Kina nani walimpigia JK kura ya Hapana?

Bubu ataka kusema,
Nadhani umesahau kuwa mwandosya ktk chaguzi zake zote ushindi wake umekuwa na matatizo. navyosikia huko Mbeya kama sio CCM kusimama imara alikuwa nje ktk chaguzi zote ikiwa na hii ya majuzi. kwa hiyo tuwe makini sana tunapotaka kupima uwezo wa watu kwani mzani wako inaonyesha wazi umemweka JK na jiwe la kilo nzima ktk Ujazo lakini Mwandosya hana kipimo upande wa pili isipokuwa elimu yake.
Jk kama rais amefanya nini?....well wewe ulitaka afanye kipi!... wanavyosema wao kaweka ahadi ambazo anazitimiza na Mwandosya ni mmoja kati ya wafanyakazi wake. if he had failed ni kutokana na hao kina Mwandosya kwani ndio mawaziri wanaoendesha hizo wizara.
kulingana na mtazamo wako ni wazi hakuna kiongozi yeyote aliyepata mafanikio nchini Tukiondoa Nyerer kisiasa kwani Tanzania bado ni maskini.
 
Bubu ataka kusema,

Duh! mjomba naona tunatazama shilingi mbili tofauti kabisa. Hapa kidogo unajipiga kanzu mwenyewe kwani maelezo yako ya awali yananipa picha tofauti kabisa. Kwanza umemsifia Mwandosya kwa elimu yake hukuzungumzia kabisa maswala ya uwezo wake kubadilisha jamii yetu...Umeitumia elimu yake kama mafanikio zaidi ya JK leo tunampa JK urais akiwa na miaka 55 unasema hayo sio mafanikio hadi pale atakapoweza kutumia vizuri nafasi hiyo. Well, ktk siasa nadhani hata Mwandosya bado hajaitumia elimu yake ktk siasa labda darasani - ikwa hiyo ngoma draw.
Pili binafsi nashindwa sana kuelewa sisi wadanganyika tunachukulia Siasa kama vile ni Upinzani kati ya mtu na mtu badala ya Upinzani wa mrengo wa vyama. Tumefikia kuwatazama viongozi wetu kwa tofauti zao ktk mrengo ndani ya chama kimoja. Mwandosya hata kama hakubaliani na JK bado ni mfuasi wa siasa za CCM ila hakubaliani na uongozi wa JK ktk baadhi ya sera ama JK himself.
Leo hii mimi nimeingia Chadema kwa sababu ya mrengo wa chama hicho. kama CCM au CUF ama TLP wangekuwa Conservative ningejiunga na moja ya vyama hivyo lakini sii kwa sababu huko Chadema kuna Freeman na Zitto. Kila naposoma hoja nyingi za watu huwa nazidi kujenga wasiwasi wangu ktk kuwaelewa wadanganyika kuelewa kwao ktk hili somo jipya la siasa zinazofungamana na mbinu bora za kuimarisha maisha ya wananchi.

I believe kuwa maendeleo ya Tanzania yataletwa na Mtanzania regardless of his color, dini ama gender na ni Mtanzania pekee anayetakiwa kupewa kipaumbele ktk nafasi muhimu za kuzalisha uchumi wa nchi yetu hivyo kuboresha maisha yao. Na wale wote wanao hujumu uchumi wa nchi yetu wanatakiwa kuchukuliwa hatua kali kuhakikisha tunafika kule tuendako iwe tunaongozwa na JK ama Mwandosya.
Hivi sasa tumevamia hili bus ( band wagon) tunazugushwa mitaani na wapo watu wana enjoy kuzunguka huku wakiwa ndani ya gari hili la CCM. hawana haraka ama hawana haja ya kufika, the more safari inavyozidi kuwa ndefu, the more wana enjoy the ride!
Jamani, wanabodi nadhani ipo haja ya kuanzisha mjadala unaohusu elimu ya siasa ambayo itatupa picha halisi ya tofauti zilizopo ktk baadhi ya vyama vyetu na sio kutazama watu na elimu zao while they stand for nothing!
Waliopiga kura za hapana kwa JK ni wafuasi wa CCM na wana tatizo lna uongozi wa JK ktk kufuata mrengo, ilani, sera na katiba ya CCM, nje ya hapo sisi sote ni vipofu ktk elimu ya siasa..

Huwezi kubadilisha jamii bila ya kuwa na nafasi ya kufanya hivyo. Kikwete amepata nafasi chungu nzima za kubadilisha jamii na mpaka sasa hivi Watanzania hatujaona mafanikio yake. Mwandosya kama mhadhiri amepata nafasi ya kubadilisha jamii katika nyanja ya elimu na amechangia sana katika kuongeza idadi ya wahandisi ndani na nje ya Tanzania, kwangu mimi Mwandosya amekuwa na more positive impact kwenye jamii ya Kitanzania ukilinganisha na Kikwete. Alipokuwa pale nguvu na nishati kama Waziri ndiyo kashfa ya IPTL ilipotokea chini ya uangalizi wake wa wizara hiyo. Alipokuwa mambo ya nje kashfa chungu nzima ikiwemo ya Rada, kusaini mikataba mibovu ya madini ambayo mpaka leo ni siri. Yeye kama kiongozi mmoja wa juu hakukemea lolote kuhusiana na kashfa mbali mbali za awamu ya tatu na hata alitetea ununuzi wa rada.

Kama Rais bado analinda kashfa dhidi ya viongozi wa awamu ya tatu, bado hajafanya lolote kuhakikisha Tanzania inanufaika na madini yake, amechangia kwa namna moja au nyingine kuhusiana na Richmonduli, Buzwagi, BOT na kuongezeka kwa gharama za maisha kwa Watanzania walio wengi, haya siyo mafanikio hata kidogo.

Bado ni mwanasiasa wa kupanda majukwaani na kutoa hotuba nzuri ambazo hazina ufuatiliaji wowote. Kwa mfano juzi amezungumza jukwaani kuyataka makampuni ya kigeni yawalipe wataalamu wa Kitanzania sawa sawa na wataalamu wa kigeni, kwa mara nyingine tena hakusema lolote ni jinsi gani atafuatilia kuhakikisha hili linatendeka.

Kwa maoni yangu alipashwa kuwaita viongozi wa juu wa makampuni hayo Ikulu kuzungumza nao juu ya swala hili kwa kina, halafu kuwataka wampe ripoti baada ya mwezi au hata miezi miwili ili kujua utekelezaji wa hili umefikia wapi. Hivyo ndio kiongozi anatakiwa afanye ili kuhakikisha anapata mafanikio katika sera zake mbali mbali. Mabilioni ya Kikwete, mafanikio ni ZERO, ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya mpaka sasa hivi mafanikio ni ZERO, maisha bora kwa kila Mtanzania mpaka sasa hivi mafanikio ni ZERO! au waulize Watanzania juu ya hili ili usikie maoni yao.

Mie naona mtu tu aliyetaka uraisi lakini hana sera zozote na uwezo wa kuiongoza Tanzania. Bado ana muda mwingi wa kubadilisha mawazo ya Watanzania wengi kuhusu urais wake, but so far he has achieve NOTHING in the office.
 
Jamani eeehhh!!! hawa jamaa wakiamua kumpiga chini mwandosya, wanaweza na hakuna madhara yoyote yatakayotokea tanzania. Mnakumbuka ushabiki wa mrema mwaka 1995??? Ni nani leo hii anayemzungumzia mrema???Nani anayemzungumzia kolimba leo hii??? Nani anayemzungumzia aboud jumbe leo hii??? tena jumbe mkumbuke alikuwa ni raisi wa zanzibar!!!

Ni lazima mjue tanzania kuna umafia wa hali ya juu. Huyo jamaa wanaweza kumtosa na hakuna chochote kinachoweza kufanyika. Tutapiga blaaa blaaa, hapa lakini ukweli ni kwamba huyo jamaa (prof.mwandosya) hamnyimi usingizi kikwete.

i support u musee..dtas our Tanzania ya sasa
 
Babu: hilo darasa ndugu yangu na linaendana kabisa na jina lako. Sina cha kuongeza zaidi ya kusema ahsante sana!
 
