Mjenzi kakwangua barabara sehemu tatu tofauti na kulazimisha magari kupita juu ya tuta kuwa kero, alianza kukwangua kipande cha polisi ufundi hadi JKT Mgulani kabla hajaweka lami akaacha hapo na kuhamia kukwangua kuanzia mataa ya TIA mpaka mzunguko wa sabasaba na penyewe amepaacha hivyohivyo na kwenda kukwangua eneo la mzunguko wa bandari. kero zaidi ni pale inapoonekana kuna greda 2 tu site na zenyewe zime paki tu.