Vijumba vilivyopo pembeni ya barabara ya Morogoro Road vinatia aibu na fedheha kwa Watanzania

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,293
Pamoja na kujitahidi kuwa na barabara za kisasa ambazo zinachangia kupendezesha mandhari ya nchi, lkn muonekano huu wa vijumba vilivyochoka pembezoni mwa barabara vinafanya upendezaji huo uwe ni sawa na mtu alievaa nguo nzuri, lkn chini amevaa viatu vichafu na vya kutoboka.

Kwa wenzetu mfano Afrika kusini unakuta maeneo mengi ya barabara kubwa kama hiyo yamejaa viwanda vikubwa vikubwa, maduka makubwa (malls), majumba ya kisasa nk.

Ukiachilia mbali South Africa, hata hapo bongo ukiangalia mazingira ya pembeni ya barabara ya Bagamoyo road ni tofauti na mbali na mazingira ya Morogoro road. Bagamoyo raod nyumba nyingi zimekaa kimpangilio na kimuonekano mzuri kuliko Bagamoyo road na hata Kilwa road.

Nafikiri wazee wa miundo mbinu, na wale wanaohitaji kuona nchi yetu inang'aa kila sehemu wangekaa wakaliangalia hili vizuri. Wawashauri wale wote waliojenga pembezoni mwa barabara ya Morogoro road wajenge mijengo itayopendezesha muonekano wa barabara, na wale ambao hawana uwezo walazimishwe kuuza maeneo yao kwa wale wenye uwezo wa kujenga viwanda, maduka makubwa (malls), sheli za mafuta, majumba ya maana nk ili mtu anapokuja kwa mara ya kwanza aanze kuona mabadiliko kuanzia upande wa barabara mpaka majengo ya pembezoni.

Tukiachana na ukubwa wa barabara, kwangu mimi Bagamoyo road ndio barabara ambayo imejengwa kimuonekano mzuri kuliko barabara zote zinazotoka mikoani na nje ya nchi kuingia Dar es salaam including Kilwa road na hiyo Bagamoyo road yenyewe.
 

Attachments

  • Screenshot_20231108-050945.jpg
    Screenshot_20231108-050945.jpg
    118.4 KB · Views: 2
Back
Top Bottom