1.
Kikwete mpaka sasa hivi hana mafanikio yeyoye katika ukumbi wa kisiasa. Nimeomba mniambie katika sehemu mbali mbali alizopitia katika siasa ni mafanikio gani aliyoyapata ambayo yanaweza kabisa kutamkwa na Watanzania walio wengi kwamba ni mafanikio ya Kikwete, mpaka sasa hivi hakuna aliyeweza kufanya hivyo. Hakuna debate katika kumpata mgombea wa CCM nina hakika kabisa kama kungekuwa na debate ya kila mgombea anataka kuiongoza vipi CCM na Tanzania basi Kikwete angeanguka vibaya sana maana hana uwezo wa kujieleza.

Mkuu ukweli ni kwamba hili ni swali linatakiwa kujibiwa na wewe, yaani kinachomfanya Mwandosya awe zaidi ya Muungwana, unayoyasema hapo juu hayaelezi any fact either on Muungwana au Mwandosya,

2.
Katika maisha ya mwanadamu ili kupima mafanikio aliyoyapa hapa duniani mnalenga kuangalia ni nyanja ipi alikuwa anajishughulisha nayo hapa duniani, kwa Kikwete ni siasa ambayo mpaka sasa hivi hakuna yeyoye anayeweza kupinpoint mafanikio yake
,

Mafanikio kisiasa ya Muungwana, bado huyaoni kuweza kuwa kuibuka mshindi katika urais, kutoka kwenye wananchi 45 millioni, huyu mtu mmoja kuweza kuibuka mshindi, unasema mafanikio yake kisiasa huyaoni au huyajui, are you serious?

3.
na kwa Mwandosya ni elimu na amechangia kutoa wataalamu mbali mbali katika sekta ya wahandisi ambao wapo Tanzania na nchi mbali mbali duniani, kwangu mimi hayo ni mafanikio makubwa.

Ndio maana Muungwana, akamua kumpa uwaziri katika serikali yake ili amsaidie kuleta mafanikio katika kazi ya wananchi kwa taifa ,kazi ambayo sisi wananchi tumemkabidhi Muungwana, na sio Mwandosya.

4. [
B]Kikwete maji yalimfika shingono kutokana na makundi ndani ya CCM, havyo alikuwa hana jinsi ila kuweka distance kati yake na mtandao, [/B]

Kugundua hilo tatizo la makundi na kulifanyia kazi, ni dalili za uwezo mkubwa kisiasa, ndio maana tukampa urais au?

5.
je hiyo dustance aliyoiweka ni ya kweli au ni kiini macho katika kuzuga Watanzania!? Hili inabidi tusubiri tuone litachanua vipi.

Hili tunaongea lugha moja, na tuendelee kukata ishus mkuu Bubu, safi sana.
__________________
 
Bubu ataka kusema,
Nadhani umesahau kuwa mwandosya ktk chaguzi zake zote ushindi wake umekuwa na matatizo. navyosikia huko Mbeya kama sio CCM kusimama imara alikuwa nje ktk chaguzi zote ikiwa na hii ya majuzi. kwa hiyo tuwe makini sana tunapotaka kupima uwezo wa watu kwani mzani wako inaonyesha wazi umemweka JK na jiwe la kilo nzima ktk Ujazo lakini Mwandosya hana kipimo upande wa pili isipokuwa elimu yake.
Jk kama rais amefanya nini?....well wewe ulitaka afanye kipi!... wanavyosema wao kaweka ahadi ambazo anazitimiza na Mwandosya ni mmoja kati ya wafanyakazi wake. if he had failed ni kutokana na hao kina Mwandosya kwani ndio mawaziri wanaoendesha hizo wizara.
kulingana na mtazamo wako ni wazi hakuna kiongozi yeyote aliyepata mafanikio nchini Tukiondoa Nyerer kisiasa kwani Tanzania bado ni maskini.

Chaguzi zote za CCM zina matatizo au umesahau kwamba katika kupata mgombea wa CCM katika kinyang'anyiro cha 2005 rushwa alias takrima tena ya dollar ilikuwa inagawiwa nje nje pale dodoma ili kuhakikisha jamaa anaibuka kidedea? Kwa maana nyingine Kikwete bila takrima asingeibuka kama mgombea wa CCM na hili siyo siri. Butiku aliomba kujua hizi pesa zilikuwa zinatoka wapi na hao waliokuwa wanazigawa walikuwa wanafanya hivyo kwa madhumuni yapi kwa CCM na Tanzania. Mpaka leo hakuna aliyemjibu Butiku swali lake.

