzi ...kwani hatakuwa waziri mkuu wa kwanza wa nchi hii kuwa waziri baada ya kuwa waziri mkuu....sumaye ana rekodi ya kuwa waziri mkuu kwa muda mrefu zaidi na bado umri wake ni wa kadiri....kwa rais ambaye hatataka upinzni wa ndani lazima asicheze mbali na watu kama sumaye,mwandosya na kigoda.
 
Inawezakana mtu aliyewahi kuwa Waziri Mkuu kuwa waziri wa kawaida?

Hebu nifahamisheni!

Hili ni jambo la kawaida sana katika nchi za wenzetu. Rejea Israel, tena sio tu waziri mkuu, hata rais (kwao waziri mkuu ni kama rais kwetu). Huko US, sio kuwa waziri, bali kurudi kufundisha kama alikuwa mwalimu. Hujasikia Dr Condoleze Rice anarudi zake kufundisha Stanford baada ya term yao kwisha? Ni kwetu ambao huwa tuna-complicate maisha, ukishakuwa na cheo basi inakuwa taaaaabu!
 
Mwandosya na kikwete ni km dunia na mbingu.. hawafanani kwa vile wkt kikwete ana rekodi katika medani ya kisiasa mwandosya ana rekodi katika medani ya kitaaluma. Kwa bahati mbaya mwandosya anashindanishwa ktk medani ambayo si nyanja yake...ila km walivyo wasome wengine wanaodhani neema inapatikana ktk siasa tu hapa bongo..yeye naye kajitia ktk mkumbo huo...lakini hana mvuto labda kwa watu wa kabila lake.
 
Kama isingekuwa dirty politics Profesa angekuwa Rais, na kama na yeye angeamua kucheza dirty politics huenda angeweza kushinda. kwa sababu wengi wenye akili ndani ya CCM walikuwa wanafahamu nani anatakiwa kuongoza nchi. Ni wazi wanaona kuwa uchumi wa sasa hivi wa Tanzania umepiga hatua na hautakiwi kuendeshwa kiujanja ujanja, unahitaji mtu mwenye vision na mwenye uwezo kuliko Mkapa (sio mwenye uwezo wa Chini) anayeweza kukijenga chama cha mapinduzi na kupunguza uchafu uliopo na kiwe chenye nguvu, na uchumi wa nchi uwe na nguvu zaidi.
Lakini kwa mazingira ya sasa ya Tanzania itakuwa ni political suicide kama akijiondoa kwenye Chama, na sidhani kama JK atamuondoa kwenye nafasi yake, nadhani kutokana na jinsi walivyo na chuki binafsi JK ataonesha "superiority yake" kwa kumfanya subordinate wake kwenye cabinate. Na inawezekana kabisa kuwa jamaa ni marafiki maadui na kama Prof angekuwa rais huenda angemuweka angempa JK wizara kama alivyofanya.
 
Bongolander,

Wanaojua siasa za UK, wanajua ugomvi wa Blair na Brown, lakini kwa pamoja wameongoza nchi hii kwa miaka 10 kwa mafanikio makubwa sana. Kila mmoja wao alikuwa anafanya juhudi kubwa ili kumzidi mwenzake, matokeo ni faida kwa nchi.

Kwa TZ, JK angekubali kumfanya prof. waziri mkuu naamini serikali ingechapa kazi kweli kweli.

Kwa kumfahamu kwangu prof. naamini kama yeye angelikuwa rais, basi angempa nafasi ya maana JK.

Lakini tatizo ni wapambe ambao ndio muda wote wanaendeleza vijembe hata mahali ambapo wahusika wenyewe hawana ugomvi tena. Prof. hawezi kuondoka CCM maana atakuwa amejiua kisiasa, watu wanaojua utendaji wake ni kule kwenye jimbo lake na huko huko CCM na serikali. Huku nje itakuwa ni sawa na shark kuachwa jangwani, atakufa baada ya muda mfupi.
 
hili suala la Kummpendekeza Sumaye ndani ya Baraza Jipya,itakuwa heko kwa Muungwana,atakuwa ameamua kuvunja maklundi kabisa katika chama..lets wait ,nai mwenye inside info?
nijuavyo mimi kabla ya Muungwana kuteua mtu huwa anamuita kwanza ikulu wandiscuss then ndio anamteua thus why imekuwa rahisi sana kwa mambo ya JK kuvuja hata kabla hajateuwa mtu
 
Nasikia harufu ya nyundonzito, coming back na jina jipya kwenye hii topic, just me! Lakini it sad as a nation tunapoanza kujadili nani alipigaje kura yake, that is very low in my opinioni, na viongozi etu watafurahi sana kuona mjadala wa aina hii! kutoka kwetu smart wananchi

Mkubwa uko sahihi sana kwani wakati sasa tunaona ramani ya wapi tuendako mnataka kuturejesha zama za ujima;hii ni hatari na kinyume kabisa cha tafsiri ya KURA.

Sisi wengine ni vijana,tunapenda kujifunza humu JF,ni imani hiyo ndiyo inayotuleta ktk darasa hili ili tupate kujifunza kwa dhati.
 
CCM, bwana!!! wataaram kwerikweri!!!

1995 baada ya Mkapa kushinda tiketi ya kugombea urais kupitian chama hilo tukawa pia tumeshachaguliwa rais wa 2005!!! Tumeingia kichwakichwa sasa tunalalamika!

The same Mchakato wa 2005 yaelekea tushachaguliwa rais wa 2015!!

Wajameni tusichague Rais kwa ushabiki!! Pia mtu kumzidi kiuwezo rais aliye madarakani si kigezo sahihi kujua rais bora (Yawezekana wote hovyoo). Tuchague rais anaefaa kuiongoza nnji kulingana na mahitaji ya nnji kwa wakati huo. Hivi mwafikiri Nyerere anaweza kuongoza nnji zama hizi??? Mwandosya namkubali sana sana ila si wakati wake.

Kama atatulia mpaka 2015, ana uhakika wa kura 1 toka kwangu!!!
 
Mkuu PM,

Heshima mbele, ni marekebisho tu hata Malecela, alipotoka u-PM alikuwa waziri wa usalama(Waziri Asiyekuwa na Wizara Maaalum), kwa kipindi kifupi mpaka Mkapa, alipoingia na kuwaita yeye na Msuya, na kuwaambia kuwa hatawapa uwaziri tena.
 
Bila ubishi wowote Mwandosya ni zaidi kuliko Kikwete. Kikwete hana ubavu wa kushindana na Mwandosya siku yoyote ile, ashukuru mungu rushwa wenyewe CCM wanaita takrima ilimbeba na kuibuka kidedea kama mgombea wa CCM. CCM wangekuwa wana mfumo wa kutafuta mgombea kwa kufanya mijadala (debate) kila mgombea angekuwa anazungumzia sera zake anakotaka kuipeleka Tanzania kama akichaguliwa kuwa rais, basi Kikwete hata katika 3 bora asingekuwemo.
Jamaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom