Kilwa Road baada ya kumalizika imeanza kuharibika!

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,619
2,567
Barabara ya Kilwa inapitika vizuri baada ya kazi ya ujenzi kumalizika. Ila tatizo ni mifereji. Kuna uzembe kiasi kwamba sehemu kadhaa zimeanza kuonyesha mmomonyoko hasa kuanzia kwa Aziz Ali hadi Mbagala Rangi Tatu.

Pili, baadhi ya madreva wanaegesha magari yao kwenye sehemu iliyoachwa wazi (katikati ya barabara) hasa kwa Aziz Ali, Mtoni-Mtongani na maeneo ya Mbagala Rangi Tatu.

Tatu, kwenye 'round abouts' kumeanza kuonyesha uharibifu pia. Kunakuwa na matutamatuta kwenye lami. Baadhi ya watu wanasema barabara haikujengwa kwa ubora unaotakiwa kwa vile ulikuwa msaada kutoka serikali ya Japan, hivyo wahusika hawana uchungu na fedha iliyotumika na ndio maana mifereji imeachwa bila kujengwa vizuri au sehemu zile ambazo imejengwa siyo kwa ubora unaotakiwa.

Nne, kwa vile barabara yenyewe imejengwa bila ya kuwekwe njia za dharura, madreva wanatumia nafasi inayotumiwa na waenda kwa mguu ili kugeuza gari kama wanataka kurudi walikotoka au kama kuna haja ya kwenda kwenye kituo cha mafuta.

Je, wengine ambao mmeshatumia barabara hiyo mnasemaje?

========
August 2011:

Magufuli kwa kuwafanya Kajima warudie barabara ya Kilwa, umeonyesha leadership!
Balozi wa Japan pamoja na Waziri Magufuli wametangaza kuwa barabara ya Kilwa iliyojengwa chini ya kiwango, kurudiwa tena kujengwa upya.

Balozi wa Japan ameomba msamaha kwa kampuni ya Kajima kutokujenga kwa kiwango barabara hiyo. Kampuni ya Kajima itarudia kujenga kwa gharama zake.

Ahsante Kikwete, ahsante Magufuli, ahsante Balozi wa Japan.

Makosa yametendeka, makosa yameonekana, makosa yamekubalika, makosa yanarekebishwa. Huo ndio uongozi mahiri na si kulalama tu kutwa kucha.
 
For the past two years engineers had been working on a damaged section along Kilwa Road near Karibu Textile Mills (KTM) in Temeke District, Dar es Salaam without success. The repair work is yet to be completed.

01_11_pwnr8h.jpg

Serikali ya Japan [kupitia ubalozi wake hapa nchini] imekubaliana na Wizara ya Ujenzi kuwa Barabara ya Kilwa haistahili kupokelewa.

Kutokana na hali hiyo Magufuli ameshinikiza mkandarasi airudue upya jambo ambalo Wajapani [kupitia Balozi] wamelikubali akiwemo mkandarasi [Kajma] mwenyewe. Ikumbukwe fedha za ujenzizilitolewa na Serikali ya Japan.

Ngereja na Mkulo wanasubili nini kuiga mfano huo kuhusu umeme na misamaha ya kodi?!!
 
Kwa nini wetu waadhibiwe na sio wao wanaorudia tena tuna uhakika gani wataweka yenye kiwango wizi mtupu
 
Yah kwa kweli ile road huitaji kuwa mhandisi kugundua mapungufu hata kama ni msaada!
 
Balozi wa Japan pamoja na Waziri Magufuli wametangaza kuwa barabara ya Kilwa iliyojengwa chini ya kiwango, kurudiwa tena kujengwa upya.

Balozi wa Japan ameomba msamaha kwa kampuni ya Kajima kutokujenga kwa kiwango barabara hiyo. Kampuni ya Kajima itarudia kujenga kwa gharama zake.

Ahsante Kikwete, ahsante Magufuli, ahsante Balozi wa Japan.

Makosa yametendeka, makosa yameonekana, makosa yamekubalika, makosa yanarekebishwa. Huo ndio uongozi mahiri na si kulalama tu kutwa kucha.
 
Habari njema hii kwani barabara ile ipo chini sana ya kiwango,ila naomba kujua inakuwaje balozi ndio atoe tamko? au kajima ni kampuni ya serikali.
 
Serikali ya Japan [kupitia ubalozi wake hapa nchini] imekubaliana na Wizara ya Ujenzi kuwa Barabara ya Kilwa haistahili kupokelewa. Kutokana na hali hiyo Magufuli ameshinikiza mkandarasi airudue upya jambo ambalo Wajapani [kupitia Balozi] wamelikubali akiwemo mkandarasi [Kajma] mwenyewe. Ikumbukwe fedha za ujenzizilitolewa na Serikali ya Japan.
Ngereja na Mkulo wanasubili nini kuiga mfano huo kuhusu umeme na misamaha ya kodi?!!

Ngereja kisha irudisha Dowans kwa jina jipya, mbona husemi hilo?
 
bara bara ya kilwa road?????????? Eh eh eh eh rudia tena gamba..

balozi wa japan pamoja na waziri magufuli wametangaza kuwa barabara ya kilwa iliyojengwa chini ya kiwango, kurudiwa tena kujengwa upya.

Balozi wa japan ameomba msamaha kwa kampuni ya kajima kutokujenga kwa kiwango barabara hiyo. Kampuni ya kajima itarudia kujenga kwa gharama zake.

Ahsante kikwete, ahsante magufuli, ahsante balozi wa japan.

Makosa yametendeka, makosa yameonekana, makosa yamekubalika, makosa yanarekebishwa. Huo ndio uongozi mahiri na si kulalama tu kutwa kucha.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
kajima,kajima,kajima a company of repute leo hii inaambiwa itengeneze upya barabara-yaani kajima must now be so desperate ku risk reputation yao
 
Asante mkuu kwa habari, nyie wengine mnasubiri source hii inadhihirisha jinsi gani hamjishuhurishi kufanya tafiti za source
 
Back
Top Bottom