Huwezi kuwalinganisha watu wawili ambao wapo katika nyanja tofauti za uchumi kwa kutumia kigezo kimoja. Mwandosya hana muda mrefu katika anga za kisiasa ukilinganisha na Muungwana. Hivyo itakuwa si haki kutumia siasa pekee yake kuwalinganisha hawa watu wawili. Kwenye siasa Kikwete mpaka sasa hivi ni ZERO, na kwenye elimu ushahidi wa mafanikio ya Mwandosya ni belele.

Sera za kuingalia upya mikataba ya madini mpaka sasa hivi hazina mafanikio wa kulaumiwa ni akina Mwandosya, sera za kutosaini mikataba mipya ya madini mpaka mikataba yote iangaliwe upya halafu bado wakasaini Buzwagi wa kulaumiwa ni akina Mwandosya, sera za mabilioni ya Kikwete ambazo ni total failure, sera za ari, mpya, nguvu mpya na kasi mpya sera za maisha bora kwa kila Mtanzania zote hizi zimewakatisha tamaa Watanzania wa kulaumiwa ni akina Mwandosya :confused: sasa yeye kama ndiye aliyewateua katika nyadhifa mbali mbali na anaona wanamuangusha katika kutimiza sera zake ana ngoja nini kuwafukuza kazi kwa manufaa ya umma!? :confused:
 
Bubu ataka kusema,
Nadhani umesahau kuwa mwandosya ktk chaguzi zake zote ushindi wake umekuwa na matatizo. navyosikia huko Mbeya kama sio CCM kusimama imara alikuwa nje ktk chaguzi zote ikiwa na hii ya majuzi. kwa hiyo tuwe makini sana tunapotaka kupima uwezo wa watu kwani mzani wako inaonyesha wazi umemweka JK na jiwe la kilo nzima ktk Ujazo lakini Mwandosya hana kipimo upande wa pili isipokuwa elimu yake.
Jk kama rais amefanya nini?....well wewe ulitaka afanye kipi!... wanavyosema wao kaweka ahadi ambazo anazitimiza na Mwandosya ni mmoja kati ya wafanyakazi wake. if he had failed ni kutokana na hao kina Mwandosya kwani ndio mawaziri wanaoendesha hizo wizara.
kulingana na mtazamo wako ni wazi hakuna kiongozi yeyote aliyepata mafanikio nchini Tukiondoa Nyerer kisiasa kwani Tanzania bado ni maskini.

Mkandara,

Prof. Mwandosya hana matatizo yoyote kwenye chaguzi zake kule Mbeya. Kwenye ubunge anapita bila kupingwa.

Hata uchaguzi wa NEC mwaka 2002 alishinda kwa kura nyingi sana.

Hii ilikuwa mara ya kwanza kupata upinzani mkubwa, lakini bado kaibuka kwa ushindi wa asilimia 60.

Labda aliyekuambia amekosea majina. Wabunge wengine ndio wanamtumia prof kuwasaidia kule ili wasianguke akiwemo waziri wa afya prof. Mwakyusa.

Angalia source ya info hiyo , naona sio sahihi kabisa.
 
1.

Mkuu ukweli ni kwamba hili ni swali linatakiwa kujibiwa na wewe, yaani kinachomfanya Mwandosya awe zaidi ya Muungwana, unayoyasema hapo juu hayaelezi any fact either on Muungwana au Mwandosya,

2. ,

Mafanikio kisiasa ya Muungwana, bado huyaoni kuweza kuwa kuibuka mshindi katika urais, kutoka kwenye wananchi 45 millioni, huyu mtu mmoja kuweza kuibuka mshindi, unasema mafanikio yake kisiasa huyaoni au huyajui, are you serious?

3.

Ndio maana Muungwana, akamua kumpa uwaziri katika serikali yake ili amsaidie kuleta mafanikio katika kazi ya wananchi kwa taifa ,kazi ambayo sisi wananchi tumemkabidhi Muungwana, na sio Mwandosya.

4. [

Kugundua hilo tatizo la makundi na kulifanyia kazi, ni dalili za uwezo mkubwa kisiasa, ndio maana tukampa urais au?

5.

Hili tunaongea lugha moja, na tuendelee kukata ishus mkuu Bubu, safi sana.
__________________

Heshima Mbele Mkuu,

Kuibuka kuwa Rais katika umati wa 35 millioni ni achievement kubwa sana, lakini je aliibuka kidedea kwa njia za halali?

Kama harakati za kumpata mgombea wa CCM zingekuwa zimefanyika kihalali kabisa basi mimi naamini kabisa jamaa asingeipata nafasi hiyo. Hana vigezo vyovyote huko alikopitia miaka ya nyuma vinavyoonyesha kwamba ni kiongozi bora.

Hili tatizo la makundi, the jury is still out, let's wait and see the outcome of this after few years. Mimi naamini kabisa bado kuna makundi ndani ya CCM na yaliyotokea Dodoma siku chache zilizopita sidhani kama yameua makundi hayo. I may be wrong, but I doubt it.
 
Mkuu Bubu,

You have the right stuff, lakini unachanganya ishus mbili hapa, uhalali wa uchaguzi na uwezo wa mshindi,

ni lazima kwanza uthibitishe kuwa wagombea wengine wote hawakuvunja huo uhalali, ndipo umhukumu mgombea aliyeshinda, otherwise hiyo inakuwa ni part ya uwezo wenyewe wa ushindi ambao Mwandosya anahitaji kumheshimu Muungwana, kwa kuweza kuwa nao maana hiyo ni skill,

Otherwise heshima mbele kwa kuwa na hoja!
 
Kwangu mimi vyote hivyo vya uhalali wa uchaguzi na uwezo wa ushindi inaonyesha kwamba mshindi alikuwa hana imani na uwezo wake kama kiongozi ndio maana akaona bora anunue kura tena kwa forex ili kuibuka kidedea, vinginevyo kama angekuwa anajiamini kwa uwezo aliokuwa nao kama kiongozi kusingekuwa na sababu ya kutoa takrima alias rushwa. Hakuwa na vigezo vyovyote vya kuwaonyesha wapiga kura mafanikio mbali mbali aliyoyapata katika anga za kisiasa. Mkuu nimeshasema hapa kwamba chaguzi zote za CCM zina kasoro ya namna moja au nyingine. Watanzania wengi walitegemea kwamba mgombea wa CCM 2005 angekuwa ni yeye hivyo kama kiongozi angekuwa mstari wa mbele kabisa kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa hauna mizengwe ya aina yeyote ile ili mshindi apatikane kihalali, lakini wana mtandao siku nyingi walishaanza kukusanya mabulungutu dhidi ya kinyanga'anyiro hicho.
 
@Field Marshall ES

Mafanikio kisiasa ya Muungwana, bado huyaoni kuweza kuwa kuibuka mshindi katika urais, kutoka kwenye wananchi 45 millioni, huyu mtu mmoja kuweza kuibuka mshindi, unasema mafanikio yake kisiasa huyaoni au huyajui, are you serious?

Mkuu, naheshimu mawazo yako, lakini napingana na wewe katika takwimu hizo hapo juu. Kabla sijaongelea ushindi wenye mawaa wa JK, ningeomba kwanza kupingana na wewe katika takwimu hizo. Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC), matokeo yanaonyesha kuwa idadi ya kura zote zilizopigwa mnamo mwaka 2005 katika uchaguzi mkuu wa raisi ni 11,365,477 (95.70%). Zilizokataliwa ni 510,450 (4.30%). Kati ya kura zote hizo, Kikwete alipata kura 9,123,952 (80.28%) akifuatiwa na Mbowe, kura 668,756 (5.88%). Wagombea wengine sijaweka hapa, kura zao zilikuwa kidogo sana. Jumla ya wapigakura wote walioandikishwa mwaka huo 2005 ni 16,401,694. Kwa takwimu hizi basi, utagundua kuwa sio Watanzania wengi walipiga kura mwaka 2005, yaani chini ya nusu ya Watanzania wote ambao kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002 tulikuwa 34,569,232
Sasa wewe hiyo idadi ya watu milioni 45 umeitoa wapi?
Najua wewe ni kada wa chama tawala, lakini ningeomba tuwe na ushabiki wa kweli.
Vyanzo vya takwimu zangu ni tovuti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC (http://www.nec.go.tz/results/2005_pres_candidate_results.pdf) na tovuti ya serikali ya Tanzania (http://www.tanzania.go.tz/census/regions.htm).
Nawasilisha.
 
Bubu ataka kusema,
Nadhani umesahau kuwa mwandosya ktk chaguzi zake zote ushindi wake umekuwa na matatizo. navyosikia huko Mbeya kama sio CCM kusimama imara alikuwa nje ktk chaguzi zote ikiwa na hii ya majuzi. kwa hiyo tuwe makini sana tunapotaka kupima uwezo wa watu kwani mzani wako inaonyesha wazi umemweka JK na jiwe la kilo nzima ktk Ujazo lakini Mwandosya hana kipimo upande wa pili isipokuwa elimu yake.
Jk kama rais amefanya nini?....well wewe ulitaka afanye kipi!... wanavyosema wao kaweka ahadi ambazo anazitimiza na Mwandosya ni mmoja kati ya wafanyakazi wake. if he had failed ni kutokana na hao kina Mwandosya kwani ndio mawaziri wanaoendesha hizo wizara.
kulingana na mtazamo wako ni wazi hakuna kiongozi yeyote aliyepata mafanikio nchini Tukiondoa Nyerer kisiasa kwani Tanzania bado ni maskini.

Nitakurudia kwa hili lakini kwa hakika umenena sivyo. Ni mawili makuu: either hauna upeo mzuri wa siasa za awamu ya nne au na wewe ni mwanamtandao.
 
Bubu ataka kusema,
Nadhani umesahau kuwa mwandosya ktk chaguzi zake zote ushindi wake umekuwa na matatizo. navyosikia huko Mbeya kama sio CCM kusimama imara alikuwa nje ktk chaguzi zote ikiwa na hii ya majuzi. kwa hiyo tuwe makini sana tunapotaka kupima uwezo wa watu kwani mzani wako inaonyesha wazi umemweka JK na jiwe la kilo nzima ktk Ujazo lakini Mwandosya hana kipimo upande wa pili isipokuwa elimu yake.
Jk kama rais amefanya nini?....well wewe ulitaka afanye kipi!... wanavyosema wao kaweka ahadi ambazo anazitimiza na Mwandosya ni mmoja kati ya wafanyakazi wake. if he had failed ni kutokana na hao kina Mwandosya kwani ndio mawaziri wanaoendesha hizo wizara.
kulingana na mtazamo wako ni wazi hakuna kiongozi yeyote aliyepata mafanikio nchini Tukiondoa Nyerer kisiasa kwani Tanzania bado ni maskini.

Hapana mkuu.
Habari hizo hapo juu kuwa Mwandosya bila sisiemu Mbeya kukaa sawa angeshindwa sio kweli kabisa, ni mbinu chafu tu za wanamtandao kutaka kuonyesha kuwa wanakubalika Mbeya, kitu ambacho sio kabisa. Wana sisiemu wa kule walifanya kile ambacho wanamtandao hawakukitarajia, kumbwaga Mwang'onda na kumpa kura Mwandosya, na Mwang'onda aliondoka uku mbini hata kabla ya matokeo hayajatoka. Wanamtandao walikuwa wanaelekea siko, ndio maana baadhi ya mikoa wakawapiga breki mbaya, ikiwemo Mbeya. Mwandosya aligombe uongozi NEC akitokea mkoani Mbeya, hakuwepo katika kura za zile nafasi 20 bara wala wazazi. Kumbuka zomea zomea ya viongozi, Mbeya walikubuhu.
Kitu kimoja tu ambacho naungana na wewe ni kuhusu tetesi za bifu ya chini chini ambayo hakuna hata mmoja kati ya JK na Mark Mwandosya yuko tayari kuelezea. Kwamba, kwa nini JK hajafika Mbeya tangu achaguliwe kuwa raisi mwaka 2005? Mara ya mwisho kufika ilikuwa ni wakati wa kampeni za uraisi mwaka huo.
Labda ES na Mkandara mna ufafanuzi na suala hili, naomba mwanga kidogo.
 
Kwa hiyo unataka kusema Mwandosya anapendwa sana mkoani Mbeya!Unakumbuka vizuri ziara ya JK mkoani Mbeya wakati wa uchaguzi?...unakumbuka kuwa aliwasisitiza wananchi kumchagua Mwandosya na kuwa anamhitaji sana mtu huyu. Wapo wagombea ambao hakuwapigia debe kabisa na Mwandosya siii mmojawapo.
Kama kulikuwepo na kampeni dhidi yake nina hakika asingewa ktk majina ya wagombea CCM Mbeya kwani kama waliweza kumwngusha Sumaye na wengine toka kambi ya Mkapa/Malecela.
Mimi nadhani haya maswala ya JK na Mwandosya ni uvumi mtupu ambao umelenga kuonyesha kuwa Mwandosya is a good hard working politician.
Kama kuna beef basi naweza kubali kati ya mwandosya na EL kwani huyu ndiye hupenda kujenga beef na watu ovyo bila sababu ya maana. Otherwise, JK bad ni rais wetu ka ushindi wa asilimia 80. kutopiga kura mwetu hakuwezi kuondoa ushindi wake wala kudhoofia percentage hiyo. haiwezekani watu wote millioni 34 wapige kura na haijawahi tokea duniani the entire population kupiga kura. Licha ya kura hata statistics zozote zile hutumia watu wachache kupata kuelewa asilimia ya maoni ya wananchi kwa ujumla.
JK katupiga bao na ambition yake imekamilika hata ktk achievements zake ni lazima tutaweka his excellente - Hon mr Mpezidaaaa!
 
Najua wewe ni kada wa chama tawala, lakini ningeomba tuwe na ushabiki wa kweli.

Mkuu wangu either una hoja kuhusiana na hii ishu au huna, kwa sababu niliyoyasema mimi hayahusiani kabisa na hizo namba ulizozitoa, mimi nimemaanisha kuwa kwa hesabu za haraka, sasa hivi tuko wabongo 45 millioni, sikusema habari za waliopiga kura 2005, wala waliopiga kura mahali popote, sasa sielewi wewe hayo umeyatoa wapi mkuu?

Halafu aliyekwambia mimi ni kada wa chama chochote ni nani? je wewe ni kada wa nini? mkuu wangu haya ya kizamani tulishayapita siku nyingi, point yangu ilikuwa Muungwana, kati ya wabongo 45 millioni, ameweza kuibuka rais, huwezi sema hana mafanikio ya siasa, FULL STOP.

Sasa ahsante kwa elimu ya namabaz, isipokuwa in the future uliza kama huelewi badala ya kutoa hukumu bila ya kesi ya msingi, ila ningependa kujua wewe ni kada wa nini?
 
Unakumbuka vizuri ziara ya JK mkoani Mbeya wakati wa uchaguzi?...unakumbuka kuwa aliwasisitiza wananchi kumchagua Mwandosya na kuwa anamhitaji sana mtu huyu.

Hakusema Mwandosya bali alisema prof.alikuwa ana maana huyo mwana mtandao waziri wa afya sijuhi anaitwa nani?
 
Tatizo nini wazee wangu,sera ni zilezile hivyo ata angeingia Issa Shivji ambaye mimi ninamuita statist angekuwa kama hao walio mtangulia.Swala la msingi ni kubadilisha sera na katiba ya chama.Mwandosya,Muungwana kama alivyoitwa na baadhi ya walionitangulia hapo juu wanatumikia sera na katiba moja ya chama ambayo imejaa matatizo.Haroub Othman alikuwa anasema mabadiliko yaliyofanywa na chama ni kisura tuu,lakin hategemei kutoka jipya lolote katika timu hii mpya.
Yako mambo mawili ambayo nadhani Muungwana anajaribu kujikosha mbele ya watu.Kwanza anataka kuua makundi ili kusiwe na mgongano kwani tayari yu madarakani.Kazi ya wanamtandao ilikwisha isha na hana matatizo tena kwani 2010 CCM wanakawaida ya kuachiana mgombea mmoja tu aweze kuchukua fomu.Principle of oligarchy inasema the one who elect is the one who loose.Wanamtandao wameshapoteza.
Pili amehamua kujiweka mbali kidogo namfadhili wake Rostam Aziz kwani inaweza kumletea shida hapo baadaye kwani wahindi wanamatatizo sana ktk biashara zao sasa ikionekana anapata backup ya mnene ni ngoma mzito.
Ukweli bado kazi ni kubwa kweli kweli.
 
alivyosema ES ni sawa sawa tu kuhusiana na hiyo population, hiyo inatokana na kwamba waliopiga kura ni wale ambao ni above 18, sasa fikiria kuna wangapi ambao ni below that gap, halafu vile vile angalia amabao hawakupiga kura, then angalia kura zilizoharibika (kumaanisha hazikuhesabiwa) !!
 
Hapa tunazungumzia mafanikio ya kiutendaji ama ya kisiasa?
Kisiasa JK ameshampiga bao sana Prof, kielimu Prof yuko mbele labda tuhoji kiutendaji.
 
Kwa hiyo unataka kusema Mwandosya anapendwa sana mkoani Mbeya!Unakumbuka vizuri ziara ya JK mkoani Mbeya wakati wa uchaguzi?...unakumbuka kuwa aliwasisitiza wananchi kumchagua Mwandosya na kuwa anamhitaji sana mtu huyu. Wapo wagombea ambao hakuwapigia debe kabisa na Mwandosya siii mmojawapo.
Kama kulikuwepo na kampeni dhidi yake nina hakika asingewa ktk majina ya wagombea CCM Mbeya kwani kama waliweza kumwngusha Sumaye na wengine toka kambi ya Mkapa/Malecela.
Mimi nadhani haya maswala ya JK na Mwandosya ni uvumi mtupu ambao umelenga kuonyesha kuwa Mwandosya is a good hard working politician.
Kama kuna beef basi naweza kubali kati ya mwandosya na EL kwani huyu ndiye hupenda kujenga beef na watu ovyo bila sababu ya maana. Otherwise, JK bad ni rais wetu ka ushindi wa asilimia 80. kutopiga kura mwetu hakuwezi kuondoa ushindi wake wala kudhoofia percentage hiyo. haiwezekani watu wote millioni 34 wapige kura na haijawahi tokea duniani the entire population kupiga kura. Licha ya kura hata statistics zozote zile hutumia watu wachache kupata kuelewa asilimia ya maoni ya wananchi kwa ujumla.
JK katupiga bao na ambition yake imekamilika hata ktk achievements zake ni lazima tutaweka his excellente - Hon mr Mpezidaaaa!

Mkandara,

Naona hili bado unaendelea kulirudia wakati sio sahihi.

Prof Mwandosya alichaguliwa bila kupingwa kwenye ubunge mara mbili yaani 2000 na 2005, sasa hili la JK kumpigia kampeni linatoka wapi? Unaweza kusoma hapa kama bado huamini, search bila kupingwa.

http://www.uchaguzitanzania.com/new...TTCL-mafao-yao-kabla-ya-kuwapunguza/print/697

Ni katika wabunge wachache sana kama sio pekee ambao wameupata ubunge mara mbili bila kupingwa.

Binafsi sisemi kwamba bado kuna ugomvi kati ya JK na Mwandosya ila nataka kusahihisha hiyo hoja yako kwamba Mwandosya alikuwa na matatizo ya uchaguzi kule Mbeya.

JK alivyokuwa Mbeya wakati wa kampeni alitumia muda mwingi kuelezea kwamba yeye hana ugomvi na Prof. Lengo lilikuwa kwa yeye
kujipigia kampeni maana Mbeya kulikuwa na dhana kwamba anamfanyia visa Mwandosya.

Narudia tena, uchaguzi pekee ambao Mwandosya amepata mpinzani ni huu wa CCM NEC mwaka huu lakini na wenyewe kashinda kwa asilimia 60, je huko ni kuwa na matatizo?

Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2000, prof alitumia muda wote kuwasaidia wabunge wa Kyela (Mwakipesile) na Rungwe Magharibi (prof. Mwakyusa)kuwapigia kampeni na hao wawili waliponea chupu chupu.
 
Back
Top Bottom